Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

69. Ninaona Ukweli wa Upotovu wa Watu

Li Heng    Jiji la Suqian, Mkoa wa Jiangsu

Miongoni mwa maneno ambayo kwayo Mungu humfichua mwanadamu nilipata kifungu hiki, “Ilisemwa hapo awali kwamba watu hawa ni uzao wa joka kubwa jekundu. Kwa kweli, ili kuwa wazi, wao ni mfano halisi wa joka kubwa jekundu” (“Ufafanuzi wa Tamko la Thelathini na Sita” katika Neno Laonekana katika Mwili). Nilidhani hili halikunihusu. Ilionekana kwangu kwamba Mungu alifichua maneno haya kwa wale wanaomiliki mamlaka, kwa sababu wao ni joka kubwa jekundu lililobadilishwa; wao hufanya maovu, matendo ya kuasi, kumpinga Mungu, kuivuruga na kuiharibu kazi ya Mungu, na kuwadhulumu kwa ukatili watu wateule wa Mungu. Mimi, kwa upande mwingine, ni muumini katika Mungu anayetimiza wajibu wake kanisani, na hata kama mimi ni mpotovu, sijawakaribia kwa uovu, wala upotovu si wa kina sana. Ningewezaje kuwa joka kubwa jekundu lililobadilishwa? Hilo lilikuwa hivyo mpaka uzoefu ukanifanya kutambua kwamba kiini cha asili yangu kilikuwa sawa na kile cha joka kubwa jekundu, na kwamba nilikuwa, bila shaka, joka kubwa jekundu lililobadilishwa.

Kulikuwa na shemasi wa kike katika kanisa letu ambaye hakuwa na uangalifu katika kutimiza wajibu wake na mara nyingi alisahau kuhudhuria mikutano midogo ya vikundi. Nilifanya ushirika naye, nikisema, "Hupaswi kutowajibika sana kuhusu wajibu wako, na huwezi kughilibu upendavyo kuupitia. Hupaswi kuzingatia sana familia yako, kwa kuwa hili likiendelea, ukisahau hata mikutano yetu midogo ya vikundi, unajua jinsi madhara yatakavyokuwa makubwa? …"Baada ya kusema hayo, hakukataa kukubali tu, alitoa visingizio na kupeana sababu za kunipinga. Katika moyo wangu, niliwaza, "Yeye hawezi kuwa kusudi la wokovu wa Mungu, anaweza? Yeye ni mtu asiyestahili kutumiwa na Mungu, au mtu mwovu anayefichuliwa kwangu? " Nilianza kuangalia kwa karibu kutafuta mtu wa kuchukua nafasi yake kwa mikutano yangu midogo. Mara tu nilipopata mtu aliyefaa kwa kazi hiyo, nilipanga kumuondoa. Lakini mtu aliyefaa aliniepuka, kwa hiyo baada ya muda chaguo langu la pekee lilikuwa kufanya ushirika na yule shemasi tena, na baadaye akaelewa kuwa ameshindwa kutekeleza wajibu wake na alikuwa wa kutowajibia na mzembe, na alitaka kulipia makosa yake ya zamani. Lakini bado, daima nilihisi kama halikutosha, na sikuwa na upendo mwingi kwake baada ya hayo. Wakati mmoja, nilimtaka awe na mkutano na familia moja mwenyeji ambayo ilikuwa mbali kidogo, lakini alikataa, akisema hakuwa tayari kwenda. Hasira moyoni mwangu ilivimba wakati aliposema hilo. Nilitaka kumfukuza papo hapo, kumtupa kwa kikundi chake kidogo cha awali, na kumsahau, kwa sababu watu kama yeye ni shida kubwa, nilifikiri, mwenye machagu katika kutimiza wajibu wao, kufanya kile wanachopenda na kupuuza kile wasichopenda. Yeye hunipinga katika chochote nisemacho na hashikilii mipango ya kanisa kwake, hivyo ni manufaa gani kanisa linapata kumweka? Anapaswa tu kufukuzwa, na yeye anastahili kila chozi litakalombubujika kuhusu hilo! Alipanda hilo na ni sharti alivune, na ingawa nilijua kuwa kuwafukuza watu kwa ugeugeu huenda kinyume na kanuni, wazo hilo liliendelea kunijia akilini mwangu, sikuweza kulidhibiti, na moyoni mwangu lilinisumbua daima, likifanya hali yangu kuwa shaghalabaghala kabisa. Yote niliyoweza kufanya ni kuomba kwa Mungu, "Mungu, dada yangu hanitii, na ninataka kumfukuza na kumwona akifikwa na maumivu na mateso. Ninahisi kama nitalipuka ikiwa sitamfukuza. Sitaki pia kutenda kwa wazo langu la ghafla au bila subira na kwa kiburi, sitaki kuikosea tabia Yako kwa makusudi. Mungu, nakusihi Uniokoe!" Baada ya kuomba, hamu yangu ya kumfukuza haikuwa na nguvu kama hapo awali, na nilikuwa na utulivu zaidi. Na kisha kifungu cha neno la Mungu kilielea juu ya akili yangu, "Maonyesho ya joka kubwa jekundu ni upinzani Kwangu, ukosefu wa ufahamu na ujuzi wa maana ya maneno Yangu, mateso ya mara nyingi Kwangu, na kutafuta kutumia hila kuingilia usimamizi Wangu. Shetani hudhihirishwa ifuatavyo: kushindana na Mimi juu ya mamlaka, kutaka kuwamiliki watu wangu wateule, na kutoa maneno hasi ili kuwadanganya watu Wangu" ("Tamko la Tisini na Sita" katika Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu yalinishtua. Si tabia yangu ni sawa na ya joka kubwa jekundu kabisa? Joka kubwa jekundu humpinga Mungu, humtesa Mungu, na kuingilia kazi ya Mungu. Si hivyo hasa ndivyo niliyokuwa nikifanya? Kufukuza mtu kufuatana na wazo langu la ghafla kungekuwa kujifanya shetani, Shetani mmoja, ambaye huvuruga na kuangamiza kazi ya Mungu ya wokovu miongoni mwa binadamu. Mungu, nilikuwa kweli joka kubwa jekundu ililobadilishwa. Katika ushirika wa mtu nilisoma, "Angalia jinsi joka kubwa jekundu humtesa Mungu na ukatili wake kwa watu wateule wa Mungu, kisha angalia upinzani na uasi kwa Mungu ndani yako mwenyewe. Angalia uhusiano wako wa fujo na watu walioteuliwa na Mungu. Kuna mifundo mingi mno na ubinafsi ndani yako. Una tofauti gani na joka kubwa jekundu? … Watu wengi huwa hawaelewi sumu za joka kubwa jekundu ambazo hujificha ndani yao. Wao hufikiri kuwa joka kubwa jekundu ni ovu mno, na wao hujiambia kuwa watakapomiliki mamlaka, watakuwa bora zaidi kuliko joka kubwa jekundu, lakini ndivyo hivyo hali kweli? Ungeshika mamlaka hivi sasa, ni kiasi gani ungekuwa bora zaidi kuliko joka kubwa jekundu? Unaweza kufanya vizuri zaidi kuliko joka kubwa jekundu? Ukweli ni kwamba joka kubwa jekundu kushika mamlaka hakuna tofauti na wanadamu wowote wapotovu. Ikiwa joka kubwa