01Tunamwamini Bwana na tumesamehewa dhambi zetu, kwa hivyo ni kwa nini bado sisi hutenda dhambi mara nyingi?

Ingawa tumesamehewa dhambi zetu kupitia imani yetu katika Bwana, na tunastahili kumwomba Mungu na kufurahia neema na baraka Zake, bado tumezuiwa na asili zetu za dhambi. Hatuna budi kutenda dhambi na kumpinga Mungu, na hatuwezi kujinasua kutoka katika kuishi dhambini. Tunaendelea kusema uwongo na kumdanganya Mungu kwa ajili ya hadhi na sifa; hasa wakati ambapo kazi ya Mungu inatofautiana na mawazo yetu, tuna uelekeo wa kumlaumu, kumhukumu, na hata kumkataa au kumkana. Bila shaka, mwanadamu mara nyingi hufanya dhambi na kumpinga Mungu kwa sababu ya asili yake ya dhambi.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Kwa kuwa najua kwamba ndani yangu (yaani, ndani ya mwili wangu,) hakuna kitu chochote chema: kwa sababu kutaka kumo ndani yangu, lakini jinsi ya kutenda lililo jema sipati” (Warumi 7:18).

“Lakini naiona sheria nyingine katika viungo vya mwili wangu, inayopigana dhidi ya sheria ya akili yangu, na kunileta katika ufungwa wa sheria ya dhambi ambayo iko katika viungo vya mwili wangu. Ole wangu, mimi mnyonge! ni nani ambaye ataniokoa kutoka kwa mwili wa kifo hiki?” (Warumi 7: 23–24).

02Je, watu wanaweza kuingia katika ufalme wa Mungu ikiwa asili zao za dhambi hazijatatuliwa na hawajatakaswa?

Mungu alisema, “Kuweni watakatifu; kwani mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:45). “Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34–35). Mungu ni mtakatifu na mwenye haki, na ufalme wa mbinguni ndipo Mungu anatawala, ni nchi takatifu; Mungu kamwe hawezi kuwaruhusu wale wenye asili ya dhambi na wanaopenda dhambi waingie katika ufalme Wake. Hii imebainishwa na tabia Yake ya haki. Ni wazi kwamba asili ya dhambi ya mwanadamu isipotatuliwa, hakuna namna kabisa kwake kuepuka dhambi, kutakaswa, na kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Kwa sababu tukitenda dhambi makusudi baada ya sisi kupokea maarifa ya ukweli, hakuna tena dhabihu ya dhambi, lakini kuitafuta kwa hofu hukumu na uchungu mkali, ambao utawala maadui” (Waebrania 10:26–27).

“Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni. Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu” (Mathayo 7:21–23).

“Kuweni watakatifu; kwani mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:45).

“Bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14).

“Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34–35).

03Tunawezaje kuepuka dhambi na kutakaswa?

Unabii wa Biblia, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote” (Yohana 16:12-13). “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17). Mungu alituahidi kwamba Atakuja tena katika siku za mwisho, kwamba Ataonyesha ukweli wote kwa ajili ya utakaso na wokovu wa wanadamu, Atatekeleza kazi ya hukumu Akianzia katika nyumba ya Mungu, Atatatua kabisa asili ya dhambi na tabia ya kishetani ya mwanadamu, na kuwakomboa watu kutoka dhambini ili waweze kupata utakaso na kuletwa katika ufalme wa mbinguni.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” (Waebrania 9:28).

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote” (Yohana 16:12–13).

“Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:48).

“Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

“Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17).

“Na itatimia, kuwa katika nchi nzima, alisema Yehova, sehemu mbili hapo ndani zitakatwa na watakufa; lakini ya tatu itawachwa humo. Na nitaileta sehemu ya tatu na kuipitisha kwa moto, na nitawasafisha jinsi fedha isafishwavyo, na kuwajaribu jinsi dhahabu ijaribiwavyo; wataliita jina Langu, na nitawasikia: Nitasema, ni watu Wangu, nao watasema, Yehova ni Mungu wangu” (Zekaria 13:8–9).

“Wamebarikiwa wale wanaofanya amri zake, ili wawe na haki ya mti wa uzima, na waweze kuingia mjini humo kupitia malango yake” (Ufunuo 22:14).

Jinsi Mwanadamu Anaweza Kutakaswa Upotovu

Tovuti Rasmi