36. Ni watu wangapi wa dini watakaorudi kwa Mungu katika maafa?

Maneno Husika ya Mungu:

Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 26” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Watu wengine husema, “Mwishowe, ni watu wangapi ndani ya jamii za dini wataweza kumwamini Mwenyezi Mungu?” Soma zaidi kuhusu maneno ya Mwenyezi Mungu na utajua. Kwa sasa, lango la neema halijafungwa bado, na hatujafika wakati wa maafa makubwa. Hasa wakati wa maafa makubwa, kutakuwa na watu wengine ndani ya jamii ya dini wanaorudi kwa Mungu kwa viwango mbalimbali. Hii ndiyo sababu huwezi kuamua kwa sasa “Wale wote ndani ya dunia ya dini wasiomkubali Mwenyezi Mungu lazima waangamie.” Bado kuna muda kiasi. Katika wakati huu, unajua ni nani katika jamii za dini ambaye atamkubali Mungu na nani hatamkubali Mungu? Hili ni jambo ambalo hatuwezi kuona vizuri; ni Mungu pekee anayejua. Hata hivyo, tunapoeneza injili na kushuhudia kuhusu Mungu kwa watu wa dini, tunapata kwamba wanakataa hili. Wote wanampinga na kumshutumu Mwenyezi Mungu. Je, sote hatujaona hili? Na kwa hiyo, kueneza injili kwa watu wa dini ni vigumu sana. Hili linaamua kwamba wale walio ndani ya dunia za dini ambao hatimaye watarudi kwa Mwenyezi Mungu ni wachache sana kwa idadi. Hii ni kwa sababu wanazuiwa vikali na wachungaji, wazee na fikira za dini; wamedanganywa kwa kina na uenezaji wa habari hasi. Hawana mioyo ya kutafuta ukweli na kuchunguza njia ya kweli. Je, hili si kweli? Ukienda katika eneo la dini kueneza injili, utakutana na yafuatayo: Kwanza, utakataliwa na kukumbushwa makosa yako; pili, utaaibishwa; tatu, utashambuliwa kwa pamoja, au kukejeliwa na kushutumiwa. Hata kutakuwa na watu watakaokupiga picha bila idhini yako na kuionyesha kwa wengine wote ndani ya kanisa na kusema, “Mtu huyu amekuja kueneza injili ya Mwenyezi Mungu. Hakuna mtu anayepaswa kumpokea.” Hivi ndivyo jinsi dunia ya dini inamtendea yeyote anayekuja kueneza injili ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Hili linaonyesha nini? Dunia ya dini kwa muda mrefu imefanya kazi kama ngome imara ya wapinga Kristo na imekuwa sehemu ya nguvu ovu za Shetani. Hata hivyo, huwezi kusema kwamba hakuna mtu kutoka dunia ya dini anayeweza kuokolewa—kuna wale wanaoweza kuokolewa, ni kwamba tu ni wachache sana, sana kwa idadi.

Umetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha, Juzuu ya 132

Watu wengine wanauliza, “Kwa nini unasema kwamba hakutakuwa na watu wengi kutoka ndani ya dini wanaokubali kazi ya Mungu kabla ya maafa makubwa? Sidhani hilo ni jambo la hakika.” Kutoka ndani ya waumini wa Enzi ya Neema, ndani ya kanisa lolote, wengi wao wako hapo kufuatilia ukweli kwa kweli, au kula mkate Wake hadi washibe tu? Watu wengi wako hapo ili kula mkate Wake hadi washibe tu. Je, hakuna watu wengi ambao wamepagawa na pepo, wanaoongea kwa ndimi, kupokea ufunuo, kuona maono, kuponya magonjwa, kufukuza pepo, na kuonyesha miujiza? Wale ambao wamepagawa na pepo wanaunda sehemu, wale wanaokula mkate Wake hadi washibe tu wanaunda sehemu, na wengine ambao ni wapinga Kristo na waovu wanaochukia ukweli pia wanaunda sehemu. Na tena kuna watu waliokanganywa ambao hawana ufahamu hata kidogo wa ukweli. Punde tunapoondoa makundi haya ya watu, wale waliobakia ambao wanapenda ukweli watakuwa wengi? Je, hata watajumuisha asilimia kumi kwa jumla? La, haiwezekani! Je, hii si hali halisi ya mambo? Kwa hiyo, wale walio ndani ya jamii ya dini ambao wataweza kurudi mbele za Mungu kabla ya maafa makubwa ni idadi ndogo sana ya watu; hawatajumuisha walio wengi hata kidogo, kwa sababu watu walio ndani ya dini wanaopenda ukweli daima wamekuwa wachache sana kwa idadi. Huu ni ukweli kamili, na hausemwi bila msingi.

Umetoholewa kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha, Juzuu ya 133

Iliyotangulia: 35. Kwa nini Mungu atawaweka wale wanaokataa kumkubali Mwenyezi Mungu katika maafa?

Inayofuata: 37. Mabadiliko ya tabia ni nini?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

3. Tofauti ni ipi kati ya kazi ya Mungu mwenye mwili na kazi ya Roho?

Wokovu wa Mungu kwa mwanadamu haufanywi moja kwa moja kupitia njia ya Roho ama kama Roho, kwani Roho Wake hawezi kuguzwa ama kuonekana na mwanadamu, na hawezi kukaribiwa na mwanadamu. Kama Angejaribu kumwokoa mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya Roho, mwanadamu hangeweza kupokea wokovu Wake. Na kama sio Mungu kuvalia umbo la nje la mwanadamu aliyeumbwa, mwanadamu hawangeweza kupokea wokovu huu. Kwani mwanadamu hawezi kumkaribia kwa njia yoyote ile, zaidi kama jinsi hakuna anayeweza kukaribia wingu la Yehova. Ni kwa kuwa mwanadamu wa kuumbwa tu, hivyo ni kusema, kuliweka neno Lake katika mwili Atakaogeukana kuwa, ndio ataweza kulifanya neno yeye Mwenyewe ndani ya wale wote wanaomfuata. Hapo ndipo mwanadamu atasikia mwenyewe neno Lake, kuona neno Lake, na kupokea neno Lake, kisha kupitia hili aokolewe kamili.

2. Dunia ya kidini inaamini kwamba maandiko yote yametolewa na msukumo wa Mungu na yote ni maneno ya Mungu; mtu anafaaje kuwa na utambuzi mintarafu ya kauli hii?

Si kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa binadamu, na ufasiri wa ajabu wa binadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni tafsiri sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahihi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote zaidi ya maarifa uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa manabii ulikuwa umetolewa na Mungu mwenyewe: Unabii wa Isaya, Danieli, Ezra, Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, watu hawa walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii wa Agano la Kale. Wakati wa Enzi ya Sheria watu hawa, ambao walikuwa wamepokea ufunuo wa Yehova, walizungumza unabii mwingi, ambao ulisemwa na Yehova moja kwa moja.

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki