Programu ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Sikiliza sauti ya Mungu na ukaribishe kurudi kwa Bwana Yesu!

Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

91 Makazi Yangu Yako Wapi

1

Kwa karatasi yangu ndogo na brashi, nachora nyumba ndogo.

Mama yuko ndani ya nyumba, Baba yuko ndani pia.

Mimi na dadangu tunacheza juani.

Sote tunahisi joto jua linapotuangazia.

Mama anatabasamu, Baba anatabasamu pia.

Dada wanatabasamu, sote tunafurahia.

Hii ni familia yangu hapa, iliyochorwa kwenye karatasi yangu.

Picha katika ndoto zangu. Yote imo katika ndoto zangu.

2

Nikichukua mkoba wangu mdogo, naenda mahali pageni.

Baba yuko ndani lakini Mama yuko nje.

Nachukua sanduku langu dogo,

nakwenda nyumbani nilikokujua wakati mmoja.

Mama yuko ndani, Baba yuko nje.

Nikiwa nimeshikilia kidete mkoba wangu, nazurura barabarani.

Nikihisi mpweke, nisiwe na hakika pa kwenda.

Sanduku langu ndogo hapa ni mwenzangu wa pekee.

Haya ndiyo makazi yangu pekee, makazi nisiyoweza kuepa.

3

Makazi yangu yako wapi? Eh yanaweza kuwa wapi?

Katika ulimwengu mkubwa sana, bado hakuna mahali pangu.

Nani anayeweza kunipeleka kwenye makazi katika ndoto zangu,

iliyomo katika mchoro wangu, iliyomo katika ndoto zangu?

Makazi yangu yako wapi? Eh yanaweza kuwa wapi?

Katika dunia kubwa sana, bado hakuna makazi pangu.

Nani anayeweza kunipa makazi mazuri,

makazi yaliyomo katika michoro yangu,

Makazi yaliyomo katika ndoto zangu,

makazi yaliyomo katika ndoto zangu?

4

Hapa, nina makazi. Nina makazi.

Lakini siyo niliyochora kwenye karatasi yangu.

Sio sanduku langu ndogo, ni mahali ninapoota kuhusu.

Mama na baba wako ndani, pia mimi na dada yangu.

Ni makazi ambamo roho zetu zinaweza kupumzika hatimaye,

makazi yaliyojaa uzuri, yaliyojaa uzuri na matumaini.

Ni makazi (ni makazi)

ambamo roho zetu zinaweza kupumzika hatimaye

(roho zinaweza kupumzika hatimaye),

makazi yaliyojaa uzuri, yaliyojaa uzuri na matumaini.

Da da la da la da. Da la da la da la.

Da la da la da la da. Da la da la da la.

Da la da la da. Da la da la da la.

Da la da la da la da. Da la da la da la.

Da la da la da. Da la da la da la.

Da la da la da la da. Da la da la da la.

Ni makazi yaliyojaa uzuri, makazi yaliyojaa uzuri, uzuri na matumaini.

Iliyotangulia:Upendo wa Mungu Unauzingira Moyo Wangu

Inayofuata:Nina Furaha Kuu Kupata Upendo wa Mungu

Maudhui Yanayohusiana