Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Ushuhuda kwa Kristo wa Siku za Mwisho

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

29. Kupagawa ni nini? Kupagawa hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:

Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. … Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili.

Umetoholewa kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, “Mimi ni Mungu!” Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. … Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!

Umetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:

Watu waliopagawa na mashetani ni wale ambao wameingiliwa na kudhibitiwa na pepo wabaya. Onyesho kuu ni kuwa na maradhi ya saikolojia, au kutokuwa na akili timamu nyakati nyingine, kupoteza kabisa mantiki ya kawaida. Wanamwamini Mungu lakini hawawezi kukubali ukweli na wanaweza tu kuvuruga. Hii ndiyo maana, ingawa wanamwamini Mungu, hawawezi kuokolewa na lazima waondolewe. Wengi wa watu ambao wamepagawa na pepo wabaya ni vikaragosi wa Shetani na huvuruga kazi ya Mungu. Kuna maonyesho kumi makuu kama yafuatayo:

1. Wale wote wanaojifanya kuwa Mungu au Kristo wamepagawa na pepo wabaya.

2. Wale wote wanaojifanya kuwa na roho za malaika wamepagawa na pepo wabaya.

3. Wale wote wanaojifanya kuwa Mungu mwingine mwenye mwili wamepagawa na pepo wabaya.

4. Wale wote wanaosema kwamba maneno ya Mungu ni yao wenyewe au ambao wanawafanya wengine wachukulie maneno yao kama maneno ya Mungu wamepagawa na pepo wabaya.

5. Wale wote wanaojifanya kutumiwa na Roho Mtakatifu ili kuwafanya wengine wawafuate na kuwatii wamepagawa na pepo wabaya.

6. Wale wote wanaozungumza kwa ndimi mara nyingi, wanaofafanua ndimi na wanaweza kuona kila aina za maono ya miujiza, au ambao mara nyingi wanaonyesha dhambi za wengine wamepagawa na pepo wabaya.

7. Wale wote ambao mara nyingi husikia sauti za mwujiza za pepo au milio ya pepo au ambao mara nyingi huona mazimwi, na wale wote ambao kwa dhahiri ni wenye akili punguani wamepagawa na pepo wabaya.

8. Wale wote ambao wamepoteza fikira ya kawaida ya binadamu, wanaozungumza kwa maneno yenye kichaa mara kwa mara, wanaojizungumzia mara nyingi, wanaozungumza upuuzi au wanaosema mara nyingi kwamba Mungu amewaagiza na kwamba Roho Mtakatifu amewagusa pia wamepagawa na pepo wabaya.

9. Wale wote ambao wana matukio ya tabia isiyo ya kawaida, wanaotenda kipuuzi, ambao wakati mwingine ni wajinga, na hawawezi kuzungumza na wengine kwa kawaida ni watu ambao wamepagawa na pepo wabaya. Wale wote ambao wanaainishwa kama wasenge ni aina ya watu ambao wamepagawa na mashetani na ni miongoni mwa wale ambao wataondolewa.

10. Watu wengine kwa desturi ni wa kawaida kabisa lakini, kwa kipindi cha miezi kadhaa au mwaka mmoja au miaka miwili, huenda wakachokozwa na kukuza ugonjwa wa akili. Wakati wa ugonjwa huo wako sawa tu na wale ambao wamepagawa na roho wabaya. Ingawa watu hawa ni wa kawaida wakati mwingine, pia wanaainishwa kama waliopagawa na mashetani. (Ikiwa mtu ana ugonjwa wa akili miaka mingi kabla lakini amekuwa sawa kwa miaka mingi baadaye, anaweza kuelewa na kukubali ukweli kama imani yake, na kupitia mabadiliko kiasi, hawezi kuainishwa kama aliyepagawa na pepo wabaya.)

Mtu ambaye amepagawa na mashetani amemilikiwa na kudhibitiwa kikamilifu na Shetani, ni wa Shetani, na amelaaniwa.

Umetoholewa kutoka katika “Ili Kufanya Kazi ya Kanisa Vizuri Mtu Lazima Aweze Kutambua Kati ya Aina Kadha za Watu” katika Mipango ya Kazi

Kuna aina mbili tu za hali ambapo roho waovu humdanganya mwanadamu: Moja ni kazi isiyo ya kawaida ya roho waovu, na nyingine ni roho waovu waliopata mwili tena kama binadamu. Wale wanaopinga Mungu na ukweli kama vile pepo ambaye ni joka kuu jekundu pia ni roho waovu; wao ni wenye kudhuru kwa siri zaidi, wenye nia mbaya zaidi. Baadhi ya roho waovu hutawala miili ya watu wakati fulani katika maisha yao; roho wengine waovu ni kupata mwili tena kwa pepo. Ingawa kwa nje hakuna kazi isiyo ya kawaida ya roho waovu na huwezi kuona dalili yoyote ya umiliki na pepo, wao hupinga ukweli kwa mhemko; wao humkataa na kumpinga Mungu kwa hasira. Pepo waliopata mwili tena si wa mwujiza, bali ni wa kawaida. Hata hivyo, ni dhahiri shahiri kuwa wao ni adui wa ukweli. Joka kubwa jekundu ni la kundi la pepo waliopata mwili tena, na wanasiasa wote na wakuu wa nchi wanaompinga Mungu pia ni pepo waliozaliwa tena. Kusema kwamba wale tu ambao wana kazi ya roho waovu wamepagawa na pepo na wao wenyewe ni pepo waovu hakukubaliani na uhalisi. Baadhi ya roho waovu hujificha ndani zaidi na huwezi kuwatambua; wao ni wa kundi la pepo waliopata mwili tena.

Umetoholewa kutoka katika “Maswali na majibu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha VIII

Iliyotangulia:Kuna tofauti zipi kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya pepo wabaya?

Inayofuata:Kwa nini Mungu hawaokoi wale wanaofanyiwa kazi na pepo wabaya na wale waliopagawa?

Maudhui Yanayohusiana

 • Kristo wa uongo ni nini? Kristo wa uongo anaweza kutambuliwaje?

  Maneno Husika ya Mungu: Yeye Aliye mwili wa Mungu Atakuwa na dutu ya Mungu, na Yule Aliye Mungu katika mwili Atakuwa na maonyesho ya Mungu. Kwa maana …

 • Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Kazi ya Roho Mtakatifu hudhihirishwaje?

  Maneno Husika ya Mungu: Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea…

 • Dunia ya kidini inaamini kwamba maandiko yote yametolewa na msukumo wa Mungu na yote ni maneno ya Mungu; mtu anafaaje kuwa na utambuzi mintarafu ya kauli hii?

  Si kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa binadamu, na ufasiri wa ajabu wa binadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni tafsiri sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahihi kabisa wa ukweli. Maoni yao juu ya vitu fulani si chochote zaidi ya maarifa uzoefu binafsi, au kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Utabiri wa manabii ulikuwa umetolewa na Mungu mwenyewe: Unabii wa Isaya, Danieli, Ezra, Yeremia, na Ezekieli, ulitoka moja kwa moja kwa Roho Mtakatifu, watu hawa walikuwa ni waonaji maono, walipokea Roho ya Unabii, wote walikuwa ni manabii wa Agano la Kale. Wakati wa Enzi ya Sheria watu hawa, ambao walikuwa wamepokea ufunuo wa Yehova, walizungumza unabii mwingi, ambao ulisemwa na Yehova moja kwa moja.

 • Kwa nini inasemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote wanaitembea njia ya Mafarisayo? Ni nini asili yao?

  Tazama tu viongozi wa kila madhehebu—wote ni wa kujigamba na kujidai, na wanafafanua Biblia nje ya muktadha na kulingana na ubunifu wao wenyewe. Wote wanategemea zawadi na maarifa kufanya kazi yao. Kama hawangekuwa na uwezo wa kuhubiri chochote, wale watu wangewafuata? Wao, hata hivyo, wanamiliki ufahamu fulani, na wanaweza kuhubiri kuhusu mafundisho fulani, au wanajua jinsi ya kuwashawishi wengine na jinsi ya kutumia ustadi kadhaa. Wanatumia haya kuwaleta watu mbele yao wenyewe na kuwadanganya. Kwa jina, watu hao humwamini Mungu, lakini katika uhalisi wanafuata viongozi wao. Wakikutana na mtu akihubiri njia ya kweli, baadhi yao husema, “Lazima tutafute ushauri kwa kiongozi wetu imani.” Imani yao lazima impitie mwanadamu; hilo si tatizo? Viongozi hao wamekuwa nini, basi? Hawajakuwa Mafarisayo, wachungaji waongo, wapinga Kristo, na vikwazo kwa kukubali kwa watu njia ya kweli?