Ni lazima ujue aina ya watu ambao Ninataka; wale walio najisi hawakubaliki kuingia katika ufalme, wale walio najisi hawakubaliki kuchafua nchi takatifu. Ingawa unaweza kuwa umefanya kazi nyingi, na umefanya kazi kwa miaka mingi, mwishowe kama bado wewe ni mwovu kupindukia—hakuvumiliki kwa sheria ya Mbinguni kwamba wewe unataka kuingia katika ufalme wangu! Tangu mwanzo wa dunia hadi leo, kamwe Sijatoa njia rahisi ya kuingilia ufalme Wangu kwa wale wenye neema Yangu. Hii ni sheria ya Mbinguni, na hakuna awezaye kuivunja. Ni lazima utafute uzima. Leo, wale watakaofanywa wakamilifu ni wa aina sawa na Petro: ni wale ambao hutafuta mabadiliko katika tabia yao wenyewe, na wako tayari kuwa na ushuhuda kwa Mungu na kutekeleza wajibu wao kama kiumbe wa Mungu. Ni watu kama hawa pekee watakaofanywa wakamilifu. Kama wewe tu unatazamia tuzo, na hutafuti kubadilisha tabia ya maisha yako mwenyewe, basi juhudi zako zote zitakuwa za bure—na huu ni ukweli usiobadilika!
Kimetoholewa kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea”
Unajua tu kuwa Yesu atashuka siku za mwisho, lakini atashuka jinsi gani hasa? Mwenye dhambi kama wewe, aliyetoka tu kukombolewa, na hajabadilishwa bado, ama kukamilishwa na Mungu, unaweza kuufuata roho wa Mungu? Kwa wewe, wewe ambaye ni wa nafsi yako ya zamani, ni kweli kuwa uliokolewa na Yesu, na kwamba huhesabiwi kama mwenye dhambi kwa sababu ya wokovu wa Mungu, lakini hii haithibitishi kwamba wewe si mwenye dhambi, na si mchafu. Unawezaje kuwa mtakatifu kama haujabadilishwa? Ndani, umezingirwa na uchafu, ubinafsi na ukatili, na bado unatamani kushuka na Yesu—huwezi kuwa na bahati namna hiyo! Umepitwa na hatua moja katika imani yako kwa Mungu: umekombolewa tu, lakini haujabadilishwa. Ili uipendeze nafsi ya Mungu, lazima Mungu Mwenyewe afanye kazi ya kukubadilisha na kukutakasa; ikiwa umekombolewa tu, hautakuwa na uwezo wa kufikia utakatifu. Kwa njia hii hautahitimu kushiriki katika baraka nzuri za Mungu, kwani umepitwa na hatua kwa kazi ya Mungu ya kusimamia mwanadamu, ambayo ni hatua muhimu ya kubadilisha na kukamilisha. Na basi wewe, mwenye dhambi aliyetoka tu kukombolewa, huna uwezo wa kurithi urithi wa Mungu moja kwa moja.
Kimetoholewa kutoka katika “Kuhusu Majina na Utambulisho”
Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za uasi, ni mchafu kiasi cha kusikitisha, na ni kitu chenye najisi. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi na kuna maonyesho mengi sana ya mwili; hii ndiyo maana Mungu hudharau mwili wa mwanadamu kwa kiwango fulani. Watu wanapotupa mambo machafu, potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini bado wasipoachana na uchafu na upotovu, basi bado wanamilikiwa na Shetani. Ujanja, udanganyifu, na ukora wa watu yote ni mambo ya Shetani. Wokovu wa Mungu kwako ni ili kukuokoa kutoka katika mambo haya ya Shetani. Kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa; yote inafanywa ili kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini hadi kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena pingu na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unamilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na huwezi kupokea urithi wa Mungu. Mara tu unapotakaswa na kufanywa mkamilifu, utakuwa mtakatifu, utakuwa mtu wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na kuwa mtu anayemfurahisha Mungu.
Kimetoholewa kutoka katika “Utendaji (2)”
Watu husema Mungu ni Mungu wa haki, na kwamba mradi tu mwanadamu atamfuata mpaka mwisho, basi Hatakuwa na upendeleo kwa mwanadamu, kwani Yeye ni mwenye haki. Je, mwanadamu akimfuata mpaka mwisho kabisa, Mungu anaweza kumtupa mwanadamu nje? Sina upendeleo kwa mwanadamu yeyote, na Huwahukumu wanadamu wote kwa tabia Yangu ya haki, ilhali kuna mahitaji yanayofaa Ninayohitaji kutoka kwa mwanadamu, na Ninahitaji yakamilishwe na wanadamu wote, bila kujali ni nani. Sijali kiwango cha kufuzu kwako au kuheshimiwa kwako; najali tu kama utatembea kwa njia Yangu, na kama unapenda na una kiu ya ukweli. Kama huna ukweli, na unaleta aibu katika jina Langu, na matendo yako ni kinyume cha njia Yangu, kufuata tu bila kujali, basi wakati huo nitakupiga na kukuadhibu kwa uovu wako, na utakuwa na nini la kusema? Utaweza kusema Mungu si mwenye haki? Leo kama umezingatia maneno ambayo nimenena, basi wewe ni mtu ambaye Namkubali. Unasema umeumia ukifuata Mungu, kwamba umemfuata kwa marefu na mapana, na umeshiriki na yeye katika wakati mzuri na mbaya, lakini hujaishi kulingana na maneno yaliyosemwa na Mungu; unataka tu kukimbia huku na kule kwa ajili ya Mungu na kujitumia kwa ajili ya Mungu kila siku, na hujafikiria kuishi kwa kudhihirisha maisha yenye maana. Unasema pia, “Kwa vyovyote, naamini Mungu ni mwenye haki. Nimeteseka kwa ajili Yake, nikashughulika kwa ajili Yake, kujitoa kikamilifu Kwake, na nimefanya bidii ingawa sijapata kutambuliwa; Yeye hakika atanikumbuka.” Ni ukweli kwamba Mungu ni mwenye haki, na haki hii haijatiwa doa na uchafu wowote: Haina mapenzi ya binadamu, na haijatiwa doa na mwili, ama kitendo chochote cha binadamu. Wale wote ambao ni waasi na wako kwa upinzani, na hawazingatii njia Zake wataadhibiwa; hakuna atakayesamehewa, na hakuna atakayeepuka! Watu wengine husema, “Leo nakimbia juu yako; mwisho ukifika, utanipa baraka kidogo?” Sasa Nakuuliza, “Umezingatia maneno Yangu?” Haki unayoongelea inategemea matendo. Unafikiria kwamba Mimi ni mwenye haki, na asiye na mapendeleo kwa binadamu wote, na kwamba wale wanifuatao hadi mwisho wataokolewa na kupata baraka Yangu. Kuna maana ya ndani kwa maneno Yangu kwamba “wale wote wanifuatao hadi mwisho wataokolewa”: Wale wanifuatao mpaka mwisho ndio Nitakaowapata, ni wale, baada ya kushindwa Nami, watautafuta ukweli na kufanywa wakamilifu. Ni hali gani umepata? Umepata kunifuata hadi mwisho, lakini nini kingine? Je, umezingatia maneno Yangu? Umekamilisha moja kati ya tano ya mahitaji Yangu, ilhali huna mpango wa kumaliza manne yaliyobaki. Umepata ile njia rahisi, na ukafuata ukifikiria umebahatika. Kwa mtu kama wewe, haki Yangu ni adabu na hukumu, ni adhabu ya haki, na ni adhabu ya haki kwa watenda maovu wote; wale wote wasiotembea kwa njia Yangu wataadhibiwa, hata kama watafuata mpaka mwisho. Hii ndio haki ya Mungu.
Kimetoholewa kutoka katika “Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu”
Labda mnawaza kwamba kwa kuwa wafuasi kwa miaka mingi mnaweka bidii bila kujali hali yoyote, hivyo kwa namna yoyote mnaweza kupata bakuli la wali katika nyumba ya Mungu kwa kuwa watendaji huduma. Ningesema wengi wenu mnafikiri hivi kwa sababu siku zote hadi sasa mmekuwa mkifuatilia kanuni ya jinsi ya kujinufaisha na jambo fulani na kutokuwa na manufaa kwa wengine. Hivyo Mimi nawaambia sasa kwa uzito kabisa: Sijali jinsi kazi yako ya bidii ni ya kusifiwa, jinsi sifa zako ni za kuvutia, jinsi unavyonifuata Mimi kwa karibu, jinsi ulivyo mashuhuri, au jinsi umeendeleza mwelekeo wako; mradi hujafanya kile ambacho Nimedai, hutaweza kupata sifa Zangu kamwe. Yafuteni hayo mawazo na hesabu zenu zote mapema iwezekanavyo, na muanze kuyachukulia madai Yangu kwa makini. Vinginevyo, Nitawafanya watu wote wawe majivu ili Niitamatishe kazi Yangu, na hali ikiwa bora zaidi Niigeuze miaka Yangu ya kazi na kuteseka kuwa utupu, kwa sababu Siwezi kuwaleta katika ufalme Wangu maadui Wangu na watu waliojawa na maovu kwa mfano wa Shetani, katika enzi ijayo.
Kimetoholewa kutoka katika “Dhambi Zitamwelekeza Mwanadamu Jahanamu”