Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda kwa Kristo wa Siku za Mwisho

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

1. Hukumu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Ikifika kwa neno “hukumu,” utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Baada ya kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, tunaweza kuona ukweli kwamba chanzo cha ukweli ni Mungu, na chanzo cha vitu vyote chanya ni Mungu. Palipo na vurugu na upotovu wa Shetani na dhambi ya kumpinga Mungu, hapo hukumu na kuadibu kwa Mungu kwa hakika hufuata. Popote ambapo hukumu ya Mungu ipo, pana kuonekana kwa ukweli na ufunuo wa tabia ya Mungu. Ukweli na tabia ya Mungu hufichuliwa wakati wa hukumu na kuadibu kwa Mungu. Palipo na ukweli pekee ndipo pana hukumu na kuadibu; palipo na hukumu na kuadibu pekee ndipo pana ufunuo wa tabia ya Mungu ya haki. Kwa hivyo, popote ambapo hukumu na kuadibu kwa Mungu kupo hapo tunapata nyayo za kazi ya Mungu, na ndiyo njia ya kweli zaidi ya kutafuta kuonekana kwa Mungu. Mungu pekee ndiye ana mamlaka ya kutoa hukumu, na Kristo pekee ndiye ana uwezo wa kuhukumu wanadamu waliopotoka. Hii inathibitisha na kuonyesha kwamba Mwana wa Adamu—Kristo—ndiye Bwana wa hukumu. Bila ya hukumu na kuadibu kwa Mungu watu hawana njia ya kupata ukweli, na hukumu na kuadibu ni kule kunakoonyesha tabia ya Mungu ya haki, kwa kuwapa wanadamu fursa ya kumjua Mungu. Mchakato ambao kwao wanadamu wanauelewa ukweli ni mchakato ambao kwao wanamjua Mungu. Ukweli kwa wanadamu waliopotoka ni hukumu, uchunguzi, na kuadibu. Kinachofichuliwa na ukweli hasa ni haki ya Mungu, uadhama, na ghadhabu. Watu ambao wanauelewa ukweli wanaweza kujikomboa kutokana na upotovu na kujinasua kutokana na ushawishi wa Shetani. Hii inatokana kabisa na nguvu na uweza wa maneno ya Mungu. Mungu anawaokoa watu na kuwakamilisha watu ili kuwaruhusu watu waelewe ukweli na kupata ukweli. Kadiri watu wanapozidi kuelewa ukweli, ndipo wanapozidi kumjua Mungu. Kwa njia hii, watu wanaweza kuachana na upotovu na kufikia utakaso. Watu wanapoishi kwa kudhihirisha ukweli na kuingia katika uhalisi wa ukweli, watakuwa wanaishi katika nuru, wanaishi katika upendo, na wanaishi mbele ya Mungu. Haya ndiyo matokeo ambayo Kristo hutimiza kwa kuwasilisha ukweli na kutoa hukumu. Kwa kweli, maneno yote yanayosemwa na Mungu ni ukweli na ndiyo hukumu kwa jamii ya wanadamu. Haijalishi ni enzi gani, maneno ambayo Mungu ananena yana athari ya hukumu. Katika Enzi ya Sheria, maneno ya Yehova Mungu yalikuwa ndiyo hukumu ya wanadamu waliopotoka. Katika Enzi ya Neema, maneno yaliyonenwa na Bwana Yesu ndiyo yaliyokuwa hukumu ya wanadamu waliopotoka. Sasa katika Enzi ya Ufalme, yote ambayo Mwenyezi Mungu anasema katika kazi Yake ya kuhukumu na kuadibu ni hukumu hata zaidi, ambayo hatimaye yatafanya jamii ya wanadamu iweze kuona kwamba hukumu na kuadibu kwa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu ni upendo mkubwa wa Mungu. Kile ambacho hukumu na kuadibu kwa Mungu hutoa kwa jamii ya wanadamu ni wokovu na ukamilifu. Ni kwa kukubali na kutii hukumu na kuadibu kwa Mungu pekee ndipo mtu hupata upendo wa kweli wa Mungu na wokovu kamili. Wale watu wote ambao wanakataa kukubali hukumu na kuadibu kwa Mungu watapata adhabu ya Mungu na watazama katika uharibifu na kuangamia kabisa….

Umetoholewa kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu

Iliyotangulia:Swali la 41: Tumeona mazungumzo mengi kwa mtandao na serikali ya Kikomunisti ya Kichina na ulimwengu wa kidini wakilisingizia, kulikashifu, kulishambulia na kulitahayarisha Kanisa la Mwenyezi Mungu (kama vile “tukio la 5.28” huko Zhaoyuan, jimbo la Shandong). Tunajua pia kuwa CCP ni bora mno kwa kudanganya na kunena uongo na kupinda ukweli ili kuwahadaa watu, na vilevile kuwa bora sana katika kuyakashifu, kuyashambulia na kuyahukumu yale mataifa ambayo ina chuki kwayo, hivyo neno lolote ambalo CCP husema ni lazima lisiaminiwe kabisa. Lakini mambo mengi yanayosemwa na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa ni sawa na yale ambayo CCP huyasema, hivyo ni jinsi gani tunafaa kutambua maneno ya kashfa, ya kutahayarisha yanayotoka kwa CCP na ulimwengu wa kidini?

Inayofuata:Kwa nini inamlazimu Mungu kuwahukumu na kuwaadibu watu?

Maudhui Yanayohusiana

 • Mungu amekuwa mwili nchini China katika siku za mwisho; ni msingi gani upo kwa jambo hili katika unabii wa Biblia na katika maneno ya Mungu?

  Katika maeneo mengi, Mungu Alitabiri kupata kundi la washindi katika nchi ya Sinim. Ni upande wa Mashariki mwa ulimwengu ambapo washindi wanapatikana, hivyo nchi ambapo Mungu kupata mwili mara ya pili Atatua bila shaka ni nchi ya Sinim, mahali ambapo joka jekundu linaishi. Hapo Mungu Atawapata warithi wa joka kuu jekundu na litashindwa na kuaibishwa.

 • Madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

  Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu.

 • Ni nini tofauti muhimu kati ya kuokolewa na wokovu?

  Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.

 • Bwana Yesu Mwenyewe alitabiri ya kwamba Mungu angepata mwili katika siku za mwisho na kuonekana kama Mwana wa Adamu ili kufanya kazi

  Yesu alisema kwamba Angewasili kama Alivyoondoka, lakini unajua maana halisi ya maneno Yake? Je, angeweza kwa kweli kukwambia? Unajua tu kwamba Atawasili kama Alivyoondoka juu ya wingu, lakini unajua hasa jinsi Mungu Mwenyewe hufanya kazi Yake? Ikiwa ungeweza kuona kweli, basi maneno ya Yesu yanapaswa kuelezwa vipi?