XI Maneno Bora Zaidi Juu ya Kuingia Katika Uhalisi wa Ukweli

(V) Maneno Juu ya Kuelewa Kazi ya Roho Mtakatifu na Kutambua Kazi ya Pepo Wabaya

45. Kazi ya Roho Mtakatifu inaweza kugawanywa katika sehemu tatu: Kazi ya Mungu mwenyewe, kazi ya wanadamu wanaotumiwa, na kazi kwa wale wote walioko katika mkondo wa Roho Mtakatifu. Miongoni mwa hizo tatu, kazi ya Mungu ni kuongoza enzi nzima; kazi ya wanadamu wanaotumiwa ni kuwaongoza wafuasi wote wa Mungu kwa kutumwa au kupokea maagizo kwa ajili ya kazi ya Mungu mwenyewe; na wanadamu hawa ndio wanaoshirikiana na kazi ya Mungu; kazi inayofanywa na Roho Mtakatifu kwa wale waliopo katika mkondo wake ni kudumisha kazi Yake yote, yaani, kudumisha usimamizi wote na kudumisha ushuhuda Wake, na wakati uo huo kuwakamilisha wale wanaoweza kukamilishwa. Sehemu hizi tatu ni kazi kamili ya Roho Mtakatifu, lakini bila kazi ya Mungu Mwenyewe, kazi yote ya usimamizi inaweza kutuama.

kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

46. Kazi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, bila kujali ni kazi ya Mungu mwenyewe au ni kazi ya watu wanaotumiwa, ni kazi ya Roho Mtakatifu. Kiini cha Mungu Mwenyewe ni Roho, ambaye anaweza kuitwa Roho Mtakatifu au Roho mwenye nguvu mara saba. Kwa jumla, Wao ni Roho wa Mungu. Ni kwamba tu Roho wa Mungu anaitwa majina tofauti katika enzi tofauti tofauti. Lakini kiini Chao bado ni kimoja. Hivyo, kazi ya Mungu Mwenyewe ni kazi ya Roho Mtakatifu; kazi za Mungu mwenye mwili hazitofautiani na kazi za Roho Mtakatifu. Kazi ya wanadamu wanaotumiwa pia ni kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwamba tu kazi ya Mungu ni onyesho kamili la Roho Mtakatifu, na hakuna tofauti, ilhali kazi ya wanadamu wanaotumiwa inachanganyika na mambo mengi ya kibinadamu, na wala sio uonyeshaji wa moja kwa moja wa Roho Mtakatifu, wala uonyeshaji kamili.

kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

47. Ingawa Roho Mtakatifu hufanya kazi katika njia nyingi tofauti tofauti na kulingana na kanuni nyingi, haijalishi kazi imefanyikaje au kwa watu wa aina gani, kiini ni tofauti daima, na kazi Anazofanya kwa watu tofauti zote zina kanuni na zote zinaweza kuwakilisha kiini cha mhusika anayefanyiwa kazi. Hii ni kwa sababu kazi ya Roho Mtakatifu ni mahususi kabisa kwa mapana yake na inapimika. Kazi inayofanywa katika mwili uliopatikana si sawa na kazi inayofanywa kwa watu, na kazi hii pia inatofautiana kulingana na ubora mbali mbali wa tabia za watu. Kazi inayofanywa katika mwili uliopatikana si sawa na kazi inayofanywa kwa watu, na katika mwili uliopatikana Hafanyi kazi ile ile kama aliyoifanya kwa watu. Kwa ufupi, haijalishi Anafanya kazi jinsi gani, kazi katika vitu mbalimbali haifanani, na kanuni ambazo Anazitumia kufanya kazi zinatofautiana kulingana na hali na asili ya watu mbalimbali. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa watu tofauti tofauti kulingana na kiini chao cha asili na haweki mahitaji ambayo ni zaidi ya kiini chao cha asili, na wala Hafanyi kazi zaidi ya ubora halisi wa tabia yao. Kwa hivyo, kazi ya Roho Mtakatifu kwa mwanadamu inawaruhusu watu kuona kiini cha lengo la kazi hiyo. Kiini asili cha mwanadamu hakibadiliki; ubora halisi wa tabia ya mwanadamu ina mipaka. Kama Roho Mtakatifu anawatumia watu au anafanya kazi kwa watu kazi, kazi hiyo siku zote inafanywa kulingana na tabia za watu ili waweze kunufaika kutoka kwayo. Roho Mtakatifu anapofanya kazi kwa wanadamu wanaotumiwa, karama zao na tabia zao halisi zinatumiwa pia na wala haziachwi. Tabia zao halisi zinatumiwa zote kwa ajili ya kutoa huduma kwa kazi. Tunaweza kusema kuwa Anafanya kazi kwa kutumia sehemu zilizopo za wanadamu ili kupata matokeo yatendayo kazi. Kinyume chake, kazi inayofanyika katika mwili uliopatikana ni yenye kumwonyesha Roho moja kwa moja na wala haichanganywi na akili na mawazo ya mwanadamu, haifikiwi na karama za mwanadamu, uzoefu wa mwanadamu au hali ya ndani ya mwanadamu.

kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

48. Wale wote walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu wanamilikiwa na uwepo na nidhamu ya Roho Mtakatifu na wasiokuwemo katika mkondo wa Roho Mtakatifu wako chini ya utawala wa Shetani na hawana kazi yoyote ya Roho Mtakatifu. Walio katika mkondo wa Roho Mtakatifu ni wale wanaoikubali kazi mpya ya Mungu, wanaoshiriki katika kazi mpya ya Mungu. Iwapo walio ndani ya mkondo huu hawana uwezo wa kushirikiana, na hawawezi kuweka ukweli unaotakiwa na Mungu katika vitendo wakati huu, basi watafundishwa nidhamu, na hali ikiwa mbaya zaidi kuachwa na Roho Mtakatifu. Wale ambao wanakubali kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wataishi katika mkondo wa Roho Mtakatifu, wapokee utunzaji na ulinzi wa Roho Mtakatifu. Wale ambao wako tayari kuweka ukweli katika vitendo wanapewa nuru na Roho Mtakatifu na wale wasiotaka kuweka ukweli katika vitendo wanafundishwa nidhamu na Roho Mtakatifu na huenda hata wakaadhibiwa. Bila kujali wao ni aina gani ya watu, ilimradi tu wamo katika mkondo wa Roho Mtakatifu, Mungu atawawajibikia wote wanaoikubali kazi Yake mpya kwa minajili ya jina Lake. Wale wanaolitukuza jina Lake na wako radhi kuweka maneno Yake katika vitendo watapokea baraka Zake; wale wasiomtii na wasioyaweka maneno Yake katika vitendo watapokea adhabu Yake.

kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

49. Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu. Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wanamiliki ubinadamu na daima hufuatilia ukweli. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu, hali zao huwa nzuri zaidi na zaidi, na ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na ingawa ushirikiano wao mwingine unaweza kuwa mpumbavu, motisha zao ziko sahihi, kuingia kwao ni kwa hali nzuri, hawajaribu kukatiza, na hakuna nia mbaya ndani yao.

kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili

50. Wakati kitu kinakufanyikia, je, kinakuja kutoka kwa Roho Mtakatifu, na je, unapaswa kukiheshimu, au kukikataa? Utendaji halisi wa watu huibua mengi ambayo ni ya mapenzi ya kibinadamu ilhali ambayo watu daima huamini kutoka kwa Roho Mtakatifu. Mengine hutoka kwa roho waovu, ilhali watu bado hudhani yanatoka kwa Roho Mtakatifu, na wakati mwingine Roho Mtakatifu huwaongoza watu kutoka ndani, ilhali watu wanaogopa kwamba mwongozo kama huo hutoka kwa Shetani, na hawathubutu kutii, wakati kwa kweli ni nuru ya Roho Mtakatifu. Hivyo, bila utofautishaji hakuna njia ya kupitia wakati uzoefu kama huo kwa hakika unakufanyikia, na bila utofautishaji, hakuna njia ya kupata maisha. Roho Mtakatifu hufanya kazi vipi? Roho waovu hufanya kazi vipi? Nini hutoka kwa mapenzi ya mwanadamu? Na ni nini hutoka kwa mwongozo na nuru ya Roho Mtakatifu? Kama unaelewa amri za kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mwanadamu, basi utaweza kukuza maarifa yako na kutofautisha katika maisha yako ya kila siku na wakati wa uzoefu wako halisi; utakuja kumjua Mungu, utaweza kumwelewa na kumtambua Shetani, hutachanganyikiwa katika kutii ama kufuatilia kwako, na utakuwa mtu ambaye fikira zake zi wazi, na ambaye hutii kazi ya Roho Mtakatifu.

kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili

51. Hakika Mungu hufanya kazi nyingi kwa watu, wakati mwingine kuwajaribu, wakati mwingine kusababisha mazingira ya kuwatuliza, na wakati mwingine kuzungumza maneno ili kuwaongoza na kurekebisha upungufu wao. Wakati mwingine Roho Mtakatifu huwaongoza watu kwenye mazingira yaliyotayarishwa na Mungu kwao ili wagundue mambo mengi ambayo hawana. Kupitia kile ambacho watu husema na kufanya, jinsi ambavyo watu huwatendea wengine na kuvishughulikia vitu, bila wao kujua, Roho Mtakatifu huwapa nuru kuhusu vitu vingi ambavyo hawakuvielewa hapo zamani, Akiwaruhusu waone mambo mengi na watu kwa uwazi zaidi, Akiwaruhusu wabaini mengi kuhusu yale ambayo hawakuyajua hapo zamani.

kutoka katika “Kuhusu Uzoefu” katika Neno Laonekana katika Mwili

52. Wakati mwingine Mungu hukupa aina fulani ya hisia—unapoteza starehe yako ya ndani kabisa, na unapoteza uwepo wa Mungu, na wewe unakuwa katika giza. Hii ni aina ya usafishaji. Wakati wowote unapofanya kitu kinaenda mrama au kugonga ukuta. Hii ni nidhamu ya Mungu. Unaweza kufanya kitu na usiwe na hisia yoyote dhahiri kukihusu, na wengine hawajui pia, lakini Mungu anajua. Yeye hatakuacha, na Atakufundisha nidhamu. Kazi ya Roho Mtakatifu ni yenye kina sana. Kwa makini sana Anatazama kila neno na tendo la watu, kila tendo na mwendo wao, na kila wazo lao na fikira ili watu waweze kupata ufahamu wa ndani wa vitu hivi. Unafanya kitu mara moja na kinaenda mrama, unakifanya tena na bado kinaenda mrama, na hatua kwa hatua utapata kuelewa kazi ya Roho Mtakatifu. Kupitia mara nyingi za kufundishwa nidhamu, utajua cha kufanya ili kuwa sambamba na mapenzi ya Mungu na kile kisichoambatana na mapenzi Yake. Mwishowe, utakuwa na majibu sahihi kwa uongozi wa Roho Mtakatifu ndani yako. Wakati mwingine utakuwa muasi na utakemewa na Mungu kutoka ndani. Haya yote hutoka kwa nidhamu ya Mungu. Kama humthamini Mungu, kama unaidharau kazi Yake, Hatashughulika nawe hata kidogo. Kadiri unavyoyachukulia maneno ya Mungu kwa makini, ndivyo Atakavyokupa nuru zaidi.

kutoka katika “Ni Lazima Wale Wanaofaa Kukamilishwa Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

53. Wakati wa kukupa nuru ili uelewe kitu, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa haraka sana nyakati nyingine, huku nyakati nyingine, Roho Mtakatifu hukufanya upitie uzoefu kwa muda kabla ya kukuruhusu ukielewe pole pole. Sio kwamba Yeye hakuruhusu kupitia chochote na Anakuruhusu tu uelewe maneno machache makavu. Je, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa kufuata kanuni gani? Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa kanuni ya kukupangia mazingira na kuwapanga watu, matukio, na vitu ili kukuruhusu uweze kua ndani yao na uelewe ukweli pole pole katika muda wa kuupitia. Hakupi maneno machache rahisi—kukutia moyo, au kukupa nuru, au kukutolea mwanga mdogo—wala hakupi maneno machache makavu na mafundisho. Badala yake, Anakuruhusu kujifunza, na kukua hatua kwa hatua kwa kupitia matukio, mazingira tofauti, na watu matukio, na vitu tofauti. Anakufanya uelewe ukweli pole pole kupitia mchakato huu wa ukuaji. Kwa hivyo, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa kufuata kanuni ya kawaida kabisa; Yeye hutii kabisa muundo wa asili wa maendeleo ya binadamu Anapofanya kazi, bila kutumia shurutisho lolote.

kutoka katika “Unaweza Kupata Ukweli Baada ya Kumkabidhi Mungu Moyo Wako Halisi” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

54. Roho Mtakatifu ana njia ya kutembea katika kila mtu, na humpa kila mtu fursa za kukamilishwa. Kupitia uhasi wako unajulishwa upotovu wako mwenyewe, na kisha kwa njia ya kuacha uhasi utapata njia ya kutenda, na huku ndiko kukamilishwa kwako. Aidha, kwa njia ya mwongozo na mwangaza wa siku zote wa mambo fulani chanya ndani yako, utatimiza shughuli yako kwa kuamili na kukua katika umaizi na kupata utambuzi. Wakati hali zako ni nzuri, uko tayari hasa kusoma neno la Mungu, na hasa tayari kumwomba Mungu, na unaweza kuyahusisha mahubiri unayoyasikia na hali zako mwenyewe. Kwa nyakati kama hizo Mungu hukupatia nuru na kukuangaza ndani, na kukufanya utambue mambo fulani ya kipengele chanya. Huku ni kukamilishwa kwako katika kipengele chanya. Katika hali hasi, wewe ni dhaifu na hasi, na huhisi kuwa huna Mungu moyoni mwako, lakini Mungu hukuangaza, akikusaidia kupata njia ya kutenda. Kutoka nje ya hili ni kupata ukamilisho katika hali chanya.

kutoka katika “Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili

55. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa kanuni hii: kupitia ushirikiano na watu, kupitia kwa wao kuomba kimatendo, kumtafuta na kusonga karibu na Mungu, matokeo yanaweza kupatikana na wanaweza kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Si kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kivyake, au mwanadamu anafanya kazi kivyake. Wote ni wa muhimu, na jinsi wanadamu wanavyoshiriki zaidi na jinsi wanavyotaka zaidi kufikia viwango vya mahitaji ya Mungu, ndivyo kazi ya Roho Mtakatifu inaimarika. Ni ushirikiano halisi tu wa wanadamu, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo vinaweza kutoa matukio halisi na ufahamu wa kweli wa kazi ya Mungu. Hatua kwa hatua, kupitia kwa mazoea kwa njia hii, mwanadamu mkamilifu hatimaye huzalishwa. Mungu hafanyi vitu vya miujiza; katika dhana za mwanadamu, Mungu ni mwenye uweza, na kila kitu kinafanywa na Mungu—na hutokea kwamba watu wanasubiri tu bila kufanya chochote, hawasomi maneno ya Mungu au kuomba, na wanasubiri tu kuguswa na Roho Mtakatifu. Walio na ufahamu sahihi, hata hivyo, wanaamini hili: matendo ya Mungu yanaweza kufikia pale ambapo ushirikiano wangu umefikia, na athari ya kazi ya Mungu kwangu inategemea namna ninavyoshirikiana. Mungu anenapo, ninapaswa kufanya lolote niwezalo na kuyaelekea maneno ya Mungu; hili ndilo ninapaswa kufanikisha.

kutoka katika “Jinsi ya Kujua Uhalisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

56. Kuna sharti moja kwa kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya watu. Bora wana hamu na wanatafuta na hawasitisiti ama kuwa na shaka kuhusu matendo ya Mungu, nao wanaweza kushikilia wajibu wao kila wakati, hivi tu ndivyo wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila hatua ya kazi ya Mungu, kinachohitajika kwa wanadamu ni imani kuu na kutafuta mbele za Mungu—kupitia tu kwa mazoea ndipo watu wataweza kugundua jinsi Mungu Anavyopendeka na jinsi Roho Mtakatifu Anavyofanya kazi ndani ya watu. Usipopata uzoefu, usipoihisi njia yako kupitia hayo, usipotafuta, hutapata chochote. Lazima uhisi njia yako kupitia mazoea yako, na kwa kupitia mazoea yako tu ndipo utaona matendo ya Mungu, na kugundua maajabu Yake na mambo Yake yasiyoeleweka.

kutoka katika “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

57. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao; wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, kazi hii inalingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na ni katika maisha halisi pekee ndio watu wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.

kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili

58. Mungu anafanya kazi ndani ya wale wanaotafuta na kulithamini neno la Mungu. Kadri unavyolithamini neno la Mungu, ndivyo Roho wa Mungu atakavyofanya kazi zaidi ndani mwako. Kadri mtu anavyolithamini neno la Mungu, ndivyo nafasi yake ya kukamilishwa na Mungu inavyokuwa kubwa. Mungu anawakamilisha wale ambao wanampenda Yeye kwa kweli. Anawakamilisha wale ambao mioyo yao iko katika amani mbele Yake. Ukiithamini kazi yote ya Mungu, ukiuthamini mwanga wa Mungu, ukiuthamini uwepo wa Mungu, ukithamini kujali na kuwekwa kwa Mungu, ukithamini jinsi neno la Mungu linakuwa ukweli wako na utoaji wa maisha, unafuata zaidi moyo wa Mungu. Ukiithamini kazi ya Mungu, ukiithamini kazi yote ambayo Mungu Amefanya juu yako, Mungu Atakubariki na kufanya kila kitu kilicho chako kuongezeka.

kutoka katika “Mungu Anakamilisha Wale Wanaoufuata Moyo Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili

59. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ili kuwapa watu nuru, Yeye kwa ujumla kuwapa ufahamu wa kazi ya Mungu, na ya kuingia kwao ya kweli na hali ya ukweli, na pia Huwapa azimio, huwaruhusu kuelewa kusudi la hamu la Mungu na mahitaji yake kwa ajili ya mtu leo, Huwapa azimio la kufungua njia zote. Hata wakati ambapo watu wanapitia umwagaji damu na sadaka ni lazima watende kwa ajili ya Mungu, na hata kama wanakumbana na mateso na dhiki, lazima bado wampende Mungu, na wasiwe na majuto, na lazima wawe shahidi kwa Mungu. Azimio la aina hii ni misisimko ya Roho Mtakatifu, na kazi ya Roho Mtakatifu—lakini jua kwamba hujamilikiwa na misismko kama hii kila wakati. Wakati mwingine katika mikutano unaweza kuhisi kuongozwa mno na kupata msukumo nawe unatoa sifa kubwa zaidi na unacheza. Unahisi kwamba una ufahamu usioaminika wa yale wengine wanashiriki, unahisi mpya kabisa kwa ndani, na moyo wako uko wazi kabisa bila hisia yoyote ya utupu—haya yote yanaungamanishwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama wewe ni mtu ambaye huongoza, na Roho Mtakatifu anakupa nuru na mwangaza usio wa kawaida unapoenda kanisani kufanya kazi, akikufanya uwe mwenye bidii wa kushangaza, mwenye kuwajibika na kitilia maanani kazi yako, hii inafungamanisha kazo ya Roho Mtakatifu.

kutoka katika “Utendaji (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

60. Ni matokeo yapi yanayotimizwa na kazi ya Roho Mtakatifu? Unaweza kuwa mpumbavu, na kunaweza kuwa hakuna utofautishaji wowote ndani yako, lakini Roho Mtakatifu anapaswa tu kufanya kazi ili kuwe na imani ndani yako, ili wewe daima uhisi kwamba huwezi kumpenda Mungu vya kutosha, ili uwe tayari kushiriki, uwe tayari kushiriki bila kujali ugumu mkuu ulio mbele. Mambo yatakufanyikia na haitakuwa wazi kwako iwapo yanatoka kwa Mungu ama kwa Shetani, lakini utaweza kungoja, na hutakuwa baridi wala mzembe. Hii ndiyo kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao, watu bado hukabiliwa na ugumu wa kweli, wakati mwingine wanalia, na wakati mwingine kuna mambo ambayo hawawezi kuyashinda, lakini hii yote ni hatua ya kazi ya kawaida ya Roho Mtakatifu. Ingawa hawashindi mambo hayo, na ingawa, wakati huo, wao ni dhaifu na hulalamika, baadaye bado wanaweza kumpenda Mungu na imani dhabiti. Ubaridi wao hauwezi kuwazuia kuwa na uzoefu wa kawaida, na bila kujali kile watu wengine husema, na jinsi wanavyowashambulia, bado wanaweza kumpenda Mungu. Wakati wa maombi, daima wanahisi kwamba walikuwa wadeni wa Mungu sana, na wanaamua kumridhisha Mungu na kuukataa mwili wakati wanakabiliwa na mambo kama hayo tena. Nguvu hii inaonyesha kuna kazi ya Roho Mtakatifu ndani yao, na hii ndiyo hali ya kawaida ya kazi ya Roho Mtakatifu.

kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili

61. Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake ya kishetani na iliyopotoka, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Hiyo ni kusema, maisha ya mwanadamu yanakua zaidi na zaidi, na tabia upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maisha ya mwanadamu.

kutoka katika “Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

62. Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia ndani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba. Kazi ya roho waovu huharibu uhusiano wa kawaida kati ya mwanadamu na Mungu, na huvuruga maono ya awali ya watu au njia yao ya awali ya kuingia katika maisha, katika mioyo yao hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, daima mambo hufanyika ambayo huwasababishia vurugu na kuwatia pingu, na mioyo yao haiwezi kupata amani, kuacha upendo wao wa Mungu bila nguvu, na kuwafanya kusononeka. Hayo ndiyo maonyesho ya kazi ya Shetani. Kazi ya Shetani inadhihirishwa katika yafuatayo: kutoweza kushikilia msimamo na kuwa na ushuhuda, kukusababisha kuwa mtu ambaye ana makosa mbele ya Mungu, na ambaye hana uaminifu kwa Mungu. Kwa kuingilia kwa Shetani, unapoteza upendo na uaminifu kwa Mungu ndani yako, unaondolewa uhusiano wa kawaida na Mungu, hufuatilii ukweli, ama kujiendeleza, unarudi nyuma, na kuwa baridi, unajipendeza, unaachia uenezaji wa dhambi, na huchukii dhambi; zaidi ya hayo, kuingilia kwa Shetani kunakufanya mpotovu, kunasababisha mguso wa Mungu kutoweka ndani yako, na kunakufanya kulalamika kuhusu Mungu na kumpinga Yeye, kukufanya uwe na shaka na Mungu, na hata kuna hatari ya wewe kumwacha Mungu. Hii yote ni kazi ya Shetani.

kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili

63. Leo kunao baadhi ya pepo wabaya wanaofanya kazi kupitia kwa mambo yasiyo ya ulimwenguni humu ili kumpotosha mwanadamu; hilo si chochote bali ni uigaji kwa upande wao, kumpotosha mwanadamu kupitia kwa kazi ambayo kwa sasa haifanywi na Roho Mtakatifu. Pepo wengi wabaya huiga ufanyaji wa miujiza na uponyaji wa magonjwa; si chochote ila kazi ya pepo wabaya, kwani Roho Mtakatifu hafanyi tena kazi kama hiyo leo. Wale wote wanaokuja baadaye na wanaoiga kazi ya Roho Mtakatifu—ni pepo wabaya. Kazi yote iliyotekelezwa Israeli wakati huo ilikuwa ile ya rohoni. Hata hivyo, Roho Mtakatifu sasa hafanyi kazi kwa njia hiyo, na kazi yoyote kama hiyo inayofuata ni shughuli na usumbufu wa Shetani na wa pepo waovu. Lakini huwezi kusema kwamba mambo yote ya rohoni ni shughuli ya pepo waovu. Hili linategemea enzi ya kazi ya Mungu.

kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

64. Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi. … Ikiwa, wakati wa siku za mwisho, Mungu bado Angeonyesha ishara na maajabu, na bado Angetoa mapepo na kuponya wagonjwa—kama Angefanya vilevile ambavyo Yesu Alifanya—basi Mungu Angekuwa Anarudia kazi ile ile, na kazi ya Yesu isingekuwa na maana au thamani yoyote. Hivyo, Mungu Anatekeleza hatua moja ya kazi katika kila enzi. Mara tu kila hatua ya kazi Yake inapokamilika, baada ya muda mfupi inaigizwa na roho wachafu, na baada ya Shetani kuanza kufuata nyayo za Mungu, Mungu Anabadilisha na kutumia mbinu nyingine. Mara Mungu Anapokamilisha hatua ya kazi Yake, inaigizwa na roho wachafu. Lazima muelewe vizuri hili.

kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

65. Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, “Mimi ni Mungu!” Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. … Huwezi kuleta njia mpya ama kumwakilisha Roho. Huwezi kueleza kazi ya Roho ama maneno Anenayo. Huwezi kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ama ile ya Roho. Huwezi kuelezea hekima, ajabu na mambo ya Mungu yasiyoeleweka, ama tabia yote ambayo Mungu humwadibu mwanadamu kupitia kwayo. Kwa hivyo madai yako ya kila mara ya kusema kuwa wewe ni Mungu hayajalishi; unalo tu jina lakini huna dutu.

kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

66. Watu wengine husema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao nyakati zote. Hili haliwezekani. Ikiwa wangesema kwamba Roho Mtakatifu yuko nao kila mara, hilo lingekuwa la kweli. Ikiwa wangesema kwamba fikira na hisi zao ni za kawaida nyakati zote, hilo pia lingekuwa la kweli, na lingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu yuko nao. Ikiwa wanasema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kila mara, kwamba wanapata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na wanapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida. Ni la rohoni kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu kama hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Ale, na lazima Apumzike—sembuse mwanadamu. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na hisia na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, wao ni wenye uwezo wa kustahimili mateso na hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la rohoni kabisa? Kazi ya pepo mwovu ni ya rohoni, na mambo haya ni yasiyofikiwa na mwanadamu. Wale wasioweza kutofautisha huwa na wivu wanapoona watu kama hao, na husema kwamba imani yao katika Mungu ni thabiti sana, na wana imani kubwa, na kwamba wao huwa si wadhaifu kamwe. Kwa kweli, hili ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Hiyo ni kwa sababu watu wa kawaida huwa na udhaifu wa binadamu usioepukika; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na kuwepo kwa Roho Mtakatifu.

kutoka katika “Utendaji (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

67. Wakati mwanadamu ana ufahamu kiasi wa Mungu, yuko tayari kuteseka kwa ajili Yaake na kuishi kwa ajili Yake. Hata hivyo, Shetani bado yuko katika udhibiti wa udhaifu ndani ya mwanadamu, na bado anaweza kumfanya ateseke. Pepo wabaya bado wanaweza kufanya kazi ndani ya watu kuwaingilia, kuwasababisha wawe katika hali ya kuchanganyikiwa kimawazo, kupoteza ufahamu wao, kutokuwa watulivu kiakili na kupata upinzani katika kila jambo. Bado kuna mambo fulani ya kimawazo ndani ya binadamu au roho ambayo yanaweza kudhibitiwa na kutawaliwa na Shetani. Hii ndiyo maana haiwezekani kwako kuwa na magonjwa, matatizo na kuhisi mwenye kutaka kujitia kitanzi na wakati mwingine pia kuhisi huzuni ya dunia, au kwamba maisha hayana maana. Hiyo ni kusema, kuteseka huku bado kuko chini ya uongozi wa Shetani; ni mojawapo ya udhaifu wa kusababisha mauti wa mwanadamu. Shetani bado ana uwezo wa kutumia vile vitu ambavyo amevipotosha na kuvikanyagia chini—ni silaha ambazo Shetani anaweza kutumia dhidi ya mwanadamu. … Roho wabaya hutumia kila fursa kutenda kazi yao. Wanaweza kuzungumza kutoka ndani mwako au kunong’oneza ndani ya sikio lako, au la sivyo wanaweza kuyachanganya mawazo na akili yako, na wanaweza kuzuia kuguswa kwa Roho Mtakatifu ili usiweze kuuhisi. Baada ya hapo wanaanza kukuingilia, kuchanganya fikira zako na kuvuruga akili yako, wakikuwacha bila utulivu na usiye thabiti. Hiyo ndiyo kazi ambayo roho wabaya humtendea mwanadamu na, usipokuwa na utambuzi juu ya hilo, utajipata katika hatari kubwa.

kutoka katika “Maana ya Mungu Kuupitia Uchungu wa Dunia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

68. Kazi ya Roho Mtakatifu ni maendeleo ya kimatendo, ilhali kazi ya Shetani ni kurudi nyuma na hali ya ubaridi, kutotii Mungu, kumpinga Mungu, kupoteza imani kwa Mungu, na kutotaka hata kuimba nyimbo za kidini ama kuinuka na kucheza ngoma. Kile ambacho hutoka kwa nuru ya Roho Mtakatifu hakilazimishwi kwako, lakini hasa ni cha asili. Ukikifuata, utakuwa na ukweli, na usipo, basi baadaye kutakuwa na shutuma. Kama ni nuru ya Roho Mtakatifu, basi hakuna ufanyacho kitakachoingiliwa au kuzuiliwa, utawekwa huru, kutakuwa na njia ya kutenda katika vitendo vyako, na hutapatwa na vizuizi vyovyote, na kuweza kutekeleza mapenzi ya Mungu. Kazi ya Shetani huleta mambo mengi ambayo husababisha kukatiza kwako, inakufanya kutotaka kusali, kuwa mzembe sana kula na kunywa maneno ya Mungu, na kutotaka kuishi maisha ya kanisa, na inakutenganisha na maisha ya kiroho. Kazi ya Roho Mtakatifu haiingilii maisha yako ya kila siku, na haiingilii kuingia kwako katika maisha ya kawaida ya kiroho.

kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili

69. Wakati kitu kinakufanyikia katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kutofautishaje kati ya iwapo kinatoka kwa kazi ya Roho Mtakatifu ama kwa kazi ya Shetani? Wakati hali za watu ni za kawaida, maisha yao ya kiroho na maisha yao katika mwili ni ya kawaida, na mantiki yao ni ya kawaida na ya mpangilio; kwa jumla kile wanachokipitia na kuja kujua ndani yao wakati huu kinaweza kusemwa kutoka kwa kuguswa na Roho Mtakatifu (kuwa na umaizi au kumiliki maarifa ya juu juu wanapokula na kunywa maneno ya Mungu, au kuwa waaminifu wakati mambo yanawafanyikia, au kuwa na nguvu ya kumpenda Mungu wakati mambo yanafanyika—haya yote ni ya Roho Mtakatifu). Kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya mwanadamu hasa ni ya kawaida: mwanadamu hana uwezo wa kuihisi, na inaonekana kuwa ni kupitia kwa mwanadamu mwenyewe—lakini kwa kweli ni kazi ya Roho Mtakatifu. Katika maisha ya kila siku, Roho Mtakatifu hufanya kazi ndogo na kubwa kwa kila mtu, na ni tu kwamba kiwango cha kazi hii hubadilika. Watu wengine ni wa ubora mzuri wa tabia, wanaelewa mambo haraka, na nuru ya Roho Mtakatifu hasa ni kubwa ndani yao; watu wengine ni wa ubora duni wa tabia, na inachukua muda mrefu zaidi kwao kuelewa mambo, lakini Roho Mtakatifu huwagusa ndani, na wao, pia, wanaweza kutimiza uaminifu kwa Mungu—Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa wale wote wanaomfuatilia Mungu. Wakati, katika maisha ya kila siku, watu hawampingi Mungu, au kuasi dhidi ya Mungu, hawafanyi mambo ambayo yanazozana na usimamizi wa Mungu, na hawakatizi kazi ya Mungu, ndani ya kila mmoja wao Roho wa Mungu hufanya kazi kwa kiwango kikubwa au kidogo, na kuwagusa, kuwapa nuru, kuwapa nguvu, na kuwasisimua kuingia kimatendo, sio kuwa wazembe au kutamani raha za mwili, kuwa tayari kutenda ukweli, na kutamani maneno ya Mungu—hii yote ni kazi ambayo hutoka kwa Roho Mtakatifu.

Wakati hali ya watu si ya kawaida, wanatelekezwa na Roho Mtakatifu, kuna malalamishi ndani yao, motisha zao si sahihi, wao ni wazembe, wanajiingiza katika tamaa za kimwili, na mioyo yao huasi dhidi ya ukweli, na haya yote hutoka kwa Shetani. Wakati hali za watu si za kawaida, wakati wana uovu ndani yao na wamepoteza mantiki yao ya kawaida, wametelekezwa na Roho Mtakatifu, na hawawezi kumhisi Mungu ndani yao, huu ndiyo wakati Shetani anafanya kazi ndani yao. Ikiwa watu daima wana nguvu ndani yao na daima humpenda Mungu, basi kwa jumla wakati mambo yanawafanyikia yanatoka kwa Roho Mtakatifu, na yeyote wanayekutana naye ni tokeo la mipango ya Mungu. Ambayo ni kusema, wakati hali zako ni za kawaida, wakati upo katika kazi kubwa ya Roho Mtakatifu, basi haiwezekani Shetani kukufanya uyumbayumbe; juu ya msingi huu inaweza kusemwa kwamba kila kitu hutoka kwa Roho Mtakatifu, na ingawa unaweza kuwa na mawazo yasiyo sahihi, unaweza kuyakataa, na usiyafuate. Hii yote hutoka kwa kazi ya Roho Mtakatifu. Shetani huingilia katika hali zipi? Wakati hali zako si za kawaida, wakati hujaguswa na Mungu, na uko bila kazi ya Mungu, na wewe ni mkavu na bure ndani, wakati unasali kwa Mungu lakini huelewi chochote, na kula na kunywa maneno ya Mungu lakini hujapewa nuru au mwangaza—wakati kama huo ni rahisi kwa Shetani kufanya kazi ndani yako. Kwa maneno mengine, wakati umeachwa na Roho Mtakatifu na huwezi kumhisi Mungu, basi mambo mengi hukufanyikia ambayo hutoka kwa majaribu ya Shetani. Shetani hufanya kazi wakati sawa na ule Roho Mtakatifu hufanya kazi, na huingilia kwa mwanadamu wakati sawa na ule Roho Mtakatifu hugusa ndani ya mwanadamu; wakati kama huo, hata hivyo, kazi ya Roho Mtakatifu huchukua nafasi ya kwanza, na watu ambao hali zao ni za kawaida wanaweza kushinda, ambao ni ushindi wa kazi ya Roho Mtakatifu juu ya kazi ya Shetani. Lakini wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, kuna kazi kidogo sana ya Shetani; wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi bado kuna tabia ya kutotii ndani ya watu, na yote ambayo kiasili yalikuwa ndani yao bado yamo hapo, lakini na kazi ya Roho Mtakatifu ni rahisi kwa watu kujua mambo muhimu kuwahusu na tabia yao asi kwa Mungu—ingawa wanaweza tu kujiondolea hayo wakati wa kazi ya polepole. Kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni ya kawaida, na Anapofanya kazi kwa watu bado wana shida, bado wanalia, bado wanateseka, bado ni dhaifu, na bado kuna mengi ambayo si dhahiri kwao, ilhali katika hali kama hiyo wanaweza kujisitisha kurudia mazoea mabaya, na wanaweza kumpenda Mungu, na ingawa wanalia na wana dhiki ndani, bado wanaweza kumsifu Mungu; kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni ya kawaida, na si ya mwujiza hata kidogo. Watu wengi sana huamini kwamba, punde tu Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi, mabadiliko hutokea katika hali ya watu na mambo muhimu kuwahusu yanaondolewa. Imani kama hizo ni za uwongo. Roho Mtakatifu afanyapo kazi ndani ya mwanadamu, mambo baridi ya mwanadamu bado yako hapo na kimo chake kinabaki sawa na awali, lakini ana mwangaza na nuru ya Roho Mtakatifu, na hivyo hali yake ni ya kimatendo zaidi, hali ndani yake ni za kawaida, na anabadilika kwa haraka. Katika uzoefu wa kweli wa watu, kimsingi wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu au Shetani, na iwapo hawawezi kuwa na madaraka juu ya hali hizi, na hawatofautishi, basi uzoefu wa kweli hauwezekani, sembuse mabadiliko katika tabia. Hivyo, ufunguo wa kuwa na uzoefu wa kazi ya Mungu ni kuweza kubaini mambo kama haya; kwa njia hii, itakuwa rahisi zaidi kwao kupitia.

kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: (IV) Maneno Juu ya Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na ya Mwanadamu

Inayofuata: (VI) Maneno Juu ya Jinsi ya Kuelewa Tabia Yako ya ishetani na Asili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Sura ya 11

Kila binadamu anapaswa kukubali uchunguzi wa Roho Wangu, anapaswa kuchunguza kwa makini kila neno na kitendo chao, na, zaidi ya hayo,...

Je, Utatu Upo?

Baada ya ukweli wa Yesu aliyepata mwili kutokea, mwanadamu aliamini hili: Si Baba pekee aliye mbinguni, bali pia Mwana, na hata Roho...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki