Videos

Wimbo wa Kwaya ya Injili “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” Mtazamo Kimbele Uliorefushwa" Extended Preview
Kwaya “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” Onyesho la Awali: Dansi ya kugongagonga mguu chini

 • Utambulisho

  Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?

  Miongoni mwa wanadamu, ni nani aishiye katika uchungu na ambaye amevumilia maelfu ya miaka ya upotovu wa Shetani, ambaye hatamani—hana hamu—ya kuwasili kwa Mungu? Je, ni waumini na wafuasi wangapi wa Mungu katika enzi zote, ambao chini ya ushawishi wa Shetani, wamevumilia taabu na dhiki, mateso na kutengwa? Ni nani asiyetumaini kuwa ufalme wa Mungu utakuja hivi karibuni? Baada ya kuonja furaha na masikitiko ya binadamu, ni nani kati ya wanadamu asiyetamani ukweli na haki vimiliki kati ya wanadamu?

  Ufalme wa Mungu utakapokuja, siku inayosubiriwa kwa hamu na mataifa na watu wote hatimaye itafika! Wakati huu, mandhari kati ya vitu vyote mbinguni na duniani yatakuwa yapi? Maisha katika ufalme yatakuwa mazuri kiasi gani? Zikiwa na “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani,” sala za milenia zitatimia!

  Kiambata: Umati unamshangilia Mungu, umati unamsifu Mungu; watu wote wanamtaja Mungu mmoja wa kweli, Ufalme unashuka duniani mwa wanadamu.

  1. Umati unamshangilia Mungu, umati unamsifu Mungu; watu wote wanamtaja Mungu mmoja wa kweli, watu wote wanayainua macho yao kuviangalia vitendo vya Mungu. Ufalme unashuka duniani mwa wanadamu, nafsi ya Mungu ni ya fahari na yenye neema. Nani asingesherehekea kwa ajili ya hili? Ni nani asingecheza kwa furaha? Ee, Sayuni! Inua bendera yako ya ushindi umsherehekee Mungu! Imba wimbo wako wa ushindi ili ulieneze jina takatifu la Mungu!

  2. Viumbe wote duniani kote! Harakisheni kujitakasa ili muweze kufanywa kuwa sadaka kwa Mungu! Nyota juu mbinguni! Rudini kwenye maeneo yenu kwa haraka ili muonyeshe nguvu kuu ya Mungu angani! Mungu anazisikiliza sauti za watu duniani, wanaomimina upendo na uchaji wao mwingi kwa ajili Yake katika wimbo! Katika siku hii, huku viumbe wote wakirudishiwa uhai, Mungu anashuka katika dunia ya wanadamu. Katika wakati huu, mambo yalivyo, maua yote yanachanua kwa wingi, ndege wote wanaimba kwa sauti moja, vitu vyote vinajawa na furaha! Kwa sauti ya saluti ya ufalme, ufalme wa Shetani unaanguka, ukiangamizwa katika mngurumo wa wimbo wa ufalme, usiinuke tena!

  3. Nani duniani anathubutu kuinuka na kupinga? Mungu anaposhuka duniani, Analeta kuchoma, Analeta ghadhabu, Analeta maafa ya aina yote. Falme za dunia sasa ni ufalme wa Mungu! Juu angani, mawingu yanagaagaa na kujongea kama mawimbi; chini ya anga, maziwa na mito yanatapakaa na kutoa muziki wa kusonga kwa furaha. Wanyama wanaopumzika wanaibuka kutoka kwenye matundu yao, na watu wote ambao wamelala wanaamshwa na Mungu. Siku ambayo watu wote wameingojea hatimaye imefika! Wanamwimbia Mungu nyimbo nzuri sana!

  Umetoholewa kutoka katika “Wimbo wa Ufalme” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

  Shiriki Picha

  Shiriki Bango

  TUNZO NA UTEUZI

  UTEUZI RASMI

  Best Documentary Feature: Silver Award, Los Angeles Independent Film Festival Awards, United States

  Best Documentary Feature: Silver Award, Los Angeles Independent Film Festival Awards, United States

  Iliyopendekezwa

  Maudhui Zaidi Mazuri

  Bonyeza Jiunge ili kupata video na habari za hivi karibuni mara tu zinapotolewa.

  Subscribe to our site to have the latest updates sent directly to your inbox, including wonderful content such as church news, gospel videos, hymns, and written testimonies.

  More Options

  Wasiliana Nasi

  Copyright © 2024 Kanisa la Mwenyezi Mungu. All rights reserved.