Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia”

1. Tangu watu waanze kuikanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho. Sio tu kwamba hamna uhakika kuhusu kile ambacho mnapaswa kuingia kwacho; bali pia ni wajinga kuhusu kazi ya Mungu. Hili ni zaidi ya suala la hasara kwenu. Ni dosari kubwa iliyopo kwa wale walio katika ulimwengu wa dini. Hii ndiyo sababu kuu ya watu kutomjua Mungu, na hivyo dosari hii ni kasoro ya kawaida miongoni mwa wale wote wanaomtafuta. Hakuna mtu hata mmoja aliyewahi kumjua Mungu, au amekwishawahi kuuona uso Wake halisi. Ni kwa sababu hii ndipo kazi ya Mungu inakuwa ngumu kama kazi ya kuhamisha mlima au kukausha bahari. Ni watu wangapi ambao wameyatoa maisha yao kwa ajili ya kazi ya Mungu; ni wangapi wametengwa kwa sababu ya kazi Yake; ni wangapi wameteswa hadi kufa kwa ajili ya kazi Yake; ni wangapi wamelia kwa ajili ya upendo wao kwa Mungu, wamekufa pasipo haki; ni wangapi wamekutana na mateso katili na ya kinyama…? Kwamba majanga haya yatapita—hii sio kwa sababu ya watu kutokuwa na maarifa juu ya Mungu? Inawezekanaje mtu ambaye hamjui Mungu awe na ujasiri wa kusimama mbele Yake? Inawezekanaje mtu anayemwamini Mungu na bado anamtesa awe na ujasiri wa kusimama mbele Yake? Haya si makosa kwa wale walio katika ulimwengu wa kidini pekee, bali ni makosa ya kawaida kwenu na kwao. Watu wanamwamini Mungu bila kumfahamu, ni kwa sababu hii ndio watu hawamheshimu Mungu kwa dhati, na hawamchi Yeye kwa dhati. Hata kuna wale ambao, kwa majivuno makuu na hali, wanafanya kazi ambayo wanafikiria kichwani wenyewe katika mkondo huu, na wanaifanya kazi ya Mungu kulingana na matakwa yao wenyewe na tamaa zao zisizo na kadiri. Watu wengi wanafanya ovyoovyo, hawamtukuzi Mungu bali wanafuata mapenzi yao wenyewe. Je, hii si mifano mizuri ya mioyo ya watu iliyo na ubinafsi? Je, haya hayaonyeshi dalili nyingi zaidi za udanganyifu walionao watu?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

2. Katika kumfinyanga mwanadamu[1] na kuigeuza tabia yake, kazi ya Mungu kamwe haikomi, kwa kuwa wanakosa katika njia nyingi sana na wao wamepungukiwa na viwango vilivyowekwa na Yeye. Na kwa hiyo inaweza kusemwa kwamba, machoni pa Mungu, milele mtakuwa watoto waliozaliwa karibuni, wenye sifa muhimu chache sana zinazompendeza Yeye, kwa sababu ninyi ni viumbe tu mikononi mwa Mungu. Kama mtu angeingia katika ridhaa, hangechukiwa sana na Mungu? Kusema kwamba mnaweza kumridhisha Mungu leo ni kuzungumza kutoka kwa mtazamo mdogo wa miili yenu; ikiwa kweli mngelinganishwa dhidi ya Mungu, ninyi daima mngeshindwa uwanjani. Mwili wa mwanadamu haujawahi kupata ushindi. Ni kupitia tu kazi ya Roho Mtakatifu ndio inawezekana kwa mwanadamu kuwa na sifa muhimu za kukomboa. Kwa kweli, kati ya vitu vingi katika uumbaji wa Mungu, mwanadamu ni wa kiwango cha chini sana. Ingawa ni mtawala wa vitu vyote, mwanadamu ni kiumbe pekee ambaye yupo chini ya hila za Shetani, ni kiumbe pekee ambaye anashikwa kwa namna nyingi katika uharibifu wake. Mwanadamu hajawahi kuwa na ukuu juu yake mwenyewe. Watu wengi wanaishi katika uovu wa Shetani, na kuumizwa na dhihaka zake; anawaudhi kwa njia hii hata hapo watakapokuwa wamelemewa kabisa, wakistahimili kila badiliko, kila ugumu katika ulimwengu wa kibinadamu. Baada ya kuwachezea, Shetani huimaliza hatima yao. Na hivyo watu wanapita katika maisha yao yote wakiwa na mkanganyiko, wala hawajawahi kufurahia hata siku moja vitu vizuri ambavyo Mungu amewaandalia, badala yake wanajeruhiwa na Shetani na kuachwa wakiwa wameharibika kabisa. Leo wamekuwa wadhoofu na walegevu sana kiasi kwamba hawana mwelekeo wa kuzingatia kazi ya Mungu. Ikiwa watu hawana mwelekeo wa kuzingatia kazi ya Mungu, uzoefu wao utabakia kuwa vipandevipande na kutokamilika milele, na kuingia kwao kutabakia sehemu tupu milele. Katika Miaka elfu kadhaa tangu Mungu alipokuja duniani, idadi yoyote ya watu wenye mawazo ya kiburi wamekuwa wakitumiwa na Mungu kufanya kazi Yake kwa miaka mingi; lakini wale wanaoijua kazi Yake ni wachache sana takribani hawapo kabisa. Kwa sababu hii, idadi kubwa ya watu ambao hawajatajwa wanachukua jukumu la kumpinga Mungu na wakati huo huo wanafanya kazi Yake, kwa sababu, badala ya kufanya kazi Yake, kimsingi wanafanya kazi ya mwanadamu katika nafasi waliyopewa na Mungu. Je, hii inaweza kuitwa kazi? Wanawezaje kuingia? Mwanadamu amechukua neema ya Mungu na kuizika. Kwa sababu hii, kwa karne nyingi zilizopita wale wanaofanya kazi Yake wana kuingia kwa kiwango kidogo. Hawazungumzi juu ya kuijua kazi ya Mungu kwa sababu wana ufahamu kiasi kidogo wa hekima ya Mungu. Inaweza kusemwa kwamba, ingawa kuna watu wengi wanaomtumikia Mungu, wameshindwa kuona jinsi Alivyoinuliwa, na hii ndiyo sababu watu wamejifanya wao ndio Mungu wa kuabudiwa na watu.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

3. Kazi inapozungumziwa, mwanadamu anaamini kwamba kazi ni kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu, akihubiri kila sehemu, na kugharimia rasilmali kwa ajili ya Mungu. Ingawa imani hii ni sahihi, ni ya kuegemea upande mmoja sana; kile ambacho Mungu anamwomba mwanadamu si kusafiri kwenda huku na huko kwa ajili ya Mungu; ni huduma zaidi na kujitoa ndani ya roho. Ndugu wengi hawajawahi kufikiria juu ya kumfanyia Mungu kazi hata baada ya miaka mingi sana ya uzoefu, maana kazi kama mwanadamu anavyoielewa haipatani na ile ambayo Mungu anaitaka. Kwa hiyo, mwanadamu havutiwi kwa namna yoyote ile na kazi ya Mungu, na hii ndiyo sababu kuingia kwa mwanadamu ni kwa kuegemea upande mmoja kabisa. Nyinyi nyote mnapaswa kuingia kwa kumfanyia Mungu kazi, ili muweze kupata uzoefu wa vipengele vyake vyote. Hiki ndicho mnapaswa kuingia ndani. Kazi haimaanishi kutembea huku na huko kwa ajili ya Mungu; maana yake ni iwapo maisha ya mwanadamu na kile ambacho mwanadamu anaishi kwa kudhihirisha ni kwa ajili ya Mungu kufurahia. Kazi inamaanisha mwanadamu kutumia uaminifu alio nao kwa Mungu na maarifa aliyo nayo juu ya Mungu ili kumshuhudia Mungu na kumhudumia mwanadamu. Huu ndio wajibu wa mwanadamu, na yote ambayo mwanadamu anapaswa kutambua. Kwa maneno mengine, kuingia kwenu ni kazi yenu; mnatafuta kuingia wakati wa kazi yenu kwa ajili ya Mungu. Kupata uzoefu wa Mungu sio tu kuweza kula na kunywa neno Lake; na muhimu zaidi, mnapaswa kuweza kumshuhudia Mungu, kumtumikia Mungu, na kumhudumia na kumkimu mwanadamu. Hii ni kazi, na pia kuingia kwenu; hiki ndicho kila mwanadamu anapaswa kukitimiza.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

4. Kuna watu wengi ambao wanatilia mkazo tu katika kusafiri huku na huko kwa ajili ya Mungu, na kuhubiri kila sehemu, lakini hawazingatii uzoefu wao binafsi na kupuuza kuingia kwao katika maisha ya kiroho. Hiki ndicho kinasababisha wale wanaomtumikia Mungu kuwa watu wanaompinga Mungu. Kwa miaka mingi sana, wale wanaomtumikia Mungu na kumhudumia mwanadamu wanaona kufanya kazi na kuhubiri kuwa ndio kuingia, na hakuna anayechukulia uzoefu wake binafsi wa kiroho kuwa kuingia muhimu. Badala yake, wanatumia nuru ya kazi ya Roho Mtakatifu kuwafundisha wengine. Wanapohubiri, wanakuwa na mzigo mkubwa sana na wanapokea kazi ya Roho Mtakatifu, na kupitia hili wanatoa sauti ya Roho Mtakatifu. Wakati huo, wale wanaofanya kazi wanahisi kuridhika kana kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wao binafsi wa kiroho; wanahisi kwamba maneno yote wanayoyazungumza wakati huo ni ya yao wenyewe, na pia kana kwamba uzoefu wao si wazi kama walivyoeleza. Kuongezea, wao hawana fununu ya nini cha kusema kabla ya kunena, lakini Roho Mtakatifu anapofanya kazi ndani yao, wao huwa na mtiririko wa maneno usioisha na usiosita. Baada ya kuwa umehubiri kwa namna hiyo, unahisi kwamba kimo chako halisi sio kidogo kama ulivyoamini. Baada ya Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yako kwa namna ile ile mara kadhaa, basi unaamini kwamba tayari una kimo na unaamini kimakosa kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni kuingia kwako na asili yako mwenyewe. Unapopitia uzoefu huu kwa mfululizo, unakuwa mzembe kuhusu kuingia kwako. Halafu unakuwa mvivu bila kujua, na kutozingatia kabisa kuingia kwako mwenyewe. Kwa hiyo, unapowahudumia wengine, unapaswa kutofautisha waziwazi kati ya kimo chako na kazi ya Roho Mtakatifu. Hii itasaidia zaidi kuingia kwako na kunufaisha zaidi uzoefu wako. Mwanadamu akidhani kazi ya Roho Mtakatifu ni uzoefu wake binafsi ndio mwanzo wa upotovu. Hivyo, kazi yoyote mnayoifanya, mnapaswa kuzingatia kuingia kwenu kama somo muhimu.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

5. Mtu anafanya kazi ili kutimiza mapenzi ya Mungu, kuwaleta wale wote wanaoutafuta moyo wa Mungu mbele Yake, kumleta mwanadamu kwa Mungu, na kuitambulisha kazi ya Roho Mtakatifu na uongozi wa Mungu kwa mwanadamu, kwa kufanya hivyo atakuwa anayakamilisha matunda ya kazi ya Mungu. Kwa sababu hii, ni muhimu kuelewa kiini cha kufanya kazi. Kama mtu anayetumiwa na Mungu, watu wote wanafaa kumfanyia kazi Mungu, yaani, wote wana fursa ya kutumiwa na Roho Mtakatifu. Hata hivyo kuna hoja moja mnayopaswa kuielewa: Mwanadamu anapofanya kazi ya Mungu, mwanadamu anakuwa na fursa ya kutumiwa na Mungu, lakini kile kinachosemwa na kujulikana na mwanadamu sio kimo cha mwanadamu kabisa. Mnaweza tu kujua vizuri kasoro zako katika kazi yenu, na kupokea nuru kubwa kutoka kwa Roho Mtakatifu, kwa kufanya hivyo mtakuwa mnaweza kupata kuingia kuzuri katika kazi yenu. Ikiwa mwanadamu anachukulia uongozi wa Mungu kuwa ni kuingia kwake mwenyewe na kile kilichomo ndani ya mwanadamu, hakuna uwezo wa mwanadamu kuongezeka kimo. Roho Mtakatifu humpatia mwanadamu nuru anapokuwa katika hali ya kawaida; katika nyakati kama hizo, mara nyingi mwanadamu anadhani nuru anayopokea ni kimo chake mwenyewe katika uhalisi, maana Roho Mtakatifu huangazia katika njia ya kawaida: kwa kutumia kile ambacho ni cha asili kwa mwanadamu. Mwanadamu anapofanya kazi na kuzungumza, au wakati mwanadamu anapofanya maombi katika shughuli zake za kiroho, ndipo ukweli utawekwa wazi kwao. Hata hivyo, katika uhalisi, kile ambacho mwanadamu anakiona ni nuru tu iliyoangaziwa na Roho Mtakatifu (kwa kawaida, hii inahusiana na ushirikiano kutoka kwa mwanadamu) na sio kimo halisi cha mwanadamu. Baada ya kipindi cha kupitia uzoefu ambao mwanadamu anakabiliana na shida nyingi, kimo cha kweli cha mwanadamu hudhihirika katika mazingira kama hayo. Ni katika muda huo ndipo mwanadamu anagundua kwamba kimo cha mwanadamu sio kikubwa hivyo, na ubinafsi, fikira zake mwenyewe, na tamaa za mwanadamu vyote huibuka. Ni baada tu ya mizunguko kadhaa ya uzoefu kama huo ndipo wengi wa jinsi hiyo ambao wameamshwa ndani ya roho zao watatambua kwamba haukuwa uhalisi wao hapo nyuma, bali ni mwangaza wa muda tu kutoka kwa Roho Mtakatifu, na mwanadamu alipokea nuru tu. Roho Mtakatifu anapompa mwanadamu nuru ili aelewe ukweli, mara nyingi inakuwa katika namna ya wazi na tofauti, bila muktadha. Yaani, Hayajumuishi matatizo ya mwanadamu katika ufunuo huu, na badala yake Anatoa ufunuo moja kwa moja. Mwanadamu anapokabiliana na matatizo katika kuingia, basi mwanadamu anaijumuisha nuru ya Roho Mtakatifu, na huu unakuwa uzoefu halisi wa mwanadamu. … Kwa hiyo, mnapoipokea kazi ya Roho Mtakatifu, mnapaswa kujikita zaidi katika kuingia kwenu, na wakati huo huo, kuona kipi ni kazi ya Roho Mtakatifu na kipi ni kuingia kwenu, vilevile kujumuisha kazi ya Roho Mtakatifu katika kuingia kwenu, ili kwamba muweze kukalishwa Naye vizuri na kuruhusu hulka ya kazi ya Roho Mtakatifu kuletwa pamoja ndani yenu. Wakati mnapitia uzoefu wenu wa kazi ya Roho Mtakatifu, mnamjua Roho Mtakatifu, vilevile nyinyi wenyewe, na katikati ya mateso makali, mnajenga uhusiano wa kawaida pamoja na Mungu, na uhusiano baina yenu na Mungu unakuwa wa karibu siku kwa siku. Baada ya michakato mingi ya kupogolewa na kusafishwa, mnakuza upendo wa kweli kwa Mungu. Hii ndiyo sababu mnapaswa kutambua kwamba mateso, mapigo, na dhiki havitishi; kinachoogopesha ni kuwa na kazi ya Roho Mtakatifu tu lakini sio kuingia kwenu. Siku inapofika kwamba kazi ya Mungu imemalizika, mtakuwa mmefanya kazi bure; ingawa mmepitia uzoefu wa kazi ya Mungu, hamtakuwa mmemjua Roho Mtakatifu au kuwa na kuingia kwenu wenyewe. Nuru anayopewa mwanadamu na Roho Mtakatifu si ya kudumisha hisia za mwanadamu; ni kufungua njia kwa ajili ya kuingia kwa mwanadamu, vilevile kumruhusu mwanadamu kumjua Roho Mtakatifu, na kuanzia hapo anakuza moyo wa uchaji na ibada kwa Mungu.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

