Wimbo wa Kikristo | Siku ya Adhabu ya Mwanadamu Inakaribia

02/05/2020

Watu wengi huhisi kusumbuka na kuona haya

kwa sababu wametenda makosa mabaya,

na wengi wanajionea aibu

kwa sababu hawajawahi kutenda tendo lolote zuri.

Tena wapo pia wengi ambao,

mbali na kutahayari kwa ajili ya dhambi zao, wanakuwa wabaya zaidi,

wakiitoa kabisa barakoa inayoficha sura zao mbaya—

ambayo haikuwa bado imewekwa wazi kikamilifu—

ili kujaribu tabia ya Mungu.

Mungu hajali, wala hatilii maanani matendo ya mtu yeyote mmoja.

Badala yake, Mungu hufanya kazi Anayopaswa kufanya,

iwe kukusanya habari,

ama kuzunguka katika nchi au kufanya jambo ambalo linampendeza Mungu.

Katika nyakati muhimu, Mungu huendelea na kazi Yake

miongoni mwa wanadamu kama ilivyopangwa awali,

bila kuchelewa au kuwa mapema hata kidogo,

na kwa urahisi na kwa makini.

Hata hivyo, katika kila hatua ya kazi ya Mungu, wengine wanawekwa pembeni,

kwa sababu Mungu hudharau hali yao ya kujipendekeza

na hali yao ya kujifanya wanyenyekevu.

Wale wanaomchukiza Mungu sana hakika watatelekezwa,

iwe ni kwa kupenda au kwa kutopenda.

Kwa ufupi, Mungu angependa wale wote Anaowadharau

wawe mbali sana na Yeye.

Ni dhahiri kwamba, Mungu hatawahurumia

Waovu wanaobaki katika nyumba ya Mungu.

Kwa kuwa siku ya adhabu ya mwanadamu inakaribia,

Mungu haharakishi kuzitupa nje

zile nafsi zote zinazostahili dharau kutoka kwa nyumba ya Mungu.

kwa kuwa Mungu ana mpango Wake Mwenyewe.

kutoka katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Tazama zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Shiriki

Ghairi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp