Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda kwa Kristo wa Siku za Mwisho

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

13. Kuna tofauti ipi kati ya kuuelewa ukweli na kuyaelewa mafundisho?

Maneno Husika ya Mungu:

Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri kwa na namna hii: Naweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu anasema ni vizuri na kunipa hongera, hivyo inahesabika kama kuelewa neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata nuru kiasi kutoka ndani ya neno la Mungu na umefahamu umuhimu wa kweli wa neno la Mungu, ikiwa unaweza kueleza nia ya neno la Mungu na kile ambacho yatafanikisha hatimaye, punde haya yote yanaeleweka hilo linahesabika kama kuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa. Kwa sababu tu unaweza kutoa maelezo ya madoido ya maandishi ya neno la Mungu haimaanishi kuwa unalielewa. Bila kujali vile unavyoweza kueleza maandishi ya neno la Mungu bado ni mawazo na jinsi ya kufikiria kwa mwanadamu—ni bure!

Umetoholewa kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Wewe hufikiri kwamba kupata weledi wa maarifa ya ukweli ni muhimu hasa, na vile vile kukariri mafungu mengi ya maneno ya Mungu. Lakini jinsi watu wanavyoelewa neno la Mungu si muhimu hata kidogo. Ninyi hudhani ni muhimu sana kwa watu kuweza kukariri mengi ya maneno ya Mungu, kuweza kuzungumza mafundisho mengi na kugundua fomyula nyingi ndani ya maneno ya Mungu. Kwa hiyo, siku zote ninyi hutaka kuweka katika mfumo vitu hivi ili watu wote washirikiane, wakisema mambo sawa, na kuzungumza kuhusu mafundisho, ili wawe na maarifa sawa na kutii kanuni sawa—hili ndilo lengo lenu. Ninyi kufanya hili kunaonekana kuwa kwa ajili ya watu kupata ufahamu, wakati kinyume chake hamjui kwamba hili linawaleta watu katikati ya kanuni ambazo ziko nje ya ukweli wa maneno ya Mungu. Ili kuwaruhusu watu wawe na ufahamu halisi wa ukweli, ni lazima uuunganishe na uhalisi na kazi, na kutatua shida za utendaji kulingana na ukweli wa maneno ya Mungu. Ni kwa njia hii tu ndiyo watu wanaweza kuelewa ukweli na kuingia katika uhalisi, na kufanikisha matokeo kama hayo tu ndiko kuwaleta watu mbele ya Mungu kwa kweli. Ikiwa yote unayozungumzia ni nadharia za kiroho, mafundisho, na kanuni, ikiwa unaweka juhudi katika maneno sisisi tu, yote unayoweza kufanikisha ni kuwafanya watu waseme mambo sawa na kufuata kanuni, lakini hutaweza kuwaongoza watu kuelewa ukweli. Hasa hutaweza kuwafanya watu wajielewe vizuri zaidi, na kufanikisha toba na mabadiliko.

Umetoholewa kutoka katika “Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Kama mmesoma sana neno la Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandishi na hamna maarifa ya kwanza ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu wa vitendo, hamtajua neno la Mungu. Ili mradi unahusika, neno la Mungu si maisha, lakini barua bila uhai. Na kama unaamini tu barua bila uhai, huwezi kufahamu kiini cha neno la Mungu, wala kuelewa mapenzi Yake. Wakati tu unapitia neno Lake katika uzoefu wako halisi ndio maana ya kiroho ya neno la Mungu itafunguka yenyewe kwako, na ni katika uzoefu tu ambapo unaweza kufahamu maana ya kiroho ya ukweli mwingi, na ni kwa kupitia tu uzoefu ndio unaweza kufungua mafumbo ya neno la Mungu. Usipoliweka katika vitendo, basi haijalishi jinsi neno Lake lilivyo wazi, jambo pekee ambalo umeweza kushikilia ni maandishi na mafundisho tupu, ambayo yamekuwa kanuni za dini kwako. Si hili ndilo Mafarisayo walifanya? Kama mtatenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa vitendo kwenu; msipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwenu ni kidogo zaidi ya hadithi ya mbingu ya tatu. …

… Kuelea kwa kweli neno la Mungu hutokea wakati unautenda ukweli, na ni lazima uelewe ya kwamba “ni kwa kuutenda tu ukweli kunaweza kueleweka siku zote.” Leo, baada ya kusoma neno la Mungu, unaweza tu kusema ya kwamba unajua neno la Mungu, lakini huwezi kusema ya kwamba unalielewa. Baadhi wanasema kuwa njia pekee ya kutenda ukweli ni kuelewa ukweli kwanza, lakini hii ni nusu tu ya haki na sio sahihi kabisa. Kabla uwe na maarifa ya ukweli, bado hujapitia ukweli huo. Kuhisi ya kwamba unaelewa kitu unachosikia katika mahubiri sio kuelewa kweli, bali ni kuwa tu na maneno halisi ya ukweli, na si sawa na kuelewa maana halisi humo. Kwa sababu tu una ufahamu wa ukweli wa juu juu haina maana ya kwamba kweli unaelewa ukweli au kuutambua; maana halisi ya ukweli inatokana na kuwa na uzoefu wake. Kwa hivyo, wakati tu unaupitia ukweli ndio unaweza kuuelewa, na wakati tu unapitia ukweli ndio unaweza kufahamu sehemu ya undani wake. Kuwa na uzoefu wa ukweli kwa kina ni njia pekee ya kufahamu kidokezo cha ukweli, na kuelewa kiini chake.

Umetoholewa kutoka katika “Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kama maarifa ambayo unayazungumzia yanapatana na ukweli kwa kiasi kikubwa yanategemea na iwapo una uzoefu wa vitendo. Pale palipo na ukweli katika uzoefu wako, maarifa yako yatakuwa yanatekelezeka na yenye thamani. Kupitia uzoefu wako, pia unaweza kupata utambuzi na umaizi, kukuza maarifa yako, na kuongeza hekima yako na akili ya kuzaliwa katika kujiongoza. Maarifa yanayozungumzwa na watu ambao hawana ukweli ni fundisho la kidini tu, bila kujali yana nguvu kiasi gani. Mtu wa aina hii anaweza kuwa mwenye akili sana yanapokuja masuala ya kimwili lakini hawezi kutofautisha yanapokuja masuala ya kiroho. Hii ni kwa sababu watu kama hao hawana uzoefu wowote katika masuala ya kiroho. Hawa ni watu ambao hawajapata nuru katika masuala ya kiroho na kwa hivyo hawaielewi roho. Bila kujali unazungumzia kipengele gani cha maarifa, ilimradi ni asili yako, basi ni uzoefu wako binafsi, maarifa yako halisi. Kile ambacho watu wenye mafundisho tu huzungumzia, yaani, wale ambao hawana ukweli au uhalisi, huzungumzia yaweza kusemwa kuwa ni asili yao, kwa sababu mafundisho yao yamefikiwa kwa njia ya kutafakari sana na ni matokeo ya akili yao kutafakari kwa kina, lakini ni mafundisho tu, si kitu chochote zaidi ya fikira.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Chochote ambacho hakijatoka kwa uzoefu wako mwenyewe, iwe umejifunza kutoka kwa vitabu au kutoka kwa uzoefu wa watu wengine, kinakuwa mafundisho kwako. Unapokipitia, na unafikia matokeo kutoka kwa uzoefu wako, basi utapata ufahamu wa kweli, na maneno unayoyasema unapotoa ushirika yatakuwa halisi; ni hapo tu ndipo kinakuwa uhalisi wa kweli. Angalia jinsi wasioamini wanavyotafiti nadharia fulani: Wanatafiti kutoka kwa kile kilichoandikwa tu, wanatafiti mafundisho na kuyapima na kisha kufikia mahitimisho yao. Hasa wanateolojia na wachungaji, na vile vile wasomi na watafiti wa teolojia, baada ya kusoma fungu la maneno ya Mungu, hawatafuti ukweli au kutafuta ufahamu wa kweli wa Mungu kutoka kwa uzoefu wa utendaji. Badala yake, wanachunguza na kupima nadharia mbalimbali na hatimaye kufikia mahitimisho fulani. Kwa hiyo, mahitimisho ambayo wanafikia ni halisi au ya mafundisho ya dini? Yote ni mafundisho? Hii ni kwa sababu walifikia mahitimisho haya kwa msingi wa utafiti wa maandishi maalum na majadiliano, na sio kwa msingi wa uzoefu wao wenyewe. Mahitimisho yaliyofikiwa kutoka kwa utafiti wa maandishi halisi na kutoka kwa kutafiti vitu vilivyorekodiwa katika Biblia, yameunda nadharia ya aina moja, inayoitwa nadharia ya teolojia. Hakuna ufahamu kutoka kwa uzoefu katika hili, na hakuna nuru ya Roho Mtakatifu. Ufahamu wa kina kutoka kwa nuru ya Roho Mtakatifu unazidi ule unaotoka kwa maana ya juu juu ya maneno; hauwezi kuelezwa kwa lugha yoyote ya juu juu. Roho Mtakatifu atakupa nuru na mwangaza wakati tu utakapotafuta ukweli baada ya kuingia katika uzoefu. Vitu ambavyo Roho Mtakatifu huvipa nuru na kuviangaza kwa ajili yako ni vitu ambavyo ni halisi zaidi na vitu ambavyo ni vya ukweli zaidi kwako, na hivi ndivyo vitu ambavyo huwezi kuvipata kutoka katika Biblia bila kujali jinsi unavyoichunguza kwa bidii. Kwa hiyo leo, Mungu anatutaka tupitie neno la Mungu. Kama, katika uzoefu wetu wa neno la Mungu, Roho Mtakatifu anatupa nuru, basi tunaweza kufikia ufahamu wa kweli wa maneno ya Mungu. Ufahamu huu wa kweli hauwezi kufikiwa bila kujali jinsi unavyochunguza maana halisi ya maneno ya Mungu kwa bidii; hili ni jambo ambalo haliwezi kufikiwa na fikira za binadamu, na kitu ambacho huwezi kukiwazia, bila kujali unavyojaribu kwa bidii jinsi gani. Kwa hiyo, ni ukweli unaopokewa kutoka kwa uongozi, nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu pekee ndio ufahamu wa kweli wa Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Maswali na majibu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha I