6. Mungu amewaaminia wanadamu vitu vingi sana na Amezungumza bila kikomo juu ya kuingia kwao. Lakini kwa sababu ubora wa tabia ya watu ni duni mno, maneno mengi ya Mungu yameshindwa kuanza kustawi. Kuna sababu mbalimbali za huu ubora duni wa tabia, kama vile uharibifu wa mawazo na maadili ya binadamu, na kutokuwa na malezi mazuri; imani za usihiri zilizojaa moyoni mwa mwanadamu; mitindo ya maisha iliyopotoka ambayo imeweka maovu mengi katika sehemu ya ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu; maarifa ya juujuu ya utamaduni, na takribani asilimia tisini na nane ya watu ambao hawana elimu ya utamaduni na, aidha, watu wachache sana wanaopata viwango vya juu vya elimu ya utamaduni. Kwa hivyo, kimsingi watu hawajui ni nini maana ya Mungu au Roho, bali wana taswira hafifu ya Mungu na isiyoeleweka vizuri kama iliyopatikana kutoka kwa imani ya usihiri. Ushawishi wenye madhara ambao maelfu ya miaka ya “roho wa juu sana wa utaifa” umeacha ndani kabisa ya moyo wa mwanadamu pamoja na fikira za kikabaila ambazo watu wamefungwa nazo na kutiwa minyororo, bila uhuru wowote, na kusababisha watu kutokuwa na hamasa au ustahimilivu, hawana shauku ya kusonga mbele, lakini badala yake wanakuwa baridi na kurudi nyuma, wakiwa na akili ya utumwa ambayo ina nguvu sana, na kadhalika—sababu hizi zimetengeneza taswira chafu na mbaya kwa mitazamo ya njozi, mawazo, maadili, na tabia ya binadamu. Inaonekana, wanadamu wanaishi katika dunia ya giza la kutisha, na hakuna anayetafuta kusonga mbele miongoni mwao, hakuna anayefikiria kwenda katika ulimwengu ulio bora. badala yake, wanaridhika na waliyo nayo maishani, kutumia siku zao kuzaa na kuwalea watoto, wakikazana, wakitoka jasho, wakifanya kazi zao, wakiwa na njozi ya kuwa na familia ya raha na yenye furaha, ya upendo wa ndoa, ya watoto wenye upendo, ya maisha yenye furaha katika miaka yao ya uzeeni wanapoishi kwa kudhihirisha maisha yao kwa amani. … Kwa makumi, maelfu, makumi ya maelfu ya miaka hadi sasa, watu wamekuwa wakipoteza muda wao kwa njia hii, hakuna anayetengeneza maisha makamilifu, wanapigana tu wenyewe kwa wenyewe katika ulimwengu huu wa giza, wakipambana kupata umaarufu na utajiri, na kufanyiana njama wao kwa wao. Nani amewahi kutafuta mapenzi ya Mungu? Kuna mtu yeyote aliyewahi kutilia maanani kazi ya Mungu? Sehemu hizi zote za binadamu zinazomilikiwa na ushawishi wa giza zimekuwa asili ya mwanadamu tangu zamani, kwa hiyo ni vigumu sana kutekeleza kazi ya Mungu na hata watu hawana moyo wa kuzingatia kile ambacho Mungu amewaaminia leo.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

7. Shughuli za kishirikina ambazo watu wanashughulika nazo ndizo Mungu anazichukia sana, lakini watu wengi bado hawawezi kuachana nazo, wakifikiri kwamba shughuli hizi za kishirikina zimeamriwa na Mungu, na hata leo bado hawajaziacha kabisa. Mambo kama mipango ambayo vijana hufanya kwa ajili ya sherehe za arusi au mahari, zawadi za pesa, dhifa, na maneno mengine na virai vinavyohusiana na matukio ya sherehe; maneno ya zamani ambayo yamerithishwa; shughuli zote za kishirikina zisizokuwa na maana zinazofanywa kwa niaba ya wafu na taratibu za mazishi; yote haya yanachukiwa sana na Mungu. Hata siku ya ibada (ikiwemo Sabato, kama inavyoadhimishwa na ulimwengu wa dini) inachukiwa naye; mahusiano ya kijamii na mawasiliano ya kidunia kati ya mwanamme na mwanamme pia yanachukiwa na kukataliwa zaidi na Mungu. Hata Sikukuu ya Machipuko na Siku ya Krismasi, ambazo zinajulikana kwa kila mtu, haziamriwi na Mungu, sembuse wanasesere na mapambo (mashairi, keki ya Mwaka Mpya, mafataki, kandili, zawadi za Krismasi, sherehe za Krismasi, na Ushirika Matakatifu) ya sikukuu hizi—je, sio sanamu katika akili za wanadamu? Kumega mkate siku ya Sabato, mvinyo, na kitani nyembamba navyo ni sanamu zaidi. Siku zote za sherehe za kijadi ambazo ni maarufu sana nchini China, kama vile Siku ya kuinua Vichwa vya Joka, Sikukuu ya Mashua ya Joka, Sikukuu ya Majira ya Kati ya Kupukutika, Sikukuu ya Laba, na Siku ya Mwaka Mpya, na sikukuu zisizothibitika katika ulimwengu wa kidini, kama vile Pasaka, Siku ya Ubatizo, na Siku ya Krismasi, zote hizi zimepangwa na kurithishwa kwa watu wengi tangu zama za kale hadi leo, zote hazilingani kabisa na binadamu aliyeumbwa na Mungu. Ni uwezo mkubwa wa fikra za binadamu na dhana bunifu ambazo zimewaruhusu kurithishwa hadi leo. Zinaonekana kuwa hazina kasoro, lakini kwa kweli ni hila ambazo Shetani alifanya kwa binadamu. Kadri Shetani wanavyoishi katika eneo fulani, na kadri eneo hilo lilivyo nyuma kimaendeleo na kutofaa, ndivyo desturi zake za kikabaila zinakuwa nyingi zaidi. Vitu hivi vinawafunga watu kwa nguvu, bila kutoa nafasi kwa ajili ya maendeleo. Sikukuu nyingi katika ulimwengu wa kidini zinaonekana kuonyesha ubunifu mkubwa na zinaonekana kujenga daraja kwa kazi ya Mungu, lakini kweli ni vifungo visivyoshikika ambavyo Shetani hutumia kuwafunga watu ili wasije kumjua Mungu—hizi zote ni hila za ujanja za Shetani. Kwa kweli, hatua ya kazi ya Mungu inapomalizika, tayari Amekwishaharibu zana na mtindo wa wakati huo, bila kuacha alama yoyote. Hata hivyo, “waumini wasalihina” bado wanaabudu vitu hivyo vya kushikika; wakati huo huo wanaacha kile Alicho nacho Mungu, bila hata kukichunguza zaidi, wakionekana wamejawa na upendo wa Mungu lakini kwa uhalisi walimtoa ndani ya nyumba zamani sana na kumweka Shetani mezani kwa ajili ya kumwabudu. Sanamu ya Yesu, Msalaba, Maria, Ubatizo wa Yesu na Karamu ya Mwisho—watu wanavichukulia hivi kama Bwana wa Mbinguni, wanaviabudu wakati wote wakilia kwa sauti kwa kurudiarudia “Mungu Baba.” Je, huu sio utani? Hadi leo, misemo mingi ya kimapokeo kama hiyo iliyorithishwa miongoni mwa wanadamu ni chukizo kwa Mungu; inazuia kabisa njia ya kuendelea mbele kwa Mungu na, zaidi ya hayo, inasababisha vipingamizi vikubwa kwa kuingia kwa mwanadamu. Mbali na kiwango ambacho Shetani amemharibu mwanadamu, sheria ya Witness Lee, uzoefu wa Lawrence, uchunguzi wa Watchman Nee, na kazi ya Paulo, haya yote yameuteka moyo wa mwanadamu. Mungu hana namna ya kufanya kazi kwa wanadamu, kwa sababu ndani yao kuna ubinafsi mwingi, sheria, kanuni, taratibu na mifumo, na vitu kama hivi; vitu hivi, ukiongezea vitendo vya watu vya imani za kishirikina, vimewakamata na kuwaharibu wanadamu. Ni kana kwamba mawazo ya watu ni filamu ya ajabu ya kichimbakazi katika rangi kamili, ikiwa na watu wa ajabu wakiendesha mawingu, ya kubuni sana kiasi cha kuwastaajabisha watu, ikiwaacha watu wametunduwazwa na kupigwa butwaa. Kusema kweli, kazi ambayo Mungu huja kufanya leo ni hasa kushughulikia na kuondoa sifa za ushirikina za binadamu na kugeuza kabisa mtazamo wao wa akili. Kazi ya Mungu sio kile ambacho kimepitishwa kwa vizazi na kuhifadhiwa mpaka leo na binadamu; ni kazi kama ilivyoanzishwa na Yeye binafsi na kukamilishwa na Yeye, bila haja yoyote ya kuurithi urithi wa mwanadamu fulani mkuu wa kiroho, au kurithi kazi yoyote ya asili ya uwakilishi iliyofanywa na Mungu katika enzi nyingine fulani. Binadamu hawahitaji kujishughulisha na jambo lolote kati ya haya. Mungu ana mtindo mwingine leo wa kuzungumza na wa kufanya kazi, kwa hiyo mbona binadamu wajisumbue? Kama wanadamu watatembea njia ya leo katika mkondo wa sasa huku wakiendeleza urithi wa “babu” zao, hawatafikia hatima yao. Mungu huhisi kinyaa sana kwa hali hii hasa ya tabia ya mwanadamu, jinsi Anavyoichukia mno miaka, miezi na siku za ulimwengu wa binadamu.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

8. Njia bora zaidi ya kubadilisha tabia ya mwanadamu ni kuondoa vitu hivi vyenye sumu kubwa katika mioyo ya wanadamu, kuwaruhusu watu kuanza kubadilisha fikira na maadili yao. Kwanza kabisa, watu wanatakiwa kuona waziwazi kwamba kaida zote hizi za kidini, shughuli za kidini, miaka na miezi, na sikukuu zote ni za kumchukiza Mungu. Wanatakiwa kuwa huru kutoka kwa vifungo hivi vya fikira za kishirikina na kuondoa kila alama ya kishirikina iliyozama kabisa ndani. Mambo haya yote ni sehemu ya kuingia kwa mwanadamu. Mnatakiwa kuelewa kwa nini Mungu huwatoa watu katika ulimwengu usiokuwa na dini, na pia kwa nini Huwatoa katika desturi na kanuni. Hili ndilo lango la kuingia kwenu, na ingawa halina uhusiano na uzoefu wenu wa kiroho, hivi ni vizuizi vikubwa vinavyowazuia kuingia, vinavyowazuia kumjua Mungu. Vinatengeza wavu unaowakamata watu. Watu wengi husoma Biblia sana na wanaweza hata kukariri mafungu mengi kutoka katika Biblia. Katika kuingia kwao leo, watu bila kujua wanaitumia Biblia kupima kazi ya Mungu, kana kwamba msingi wa hatua hii katika kazi ya Mungu ni Biblia na chanzo chake ni Biblia. Kazi ya Mungu inapokuwa sambamba na Biblia, watu huiunga mkono kazi ya Mungu kwa nguvu zote na kumwangalia Mungu kwa taadhima mpya; kazi ya Mungu inapokuwa haifanani na Biblia, watu huwa na dukuduku sana kiasi cha kuanza kutokwa jasho, wakitafuta ndani yake msingi wa kazi ya Mungu; kama kazi ya Mungu haikutajwa katika Biblia, watu watampuuza Mungu. Inaweza kusemwa kwamba, watu wengi wanaikubali kwa hadhari sana, wanatii kwa kusita, na hawajali kuhusu kuijua kazi ya Mungu; na kuhusu mambo yaliyopita, wanashikilia nusu moja na kuacha nusu nyingine. Je, huku kunaweza kuitwa kuingia? Kushikilia vitabu vya wengine kama hazina, na kuvichukulia kama ufunguo wa dhahabu wa kufungua lango la ufalme, watu hawaonyeshi kuvutiwa na matakwa ya Mungu ya leo. Aidha, “wataalamu wengi wenye akili” katika mkono wao wa kushoto wanashikilia maneno ya Mungu, huku katika mkono wa kulia wanashikilia “kazi kuu” za wengine, kana kwamba wanataka kutafuta msingi wa maneno ya Mungu kutoka kwa kazi hizi kuu ili kuthibitisha kwa ukamilifu kwamba maneno ya Mungu ni sahihi, na hata wanatoa ufafanuzi kwa wengine kwa kuunganisha na kazi kuu, kana kwamba walikuwa wanafanya kazi. Kusema kweli, kuna “watafiti wa kisayansi” wengi miongoni mwa wanadamu ambao hawajawahi heshimu mafanikio makubwa ya kisayansi ya leo, mafanikio ya kisayansi ambayo hayana kigezo (yaani, kazi ya Mungu, maneno ya Mungu, na njia ya kuingia uzimani), hivyo watu wote “wanajitegemea,” “wakihubiri” mbali sana wakitegemea sana ufasaha wao, wakiringia “jina zuri la Mungu.” Wakati huo huo, kuingia kwao kuko hatarini na umbali wa matakwa ya Mungu unaonekana kuwa mbali sana jinsi uumbaji ulivyo mbali na wakati huu. Ni rahisi kiasi gani kufanya kazi ya Mungu? Inaonekana kwamba watu wamekwishaamua kuacha nusu yao kwa mambo ya zamani na kuleta nusu yao kwa wakati wa leo, kuwasilisha nusu kwa Shetani na kukabidhi nusu kwa Mungu, kana kwamba hii ndiyo njia ya kutuliza dhamiri yao na kuweza kuwa na hisia ya utulivu fulani. Mioyo ya watu inadhuru sana kwa siri, wanaogopa sio tu kupoteza kesho bali pia wanahofia kupoteza jana, wanaogopa sana kumkosea Shetani na kumkosea Mungu wa leo, Anayeonekana kuwa na bado kutokuwa. Kwa sababu watu wameshindwa kukuza vizuri fikira na maadili yao, wanakosa utambuzi kabisa, na kimsingi hawajui kama kazi ya leo ni ile ya Mungu au siyo. Pengine ni kwa sababu fikra za kishirikina za watu zimekita mizizi sana kiasi kwamba ushirikina na ukweli, Mungu na sanamu, vimewekwa katika kundi moja; wala hawajali kuvibainisha vitu hivi, na inaonekana kama wametesa bongo zao lakini bado mambo hayo hayajawa wazi. Na hiyo ndio maana wanadamu wamesimama katika njia zao na hawasongi mbele tena. Haya yote yanatokea kwa sababu watu hawana elimu ya itikadi ambayo ni sahihi, kitu ambacho husababisha ugumu katika kuingia kwao. Na matokeo yake, watu wanapoteza mvuto kabisa katika kazi ya Mungu wa kweli, bali wanashikilia kwa kung’ang’ania[2] kazi ya mwanadamu (kama vile watu wanaotazamwa kuwa ni watu wakubwa) kana kwamba wamepigwa chapa nayo. Je, hizi si mada mpya kabisa ambazo wanadamu wanapaswa kuingia ndani?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili

9. Mungu Amekuwa mwili katika nchi ya China, ambayo wenyeji wa Hong Kong na Taiwan wanaiita bara. Mungu Alipokuja kutoka juu na kuja duniani, hakuna mtu mbinguni wala duniani aliyejua, maana hii ndiyo maana ya kweli ya Mungu kurudi kwa namna ya siri. Amekuwa katika mwili Akifanya kazi na kuishi kwa muda mrefu, bado hakuna mtu yeyote aliyejua. Hata leo hii, hakuna mtu anayetambua. Pengine hiki kitabakia kuwa kitendawili cha milele. Mungu kuja katika mwili wakati huu sio kitu ambacho mtu yeyote anaweza kujua. Haijalishi ni kwa kiwango kikubwa kiasi gani Roho Mtakatifu Anafanya kazi, siku zote Mungu yupo katika hali ya utulivu, kamwe Hajiachilii mbali. Mtu anaweza kusema kwamba inaonekana kama hatua hii ya kazi Yake inafanyika mbinguni. Ingawa ipo wazi kabisa kwa kila mtu, hakuna anayeitambua. Mungu Atakapomaliza hatua hii ya kazi Yake, kila mtu atazinduka kutoka katika ndoto yake na kugeuza mtazamo wake wa zamani.[3] Nakumbuka Mungu Alishawahi kusema, “Kuja katika mwili wakati huu ni sawa na kuanguka katika tundu la duma.” Hii ina maana kwamba kwa sababu awamu hii ya kazi ya Mungu imemfanya Mungu kuja katika Mwili na kuzaliwa katika makazi ya joka kuu jekundu, kuja Kwake duniani wakati huu kumeambatana na hatari nyingi zaidi. Anachokabiliana nacho ni visu na bunduki na kumbi za starehe; Anavyokabiliana navyo ni vishawishi; Anaokutana nao ni umati wa watu wenye sura za wauaji. Ana hatari ya kuuawa wakati wowote. Mungu Alikuja na ghadhabu. Hata hivyo, Alikuja ili Aweze kufanya kazi ya utakasaji, ikiwa na maana kwamba kufanya sehemu ya pili ya kazi Yake inayoendelea baada ya kazi ya wokovu. Kwa ajili ya hatua hii ya kazi Yake, Mungu Amejitolea mawazo na uangalizi wa hali ya juu kabisa na Anatumia njia yoyote inayoweza kufikiriwa ili kuepuka mashambulio ya majaribu, Anajificha katika unyenyekevu Wake na kamwe haringii utambulisho Wake. Katika kumwokoa mwanadamu msalabani, Yesu Alikuwa Anakamilisha tu kazi ya wokovu; Alikuwa hafanyi kazi ya utakasaji. Hivyo ni nusu tu ya kazi ya Mungu ndiyo ilikuwa inafanywa, na kukamilisha kazi ya ukombozi ilikuwa ni nusu ya mpango Wake mzima. Kwa kuwa enzi mpya ilikuwa inakaribia kuanza na ile ya zamani kukaribia kutoweka, Mungu Baba Alianza kukusudia sehemu ya pili ya kazi Yake na Akaanza kujiandaa kwa ajili yake. Wakati uliopita, kupata mwili huku katika siku za mwisho huenda hakukutolewa unabii, na hivyo kuweka msingi wa usiri mkubwa unaozunguka ujio wa Mungu katika mwili kipindi hiki. Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu Alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari Amekwishawasili duniani. Mungu Alifanya hivi ili Aifanye kazi Yake kwa urahisi na kupata matokeo bora zaidi, na pia ilikuwa ni kwa sababu ya kuepuka majaribu zaidi. Mwanadamu anapoamka kutoka usingizini, kazi ya Mungu itakuwa imekwishakamilika zamani sana na Ataondoka, na kufunga maisha Yake ya kutembeatembea na kusafiri duniani. Kwa kuwa kazi ya Mungu inamtaka Mungu kutenda na kuzungumza Yeye binafsi, na kwa kuwa hakuna namna ambayo mwanadamu anaweza kusaidia, Mungu Ameyavumilia maumivu makali ya kuja duniani kufanya kazi Yeye Mwenyewe. Mwanadamu hawezi kushikilia nafasi ya kazi ya Mungu. Kwa hiyo Mungu Alijihatarisha mara elfu kadhaa kuliko ilivyokuwa katika wakati wa Enzi ya Neema na kuja chini mahali ambapo joka kuu jekundu linaishi ili kufanya kazi Yake, kuweka mawazo Yake yote na uangalizi katika kuokoa kundi hili la watu maskini, kulikomboa kundi hili la watu lililogeuka na kuwa rundo la samadi. Ingawa hakuna anayejua uwepo wa Mungu, Mungu Hahangaiki kwa sababu ni faida kubwa kwa kazi ya Mungu. Kila mtu ni mwovu sana, sasa inawezekanaje kila mtu avumilie uwepo wa Mungu? Ndiyo maana duniani, Mungu Anakuwa kimya siku zote. Haijalishi mwanadamu ni katili kiasi gani, Mungu wala Hazingatii hayo moyoni Mwake hata kidogo, bali Anaendelea kufanya kazi Anayotaka kufanya ili kutimiza agizo kuu ambalo Baba wa mbinguni Alimpatia. Ni nani miongoni mwenu aliyetambua upendo wa Mungu? Ni nani anayejali sana mzigo Alionao Mungu Baba kuliko Mwana Wake Anavyofanya? Ni nani awezaye kuelewa mapenzi ya Mungu Baba? Roho wa Mungu Baba Aliyeko mbinguni Anasumbuka kila mara, na Mwana Wake duniani Anaomba mara kwa mara juu ya mapenzi ya Mungu Baba, Akihofia moyo Wake kuumia. Kuna mtu yeyote anayejua kuhusu upendo wa Mungu Baba kwa Mwana Wake? Kuna mtu yeyote anayejua jinsi ambavyo Mwana mpendwa Anavyomkumbuka Mungu Baba? Wakipata shida ya kuchagua kati ya mbingu na nchi, utaona wawili Hawa wanatazamana wakati wote kutoka kwa mbali, sambamba na Roho. Ee binadamu! Ni lini mtaufikiria moyo wa Mungu? Ni lini mtaielewa nia ya Mungu? Baba na Mwana siku zote Wamekuwa Wakitegemeana. Kwa nini tena Watengane, mmoja juu mbinguni na mmoja chini duniani? Baba Anampenda Mwana Wake kama vile Mwana Anavyompenda Baba Yake. Kwa nini sasa asubiri kwa muda mrefu huku Akiwa na shauku hiyo? Ingawa Hawajatengana kwa muda mrefu, je, mtu yeyote anajua kwamba Baba tayari Amekuwa Akitaka sana kwa shauku kwa siku nyingi na Amekuwa Akitarajia kwa muda mrefu kurudi haraka kwa Mwana Wake mpendwa? Anatazama, Anakaa kwa utulivu, Anasubiri. Hii yote ni kwa ajili ya kutaka Mwana Wake mpendwa Arudi haraka. Ni lini Atakuwa tena na Mwana ambaye Anazungukazunguka duniani? Ingawa watakapokuwa pamoja tena, Watakuwa pamoja milele, Anawezaje kustahimili maelfu ya siku za utengano, mmoja juu mbinguni na mwingine chini duniani. Makumi ya miaka duniani ni kama maelfu ya miaka mbinguni. Mungu Baba Anawezaje kutokuwa na wasiwasi? Mungu Anapokuja duniani, Anakabiliana na mabadiliko mengi ya ulimwengu wa kibinadamu kama mwanadamu. Mungu Mwenyewe hana hatia, sasa kwa nini Mungu Ateseke kwa maumivu kama mwanadamu? Pengine ndiyo maana Mungu Baba Anatamani sana Mwana Wake Arudi haraka; nani awezaye kuujua moyo wa Mungu? Mungu Anampatia mwanadamu vitu vingi sana; mwanadamu anawezaje kuulipa moyo wa Mungu kikamilifu? Lakini mwanadamu anampatia Mungu kidogo sana; sasa Mungu Atawezaje kutokuwa na wasiwasi?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

10. Uumbaji wa Mungu wa ulimwengu unaanzia mbali maelfu ya miaka huko nyuma, Amekuja duniani kufanya kazi isiyoweza kupimika, na Amepitia uzoefu mkubwa wa kukataliwa na kashfa. Hakuna anayekaribisha ujio wa Mungu; kila mtu anamwangalia tu kwa jicho kavu. Katika kipindi hiki cha maelfu ya miaka ya taabu, matendo ya mwanadamu yamevunjavunja moyo wa Mungu tangu zamani sana. Wala Hazingatii tena uasi wa watu, lakini badala yake Anatengeneza mpango tofauti ili kumbadilisha na kumsafisha mwanadamu. Dhihaka na kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu Alipitia Akiwa katika mwili, Mungu Amepitia ya kutosha. Dhihaka na kashfa, mateso, dhiki, mateso ya msalaba, kutengwa na wanadamu, na kadhalika ambayo Mungu Alipitia Akiwa katika mwili, Mungu Amepitia ya kutosha. Mungu katika mwili Ameteseka kikamilifu na shida za ulimwengu wa wanadamu. Roho wa Mungu Baba wa mbinguni Aliona mambo hayo hayavumiliki na Akarudisha kichwa Chake nyuma na kufumba macho Yake, Akisubiri Mwana Wake mpendwa kurudi. Yote Anayoyatamani ni kwamba watu wote wasikie na kutii, waweze kuhisi aibu kubwa mbele ya mwili Wake, na wasiasi dhidi Yake. Anachokitamani ni kwamba watu wote waamini kwamba Mungu yupo. Aliacha zamani sana kutaka mambo makubwa kutoka kwa mwanadamu kwa sababu Mungu Amelipa gharama kubwa sana, lakini mwanadamu bado anajistarehesha,[4] haiweki kabisa kazi ya Mungu moyoni mwake.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

11. Leo wote mnajua kwamba Mungu anawaongoza watu katika njia sahihi ya uzima, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuchukua hatua inayofuata kuingia katika enzi nyingine, kwamba Anamwongoza mwanadamu kuvuka mipaka ya enzi hii ya kale ya giza, kutoka katika mwili, kutoka kwenye ukandamizaji wa nguvu za giza na ushawishi wa Shetani, ili kila mtu aweze kuishi katika ulimwengu wa uhuru. Kwa ajili ya kesho ya kupendeza, ili kwamba watu wawe wakakamavu katika hatua zao kesho, Roho wa Mungu anapanga kila kitu kwa ajili ya mwanadamu, na ili mwanadamu aweze kuwa na furaha kubwa zaidi, Mungu anajitolea jitihada Zake zote katika mwili Akiandaa njia mbele ya mwanadamu, ili siku ambayo mwanadamu anaitamani sana iweze kuja haraka. Nyote mngeweza kufurahia wakati huu mzuri; si tendo rahisi kufanya mkutano na Mungu. Ingawa hamjawahi kumjua, tayari mmekuwa pamoja naye tangu kitambo. Laiti kila mtu angeweza kukumbuka milele siku zote hizi nzuri lakini fupi, na kuzifanya kuwa mambo yao ya kuwafurahisha duniani.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (5)” katika Neno Laonekana katika Mwili

12. Kwa maelfu ya miaka, Wachina wameishi maisha ya utumwa na hii imebana sana fikira, mawazo, maisha, lugha, tabia, na matendo yao kiasi kwamba wamebaki bila uhuru wowote. Maelfu kadhaa ya miaka ya historia imewachukua watu muhimu waliomilikiwa na roho na kuwadhoofisha hadi kuwa kitu kinachofanana na maiti iliyoondokewa na roho. Wengi ni wale wanaoishi chini ya kisu cha kuchinja cha Shetani, wengi wanaishi katika makazi yanayofanana na pango la mnyama, wengi wanakula chakula kama wanachokula ng’ombe au farasi, wengi wapo katika mchafuko huko “ahera” na hawana maana kabisa. Katika umbo la nje, watu hawana tofauti na watu wa zamani, sehemu yao ya kupumzika ni kama kuzimu, na wote wanaowazunguka ni mashetani na pepo wachafu. Kwa umbo la nje, wanadamu wanaonekana kuwa ni “wanyama” wa tabaka ya juu; kwa kweli wanaishi na kukaa na mashetani wachafu. Bila mtu yeyote kuwashughulikia, watu wanaishi katika mtego uliojificha wa Shetani, na wamenaswa kabisa katika kazi zake za taabu kiasi kwamba hawawezi kutoroka. Hawakusanyiki na wapendwa wao katika makazi yao ya furaha, kuishi kwa furaha na kuyaishi maisha ya kuridhisha, bali wanaishi Kuzimu, wakishughulika na pepo na kushirikiana na mashetani. Kwa kweli, watu bado wamefungwa na Shetani, wanaishi mahali ambapo pepo wachafu wanakusanyika, na wanatawaliwa na hawa pepo wachafu, na ni kana kwamba vitanda vyao ni mahali ambapo maiti zao zimelala, kana kwamba ni sehemu zao za kustarehe.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (5)” katika Neno Laonekana katika Mwili

13. Mwanadamu anaishi bega kwa bega na wanyama, na wanatembea pamoja kwa amani, bila ugomvi au vita vya maneno. Mwanadamu ni mgumu kuridhika vile anavyowajali na anavyohusika na wanyama, na wanyama wapo kwa ajili ya kuendelea kuishi kwa mwanadamu, hasa kwa manufaa ya mwanadamu, bila wao kunufaika na chochote na kwa kumtii mwanadamu kikamilifu. Kwa namna zote, uhusiano kati ya mwanadamu na mnyama ni wa karibu[5] na wa kukubaliana[6]—na pepo wachafu, inaweza kuonekana, ni muungano kamilifu wa mwanadamu na mnyama. Hivyo, mwanadamu na pepo wachafu walio duniani hata ni marafiki wema zaidi na wasiotengana: Mwanadamu anaonekana kufarakana na pepo wachafu, lakini kimsingi ameunganika nao; wakati huo, pepo wachafu hawamnyimi mwanadamu kitu chochote, na “wanatoa” vyote walivyonavyo kwao. Kila siku, watu wanachacharika katika “kasri la mfalme wa kuzimu,” wakichezacheza na “mfalme wa kuzimu” (babu yao) na kutawaliwa naye, ili kwamba, leo, watu wamepakwa masizi, na, baada ya kuishi muda mrefu sana Kuzimuni, wana muda mrefu toka waache kutamani kurudi katika “dunia ya walio hai.” Hivyo, mara tu wanapoiona nuru, na kutazama matakwa ya Mungu, na tabia ya Mungu, na kazi ya Yake, wanahisi dukuduku na wasiwasi; bado wakitamani sana kurudi kuzimu na kuishi na mizimu. Walimsahau Mungu zamani sana, na hivyo wamekuwa wakizungukazunguka katika makaburi.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (5)” katika Neno Laonekana katika Mwili

14. Kazi na kuingia kwa uhalisia ni vya kiutendaji na vinarejelea kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu. Mwanadamu kukosa kabisa uelewa juu ya sura halisi ya Mungu na kazi ya Mungu kumesababisha shida kubwa katika kuingia kwake. Leo hii, watu wengi bado hawajui kazi ambayo Mungu anatimiza katika siku za mwisho, au kwa nini Mungu Anastahimili fedheha kubwa kupita kiasi kuja katika mwili na kusimama na mwanadamu katika makovu na majonzi. Mwanadamu hajui chochote kuhusu lengo la kazi ya Mungu, wala kusudi la mpango wa Mungu kwa ajili ya siku za mwisho. Kwa sababu mbalimbali, watu daima wanakuwa vuguvugu katika kuingia ambako Mungu anataka na wanabakia wenye shaka[7], kitu ambacho kimeleta shida kubwa katika kazi ya Mungu katika mwili. Watu wanaonekana kuwa vizuizi na, leo hii, bado wanakuwa hawana uelewa sahihi. Kwa hiyo Nitazungumza juu ya kazi ambayo Mungu anafanya kwa mwanadamu, na makusudi ya Mungu ya haraka, ili kwamba nyinyi nyote muwe watumishi waaminifu wa Mungu ambao, kama Ayubu, ni bora ufe kuliko kumkataa Mungu na utastahimili kila fedheha, na ambao, kama Petro, mtatoa utu wenu wote kwa Mungu na kuwa wandani ambao Mungu Aliwapata katika siku za mwisho. Ninawasihi kaka na dada kufanya kila kitu kilichopo ndani ya uwezo wao kutoa utu wao wote kwa mapenzi ya mbingu ya Mungu, kuwa watumishi watakatifu katika nyumba ya Mungu, na kufurahia ahadi zisizokuwa na kikomo zilizotolewa na Mungu, ili kwamba moyo wa Mungu Baba ufurahie pumziko la amani. “Kukamilisha mapenzi ya Mungu Baba” kunapaswa kuwe wito wa wote wanaompenda Mungu. Maneno haya yanapaswa kutumika kama mwongozo wa mwanadamu kwa ajili ya kuingia na dira inayoongoza matendo yake. Hili ndilo suluhisho ambalo mwanadamu anapaswa kuwa nalo. Kukamilisha kabisa kazi ya Mungu duniani na kushirikiana na kazi ya Mungu katika mwili—huu ni wajibu wa mwanadamu. Siku moja, kazi ya Mungu itakapokuwa imekamilika, mwanadamu atamuaga Anaporudi mapema kwa Baba yake mbinguni. Je, huu sio wajibu ambao mwanadamu anapaswa kuutimiza?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili

15. Kwa mwanadamu, Mungu kusulubiwa kulihitimisha kazi ya Mungu kupata mwili, Aliwakomboa binadamu wote, na Akamruhusu kuteka ufunguo wa Kuzimu. Kila mtu anadhani kwamba kazi ya Mungu imekamilika kikamilifu. Kwa uhalisia, kwa Mungu, ni sehemu ndogo tu ya kazi Yake ndiyo imekamilika. Amemkomboa tu binadamu; Hajamshinda mwanadamu, wala kubadilisha ubaya wa Shetani kwa binadamu. Hiyo ndio maana Mungu Anasema, “Ingawa mwili Wangu ulipitia maumivu ya kifo, hilo sio lengo lote la Mimi kupata mwili. Yesu ni Mwana Wangu mpendwa na Alisulubishwa msalabani kwa ajili Yangu, lakini hakukamilisha kikamilifu kazi Yangu. Alifanya tu sehemu.” Hivyo Mungu Akaanza mpango wa mzunguko wa pili ili kuendeleza kazi ya Mungu kupata mwili. Lengo kuu la Mungu ni kumkamilisha na kumpata kila mmoja aokolewe kutoka katika mikono ya Shetani, hiyo ndiyo sababu Mungu Alijiandaa tena kujihatarisha kuja katika mwili.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili

16. Katika maeneo mengi, Mungu Alitabiri kupata kundi la washindi katika nchi ya Sinim. Ni upande wa Mashariki mwa ulimwengu ambapo washindi wanapatikana, hivyo nchi ambapo Mungu kupata mwili mara ya pili Atatua bila shaka ni nchi ya Sinim, mahali ambapo joka jekundu linaishi. Hapo Mungu Atawapata warithi wa joka kuu jekundu na litashindwa na kuaibishwa. Mungu Anataka kuwaamsha watu hawa walioteseka sana, kuwaamsha kabisa, na kuwafanya waondoke katika ukungu na kulikataa joka kuu jekundu. Mungu Anataka Awaamshe kutoka katika ndoto zao, kuwafanya waelewe tabia ya joka kuu jekundu, kuutoa moyo wao wote kwa Mungu, kuinuka kutoka katika nguvu kandamizi za giza, kusimama Mashariki mwa dunia, na kuwa uthibitisho wa ushindi wa Mungu. Baada ya hapo Mungu Atakuwa Amepata utukufu. Kwa sababu hii tu, kazi ambayo ilisitishwa Israeli Mungu Aliipeleka katika nchi ambapo linakaa joka kuu jekundu na, takribani miaka elfu mbili baada ya kuondoka, Amekuja tena katika mwili ili kuendeleza kazi ya Enzi ya Neema. Mwanadamu anashuhudia kwa macho yake, Mungu Akizindua kazi mpya katika mwili. Lakini kwa Mungu, Anaendeleza kazi ya Enzi ya Neema, kwa mwachano wa miaka elfu kadhaa, na badiliko tu la eneo la kufanyia kazi na mradi wa kazi. Ingawa taswira ya mwili ambayo Mungu Ameichukua katika kazi ya leo ni mtu mwingine tofauti na Yesu, Wanashiriki hulka na mzizi mmoja, na wanatoka katika chanzo kimoja. Pengine wana tofauti za umbo la nje, lakini kweli za ndani za kazi Zao zinafanana kabisa. Hata hivyo, enzi zenyewe, ni tofauti kama ilivyo usiku na mchana. Inawezekanaje kazi ya Mungu isibadilike? Au inawezekanaje kazi ziingiliane?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili

17. Yesu alichukua umbo la Myahudi, Alifuata mavazi ya Wayahudi, na Alikua akila chakula cha Kiyahudi. Hii ni hali yake ya kawaida ya kibinadamu. Lakini Mungu katika mwili wa leo Anachukua umbo la watu wa Asia na Anakua Akila chakula cha taifa la joka kuu jekundu. Hii haiingiliani na lengo la Mungu kupata mwili. Badala yake, vinakamilishana, na zaidi vinakamilisha maana ya kweli ya Mungu kupata mwili. Kwa sababu Mungu katika mwili Anarejelewa kuwa “Mwana wa Adamu” au “Kristo,” umbo la nje la Kristo wa leo haliwezi kulinganishwa na Yesu Kristo. Hata hivyo, mwili huu unaitwa “Mwana wa Adamu” na Yupo katika sura ya mwili. Kila hatua ya kazi ya Mungu inahusisha maana ya kina sana. Sababu ya Yesu kuzaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu ni kwa sababu Alipaswa kuwakomboa wenye dhambi. Alitakiwa Asiwe na dhambi. Isipokuwa tu mwishoni Alipolazimishwa kufanana na mwili wa dhambi na kuchukua dhambi za wenye dhambi ndivyo Aliweza kuwaokoa kutoka katika laana ya msalaba ambao Mungu Alitumia kuwaadibu watu. (Msalaba ni zana ya Mungu kwa ajili ya kuwalaani na kuwarudi watu; mitajo ya kulaani na kurudi mahususi inahusu kuwalaani na kuwarudi wenye dhambi.) Lengo lilikuwa ni kuwafanya wenye dhambi wote kutubu na kutumia msalaba kuwafanya waungame dhambi zao. Yaani, kwa ajili ya kuwakomboa binadamu wote, Mungu Alijiweka Mwenyewe katika mwili uliozaliwa kwa njia ya Roho Mtakatifu na Akachukua dhambi za binadamu wote. Namna ya kawaida ya kuelezea hii ni kutoa mwili mtakatifu kwa kubadilishana na wenye dhambi wote, usawa wa Yesu kuwa sadaka ya dhambi umewekwa mbele ya Shetani ili “kumsihi” Shetani kuwarudisha binadamu wote wasio na hatia kwa Mungu. Hivyo ili kukamilisha hatua hii ya kazi ya wokovu kulihitaji utungaji mimba kwa njia ya Roho Mtakatifu. Hili lilikuwa ni sharti la lazima, “mkataba” wakati wa vita kati ya Mungu Baba na Shetani. Hii ndio maana Yesu Alitolewa kwa Shetani, ni baada ya hapo tu ndipo hatua hii ya kazi ikahitimishwa. Hata hivyo, kazi ya ukombozi ya Mungu leo tayari ni ya umuhimu usio kifani, na Shetani hana sababu ya kufanya madai, hivyo Mungu kufanyika mwili hakuhitaji utungaji mimba kwa njia ya Roho Mtakatifu, maana Mungu kwa asili ni mtakatifu na Asiye na hatia. Hivyo Mungu mwenye mwili wa wakati huu sio tena Yesu wa Enzi ya Neema. Lakini bado Yupo kwa ajili ya mapenzi ya Mungu Baba na kwa ajili ya kutimiza matamanio ya Mungu Baba. Hii inaweza kuchukuliwaje kuwa ni msemo usiokuwa na maana? Je, ni lazima Mungu kupata mwili kufuate kanuni kadhaa?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (6)” katika Neno Laonekana katika Mwili

18. Mungu Anakuja miongoni mwa wanadamu siku ya leo kwa kusudi la kubadilisha mawazo na roho zao, na taswira ya Mungu katika mioyo yao ambayo wamekuwa nayo kwa maelfu ya miaka. Kupitia fursa hii, Atamfanya mwanadamu kuwa mkamilifu. Yaani, kupitia maarifa ya mwanadamu, Atabadilisha namna wanavyomfahamu na mitazamo yao Kwake, ili kwamba maarifa yao juu ya Mungu, yaweze kuanza katika rekodi safi, na mioyo yao itakuwa imesafishwa upya na kubadilishwa. Kushughulika na nidhamu ni njia, na ushindi na kufanya upya ni malengo. Kuondoa mawazo ya kishirikina aliyonayo mwanadamu kuhusu Mungu asiye dhahiri ndilo limekuwa kusudi la Mungu milele, na hivi karibuni limekuwa suala la haraka kwake. Ni matumaini Yangu kwamba watu wote watalifikiria hili zaidi. Wabadilishe jinsi kila mtu anavyopitia uzoefu ili kwamba kusudi hili la haraka la Mungu liweze kufanyika hivi karibuni na hatua ya mwisho ya kazi ya Mungu duniani iweze kuhitimishwa kwa matokeo mazuri. Onyesheni uaminifu wenu kama mnavyopaswa, na ufariji moyo wa Mungu kwa mara ya mwisho. Ni matumaini Yangu kwamba hakuna mtu yeyote miongoni mwa kaka na dada atakayekwepa jukumu hili au kuzungukazunguka tu. Mungu Anakuja katika mwili wakati huu kwa mwaliko, na kutokana na hali ya mwanadamu. Yaani, Anakuja kumpatia mwanadamu kile alichokuwa anahitaji. Atakuja kumwezesha kila mwanadamu, wa tabia yoyote au jamii, kuona neno la Mungu na, kutoka katika neno Lake, kuona uwepo na udhihirishaji wa Mungu na kukubali ukamilishaji wa Mungu. Neno lake litabadilisha mawazo na mitazamo ya mwanadamu ili kwamba sura ya kweli ya Mungu ikite mizizi kabisa katika moyo wa mwanadamu. Hili ndilo tamanio pekee la Mungu duniani. Haijalishi jinsi gani asili ya mwanadamu ilivyo, jinsi gani asili yake ilivyo duni, au matendo yake yalivyokuwa huko nyuma, Mungu Hajali haya. Anatumainia tu mwanadamu kuisafisha kabisa taswira ya Mungu aliyonayo moyoni mwake na kuijua asili ya binadamu, na hapo Atakuwa Amebadilisha mtazamo wa kiitikadi wa mwanadamu. Anatarajia mwanadamu kuwa na shauku ya kina kwa Mungu na kuwa na mahusiano ya milele na Yeye. Hiki ndicho Mungu Anachomwomba mwanadamu.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

19. Maarifa ya maelfu kadhaa ya miaka ya utamaduni wa kale na historia vimefunga fikra na dhana na akili ya mwanadamu kwa nguvu sana kiasi cha kutoweza kupenyeka na kutoweza kubadilishwa.[8] Mwanadamu anaishi katika ngazi ya kumi na nane ya kuzimu, kana kwamba wamefukuziwa chini na Mungu, wasiweze kuona mwanga tena. Fikra za kishirikina zimemkandamiza mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu anaweza kupumua kwa shida sana na hivyo kufa kwa kukosa hewa. Hawana nguvu hata kidogo ya kupinga, kimya kimya wanaendelea kuvumilia na kuvumilia…. Hakuna hata mmoja aliyewahi kujaribu kupigana au kusimama kwa ajili ya uadilifu na haki; wanaishi maisha ambayo hayana tofauti na maisha ya mnyama, huku wakinyanyaswa na kushambuliwa na mabwana wa ushirikina, mwaka baada ya mwaka, siku baada ya siku. Mwanadamu hajawahi kufikiria kumtafuta Mungu ili kufurahia furaha duniani. Ni kana kwamba mwanadamu amepigwa, kama majani yaliyoanguka ya majira ya kupukutika, yaliyonyauka na kukauka kabisa. Mwanadamu amepoteza kumbukumbu na anaishi bila matumaini kuzimu kwa jina la ulimwengu wa kibinadamu, akisubiri ujio wa siku ya mwisho ili kwamba waweze kupotea pamoja na kuzimu, kana kwamba siku ya mwisho wanayoitamani sana ni siku watakayofurahia pumziko la amani. Maadili ya kishirikina yamempeleka mwanadamu “Kuzimu,” kiasi kwamba mwanadamu anakuwa na uwezo mdogo wa kupinga. Ukandamizaji wa aina mbalimbali umemlazimisha mwanadamu taratibu kuzama chini kabisa Kuzimu na kutanga mbali kabisa na Mungu. Sasa, Mungu Amekuwa mgeni kabisa kwa mwanadamu, na mwanadamu bado anafanya haraka kumwepuka wanapokutana. Mwanadamu hamtambui na anamtenga kana kwamba mwanadamu hajawahi kumwona hapo kabla. … Maarifa ya utamaduni wa kale kwa taratibu yamemwondoa mwanadamu kutoka katika uwepo wa Mungu na kumweka mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wana wake. Vitabu Vinne na Maandiko ya Kale ya Kiyunani Matano vimepeleka fikra na mawazo ya mwanadamu katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko ya Kiyunani, wakikuza zaidi mitazamo yao juu ya Mungu. Mfalme wa mashetani bila huruma alimtupa Mungu nje kutoka katika moyo wa mwanadamu bila wao kujua, huku akifurahia kuuchukua moyo wa mwanadamu. Baada ya hapo na kuendelea mwanadamu akawa na roho mbaya na ya uovu akiwa na sura ya mfalme wa mashetani. Chuki juu ya Mungu ilijaza kifua chao na sumu ya mfalme wa mashetani ikasambaa ndani ya mwanadamu hadi alipomalizwa kabisa. Mwanadamu hakuwa na uhuru tena na hakuweza kuvunja vifungo vya mfalme wa mashetani. Kwa hiyo, mwanadamu angeweza kuendelea kukaa pale tu na kufungwa, kujisalimisha kwake na kujitiisha kwake.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

20. Amepanda zamani sana mbegu ya kutoamini kuwa kuna Mungu ndani ya moyo mchanga wa mwanadamu, akimfundisha mwanadamu dhana za uongo kama vile, “kujifunza sayansi na teknolojia, kutambua Vipengele Vinne vya Usasa, hakuna Mungu duniani.” Si hivyo tu, ametangaza kwa kurudiarudia, “Hebu tujenge makazi mazuri sana kwa kufanya kazi kwa bidii,” akiwaomba wote kujiandaa toka wakiwa watoto kutumikia nchi yao. Mwanadamu amepelekwa mbele yake bila kujitambua, na bila kusita akajichukulia sifa (akimrejelea Mungu akiwa Ameshikilia binadamu mzima katika mikono Yake). Hajawahi kuhisi aibu au kuwa na hisia yoyote ya aibu. Aidha, bila aibu amewanyakua watu wa Mungu na kuwaweka katika nyumba yake, wakati akirukaruka kama panya mezani na kumfanya mwanadamu amwabudu kama Mungu. Ni ujahili kabisa huu Anaropoka tuhuma hizo za kushtua, “Hakuna Mungu duniani. Upepo upo kwa ajili ya sheria za asili; mvua ni unyevunyevu unaoganda na kudondoka chini kama matone; tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa uso wa ardhi kwa sababu ya mabadiliko ya jiolojia; ukame ni kwa sababu ya ukavu hewani kwa mwingiliano wa kinyuklia katika uso wa jua. Haya ni matukio ya asili. Ni sehemu gani ambayo ni tendo la Mungu?” Hata anaropoka[a] kauli kama hizi zisizo na aibu: “Mwanadamu alitokana na sokwe wa zamani, na dunia leo imeendelea kutoka katika jamii ya kale ya takribani miaka bilioni moja iliyopita. Ama nchi inaendelea au inaanguka inaamuliwa na mikono ya watu wake.” Mwanadamu amemning’iniza ukutani miguu juu kichwa chini na kumweka mezani ili kutunzwa vizuri na kuabudiwa. Anapokuwa anapiga kelele kwamba “Hakuna Mungu,” anajichukulia mwenyewe kuwa ni Mungu, na kumsukumia mbali Mungu nje ya mipaka ya dunia bila huruma. Anasimama katika sehemu ya Mungu na kutenda kama mfalme wa mashetani. Ni upuuzi mkubwa kiasi gani! Anamsababisha mtu kuteketezwa na chuki yenye sumu. Inaonekana kwamba Mungu ni adui wake mkubwa na Mungu Hapatani naye kabisa. Anafanya hila zake za kumfukuza Mungu wakati anabakia huru na hajapatikana.[9] Huyo kweli ni mfalme wa mashetani! Tunawezaje kuvumilia uwepo wake? Hatapumzika hadi awe ameisumbua kazi ya Mungu na kuiacha katika matambara na kuwa katika hali ya shaghalabaghala kabisa,[10] kana kwamba anataka kumpinga Mungu hadi mwisho, hadi mmoja kati yao awe ameangamia. Anampinga Mungu kwa makusudi na kusogea karibu zaidi. Sura yake ya kuchukiza imefunuliwa toka zamani na sasa imevilia damu na kugongwagongwa,[11] ipo katika hali mbaya sana, lakini bado hapunguzi hasira zake kwa Mungu, kana kwamba anatamani kummeza Mungu kabisa kwa mara moja ili kutuliza hasira moyoni mwake. Tunawezaje kumvumilia, huyu adui wa Mungu anayechukiwa! Ni kumalizwa kwake na kuondolewa kabisa ndiko kutaleta mwisho wa matamanio yetu ya maisha. Anawezaje kuruhusiwa kuendelea kukimbia ovyoovyo? Amemharibu mwanadamu kwa kiwango ambacho mwanadamu hajui ’mahali pa raha zote, na anakuwa mfu na hajitambui. Mwanadamu amepoteza uwezo wa kawaida wa kufikiri wa kibinadamu. Kwa nini tusijitoe sadaka uhai wetu wote kumwangamiza na kumchoma na kuondoa kabisa hofu ya hatari inayobakia na kuruhusu kazi ya Mungu kuufikia uzuri usiotarajiwa hivi karibuni? Genge hili la waovu limekuja miongoni mwa wanadamu na kusababisha hofu na shida kubwa. Wamewaleta wanadamu wote katika ukingo wa jabali, wakipanga kwa siri kuwasukumia chini wavunjike vipande vipande na kumeza maiti zao. Wana matumaini ya kuharibu mpango wa Mungu na kushindana na Mungu katika pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda.[12] Hiyo kwa vyovyote vile ni rahisi! Msalaba umeandaliwa, mahususi kwa ajili ya mfalme wa mashetani ambaye ni mwenye hatia ya makosa maovu sana. Mungu si wa msalaba tena na Amekwishamwachia Shetani. Mungu Aliibuka mshindi muda mrefu uliopita, Hahisi tena huzuni juu ya dhambi za binadamu. Ataleta wokovu kwa binadamu wote.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