jekundu linaweza kuwaua watu milioni 80, ni wangapi unaweza kuua ukishika mamlaka? Wengine husema, 'Ningeshika mamlaka, singemuua mtu yeyote.' Unapokuwa ukinena tu, mtu fulani atasimama na kukulaani, na utakasirika na kusema, 'Basi nitamuua moja tu, nitafanya jambo la pekee.' Wakati kundi moja linapoinuka kukupinga, utasema, 'Kuua kundi si jambo kubwa, joka kubwa jekundu liliua watu milioni 80. Ninaua tu kundi ndogo, hiyo ni kidogo sana kuliko joka kubwa jekundu.' Wakati watu milioni 10 watainuka kukupinga, utasema, 'Naweza kuwaua hawa watu milioni 10 pia, kwa sababu nisipofanya hivyo, nitawezaje kushikilia mamlaka?' Je, huoni tatizo hapa? Hata kama hufanyi uovu bila mamlaka, hakuna uhakika kwamba hutafanya matendo maovu utakaposhika mamlaka, kwa sababu asili za mwanadamu zote ni sawa" ("Jinsi Watu Wanavyopaswa Kushirikiana na Kazi ya Mungu ya Kumkamilisha Mwanadamu" katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha (III)). Kupitia kupata nuru na mwangaza wa maneno ya Mungu na uchambuzi wa ushirika wa mwanadamu, hatimaye niliona kwa dhahiri uso wangu wa kweli, kwamba nilikuwa joka kubwa jekundu lililobadilishwa, na kwamba hali yangu potovu haikuwa tofauti na asili ya joka kubwa jekundu. Uovu kwa asili, joka kubwa jekundu humpinga Mungu na kuwatesa watu wateule wa Mungu, kwa kiburi hutaka kupiga marufuku kazi ya Mungu ya wokovu kati ya wanadamu na kufanya ulimwengu wote kumkana Mungu. Linataka kutawala vyote ambavyo Mungu ameviumba, kumfanya binadamu kuyapigia magoti mamlaka yake. Si niliyotenda leo ni sawa na hivyo? Dada yangu hakuuelewa ukweli kwa dhahiri na hakuujali wajibu wake, lakini badala ya kumsaidia kwa roho ya upendo, nilimtaka tu kufikia matarajio yangu yote. Nilimwona akiwa wa kutowajibika katika kazi yake, kwa hiyo nikaanza kumdharau na kumchukia, na hata nikaamua kuwa alikuwa mwovu aliyefichuliwa kwangu na Mungu, likifanya fikira zangu kutokuwa tofauti na zile za joka kubwa jekundu katika uwezo wangu wa "kuendeleza bila kikomo" na "kuwaua wasio na hatia." Wakati dada yangu alipokuwa na shida za familia na alikuwa baridi, badala ya kufanya ushirika maneno ya Mungu pamoja naye ili kumsaidia kuelewa upendo wa Mungu, mahitaji, na matumaini kwa watu, nilitumia elimu na mafundisho ili kumwekea mipaka, kumleta kabisa chini ya udhibiti wangu. Si tabia yangu iliionyesha dalili sawa na za joka kubwa jekundu—kujikuza, kutoonyesha uchaji wa Mungu, na hali ya kujidai? Dada yangu alipokosa kunitii, nilimchukia kwa kina. Nilitaka kumfukuza na kumtoa nje ya kanisa. Lakini si hivyo ni vitendo viovu vya joka kubwa jekundu—"uhalifu" na "Unitii au uangamie"? Mungu, naona kwamba mimi ni shetani ambaye hukupinga, kwamba mimi ni mbaya zaidi kuliko mnyama, kwamba mimi ni asiyefaa ambaye angebwagwa zamani. Joka kubwa jekundu linaweza kuwaua watu milioni 80, lakini kama ningeshika mamlaka, ningekuwa mwovu vilevile, mwenye makosa, mhalifu. Kama si kwa mipango ya kazi na kanuni zilizofafanuliwa na kanisa, na kama si kwa usimamizi wa ndugu zangu wa kiume na wa kike, si ningekuwa nimemsukuma dada yangu kwenye "bloku ya chakari" zamani? Asili ya joka kubwa jekundu ni ovu na yenye makosa, huwa inaua bila ya kupepesa jicho, humwangamiza yeyote asiyejali au kuenda dhidi yake na mashtaka ya kubuniwa ya uhalifu, na neno moja au tendo liliokosewa mbele yalo ni kukaribisha kifo, lakini mimi si ni sawa nalo? Dada yangu hakunitii na hakufanya kile nilichotaka, ambapo nilikuwa na hasira sana kiasi kwamba nilimgeukia na nilitaka kumshambulia, kwa kweli hakuna kitu ila kumfukuza na kumtoa nje ya kanisa kuliweza kuiridhisha hasira yangu.

Uzoefu huu ulinipa ufahamu wa kweli wa asili yangu potovu. Niliona kwamba nilikuwa kweli mtu bila mantiki au dhamiri, bila shaka dhuria wa joka kubwa jekundu. Lakini pia ulinipa imani kubwa ya maneno ya Mungu. Bila kujali ni kiasi gani maneno ya Mungu yanaweza kuchoma au kama ni sawa na mawazo ya mwanadamu, kila tamko ni ukweli wa milele, usiobadilika, na karibuni upotovu wa binadamu atathibitishiwa kabisa. Mungu! Ninataka kutimiza wajibu wangu vizuri ili kukulipizia Wewe kwa wokovu, nataka kupatana na ndugu zangu wa kiume na wa kike kanisani na kufidia makosa yangu ya zamani, na kuwa mtu mpya ambaye hukufariji.

Iliyotangulia:Ni Muhimu Sana Kutii Kazi ya Roho Mtakatifu!

Inayofuata:Kazi ya Mungu ni Ya Hekima Sana!

Unaweza Pia Kupenda