Tofauti kati ya maneno ya mafundisho na ukweli ni ipi hasa? Ukweli ni vitu halisi vya neno la Mungu; unawakilisha mapenzi ya Mungu. Maneno ya mafundisho ni ya kikundi cha vitu vya juu juu, na yanawakilisha mawazo na fikira za binadamu. Hayalingani na ukweli. Vitu halisi vya ukweli ni vya utendaji sana; ni vyenye maadili na vya kuridhisha hasa. Punde mtu anapoelewa kitu halisi, moyo wake unachangamka na kuachiliwa huru—hakabiliwi tena na shutuma za kanuni. Kwa upande mwingine, maneno ya mafundisho ni matupu na yasiyo ya kweli. Ni kanuni na mambo ya desturi tu, na huwafanya watu hasa wenye kuweza kuzuiwa na kutohisi huru. Aidha, bila kujali ni maneno mangapi ya mafundisho ambayo mtu anajua, hayawezi kuleta mabadiliko katika tabia yake ya maisha. Yana faida ndogo ya msingi kwa watu. Kwa hiyo, maneno ya mafundisho hayawezi kabisa kulingana na ukweli. Ukweli unaweza kuwa uzima wa mtu. Punde mtu anapokubali ukweli utaleta mabadiliko ya tabia ya maisha. Kuelewa kiwango kikubwa cha mafundisho kunaweza tu kumletea mtu majivuno, majigambo, kiburi na kumfanya akose busara. Ni wakati tu ambapo mtu ana ukweli kama uzima wake ndiyo utendaji wake unakuwa halisi. Bila kujali ni maneno mangapi ya mafundisho mtu anaelewa, hatakuwa na uhalisi. Anapokabiliwa na suala bado hatajua cha kutenda. Wale wote ambao wanakamilishwa na Mungu ni watu walio na ukweli, wakati wale wote ambao hawajapitia kukamilishwa na Mungu ni watu wa maneno ya mafundisho. Wale walio na ukweli wanafaa kwa matumizi na Mungu. Kazi yao huzaa matunda, na wanaweza kweli kuwaleta wengine mbele za Mungu. Wale wanaolenga maneno ya mafundisho hawapati matokeo ya kweli kutoka kwa kazi yao. Hawawezi kuwapa watu riziki ya uzoefu na ufahamu wa kweli, sembuse kutumia ukweli kutatua masuala. Hii ndiyo maana hawawezi kuwaleta wengine mbele za Mungu. Mtu ambaye ana ukweli hawahepi watu wanaotafuta ukweli, na anaweza kutatua shida zote za utendaji ambazo watu wako nazo katika imani yao. Wale ambao wanasisitiza maneno ya mafundisho wanaogopa watu kutafuta ukweli kwa sababu hawana vitu vya kweli ndani yao, na mafundisho wanayozungumzia hayawezi kutatua shida za kweli. Kwa hiyo, hawathubutu kuwaagiza wengine waulize maswali, na bila shaka hawawezi hata zaidi kutatua taabu za utendaji. Wale walio na ukweli wanathubutu kukabili uhalisi; wale wanaolenga maneno ya mafundisho hawathubutu kukabili uhalisi, badala yake, wanauepuka. Hizo ndizo kanuni za kutambua kati ya ukweli na maneno ya mafundisho.

Umetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Iliyotangulia:Ni nini maana ya “acha kila kitu nyuma na kumfuata Mungu”?

Inayofuata:Kujihusisha katika sherehe ya kidini ni nini?

Maudhui Yanayohusiana

 • Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kuwili kwa Mungu hukamilisha umuhimu wa kupata mwili?

  Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu.

 • Kuna tofauti zipi muhimu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu?

  Kazi ya Mungu Mwenyewe inahusisha kazi ya wanadamu wote, na pia inawakilisha kazi ya enzi nzima. Hii ni kusema kwamba, kazi ya Mungu mwenyewe inawakilisha harakati na mwelekeo wa kazi yote ya Roho Mtakatifu, ilhali kazi ya mitume inafuata kazi ya Mungu na wala haiongozi enzi, na wala haiwakilishi mwelekeo wa kufanya kazi wa Roho Mtakatifu katika enzi nzima. Huwa wanafanya tu kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya, ambayo haihusishi kabisa kazi ya usimamizi. Kazi ya Mungu ni mradi ndani ya kazi ya usimamizi. Kazi ya mwanadamu ni wajibu tu wa wanadamu kuweza kutumika na wala haina uhusiano na kazi ya usimamizi. Kwa sababu ya utambulisho na uwakilishaji tofauti wa kazi hii, licha ya ukweli kwamba zote ni kazi za Roho Mtakatifu, kuna tofauti za wazi na bainifu kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu. Aidha, kiwango cha kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa watu wenye tambulisho tofauti inatofautiana. Hizi ni kanuni na mawanda ya kazi ya Roho Mtakatifu.

 • Matokeo ya mtu anayemwamini Mungu katika dini na ambaye hupitia mchafuko na udhibiti wa Mafarisayo na wapinga Kristo ni yapi? Mtu anaweza kuokolewa na Mungu kama anamwamini Mungu kwa njia hii?

  Kazi katika akili ya mwanadamu inafikiwa kwa urahisi sana na mwanadamu. Wachungaji na viongozi katika ulimwengu wa kidini, kwa mfano, wanategemea karama zao na nafasi zao katika kufanya kazi zao. Watu wanaowafuata kwa muda mrefu wataambukizwa na karama zao na kuvutwa na vile walivyo. Wanalenga karama za watu, uwezo na maarifa ya watu, na wanamakinikia mambo ya kimiujiza na mafundisho mengi yasiyokuwa na uhalisi (kimsingi, haya mafundisho ya kina hayawezi kutekelezeka). Hawalengi mabadiliko ya tabia za watu, badala yake wanalenga kuwafundisha watu uwezo wao wa kuhubiri na kufanya kazi, kuboresha maarifa ya watu na mafundisho makuu ya kidini. Hawalengi kuona ni kwa kiasi gani tabia ya watu imebadilika au ni kwa kiasi gani watu wanauelewa ukweli. Wala hawajali kuhusu viini vya watu, wala kujua hali za watu za kawaida na zisizo za kawaida. Hawapingi mitazamo ya watu au kufunua fikira zao, sembuse kurekebisha hali yao ya dhambi. Watu wengi wanaowafuata wanahudumia kwa karama zao za asili, na kile wanachokionyesha ni maarifa na ukweli wa kidini usioeleweka, ambao hauambatani na uhalisi na hauwezi kabisa kuwapa watu uzima.

 • Mtu anawezaje kujua asili na tabia ya Mungu?

  Mungu ndicho kile Alicho na Anacho kile anacho. Kila kitu Anachokidhihirisha na kukifichua ni viwakilishi vya dutu Yake na utambulisho Wake. Kila alicho na anacho, pamoja na dutu na utambulisho Wake vyote ni vitu ambavyo haviwezi kubadilishwa na binadamu yeyote.