Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Filamu za Kikristo | "Vita" | God Saved Me From the Hands of False Shepherds (Swahili Subtitles)

Maisha ya Kanisa   135  

Utambulisho

Filamu za Kikristo | "Vita" | God Saved Me From the Hands of False Shepherds (Swahili Subtitles)


Zhang Hui alikuwa mzee katika kanisa la nyumbani la Kichina. Kila wakati alikuwa mtafutaji mwenye bidii, na alikuwa anangojea kuja kwa Bwana. Katika miaka ya hivi majuzi, alishuhudia kanisa likikumbwa na huzuni pole pole. Roho yake mwenyewe ilififia pia na hakuwa na chochote cha kuhubiri. Zaidi ya hayo, bibi yake alifariki kwa ghafla, jambo lililomuathiri sana. Alikutana na mashahidi wawili kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwa sadfa tu. Kupitia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, roho yake yenye kiu ilipokea unyunyiziaji na chakula na aliweza kufurahia utamu wa kazi ya Roho Mtakatifu. Alihitimisha kuwa Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu na akakubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Lakini wachungaji na watumishi wenzake kutoka kwa kanisa lake wanapogundua kuwa anaamini Mwenyezi Mungu, wanafanya kila kitu wawezacho kumzuia na kumvuruga. Juhudi zao za kutumia cheo na pesa ili kumjaribu Zhang Hui zinapokosa kufua dafu, wanaamua kutumia harusi ya mwanawe ili kumshurutisha kuacha njia ya kweli. Vita vya kiroho vinaanza kimya kimya … Je, Zhang Hui ataweza kumtegemea Mungu amwezeshe kubaini hila za watumishi wenzake? Je, ataweza kuepuka mitego yao na vikwazo na kurudi kusimama mbele ya kiti cha enzi cha Mungu?


Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.


Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Wahusika wanaoonekana katika uzalishaji huu wanafanya kwa msingi wa kutotafuta faida, na hawajalipwa kwa njia yoyote. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.