Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

Video za Nyimbo za Dini   208  

Utambulisho

Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu

I

Mandhari iliyochorwa katika Biblia "Amri ya Mungu kwa Adamu" ni ya kugusa na yenye kutia moyo. Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,

uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao, mshangao na uvutiwaji.

II

Upendo wa Mungu unaofurika umepewa mwanadamu bure, upendo wa Mungu umemzunguka. Mwanadamu, maasumu na safi, bila ya wajibu wa kumnyima uhuru, huishi kwa furaha kamili machoni mwa Mungu. Mungu humtunza mtu, na mtu huishi chini ya mabawa Yake.

Yote ambayo mtu hufanya, maneno yake yote na matendo,

yamefungwa pamoja na Mungu, hayawezi kujitenga.

III

Kutoka wakati wa kwanza Mungu alipowaumba wanadamu, Mungu aliwaweka chini ya uangalizi Wake. Ni uangalizi wa aina gani huo? Ni jukumu Lake kumlinda mtu na kumchunga mtu. Anamtumainia mtu kuamini katika, kuamini katika na kuyatii maneno Yake. Hiki ndicho kitu cha kwanza ambacho Mungu alikitarajia kwa wanadamu.

IV

Akiwa na tumaini hili la kwanza, Mungu aliyasema maneno yafuatayo:

"Matunda ya kila mti wa bustani mwaweza kuyala: Lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, mema na mabaya, msiyale: kwa maana siku mtakapoyala matunda ya mti huo hakika mtakufa."

Maneno haya rahisi, yakisimamia mapenzi ya Mungu, yaonyesha kuwa kumjali mtu kulikuwa tayari katika moyo Wake.

V

Hivyo, kwa maneno haya rahisi, tunaona kilicho moyoni mwa Mungu.

Je, kuna upendo katika moyo Wake? Si kuna utunzaji na dhima?

Upendo na utunzaji wa Mungu ni jambo ambalo linaweza kuonekana na kuhisiwa. Kama wewe ni mtu wa dhamiri na una ubinadamu,

utajihisi vuguvugu, ukitunzwa na kupendwa, utajihisi mwenye heri na furaha.

VI

Unapoyahisi mambo haya, utatenda vipi mintarafu ya Mungu?

Utakuwa mwaminifu Kwake? Upendo wa staha, upendo wa staha hutakua katika moyo wako? Moyo wako utasogea karibu na Yeye? Kutokana na haya tunaona, jinsi upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa mtu. Lakini hata muhimu zaidi kuliko hili ni kwamba mtu anaweza kuuhisi na kuuelewa upendo wa Mungu.

kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana Katika Mwili

Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

Kauli Maalum: Uzalishaji huu wa video ulitengenezwa kama mradi usio wa faida na Kanisa la Mwenyezi Mungu. Video hii isisambazwe kwa mtu mwingine kwa minajili ya faida, na ni matumaini yetu kwamba kila mtu atashiriki kuigawa na kuisambaza hadharani. Wakati unapoisambaza, tafadhali sisitiza chanzo chake. Bila ridhaa ya Kanisa la Mwenyezi Mungu, hakuna shirika, kundi la kijamii, au mtu binafsi anayeweza kubadilisha au kuhudhurisha visivyo maudhui ya video hii.