Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote"

Video za Nyimbo za Dini   346  

Utambulisho

Wimbo wa Maneno ya Mungu | "Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote"


I

Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia,

unaanza kutenda wajibu wako.

Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako,

na unaanza safari ya maisha.

Vyovyote vilivyo msingi wako ama safari iliyo mbele yako,

hakuna anayeweza kuepuka utaratibu na mpango ambao Mbingu imeweka,

na hakuna aliye na amri juu ya hatima yake,

kwani ni Yule tu anayetawala juu ya vitu vyote ndiye ana uwezo wa kazi kama hii.


II

Tangu siku ambayo mwanadamu alikuja kuwepo

Mungu amekuwa imara katika kazi Yake,

Akisimamia ulimwengu huu na kuelekeza mabadiliko na kusonga kwa vitu vyote.

Kama vitu vyote, mwanadamu kwa kimya na bila kujua anapokea

uboreshaji wa utamu, mvua na umande kutoka kwa Mungu.

Kama vitu vyote, mwanadamu bila kujua anaishi chini ya utaratibu wa mkono wa Mungu.


III

Moyo na roho ya mwanadamu viko mkononi mwa Mungu,

na maisha yote ya mwanadamu yanatazamwa machoni mwa Mungu.

Bila kujali kama unaamini katika hili ua la,

chochote na vitu vyote, viishivyo au vilivyokufa,

vitageuka, vibadilike, vifanywe upya, na kupotea kulingana na fikira za Mungu.

Hivi ndivyo Mungu hutawala juu ya vitu vyote.


kutoka kwa Neno Laonekana katika MwiliBaadhi ya vifaa ni kutoka: https://stockfootage.com