01Je, wajua? Hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi ilianza zamani

Watu wengi wanaamini kwamba hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo inamaanisha kuwa, Bwana atakaporudi katika siku za mwisho, Ataandaa dawati angani ambapo Ataketi, Atafungua kitabu, na kumhukumu kila mmoja ili kuamua ikiwa atakwenda mbinguni au kuzimuni, kulingana na tabia yake. Kukisia haya yote kunaonekana kuwa kwa maana, lakini Mungu atatekeleza kila kitu kama tunavyokisia kweli? Ukweli ni kwamba hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo ilikuwa maono tu ya Yohana—si ukweli. Kwa hivyo Bwana atakaporudi, Atatekeleza hukumu ya kiti kikuu cheupe cha enzi vipi hasa?

Aya za Biblia za Kurejelea

“Na nikaona kiti kikubwa cha enzi, cheupe, na yeye akiketiye, ambaye kutoka kwa uso wake nchi na mbingu zilitoroka; na hapakupatikana mahali pao. Na nikawaona waliokufa, wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya Mungu; na vitabu vilifunguliwa: na kitabu kingine pia kikafunguliwa, ambacho ni kitabu cha uhai: na waliokufa walihukumiwa kwa mambo yale yaliyokuwa yameandikwa katika vitabu hivyo, kulingana na vitendo vyao” (Ufunuo 20:11–12).

“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47–48).

“Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana” (Yohana 5:22).

“Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

02Kwa nini Mungu analazimika kufanya hatua nyingine ya kazi—kazi ya hukumu—katika siku za mwisho?

Kazi ya Bwana Yesu ya ukombozi katika Enzi ya Neema ilisamehe tu dhambi za wanadamu. Haikuwaondolea watu tabia zao potovu; kiburi, majivuno, ubinafsi, ulafi, upotovu, udanganyifu wao, na tabia nyingine za kishetani zilisalia. Tabia hizi potovu zisipotatatuliwa, watu watatenda dhambi kila wakati, watampinga na kumsaliti Mungu, wakinaswa katika mzunguko wa kutenda dhambi na kisha kukiri, wakishindwa kuondokana na asili yao ya dhambi na kuokolewa kabisa na Mungu. Mungu amerejea akivalia mwili katika siku za mwisho ili kutuokoa kikamilifu. Ameonyesha ukweli wote ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu, na Yeye anafanya kazi ya hukumu kuanza na nyumba ya Mungu ili kutatua asili ya dhambi ya watu na tabia za kishetani, ili tuweze kuondokana na dhambi, kutakaswa, na kuokolewa na Mungu.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34–35).

“Kwa maana mimi ni Yehova Mungu wenu: kwa hivyo mtajitakasa, na mtakuwa watakatifu; kwani mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:44).

“Ninyi mnaohifadhiwa na nguvu zake Mungu kupitia imani hadi kwa wokovu ambao uko tayari kufichuliwa katika muda wa mwisho” (1 Petro 1:5).

“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” (Waebrania 9:28).

“Wamebarikiwa wale wanaofanya amri zake, ili wawe na haki ya mti wa uzima, na waweze kuingia mjini humo kupitia malango yake” (Ufunuo 22:14).

03Jinsi Mungu anavyofanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kabisa

Katika siku za mwisho, Mungu anaonyesha ukweli ili kuhukumu na kufunua asili ya kishetani ya wanadamu ya kutenda dhambi na kumpinga Mungu, na Anafichua tabia Yake ya haki na takatifu ambayo haivumilii kosa lolote. Kupitia hukumu, majaribio, usafishaji na kuadibu kwa maneno ya Mungu, watu wanaona ukweli waziwazi na kiini cha upotovu wao wa kishetani. Wanaweza kujichukia na kujikana, na kutubu kwa Mungu kwa kweli. Wanaanza kutafuta ukweli, kutia ukweli katika matendo, kuyategemea maneno ya Mungu, na kuondokana na minyororo ya asili yao ya kishetani polepole, kutakaswa na kuwa watu wanaomtii na kumwabudu Mungu kwa kweli.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote” (Yohana 16:12–13).

“Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17).

“Na itatimia, kuwa katika nchi nzima, alisema Yehova, sehemu mbili hapo ndani zitakatwa na watakufa; lakini ya tatu itawachwa humo. Na nitaileta sehemu ya tatu na kuipitisha kwa moto, na nitawasafisha jinsi fedha isafishwavyo, na kuwajaribu jinsi dhahabu ijaribiwavyo; wataliita jina Langu, na nitawasikia: Nitasema, ni watu Wangu, nao watasema, Yehova ni Mungu wangu” (Zekaria 13:8–9).

“Naye akasema, Nenda njia yako, Danieli: kwani maandishi yamefungwa na kutiliwa muhuri hadi muda wa mwisho. Wengi watatakaswa, na kufanywa weupe, na kujaribiwa; lakini waovu watatenda maovu; na hakuna kati ya waovu ataelewa, lakini wenye busara wataelewa” (Danieli 12:9-10).

04Matokeo ya kukataa kukubali hukumu ya Mungu ya siku za mwisho

Mungu anapotoa hukumu Yake ya kiti kikuu cheupe cha enzi katika siku za mwisho, kwanza Anakuwa mwili, Anaonyesha ukweli na Anafanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu, na hivyo kufanyiza kundi la washindi kabla ya maafa kuwadia. Mara kazi ya Mungu ya hukumu itakapomalizika, Atashusha maafa makubwa na kuanza kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu. Wale wanaosubiri kwa upumbavu Bwana aje juu ya wingu, ambao wanakataa kukubali kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho na ambao hawajatakaswa na kuokolewa, watakumbwa na maafa, wakilia na kusaga meno.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu” (Mathayo 7:22–23).

“Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye. Hata hivyo, Amina” (Ufunuo 1:7).

“Lakini wenye woga, na wasiosadiki, na wa kuchukiza mno, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na wanaoabudu sanamu, na waongo wote, watakuwa na sehemu yao katika ziwa linalochoma kwa moto na kiberiti: ambacho ni kifo cha pili” (Ufunuo 21:8).

“Yule aliye dhalimu, basi aendelee kuwa dhalimu; na yeye aliye mtakatifu, na awe mtakatifu bado; na yeye aliye mwenye haki, awe mwenye haki bado: na yeye aliye mtakatifu, awe mtakatifu bado. Tazama, Naja upesi; na Nina thawabu Yangu, kumpa kila mwanadamu kulingana na vile matendo yake yatakuwa” (Ufunuo 22:11–12).

Hukumu ya Kiti Kikuu Cheupe cha Enzi Ilianza Zamani

Tovuti Rasmi