21. Kutoka juu hadi chini na kuanzia mwanzo hadi mwisho, amekuwa akisumbua kazi ya Mungu na kutenda kinyume Chake. Mazungumzo yote ya “urithi wa utamaduni wa kale,” “maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale,” “mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius,” na “maandiko ya kale ya Confucius na ibada ya kishirikina” vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekeni popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na “masokwe” wa kale kwa makusudi kabisa kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu. Sio tu amemtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza[13] mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wapo tayari kumpokea Mungu na kukaribisha kwa furaha ujio wa Mungu. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi linaloungua na ubani, ni harufu nzito sana inayomaliza hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo mwanadamu hawezi kuvumilia bali kutapika tu. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii sanamu zimetapakaa, zikiwa na rangi zote za upinde wa mvua, ambazo zinaibadilisha nchi kuwa ulimwengu unaometameta, na mfalme wa mashetani amekenua, kana kwamba njama zake ovu zimefanikiwa. Wakati huo mwanadamu hana habari naye, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwishamharibu kwa kiwango ambacho amekuwa hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani kumfutilia mbali Mungu mara moja, na kumtukana na kumwangamiza, na kujaribu kuchana na kuvuruga kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu “akiingilia” kazi miongoni mwa wanadamu? Anawezaje kumruhusu Mungu kufichua uso wake wa chuki? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kutawala nguvu yake duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake? Akiwa na roho mbaya, bado anaamini kwamba yeye ni mzuri kupita kiasi. Genge hili la washiriki jinai![14] Wanakuja miongoni mwa walio na mwili wa kufa na kuendeleza starehe na kuvuruga mpangilio. Usumbufu wao unaleta kigeugeu duniani na kusababisha hofu katika moyo wa mwanadamu, na wamemharibu mwanadamu kiasi kwamba mwanadamu anafanana na wanyama wabaya wasioweza kuvumilika, wala hana tena hata chembe ya mwanadamu asilia mtakatifu. Hata wanatamani kutawala kama madikteta duniani. Wanakwamisha kazi ya Mungu ili kwamba isiweze kusonga mbele na kumfunga mwanadamu kana kwamba wapo nyuma ya kuta za shaba na chuma cha pua. Baada ya kufanya dhambi nyingi sana na kusababisha shida nyingi sana, wanawezaje kutarajia kitu chochote tofauti na kusubiri kuadibu? Mapepo na roho wa Shetani wamekuwa wakicharuka duniani na wamefunga mapenzi na jitihada za maumivu za Mungu, na kuwafanya wasiweze kupenyeka. Ni dhambi ya mauti kiasi gani! Inawezekanaje Mungu Asiwe na wasiwasi? Inawezekanaje Mungu Asiwe na ghadhabu? Wanasababisha vikwazo vya kusikitisha na upinzani kwa kazi ya Mungu. Uasi wa kutisha! Hata mapepo hao wadogo kwa wakubwa wanajivunia nguvu za Shetani mwenye nguvu zaidi na kuanza kufanya fujo. Kwa makusudi wanapinga ukweli licha ya kuuelewa vizuri. Wana wa uasi! Ni kana kwamba, sasa mfalme wao amepanda kwenda katika kiti cha enzi cha kifalme, wamekuwa wa kuridhika nafsi na kuwatendea wengine wote kwa dharau. Ni wangapi wanautafuta ukweli na kufuata haki? Wote ni wanyama kama tu nguruwe na mbwa, wakuongoza genge la nzi wanaonuka katika rundo la kinyesi na kuchomeka vichwa vyao na kuchochea vurugu.[15] Wanaamini kwamba mfalme wao wa kuzimu ni mkuu wa wafalme wote, bila kutambua kwamba si chochote zaidi ya nzi katika kitu kilichooza. Si hivyo tu, wanatoa maoni ya kashfa dhidi ya uwepo wa Mungu kwa kutegemea nguruwe na mbwa wa wazazi wao. Nzi wadogo wanadhani wazazi wao ni wakubwa kama nyangumi mwenye meno.[16] Hawatambui kwamba wao ni wadogo sana, wazazi wao ni nguruwe na mbwa wachafu mara bilioni kuliko wao wenyewe? Hawatambui uduni wao, wanacharuka kwa misingi ya harufu iliyooza ya nguruwe na mbwa hao na wana mawazo ya udanganyifu ya kuzaa vizazi vijavyo. Huko ni kukosa aibu kabisa! Wakiwa na mbawa za kijani mgongoni mwao (hii inarejelea wao kudai kuwa wanamwamini Mungu), wanaanza kuwa na majivuno na kiburi juu ya uzuri wao na mvuto wao, kwa siri kabisa wanamtupia mwanadamu uchafu wao. Na hata ni wa kuridhika nafsi, kana kwamba jozi ya mbawa zenye rangi ya upinde wa mvua zingeweza kuficha uchafu wao, na hivyo wanautesa uwepo wa Mungu wa kweli (hii inarejelea kisa cha ndani cha ulimwengu wa kidini). Mwanadamu anajua kidogo kwamba, ingawa mbawa za nzi ni nzuri za kupendeza, hata hivyo ni nzi mdogo tu aliyejaa uchafu na kujazwa na vijidudu. Kwa kutegemea uwezo wa nguruwe na mbwa wa wazazi wao, wanacharuka nchi nzima (hii inarejelea viongozi wa dini wanaomtesa Mungu kwa misingi ya uungwaji mkono mkubwa kutoka katika nchi inayomsaliti Mungu wa kweli na ukweli) kwa ukatili uliopitiliza. Ni kana kwamba mizimu ya Mafarisayo wa Kiyahudi wamerudi pamoja na Mungu katika nchi ya joka kuu jekundu, wamerudi katika kiota chao cha zamani. Wameanza kazi yao tena ya utesaji, wakiendeleza kazi yao yenye umri wa maelfu kadhaa ya miaka. Kikundi hiki cha waliopotoka ni hakika kitaangamia duniani hatimaye! Inaonekana kwamba, baada ya milenia kadhaa, roho wachafu wamekuwa wenye hila na wadanganyifu sana. Muda wote wanafikiri juu ya njia za kuidhoofisha kazi ya Mungu kwa siri. Ni werevu sana na wajanja na wanatamani kurudia katika nchi yao kufanya majanga yaliyotokea maelfu kadhaa ya miaka iliyopita. Hii takribani imfanye Mungu kulia kwa sauti kuu, na Anajizuia sana kurudi katika mbingu ya tatu ili Awaangamize. Kwa mwanadamu kumpenda Mungu ni lazima aelewe mapenzi Yake na furaha Yake na huzuni, vilevile na kile Anachokichukia zaidi. Hii itakuza zaidi kuingia kwa mwanadamu. Kadri mwanadamu anavyoingia kwa haraka, ndivyo moyo wa Mungu unavyoridhika; kadri mwanadamu anavyomtambua kwa uwazi mfalme wa mashetani, ndivyo mwanadamu anavyosogea karibu zaidi kwa Mungu, ili kwamba matamanio yake yaweze kutimizwa.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

22. Nimezungumza mara nyingi sana kwamba kazi ya Mungu ya siku za mwisho ni kwa ajili ya kubadilisha roho ya kila mtu, kubadilisha nafsi ya kila mtu, ili kwamba moyo wake, ambao umeteseka sana na kiwewe, uwe umebadilishwa, hivyo kuokoa nafsi yake, ambayo imeumizwa kwa kina zaidi na uovu; ni kwa sababu ya kuamsha roho za watu, kuyeyusha mioyo yao baridi, na kuwaruhusu kurudisha nguvu za ujana. Haya ndiyo mapenzi makubwa ya Mungu. Weka pembeni mazungumzo ya ni namna gani maisha na uzoefu wa mwanadamu ni ya kiburi au ya kina; mioyo ya watu itakapokuwa imeamshwa, wanapokuwa wameamshwa kutoka kwa ndoto zao na kujua kikamilifu madhara yaliyoletwa na joka kuu jekundu, kazi ya huduma ya Mungu itakuwa imekamilika. Siku ambayo kazi ya Mungu itakuwa imekamilika ni wakati ambapo mwanadamu ataanza rasmi njia ya imani sahihi kwa Mungu. Wakati huu, huduma ya Mungu itakuwa imekamilika: Kazi ya Mungu katika mwili itakuwa imekamilika kabisa, na mwanadamu atakuwa ameanza rasmi kufanya kazi ambayo anapaswa kufanya—atatekeleza huduma yake. Hizi ni hatua za kazi ya Mungu. Hivyo mnapaswa kutafuta kwa kupapasa kuingia kwenu katika misingi ya kujua mambo haya. Haya yote ndiyo mnayopaswa kuyajua. Kuingia kwa mwanadamu kutaboreka tu pale ambapo mabadiliko yatatokea ndani kabisa ya moyo wake, maana kazi ya Mungu ni wokovu kamili wa mwanadamu—mwanadamu aliyekombolewa, ambaye bado anaishi chini ya nguvu za giza, na ambaye hajawahi kuzinduka kutoka katika eneo hili la kusanyiko la pepo; ili kwamba mwanadamu aweze kuwekwa huru dhidi ya milenia ya dhambi, na kuwa wapendwa wa Mungu, kumkanyaga kabisa joka kuu jekundu, kuanzisha ufalme wa Mungu, na kuupumzisha moyo wa Mungu mapema, ni kutoa mawazo bila woga, bila kubania, kwa chuki inayovimbisha kifua chenu, kuondoa kabisa vijidudu hivyo, kuwafanya muache maisha haya ambayo hayana tofauti na maisha ya ng’ombe au farasi, ili msiwe watumwa tena, ili msiweze kukanyagwa tena au kuamrishwa na joka kuu jekundu; hamtakuwa tena wa taifa hili lililoanguka, hamtakuwa tena wa joka kuu jekundu lenye chuki, hamtafungwa nalo tena. Kiota cha pepo hakika kitachanwachanwa na Mungu, na mtasimama kando ya Mungu—nyinyi ni wa Mungu, na sio wa milki hii ya watumwa. Mungu ameichukia sana jamii hii ya giza toka zamani. Anasaga meno Yake, Akitamani kumkanyaga mwovu huyu, joka wa zamani mwenye chuki, ili kwamba asiinuke tena, na hatamnyanyasa tena mwanadamu; Hatasamehe matendo yake ya zamani, Hatavumilia udanganyifu wake kwa mwanadamu, atalipiza kisasi kwa kila kosa alilofanya katika enzi zote; Mungu hatamhurumia hata kidogo huyu kiongozi wa uovu wote,[17] Atamharibu kabisa.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili

23. Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanazunguka kila kona, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi,[18] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida.[19] Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu kwa kufumba na kufumbua, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, na hawana hata chembe ya wema, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! Nani ambaye ameikumbatia kazi ya Mungu? Nani ametoa maisha yake au kumwaga damu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa kizazi baada ya kizazi, kutoka kwa wazazi hadi watoto, mwanadamu aliyepo katika utumwa bila heshima amemfanya Mungu mtumwa—hii inawezaje kukosa kuamsha hasira? Maelfu ya miaka ya chuki ikiwa imejaa kifuani, milenia ya dhambi imeandikwa katika moyo—inawezekanaje hii isichochee chuki? Kumlipiza Mungu, kuuondoa kabisa uadui wake, usimwache kutangatanga tena, na usimruhusu kufanya fujo zaidi kama anavyotaka! Sasa ndio wakati: Mwanadamu ana muda mrefu tangu akusanye nguvu zake zote, amejitolea nguvu zake zote, amelipa kila gharama, kwa hili, kuchana uso uliojificha wa pepo hili na kuwafanya watu, ambao wamepofushwa na kuvumilia kila aina ya mateso na taabu, kuinuka kutoka katika maumivu na kurudi kwa ibilisi huyu wa zamani. Kwa nini kuweka kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini kutumia mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini kutumia nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini asimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini kumbana Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Wema upo wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu upo wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini kusababisha matamanio makubwa kiasi hicho kwa Mungu? Kwa nini kumfanya Mungu kuita tena na tena? Kwa nini kumlazimisha Mungu kumhofia Mwana Wake mpendwa? Kwa nini jamii hii ya giza na mbwa wao walinzi wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba? Kwa nini mwanadamu haelewi, mwanadamu anayeishi katika maumivu na mateso? Mungu amevumilia mateso makubwa kwa ajili yenu, kwa maumivu makubwa Amemtoa Mwanawe wa pekee, mwili wake na damu, kwa ajili yenu, sasa kwa nini bado mnakuwa vipofu? Katika mtazamo mzima wa kila mtu, mnakataa ujio wa Mungu, na mnakataa urafiki wa Mungu. Kwa nini mnakosa busara kiasi hicho? Mko tayari kuvumilia uonevu katika jamii ya giza kama hii? Kwa nini, badala ya kujaza tumbo lenu kwa milenia ya uadui, mnajidanganya wenyewe kwa “kinyesi” cha mfalme wa pepo?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili

24. Hatua za kazi ya Mungu duniani zinahusisha shida kubwa: Udhaifu wa mwanadamu, upungufu, utoto, ujinga na kila kitu cha mwanadamu—kila kimoja kimepangwa kwa uangalifu sana na kuangaliwa kwa hadhari sana na Mungu. Mwanadamu ni kama duma wa kutisha ambaye mtu hathubutu kumtega au kumchokoza; anapoguswa tu anauma, au vinginevyo anaanguka chini na kupoteza mwelekeo wake, na ni kana kwamba, akipoteza umakini kidogo tu, anarudia uovu tena, au anampuuza Mungu, au anakimbia kwa baba yake nguruwe au mama yake mbwa kuendeleza mambo machafu ya miili yao. Ni kizuizi kikubwa kiasi gani! Katika kila hatua ya kazi Yake haswa, Mungu anawekwa katika majaribu, na takribani kila hatua inaleta hatari kubwa. Maneno yake ni ya kweli na ya uaminifu, na bila uovu, lakini nani yupo tayari kuyakubali? Nani yupo tayari kutii kikamilifu? Inavunja moyo wa Mungu. Anafanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya mwanadamu, Anasongwa na wasiwasi kuhusu maisha ya mwanadamu na Anauonea huruma udhaifu wa mwanadamu. Amevumilia shida nyingi katika kila hatua ya kazi Yake, kwa kila neno Analozungumza; Yupo katikati ya mwamba na sehemu ngumu, na kufikiria juu ya udhaifu wa mwanadamu, ukaidi, utoto, na vile alivyo hatarini wakati wote … tena na tena. Nani amewahi kulijua hili? Nani anaweza kuwa na imani? Nani anaweza kufahamu? Anachukia dhambi za wanadamu daima, na ukosefu wa uti wa mgongo, mwanadamu kutokuwa na uti wa mgongo, ndiko kunamfanya kuwa na hofu juu ya hatari aliyonayo mwanadamu, na kutafakari njia zilizopo mbele ya mwanadamu; siku zote, anapoangalia maneno na matendo ya mwanadamu, je, yanamjaza huruma, hasira, na siku zote vitu hivi vinamletea maumivu moyoni Mwake. Hata hivyo, wasio na hatia wamekuwa sugu; kwa nini ni lazima Mungu siku zote afanye vitu kuwa vigumu kwao? Mwanadamu dhaifu, ameondolewa kabisa uvumilivu; kwa nini Mungu awe na hasira isiyopungua kwa mwanadamu? Mwanadamu aliye dhaifu na asiye na nguvu hana tena uzima hata kidogo; kwa nini Mungu anamkaripia siku zote kwa ukaidi wake? Nani anayeweza kuhimili matishio ya Mungu mbinguni? Hata hivyo, mwanadamu ni dhaifu, na yupo katika dhiki sana, Mungu ameisukuma hasira Yake ndani kabisa moyoni Mwake, ili kwamba mwanadamu ajiakisi mwenyewe taratibu. Ilhali mwanadamu, aliyepo katika matatizo makubwa, hazingatii hata kidogo mapenzi ya Mungu; amedondoshwa miguuni na mfalme mzee wa pepo, na bado haelewi kabisa, siku zote anajiweka dhidi ya Mungu, au si moto wala baridi kwa Mungu. Mungu amezungumza maneno mengi sana, lakini nani ambaye ameyazingatia? Mwanadamu haelewi maneno ya Mungu, lakini bado hashtuki, bila kuwa na shauku, na hajawahi kuelewa kabisa hulka ya ibilisi wa kale. Watu wanaishi Kuzimu, lakini wanaamini wanaishi katika kasri la chini ya bahari; wanateswa na joka kuu jekundu, lakini bado wanadhani “wamependelewa”[20] na nchi ya joka; wanadhihakiwa na ibilisi lakini wanadhani wanafurahia ustadi wa hali ya juu wa mwili. Ni wachafu kiasi gani, ni mafidhuli kiasi gani! Mwanadamu amekutana na bahati mbaya, lakini haijui, na katika jamii hii ya giza anapatwa na ajali baada ya ajali,[21] lakini bado hajazinduka katika hili. Ni lini atakapoachana na wema wake wa kibinafsi na tabia ya mawazo ya kiutumwa? Kwa nini hajali moyo wa Mungu kiasi hicho? Je, anajifanya haoni ukandamizaji na shida hii? Je, hatamani kuwe na siku ambayo atabadilisha giza kuwa nuru? Je, hatamani zaidi kuponya uonevu dhidi ya haki na ukweli? Je, yupo tayari kutazama tu bila kufanya chochote watu wakitupilia mbali ukweli na kupindua ukweli? Je, anafurahia kuendelea kuvumilia matendo haya mabaya? Je, yupo radhi kuwa mtumwa? Je, yupo tayari kuangamia mkononi mwa Mungu pamoja na mali za taifa hili lililoanguka? Azma yako ipo wapi? Malengo yako yapo wapi? Heshima yako ipo wapi? Maadili yako yapo wapi? Uhuru wako upo wapi? Je, uko tayari kutoa maisha yako yote[22] kwa ajili ya joka kuu jekundu, mfalme wa pepo? Je, unafurahi kumwacha akutese hadi kufa? Kina chake ni vurugu na giza, mtu wa kawaida, anayeteseka na mateso kama hayo, analalamika bila kupumzika. Ni lini mwanadamu ataweza kunyanyua kichwa chake juu? Mwanadamu amekuwa kimbaumbau na amekonda, anawezaje kuridhika na ibilisi huyu katili na dikteta? Kwa nini asiyatoe maisha yake kwa Mungu mapema awezavyo? Kwa nini bado anayumbayumba, ni lini atamaliza kazi ya Mungu? Hivyo anaonewa na kunyanyaswa bila sababu yoyote, maisha yake yote hatimaye yatakuwa bure; kwa nini ana haraka hivyo ya kufika, na haraka hiyo ya kuondoka? Kwa nini hahifadhi kitu kizuri cha kumpa Mungu? Je, amesahau milenia ya chuki?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili

25. Tamaduni za asili na mitazamo ya kiakili madhubuti vimeweka kivuli katika roho safi na ya kitoto ya mwanadamu, vimeshambulia roho ya mwanadamu bila ubinadamu hata kidogo kana kwamba anaondolewa hisia na hali yoyote ya nafsi. Mbinu za mashetani hawa ni za kikatili kupita kiasi, na ni kana kwamba “elimu” na “malezi” vimekuwa ni njia za kitamaduni ambazo kwazo mfalme wa mashetani anamchinja mwanadamu; kwa kutumia “mafundisho yake ya kina” anafunika kabisa roho yake mbaya, akivaa mavazi ya kondoo ili kupata imani ya mwanadamu na halafu kusubiri mwanadamu akiwa amelala na kummeza kabisa. Masikini binadamu—wangewezaje kujua kwamba nchi ambayo kwayo wamelelewa ni nchi ya Shetani, kwamba aliyewalea kimsingi ni adui ambaye anawaumiza. Lakini bado mwanadamu hazinduki kabisa; baada ya kushibisha hasira na kiu chake, anajiandaa kulipa “wema” wa wazazi wake kwa kumlea. Hivyo ndivyo mwanadamu alivyo. Leo, bado hajui kwamba “mfalme” ambaye alimlea ni adui yake. Nchi imechafuliwa na mifupa ya wafu, Shetani anafanya wazimu bila kutulia, na anaendelea kumeza mwili wa mwanadamu huko “kuzimu,” akishiriki kaburi pamoja na mifupa ya wanadamu na akijaribu waziwazi kuwamaliza masalia wa mwisho wa mwili wa mwanadamu uliobakia matambara. Lakini mwanadamu bado ni mjinga, na hajawahi kumchukulia Shetani kama adui yake, lakini badala yake anamtumikia kwa moyo wake wote. Watu kama hao waliokengeuka hawawezi kumjua Mungu. Ni rahisi kwa Mungu kuwa mwili na kuja miongoni mwa wanadamu, Akitekeleza kazi Zake zote za wokovu? Mwanadamu, ambaye tayari amekwishajiingiza Kuzimu, anawezaje kukidhi matakwa ya Mungu?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (9)” katika Neno Laonekana katika Mwili

26. Mungu amevumilia sana kulala bila kupata usingizi kwa ajili ya kazi ya binadamu. Kutoka vina vya juu hadi vya chini, Amepanda kwenda katika kuzimu ambapo mwanadamu anaishi kupitisha siku Zake na mwanadamu, hajawahi kulalamikia uchakavu walionao wanadamu, hajawahi kumlaumu kwa ukaidi wake, lakini Anavumilia mateso makuu kadri Anavyofanya kazi Yake. Inawezekanaje Mungu awe wa kuzimu? Inawezekanaje Aishi maisha Yake kuzimu? Lakini kwa ajili ya binadamu wote, ili binadamu wote waweze kupata pumziko mapema zaidi, Amestahimili fedheha na kupitia udhalimu kuja duniani, na Aliingia mwenyewe “jahanamu” na “kuzimu,” katika tundu la duma, kumwokoa mwanadamu. Mwanadamu amestahili vipi kumpinga Mungu? Ana sababu gani tena ya kumlaumu Mungu? Anawezaje kuwa na ujasiri wa kumwangalia Mungu tena? Mungu wa mbinguni Amekuja katika nchi hii chafu zaidi ya uovu, na Hajawahi kutangaza manung’uniko au malalamiko Yake kuhusu mwanadamu, lakini badala yake Anakubali kimyakimya maangamizi[23] na ukandamizaji wa mwanadamu. Kamwe Hajawahi kujibu matakwa ya mwanadamu yasiyokuwa na msingi, hajawahi kutaka mambo mengi yanayomuelemea mwanadamu, na hajawahi kumwekea mwanadamu matakwa yasiyokuwa na msingi; Anafanya tu kazi ambazo mwanadamu alitakiwa kufanya bila malalamiko: kufundisha, kutia mwanga, kukaripia, usafishaji wa maneno, kukumbusha, kusihi, kufariji, kuhukumu na kufunua. Ni hatua gani Alizozichukua ambazo si kwa ajili ya maisha ya mwanadamu? Ingawa Ameondoa matarajio na majaliwa ya mwanadamu, ni hatua zipi zilizochukuliwa na Mungu ambazo hazikuwa kwa ajili ya majaliwa ya mwanadamu? Ni ipi kati ya hatua hizo ambayo haijawahi kuwa kwa ajili ya mwanadamu kuendelea kuishi? Ni ipi kati ya hatua hizo haikuwepo kwa ajili ya kumweka mwanadamu huru dhidi ya mateso na minyanyaso ya nguvu za giza ambazo ni nyeusi kama usiku? Ni ipi kati ya hatua hizo si kwa ajili ya mwanadamu? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu, ambao ni sawa na mama mwenye mapenzi? Ni nani awezaye kuujua moyo wa Mungu wenye shauku? Moyo wa upendo na matarajio ya shauku ya Mungu vimelipwa kwa mioyo ya baridi, na usugu, na macho yanayoonyesha kutojali, kwa makaripio ya kujirudia na matusi ya mwanadamu, kwa maneno ya mkato na dhihaka na udhalilishaji, vimelipwa kwa dhihaka ya mwanadamu, kwa kukanyagwa na kukataliwa, kwa kutokuwa na ufahamu, na kupiga kite, na farakano, na uepukaji, kwa uongo, mashambulizi na ukali. Maneno ya wema ya Mungu yamekutana na nyuso kali na ufidhuli wa vidole elfu moja vinavyotikisika. Mungu anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa.[24] Ni idadi gani ya miezi na jua, ni mara ngapi Amekabiliana na nyota, ni mara ngapi Ameondoka alfajiri na kurudi jioni, na kurushwarushwa na kugeuzwa, Akivumilia maumivu makubwa mara elfu moja kuliko maumivu Aliyoyapata Alipokuwa Anaondoka kwa Baba Yake, Akivumilia mashambulizi na “kuvunja” kwa mwanadamu, na “kumshughulikia” na “kumpogoa” mwanadamu. Unyenyekevu na kufichika kwa Mungu vimelipwa kwa upendeleo[25] wa mwanadamu, kwa mitazamo na vitendo vya mwanadamu visivyokuwa vya haki, na kutojulikana Kwake, ustahimilivu, na uvumilivu vimelipizwa kwa jicho la tamaa la mwanadamu, mwanadamu hujaribu kumkanyaga Mungu hadi afe, bila majuto, na anajaribu kumkanyagia Mungu ardhini. Mtazamo wa mwanadamu kwa namna anavyomtendea Mungu ni wa “ujanja adimu,” na Mungu ambaye Anachokozwa na kutwezwa na mwanadamu, Anakanyagwa na kuwa bapa kwa miguu ya makumi elfu ya watu wakati mwanadamu mwenyewe anasimama juu kabisa, kana kwamba angeweza kuwa “mfalme wa kasri,” kana kwamba anataka kuchukua mamlaka kamili,[26] “kuendesha mahakama akiwa nyuma ya skrini,” kumfanya Mungu kuwa makini na mwenye kanuni “mwongozaji nyuma ya matukio,” ambaye haruhusiwi kupigana au kusababisha shida; lazima Mungu achukue nafasi ya “Mtawala wa Mwisho,” ni lazima Awe “kibaraka,”[27] bila uhuru wote. Matendo ya mwanadamu hayasemeki, sasa ana sifa gani ya kutaka hili au lile kuhusu Mungu? Ana sifa gani ya kutoa mapendekezo kwa Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kumtaka Mungu amhurumie juu ya udhaifu wake? Anafaa kwa kiasi gani kupokea huruma ya Mungu? Anafaa kwa kiasi gani kupokea ukarimu wa Mungu kila mara? Anafaa kwa kiasi gani kupokea msamaha wa Mungu kila mara? Dhamiri yake ipo wapi? Alivunja moyo wa Mungu muda mrefu uliopita, ni muda mrefu toka ameuacha moyo wa Mungu katika vipande. Mungu alikuja miongoni mwa wanadamu Akiwa na nguvu nyingi na mwenye shauku kubwa, Akitegemea kwamba mwanadamu atakuwa mkarimu Kwake, hata kama ni kwa wema kiasi kidogo tu. Bado moyo wa Mungu haujafarijiwa na mwanadamu, yote Aliyoyapokea ni mashambulizi na mateso ya kuongezeka haraka;[28] moyo wa mwanadamu ni wenye tamaa sana, tamaa yake ni kubwa sana, hawezi akatosheka, siku zote ni mwenye fitina na jasiri pasi busara, hawezi kamwe kumpatia Mungu uhuru au haki ya kuzungumza, na anamwacha Mungu bila budi ila kukubali unyanyasaji, na kumruhusu mwanadamu kumtawala vyovyote apendavyo.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (9)” katika Neno Laonekana katika Mwili

27. Tangu uumbaji hadi leo, Mungu amestahimili maumivu mengi sana, na kupata mashambulizi mengi sana. Ilhali hata leo, bado mwanadamu hayalegezi matakwa yake kwa Mungu kwa urahisi, bado anamchunguza Mungu, bado hana uvumilivu Naye, na anachofanya ni kumpatia “ushauri,” na “kumkosoa,” na “kumfundisha nidhamu” kana kwamba Mungu atapotoka njia, kwamba Mungu duniani ni hayawani na Hana busara, au Atafanya fujo, au kwamba Hatafanya kitu chochote cha maana. Mwanadamu siku zote huwa na mtazamo wa aina hii kwa Mungu. Inawezekanaje isimhuzunishe Mungu? Kwa kuwa mwili, Mungu amevumilia maumivu na mateso mengi; ni vibaya kiasi gani, kumfanya Mungu akubali mafundisho ya mwanadamu? Kuwasili kwake miongoni mwa wanadamu kumemvua uhuru wote, kama vile Amefungwa Kuzimu, na Amekubali “uchunguzi” wa mwanadamu bila upinzani hata kidogo. Hii sio aibu? Katika kuja miongoni mwa familia ya wanadamu wa kawaida, Yesu amepitia uonevu mkubwa. Na kinachoumiza zaidi ni kwamba Amekuja katika ulimwengu huu wa vumbi na kujinyenyekeza Mwenyewe katika hadhi ya chini kabisa, na Amechukua mwili wa kawaida kabisa. Kwa binadamu kuwa mwembamba, je, Mungu Mwenyezi hapati shida? Je, na hii yote si kwa ajili ya binadamu? Kuna wakati wowote ambapo alikuwa Anajifikiria Mwenyewe? Baada ya kukataliwa na kuuawa na Wayahudi, na kukejeliwa na kudhihakiwa na watu, Hajawahi kulalamika mbinguni au kupinga duniani. Leo, janga hili lenye umri wa milenia limetokea tena miongoni mwa watu hawa wanaofanana na Wayahudi. Je, hawafanyi dhambi ile ile? Nini kinamfanya mwanadamu kuwa na sifa ya kupokea ahadi za Mungu? Je, hampingi Mungu na kisha kukubali baraka Zake? Kwa nini haifikii haki, au kutafuta ukweli? Kwa nini havutiwi na kile ambacho Mungu anafanya? Haki yake iko wapi? Usawa wake uko wapi? Je, ana ujasiri wa kumwakilisha Mungu? Ziko wapi fahamu zake za haki? Ni kiasi gani ambacho kile kinachopendwa na mwanadamu ndicho kile kinachopendwa na Mungu? Mwanadamu hawezi kutambua tofauti muhimu,[29] siku zote anachanganya kati ya nyeusi na nyeupe,[30] anakandamiza haki na ukweli, na anashikilia kutokuwa na haki wala usawa kwa kiwango kikubwa. Anafukuzia mbali mwanga na anarukaruka gizani. Wale wanaotafuta ukweli na haki badala yake wanafukuza mwanga, wale wanaomtafuta Mungu wanamkanyaga kwa miguu yao, na wanajipandisha angani. Mwanadamu hana tofauti na gaidi.[31] Sababu yake iko wapi? Nani anaweza kutofautisha kati ya jema na baya? Nani anaweza kushikilia haki? Nani yuko tayari kuteseka kwa ajili ya ukweli? Watu ni waovu na wana tabia za kishetani kabisa! Baada ya kumwangika Mungu msalabani wanapiga makofi na kufurahi, vilio vyao havikomi. Wako kama kuku na mbwa, wanashirikiana na kula njama, wameanzisha ufalme wao, udukuzi wao haujaachwa bila kusumbuliwa, wanafumba macho yao na kulia kwa maumivu makali zaidi na zaidi, wote wameungana pamoja, na hali ya kuvurugika imeenea kote, ni harakaharaka na hai, na wale ambao wanajishikamanisha kwa wengine kijinga wanazidi kuibuka, wote wakiwa wameshikilia majina “mashuhuri” ya mababu zao. Hawa mbwa na kuku wamemweka Mungu mbali na akili zao, na hawajawahi kuzingatia kabisa hali ya moyo wa Mungu. Si ajabu kwamba Mungu anasema mwanadamu ni kama mbwa au kuku, mbwa anayebweka anayewafanya mia wengine kutoa mlio mkali; kwa nia hii, kwa makelele mengi ameileta kazi ya Mungu katika siku ya leo, bila kujali kazi ya Mungu ni ya namna gani, bila kujali kuna haki, bila kujali Mungu ana nafasi Yake ya kuweka miguu Yake, bila kujali kesho itakuwaje, uduni wake, na hali yake ya kuwa mchafu. Mwanadamu hajawahi kufikiria juu ya mambo kiasi hicho, hajawahi kuhofia kesho, na amekusanya yale yote ambayo ni ya manufaa na ya thamani na kuyakumbatia, na bila kumwachia Mungu chochote isipokuwa mabaki na makombo.[32] Binadamu ni katili kiasi gani! Hana hisia hata kidogo kwa Mungu, na baada ya kuteketeza kila kitu cha Mungu, anamrusha Mungu nyuma yake na kuacha kujali kabisa kuhusu uwepo wake. Anamfurahia Mungu, halafu anampinga Mungu, na anamkanyagia chini ya miguu yake, wakati mdomoni mwake anamshukuru na kumsifu Mungu; anamwomba Mungu, na anamtegemea Mungu, wakati huo pia anamdanganya Mungu; “analiinua” jina la Mungu, na kuutazama uso wa Mungu, halafu pia bila haya na bila kuwa na aibu anakaa katika kiti cha enzi cha Mungu na “kuhukumu” “udhalimu” wa Mungu; kutoka katika kinywa chake yanatoka maneno haya “anapaswa kumshukuru Mungu,” na anatazama katika maneno ya Mungu, halafu katika moyo wake anavurumisha shutuma kwa Mungu; ni “mvumilivu” kwa Mungu halafu anamkandamiza Mungu, na kinywa chake kinasema ni “kwa ajili ya Mungu”; mikononi mwake ameshikilia vitu vya Mungu, na kinywani mwake anatafuna chakula ambacho Mungu amempatia, bado macho yake yanamtazama Mungu yakiwa hayana hisia kabisa, kana kwamba anatamani kummeza; anautazama ukweli lakini anasisitiza kuwa ni hila za Shetani; anatazama haki lakini analazimisha iwe kujikana nafsi; anatazama matendo ya mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni kile Mungu alicho; anatazama karama za asili za mwanadamu lakini anasisitiza kuwa ni ukweli; anatazama matendo ya Mungu lakini anasisitiza kuwa ni kiburi na majivuno, majigambo na haki binafsi; mwanadamu anapomwangalia Mungu anasisitiza kumpachika uanadamu, na anajitahidi sana kumweka katika kiti cha kiumbe aliyeumbwa akishirikiana na Shetani; anajua kweli kabisa ni matamshi ya Mungu, bado atasema si kitu chochote zaidi ya maandiko ya mwanadamu; anajua kabisa kwamba Roho anatambulika katika mwili, Mungu anakuwa mwili, lakini anasema mwili huu ni uzao wa Shetani; anajua kikamilifu kuwa Mungu ni mnyenyekevu na hajionyeshi, lakini anasema kwamba Shetani ameaibishwa na Mungu ameshinda. Uzuri wa bure ulioje! Mwanadamu hata hafai kuwa mbwa mlinzi! Hawezi kutofautisha kati ya nyeusi na nyeupe, na hata anachanganya kwa makusudi nyeusi ndani ya nyeupe. Je, nguvu za mwanadamu na husuru ya mwanadamu vinaweza kustahimili siku ya ukombozi wa Mungu? Baada ya kumpinga Mungu kwa kukusudia, mwanadamu hakuweza kujali sana, au hata kwenda mbali sana na kumuua, asimpatie Mungu nafasi ya kujionyesha Mwenyewe. Haki iko wapi? Upendo uko wapi? Anakaa kando ya Mungu na kumsukuma Mungu apige magoti ili Aombe msamaha, kutii mipango yake yote, kuridhia hila zake zote, na anamfanya Mungu kuchukua ishara Zake zote kutoka Kwake, la sivyo anaghadhibishwa[33] na kupandwa na hasira. Inawezekanaje Mungu asiwe na maumivu katika ushawishi huo wa giza, ambao unachanganya nyeusi kuwa nyeupe? Angewezaje kukosa kuwa na wasiwasi? Kwa nini inasemwa kwamba Mungu alipoanza kazi yake ya hivi karibuni kabisa, ilikuwa kama alfajiri ya mwanzo mpya? Matendo ya mwanadamu “yana utajiri,” ni “chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima” bila kukoma “yanajaza tena” shamba la moyo wa mwanadamu, wakati “chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima” ya mwanadamu “inashindana” na Mungu bila haya;[34] wawili hawa hawapatani, na anawapa watu vitu kwa niaba ya Mungu bila hofu ya kuadhibiwa wala kuumia, wakati mwanadamu anashirikiana naye bila kujali hatari iliyopo. Na kwa athari gani? Anamtupilia mbali Mungu upande mmoja, na kumweka mbali sana, ambapo watu hawatamzingatia, akiogopa sana kwamba Atavuta usikivu wake, na anaogopa sana kwamba chemchemi isiyokoma ya maji ya uzima ya Mungu itamteka mwanadamu, na kumpata mwanadamu. Hivyo, baada ya kupitia uzoefu wa miaka mingi wa masuala ya kidunia, anakula njama dhidi ya Mungu, na hata anamfanya Mungu kuwa mlengwa wa “adhabu.” Ni kana kwamba Mungu amekuwa gogo machoni mwake, na anatamani kumnyakua Mungu na kumweka motoni ili Atakaswe na kusafishwa. Mwanadamu anapoona mahangaiko ya Mungu, anapiga kifua chake na kucheka, anacheza kwa furaha, na kusema kwamba Mungu pia Amewekwa motoni, na anasema kwamba atausafisha uchafu wa Mungu, kana kwamba hili ni la urazini na lina maana, kana kwamba hizi tu ndizo njia za haki na zenye mantiki za Mbinguni. Tabia hii ya fujo ya mwanadamu inaonekana kuwa ni ya makusudi na ya kutofahamu. Mwanadamu anafichua uso wake mbaya na roho yake mbaya, vilevile sura ya kusikitisha ya ombaomba; baada ya kufanya ghasia sana, anavaa sura ya kuhurumiwa na kuomba msamaha wa Mbingu, akifanana na udongo wa kufinyangwa. Mwanadamu siku zote hutenda kwa namna asiyotarajiwa, siku zote “anamwendesha duma kuwatisha wengine,”[b] siku zote yeye huigiza, hajali hata kidogo moyo wa Mungu, wala halinganishi hadhi yake mwenyewe. Kimyakimya anampinga Mungu, kana kwamba Mungu amemkosea, na Hapaswi kumtendea hivyo, na kana kwamba Mbingu haina macho na inafanya kwa makusudi mambo kuwa magumu kwake. Hivyo mwanadamu anapanga njama za siri, na hajali matakwa ya Mungu hata kidogo, anatazama kwa macho ya mnyama mkali, anatazama kwa hasira kila kitu Anachokifanya Mungu, hafikirii kwamba yeye ni adui ya Mungu, na ana matumaini kwamba siku itakuja ambapo Mungu atautawanya umande na kuviweka vitu wazi, na kumwokoa kutoka katika “kinywa cha duma” na kulipiza kisasa kwa niaba yake. Hata leo, watu bado hawafikiri kwamba wanatekeleza jukumu la kumpinga Mungu, jukumu ambalo limefanywa kwa enzi nyingi sana, wangewezaje kujua kwamba, katika yote wanayofanya, wamepotoka tangu zamani sana, kwamba yote waliyoyaelewa yamemezwa na bahari zamani sana.

Ni nani amewahi kukubali ukweli? Ni nani amewahi kumkaribisha Mungu kwa mikono yote? Nani amewahi kutamani uwepo wa Mungu? Tabia ya mwanadamu imeoza tangu zamani sana, na unajisi wake umefanya hekalu la Mungu lisitambulike tangu zamani sana. Mwanadamu, wakati akiendelea kufanya kazi yake, amekuwa akimdharau Mungu. Ni kana kwamba upinzani wake kwa Mungu umeandikwa kwenye jiwe, na haubadiliki, na matokeo yake ni bora alaaniwe kuliko kuendelea kuteseka “kwa kufanyiwa vibaya” na maneno na matendo yake. Inakuwaje watu kama hawa wamjue Mungu? Wanawezaje kupata pumziko kwa Mungu? Na wanawezaje kufaa kuja mbele za Mungu?

kutoka katika “Kazi na Kuingia (9)” katika Neno Laonekana katika Mwili

28. Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu. Kazi ya Mungu imefikia upeo wake—na, kufuatia, “kuingia” kwa mwanadamu[35] pia kumefikia kilele chake. Mungu amejishusha kwa kadiri Anavyoweza, na kamwe Hajawahi kuwalalamikia wanadamu au vitu vyote katika ulimwengu. Mwanadamu, wakati ule ule, anasimama juu ya kichwa cha Mungu, akimnyanyasa hadi kilele; yote yamefikia kilele chake, ni wakati wa siku ambapo haki inaonekana. Kwa nini uendelee kuacha huzuni iifunike nchi, na giza kuwavaa watu wote? Mungu ameangalia kwa miaka elfu kadhaa—kwa makumi ya maelfu ya miaka, hata—na uvumilivu Wake umekwisha kufikia kikomo chake. Amekuwa akiangalia kila hatua za wanadamu, Amekuwa akiangalia kwa makini jinsi udhalimu wa mwanadamu utafanya fujo, na bado mwanadamu, ambaye amekuwa wa kutojali kwa muda mrefu, hahisi chochote. Na ni nani aliyewahi kuangalia kwa makini matendo ya Mungu? Nani aliyewahi kuinua macho yake na kutazama mbali sana? Nani aliyewahi kusikiliza kwa makini? Nani aliyewahi kuwa mikononi mwa Mwenyezi? Watu wote wanakerwa na hofu za kubuni[36]. Je, kuna faida gani kwa rundo la nyasi kavu na majani makavu? Kitu pekee wanachoweza kufanya ni kumtesa Mungu aliye hai, Aliyepata mwili hadi kifo. Ingawa wao ni mafungu tu ya nyasi kavu na majani makavu, bado kuna kitu kimoja ambacho wao hufanya “bora zaidi”:[37] kumtesa Mungu hadi kifo Akiwa hai na kisha kulia kwamba “hilo hufurahisha mioyo ya watu.” Kikundi cha jeshi lisilofaa kabisa! La ajabu, katikati ya mkondo usiokwisha wa watu, wao hulenga uangalifu wao juu ya Mungu, wakimzunguka Yeye na zingio lisilopenyeka. Hamasa yao daima ikiwaka moto zaidi,[38] wamemzunguka Mungu katika vikundi, ili Asiweze kusonga hata kidogo. Katika mikono yao, wanashikilia kila aina ya silaha, na kumtazama Mungu kana kwamba wanamwangalia adui, macho yao yakiwa yamejaa hasira; wana hamu ya “kumshambulia Mungu kwa nguvu.” Inafaidi kweli: Kwa nini mwanadamu na Mungu wamekuwa maadui wasioweza kupatanishwa? Inawezekana kwamba kuna chuki ya muda mrefu sana kati ya Mungu wa upendo sana na mwanadamu? Inawezekana kwamba matendo ya Mungu hayana faida kwa mwanadamu? Je, hayo humdhuru mwanadamu? Mtu hulenga jicho la hasira lisiloyumba juu ya Mungu, akiogopa sana kwamba Atapasua zingio la mwanadamu, Arudi mpaka mbingu ya tatu, na mara nyingine tena Amtupe mwanadamu ndani ya gereza. Mwanadamu anajihadhari na Mungu, yeye ni mwenye wasiwasi, na hufurukuta toka upande mmoja hadi upande mwingine wa ardhi kwa mbali, akishikilia “bombomu” ambayo inamlenga Mungu kati ya wanadamu. Ni kana kwamba, Mungu akijitikisa kidogo tu, mwanadamu atafuta kila kitu Chake—mwili Wake wote na yote Anayovaa—bila kuacha kitu chochote. Uhusiano kati ya Mungu na mwanadamu hauwezi kurekebishwa. Mungu haeleweki kwa mwanadamu; mwanadamu, wakati ule ule, huyafunga macho yake kwa makusudi na kuchezacheza, asiyetaka kabisa kuona kuwepo Kwangu, na kutosamehe hukumu Yangu. Hivyo, wakati mtu hatarajii, Mimi huondoka kimya kimya, na Sitaweza tena kulinganisha nani aliye juu na nani aliye chini na mwanadamu. Wanadamu ni “wanyama” wa chini zaidi kuliko wote na Sitamani kumsikiliza tena. Kwa muda mrefu Nimerudisha neema Yangu yote mahali ambapo Mimi hukaa kwa amani; kwa kuwa mwanadamu ni mkaidi sana, ana sababu gani kufurahia zaidi neema Yangu ya thamani mno? Mimi siko tayari kutoa neema Yangu bure juu ya nguvu zilizo na uhasama Kwangu. Ningetoa matunda Yangu ya thamani juu ya wale wakulima wa Kanaani ambao ni wenye ari, na wanakaribisha kwa dhati kurudi Kwangu. Napenda tu mbingu ziendelee milele, na, zaidi ya hayo, mwanadamu asizeeke kamwe, mbingu na mwanadamu viwe vitulivu daima, na ile “misonobari na mivinje” iliyo na rangi ya kijani daima iandamane na Mungu, na daima iandamane na mbingu katika kuingia kwenye enzi kamilifu pamoja.

kutoka katika “Kazi na Kuingia (10)” katika Neno Laonekana katika Mwili

29. Hali ya Mungu kupata mwili imesababisha mawimbi mazito katika dini na madhehebu yote, “imeparaganya” mpangilio wa awali wa jamii ya kidini, na imetikisa mioyo ya wale wanaotamani sana kujitokeza kwa Mungu. Ni nani asiyeabudu? Nani hatamani kumwona Mungu? Mungu amekuwa miongoni mwa wanadamu kwa miaka mingi sana, lakini mwanadamu kamwe hajawahi kutambua. Leo, Mungu Mwenyewe amejitokeza, na Ameonyesha utambulisho Wake kwa watu—inawezekanaje hii isiupatie moyo wa mwanadamu furaha? Mungu aliwahi kushiriki furaha na huzuni pamoja na mwanadamu, na leo Ameunganika tena na mwanadamu, na kushiriki visa vya muda uliopita pamoja naye. Baada ya kutoka Uyahudi, watu hawakuweza kupata alama Yake yoyote. Wanatamani kukutana tena na Mungu, bila kujua kwamba leo wamekutana Naye tena, na kuungana Naye tena. Inawezekanaje hii isiamshe mawazo ya jana? Siku kama ya leo miaka elfu mbili iliyopita, Simoni wa Yona, uzao wa Wayahudi, alimtazama Yesu Mwokozi, alikula meza moja pamoja Naye, na baada ya kumfuata kwa miaka mingi alihisi kumpenda sana: Alimpenda sana kwa dhati, alimpenda sana Bwana Yesu. Watu wa Uyahudi hawakujua chochote kuhusu vile mtoto huyu mwenye nywele za dhahabu, Aliyezaliwa katika hori la ng’ombe, Alikuwa ni sura ya kwanza ya Mungu kupata mwili. Wote walidhani kwamba Alikuwa ni mmoja wao, hakuna aliyedhani kwamba Yupo tofauti nao—watu wangewezaje kumtambua Yesu wa kawaida kabisa? Watu wa Uyahudi walidhani kwamba alikuwa ni mtoto wa Kiyahudi wa wakati huo. Hakuna aliyemtazama kama Mungu mwenye upendo, na watu hawakufanya chochote isipokuwa kufanya maombi bila kutambua, wakiomba Awape neema nyingi na maradufu, na amani, na furaha. Walijua tu kwamba, kama milionea, Alikuwa na kila kitu ambacho mtu angetamani kuwa nacho. Lakini watu hawakumchukulia kama mtu ambaye Alikuwa mpendwa; watu wa wakati huo hawakumpenda, na walimpinga tu, na walifanya maombi Kwake yasiyokuwa na mantiki, na Hakuwahi kupinga, Aliendelea kutoa neema kwa mwanadamu, ingawa mwanadamu hakumjua. Hakufanya chochote isipokuwa kwa kimya kumpatia mwanadamu wema, upendo, na huruma, na zaidi, Alimpatia mwanadamu njia mpya ya kutenda, kumwongoza mwanadamu kutoka katika vifungo vya sheria. Mwanadamu hakumpenda, alimhusudu tu na kutambua “talanta Zake za kipekee.” Inawezekanaje mwanadamu kipofu kujua jinsi Yesu Mwokozi alipitia mateso makubwa Alipokuja miongoni mwa wanadamu? Hakuna aliyejali shida Zake, hakuna mtu aliyejua upendo Wake kwa Mungu Baba, na hakuna ambaye angejua upweke Wake; ingawa Maria alikuwa mama Yake wa kumzaa, angewezaje kujua mawazo yaliyopo moyoni mwa Bwana Yesu mwenye huruma? Nani alijua mateso yasiyoweza kutamkika Aliyoyapitia Mwana wa Adamu? Baada ya kumwomba watu wa kipindi hicho walimweka nyuma ya akili zao, na kumtupa nje Akizungukazunguka mitaani, siku baada ya siku, mwaka baada ya mwaka, na kwenda bila mwelekeo kwa miaka mingi hadi Alipofikisha miaka thelathini na mitatu, miaka ambayo ilikuwa mirefu pia mifupi. Watu walipomhitaji, walimwalika nyumbani mwao wakiwa na nyuso za tabasamu, wakijaribu kumwomba kitu—na baada ya kuwa Ametoa mchango wake kwao, walimsukuma mara moja nje ya mlango. Watu walikula kile Alichokitoa mdomoni Mwake, walikunywa damu Yake, walifurahia neema Aliyowapatia, lakini bado walimpinga, maana hawakujua nani aliwapa uhai walionao. Hatimaye, walimsulubisha msalabani, lakini bado Hakutoa hata sauti. Hata leo, bado Anabakia kimya. Watu wanakula mwili wake, wanakula chakula Anachowatengenezea, wanapita njia ambayo Ameifungua kwa ajili yao, na wanakunywa damu Yake, lakini bado wanakusudia kumkataa, kimsingi wanamchukulia Mungu ambaye Amewapatia maisha yao kama adui, na badala yake wanawachukulia wale ambao ni watumwa kama wao kama Anavyofanya Baba wa mbinguni. Katika hili, je, hawampingi kwa makusudi? Yesu aliwezaje kufa msalabani? Je, mnajua? Je, Hakusalitiwa na Yuda, ambaye alikuwa karibu kabisa Naye, na akamla, akamnywa, na akamfurahia? Je, sababu ya usaliti wa Yuda haikuwa ni kwa sababu Yesu hakuwa kitu chochote isipokuwa mwalimu mdogo wa kawaida? Ikiwa watu walikuwa wameona kwamba Yesu alikuwa si wa kawaida kabisa, na Ambaye Alitoka mbinguni, wangewezaje kumsulubisha msalabani Akiwa hai kwa masaa ishirini na nne, hadi Alipoishiwa na pumzi yote katika mwili wake? Nani awezaye kumjua Mungu? Watu hawafanyi chochote isipokuwa kumfurahia Mungu kwa tamaa isiyotosheka, lakini hawajawahi kumjua. Walipewa inchi na wamechukua maili, na wanamfanya Yesu kutii kabisa amri zao, na maelekezo yao. Ni nani ambaye ameonyesha huruma kwa huyu Mwana wa Adamu, Ambaye hana mahali pa kuweka kichwa Chake? Ni nani ambaye amewahi kufikiria kushikana mikono Naye kukamilisha agizo la Mungu Baba? Ni nani amewahi kumuwaza? Ni nani mbaye amewahi kuyajali matatizo Yake? Bila upendo hata kidogo, mwanadamu anamvuta nyuma na mbele; mwanadamu hajui nuru na uhai wake unatoka wapi, na hafanyi chochote isipokuwa kupanga kwa siri jinsi ya kumsulubisha tena Yesu wa miaka elfu mbili iliyopita, nani ambaye amepitia uzoefu wa maumivu miongoni mwa wanadamu. Je, Yesu anawatia watu moyo kuwa na chuki ya namna hiyo? Je, yote Aliyoyafanya yamesahaulika zamani? Chuki ambayo ilichanganyika kwa maelfu ya miaka itaibuka tena juu. Nyinyi vifaranga wa Wayahudi! Ni lini Yesu amekuwa adui yenu, hadi mmchukie kiasi hicho? Amefanya mengi na kuzungumza mengi—je hakuna chochote chenye manufaa kwenu? Ameyatoa maisha Yake kwenu bila kuomba kurudishiwa kitu chochote, Amejitoa mzima kwenu—kweli bado mnataka kumla Akiwa mzima? Amejitoa kwenu kikamilifu bila kuacha kitu chochote, bila kufurahia utukufu wa kidunia, wema miongoni mwa wanadamu, na upendo miongoni mwa wanadamu, au baraka zote miongoni mwa wanadamu. Watu ni wabinafsi sana Kwake, hajawahi kufurahia utajiri wote wa duniani, Amejitoa kikamilifu, moyo wa upendo wa dhati kwa mwanadamu, Amejirithisha mzima kwa mwanadamu—ni nani ambaye amemfanyia wema? Ni nani aliyewahi kumpatia faraja? Mwanadamu amemjazia mashinikizo yote, balaa yote amempatia Yeye, shida zote mbaya Alizozipitia ni mwanadamu amempatia Yeye, anamtupia lawama kwa uonevu wote, na Amezikubali kimyakimya. Je, Amewahi kumpinga mtu yeyote? Je, Amewahi kuomba fidia hata kidogo kutoka kwa mtu yeyote yule? Ni nani amewahi kumwonyesha huruma yoyote? Kama watu wa kawaida, ni nani miongoni mwenu ambaye hajawahi kuwa na kipindi cha utotoni chenye mapenzi ya dhati? Ni nani ambaye hajawahi kuwa na ujana wa kupendeza? Ni nani ambaye hana joto la wapendwa? Ni nani ambaye hana upendo wa rafiki wa karibu? Ni nani ambaye haheshimiwi na wengine? Ni nani ambaye hana familia yenye upendo? Ni nani ambaye hana faraja ya wandani wao? Je, Amekwishawahi kufurahia moja ya haya? Ni nani ambaye amewahi kumtendea wema hata kidogo? Ni nani ambaye amekwishawahi kumpatia faraja hata kidogo? Ni nani ambaye amekwishawahi kumwonyesha angalau maadili hata kidogo ya kibinadamu? Ni nani ambaye amewahi kuwa mvumilivu Kwake? Ni nani ambaye amewahi kuwa pamoja naye katika nyakati za shida? Ni nani ambaye amewahi kupitia maisha ya shida pamoja Naye? Mwanadamu bado hajaacha kumwomba Yeye; anapeleka tu maombi Kwake bila hata haya, kana kwamba kuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alipaswa kuwa ng’ombe au farasi wake, na Alipaswa kumpatia mwanadamu kila kitu chake; Asipofanya hivyo, mwanadamu hatamsamehe, hatamtendea vizuri, hatamwita Mungu, na hatamheshimu kwa kiwango cha juu. Mwanadamu ni katili sana katika mtazamo wake kwa Mungu, kana kwamba yupo ili kumtesa Mungu hadi kifo, ni baada ya hapo tu ndipo anapunguza maombi yake kwa Mungu; kama sivyo, mwanadamu hatapunguza kiwango cha matakwa yake kwa Mungu. Inawezekanaje mwanadamu kama huyu asidharauliwe na Mungu? Je, hili si janga la siku hizi? Dhamiri ya mwanadamu haionekani popote. Anasema tu atalipa upendo wa Mungu, lakini anamchanachana Mungu na kumtesa hadi kifo. Je, hii sio “mbinu ya siri” kwa imani yake kwa Mungu, iliyorithishwa kutoka kwa mababu zake? Hakuna mahali ambapo huwezi kuwakuta “Wayahudi,” na leo bado wanafanya kazi ile ile, bado wanafanya kazi ile ile ya kumpinga Mungu, na bado wanaamini kwamba wanamwinua Mungu juu? Inawezekanaje macho ya mwanadamu yamjue Mungu? Inawezekanaje mwanadamu, anayeishi katika mwili, kumchukulia Mungu kama Mungu mwenye mwili ambaye Amekuja kutoka katika Roho? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kumjua? Ukweli upo wapi miongoni mwa wanadamu? Haki ya kweli ipo wapi? Ni nani anayeweza kuijua tabia ya Mungu? Ni nani anayeweza kushindana na Mungu mbinguni? Haishangazi kwamba, Alipokuwa miongoni mwa wanadamu, hakuna aliyemjua Mungu, na amekataliwa. Inawezekanaje mwanadamu kuvumilia uwepo wa Mungu? Anawezaje kuvumilia kuruhusu mwanga kuondosha giza la ulimwengu? Je, hii yote si kujitoa kwa heshima kwa mwanadamu? Je, huku sio kuingia adilifu kwa mwanadamu? Je, kazi ya Mungu haijajikita katika kuingia kwa mwanadamu? Ningependa muunganishe kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu, na kurekebisha uhusiano kati ya mwanadamu na Mungu, na kufanya majukumu ambayo yanapaswa kufanywa na mwanadamu kwa uwezo wake wote. Kwa njia hii, kazi ya Mungu hatimaye itafikia mwisho, ikiwa ni pamoja na utukufu Wake!

kutoka katika “Kazi na Kuingia (10)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Tanbihi:

1. “Kumfinyanga mwanadamu” kunamaanisha “kumwokoa mwanadamu.”

2. “Wanashikilia kwa kung’ang’ania” inatumiwa kwa dhihaka. Kirai hiki kinaonyesha kwamba watu ni wakaidi na wasiodhibitiwa kwa urahisi, wakishikilia vitu vilivyopitwa na wakati na wasiopenda kuviachilia.

3. “Kugeuza mtazamo wake wa zamani” inahusu jinsi dhana za watu na maoni kumhusu Mungu hubadilika mara tu wanapomjua Mungu.

4. “Anajistarehesha” inaonyesha kwamba watu hawajali juu ya kazi ya Mungu na hawaioni kama muhimu.

5. “Wa karibu” inatumiwa kwa dhihaka.

6. “Wa kukubaliana” inatumiwa kwa mzaha.

7. “Wenye shaka” inaashiria kwamba watu hawana umaizi dhahiri katika kazi ya Mungu.

8. “Kutoweza kubadilishwa” imenuiwa kama tashtiti hapa, kumaanisha kwamba watu ni wagumu katika ufahamu, utamaduni na mitizamo yao ya kiroho.

9. “Huru na hajapatikana” inaonyesha kwamba shetani anapagawa na kucharuka.

10. “Hali ya shaghalabaghala kabisa” inahusu jinsi tabia ya shetani ya ukatili haivumiliki kuona.

11. “Imevilia damu na kugongwagongwa” inahusu sura mbaya ya kutisha ya mfalme wa pepo.

12. “Pambano ambalo ana nafasi ndogo sana ya kushinda” ni istiara ya mipango mibaya ya shetani yenye kudhuru kwa siri, ya uovu. Inatumiwa kwa dhihaka.

13. “Kummaliza” inahusu tabia ya kidhalimu ya mfalme wa pepo, ambaye huwaangamiza watu wote.

14. “Washiriki jinai” ni wa namna moja na “kundi la majambazi.”

15. “Kuchochea vurugu” inahusu jinsi watu ambao wana pepo husababisha ghasia, kuzuia na kuipinga kazi ya Mungu.

16. “Nyangumi mwenye meno” imetumiwa kwa dhihaka. Ni istiara ya jinsi nzi ni wadogo sana kiasi kwamba nguruwe na mbwa huonekana wakubwa kama nyangumi kwao.

17. “Kiongozi wa uovu wote” inahusu ibilisi mkongwe. Kirai hiki kinaonyesha kutopenda kabisa.

18. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.

19. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.

20. “Wamependelewa” inatumiwa kuwadhihaki watu wanaoonekana wagumu na hawajitambui.

21. “Anapatwa na ajali baada ya ajali” inaonyesha kuwa watu walizaliwa katika nchi ya joka kubwa jekundu, na hawawezi kuwa na ujasiri.

22. “Kutoa maisha yako yote” imetumika kwa namna ya kimatusi.

23. “Maangamizi” inatumiwa kuweka wazi kutotii kwa wanadamu.

24. “Anaweza tu kustahimili, Akiwa Ameinamisha kichwa, Akiwahudumia watu kama ng’ombe aliye radhi kufungwa” ni kwa asili sentensi moja, lakini hapa imegawanywa mara mbili ili kuyafanya mambo wazi zaidi. Sentensi ya kwanza inahusu matendo ya mwanadamu, huku ya pili inaonyesha mateso aliyoyapitia Mungu, na kwamba Mungu ni mnyenyekevu na Aliyefichika.

25. “Upendeleo” unahusu tabia ya watu ya ukaidi.

26. “Kuchukua mamlaka kamili” inahusu tabia ya watu ya ukaidi. Wanajitukuza, huwafunga wengine, wakiwafanya wawafuate na kuteseka kwa ajili yao. Wao ni majeshi ambayo ni ya uadui kwa Mungu.

27. “Kibaraka” inatumiwa kuwadhihaki wale ambao hawamjui Mungu.

28. “Kuongezeka haraka” inatumiwa kuonyesha tabia duni ya watu.

29. “Hawezi kutambua tofauti muhimu” inaonyesha wakati ambapo watu wanageuza mapenzi ya Mungu kuwa kitu cha kishetani, ikitaja kwa upana tabia ambayo kwayo watu humkataa Mungu.

30. “Anachanganya kati ya nyeusi na nyeupe” inahusisha kuchanganya ukweli na njozi, na haki na uovu.

31. “Gaidi” inatumiwa kuonyesha kwamba watu ni wapumbavu na hawana ufahamu.

32. “Mabaki na makombo” inatumiwa kuonyesha tabia ambazo kwazo watu humdhulumu Mungu.

33. “Anaghadhibishwa” inahusu uso mbaya wa mwanadamu aliye na hasira na aliyeudhika.

34. “Bila haya” inahusu wakati ambapo watu hawajali, na hawana uchaji kuhusiana na Mungu hata kidogo.

35. “Kuingia kwa mwanadamu” hapa inaonyesha tabia ya mwanadamu ya uasi. Badala ya kutaja kuingia kwa watu katika maisha—ambako ni kuzuri—kunahusu tabia na matendo yao mabaya. Inahusu kwa upana matendo yote ya mwanadamu yaliyo katika upinzani na Mungu.

36. “Wanakerwa na hofu za kubuni” inatumiwa kudhihaki maisha ya binadamu wa mwanadamu yasiyo na mwelekeo. Inahusu hali mbaya ya maisha ya wanadamu, ambayo watu huishi pamoja na pepo.

37. “Bora zaidi” inasemwa kwa dhihaka.

38. “Hamasa yao daima ikiwaka moto zaidi” inasemwa kwa dhihaka, na inahusu hali mbaya ya mwanadamu.

a. Maandishi ya asili yanasoma “Baadhi hata hupiga kelele.”

b. Huu ni msemo wa Kichina.

Iliyotangulia: Watu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Watu Wanaompinga Mungu

Inayofuata: Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya “Maono ya Kazi ya Mungu”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Sura ya 12

Wakati umeme unatoka Mashariki—ambapo pia ni wakati hasa Naanza kunena—wakati umeme unakuja, mbingu yote inaangazwa, na nyota zote zinaanza...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki