Wakati huo kazi ya Yesu ilikuwa ni ukombozi wa wanadamu wote. Dhambi za wote ambao walimwamini zilisamehewa; ilimradi wewe ulimwamini, Angeweza kukukomboa wewe; kama wewe ulimwamini Yeye, wewe hukuwa tena mwenye dhambi, wewe ulikuwa umeondolewa dhambi zako. Hii ndiyo ilikuwa maana ya kuokolewa, na kuhesabiwa haki kwa imani. Hata hivyo, kati ya wale walioamini, kulibaki na kitu ambacho kilikuwa na uasi na pingamizi kwa Mungu, na ambacho kilibidi kiondolewe polepole. Wokovu haukuwa na maana kuwa mwanadamu alikuwa amepatwa na Yesu kabisa, lakini ni kuwa mwanadamu hakuwa tena mwenye dhambi, na kuwa alikuwa amesamehewa dhambi zake; mradi tu uliamini, wewe kamwe hungekuwa mwenye dhambi.
Kimetoholewa kutoka katika “Maono ya Kazi ya Mungu (2)”
Kazi katika siku za mwisho ni kunena maneno. Mabadiliko makuu yanaweza kusababishwa kwa watu kupitia katika maneno hayo. Mabadiliko yanayosababishwa sasa kwa watu hawa kwa sababu ya kukubali maneno haya ni makubwa kuliko yale ya watu katika Enzi ya Neema kwa kukubali ishara na maajabu hayo. Kwani, katika Enzi ya Neema, mapepo yaliondoka kutoka kwa mwanadamu kwa kuwekewa mikono na maombi, lakini tabia potovu ndani ya mwanadamu ilibaki. Mwanadamu aliponywa magonjwa na kusamehewa dhambi zake, lakini kazi ya jinsi tabia potovu za kishetani katika mwanadamu haikutupiliwa mbali na bado iko ndani yake. Mwanadamu aliokolewa na kusamehewa dhambi zake kwa imani yake, lakini asili ya dhambi ya mwanadamu haikuchukuliwa na ikabaki naye. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kupitia mwili wa Mungu mwenye mwili, lakini hili halikumaanisha kuwa mwanadamu hakuwa na dhambi ndani yake. Dhambi za mwanadamu zingesamehewa kupitia sadaka ya dhambi, lakini mwanadamu hajaweza kutatua suala la vipi hangeweza kutenda dhambi na vile asili Yake ya dhambi ingetupiliwa mbali kabisa na kubadilishwa. Dhambi za mwanadamu zilisamehewa kwa sababu ya kazi ya Mungu ya kusulubiwa, lakini mwanadamu akaendelea kuishi katika tabia yake potovu ya zamani ya kishetani. Hivyo, mwanadamu lazima aokolewe kabisa kutoka kwa tabia potovu za kishetani ili asili ya dhambi ya mwanadamu itupiliwe mbali kabisa na isirudi tena, hivyo kukubali tabia ya mwanadamu kubadilika. Hii inampasa mwanadamu kuelewa njia ya kukua katika maisha, njia ya maisha, na jinsi ya kubadilisha tabia yake. Inamhitaji pia mwanadamu kutenda kulingana na njia hii ili tabia ya mwanadamu iweze kubadilika hatua kwa hatua na aishi chini ya nuru inayong’aa, na aweze kufanya mambo yote kulingana na mapenzi ya Mungu, atupilie mbali tabia potovu za kishetani, na kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza, hivyo kutoka kabisa katika dhambi. Ni hapo tu ndipo mwanadamu atapokea wokovu kamili. Yesu Alipokuwa Akifanya kazi Yake, maarifa ya mwanadamu juu Yake yalikuwa bado hayakuwa bayana na hayakuwa wazi. Mwanadamu aliamini kila wakati kuwa Alikuwa Mwana wa Daudi na kumtangaza kuwa nabii mkuu na Bwana mwema Aliyezikomboa dhambi za mwanadamu. Wengine, wakiwa na msingi wa imani, wakaponywa tu kwa kugusa vazi Lake; vipofu wakaona na hata wafu kurejeshwa katika uhai. Hata hivyo, mwanadamu hangeweza kutambua tabia potovu za kishetani zilizokita mizizi ndani yake na pia mwanadamu hakujua jinsi ya kuitoa. Mwanadamu alipokea neema nyingi, kama amani na furaha ya mwili, baraka ya familia nzima juu ya imani ya mmoja, na kuponywa magonjwa, na mengine mengi. Yaliyobaki ni matendo mema ya mwanadamu na kuonekana kwa kiungu; kama mtu angeishi katika huo msingi, angechukuliwa kama muumini mzuri. Waumini hao tu ndio wangeingia mbinguni baada ya kifo, ambayo ilimaanisha kuwa walikuwa wameokolewa. Lakini katika maisha yao, hawakuelewa kamwe njia ya maisha. Walitenda tu dhambi, na kisha kukiri kila wakati bila njia yoyote ya kubadili tabia yao; hii ndiyo ilikuwa hali ya mwanadamu katika Enzi ya Neema. Je mwanadamu amepokea wokovu kamili? La! Kwa hivyo, hatua ilipokamilika, bado kuna kazi ya hukumu na kuadibu. Hatua hii ni ya kumfanya mwanadamu awea safi kupitia neno, na hivyo kumpa njia ya kufuata. Hatua hii haingekuwa na matunda ama ya maana kama ingeendelea na kukemea mapepo, kwani msingi wa dhambi wa mwanadamu haungetupwa mbali na mwanadamu angekoma tu baada ya msamaha wa dhambi. Kupitia kwa sadaka ya dhambi, mwanadamu amesamehewa dhambi zake, kwani kazi ya kusulubisha imefika mwisho na Mungu Ametawala juu ya Shetani. Lakini tabia potovu ya wanadamu bado imebaki ndani yao na mwanadamu anaweza kutenda dhambi na kumpinga Mungu; Mungu hajampata mwanadamu. Hiyo ndio sababu katika hatua hii ya kazi Mungu Anatumia neno kutangaza tabia potovu ya mwanadamu na kumuuliza mwanadamu kutenda kulingana na njia sahihi.
Kimetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)”
Mwili wa mwanadamu ni wa Shetani, umejaa tabia za uasi, ni mchafu kiasi cha kusikitisha, na ni kitu chenye najisi. Watu hutamani raha ya mwili kupita kiasi na kuna maonyesho mengi sana ya mwili; hii ndiyo maana Mungu hudharau mwili wa mwanadamu kwa kiwango fulani. Watu wanapotupa mambo machafu, potovu ya Shetani, wao hupata wokovu wa Mungu. Lakini bado wasipoachana na uchafu na upotovu, basi bado wanamilikiwa na Shetani. Ujanja, udanganyifu, na ukora wa watu yote ni mambo ya Shetani. Wokovu wa Mungu kwako ni ili kukuokoa kutoka katika mambo haya ya Shetani. Kazi ya Mungu haiwezi kuwa na kosa; yote inafanywa ili kuwaokoa watu kutoka gizani. Wakati ambapo umeamini hadi kwa kiwango fulani na unaweza kuachana na upotovu wa mwili, na hufungwi tena pingu na upotovu huu, je, hutakuwa umeokolewa? Wakati ambapo unamilikiwa na Shetani huwezi kumdhihirisha Mungu, wewe ni kitu kichafu, na huwezi kupokea urithi wa Mungu. Mara tu unapotakaswa na kufanywa mkamilifu, utakuwa mtakatifu, utakuwa mtu wa kawaida, na utabarikiwa na Mungu na kuwa mtu anayemfurahisha Mungu.
Kimetoholewa kutoka katika “Utendaji (2)”
Mwishowe, mambo yaliyo ndani ya watu ambayo ni ya Shetani na mambo ya asili yao lazima yabadilike na lazima yalingane na mahitaji ya ukweli; ni kwa njia hii tu ndiyo mtu anaweza kupata wokovu kwa kweli. Iwapo, kama ulivyofanya wakati ulikuwa ndani ya dini, unatoa tu baadhi ya maneno ya mafundisho au kupiga kelele ukitaja kaulimbiu, na kisha utende vitendo vichache vizuri, uonyeshe tabia nzuri zaidi na kuepuka kutenda dhambi kiasi, dhambi zozote za waziwazi, hii bado haimaanishi kwamba umeingia katika njia sahihi ya kumsadiki Mungu. Je, kuweza kuzitii sheria kunaonyesha kwamba unaitembelea njia sahihi? Je, kunamaanisha kuwa umechagua kwa usahihi? Kama mambo ndani ya asili yako hayajabadilika, na mwishowe ungali unampinga na kumkosea Mungu, basi hili ndilo tatizo lako kubwa zaidi. Iwapo, katika imani yako kwa Mungu, hulitatui tatizo hili, basi unaweza kuchukuliwa kuwa aliyeokolewa?
Kimetoholewa kutoka katika “Wale Waliopoteza Kazi ya Roho Mtakatifu Ndio Walio katika Hatari Kubwa Zaidi”
Ikiwa mtu anaweza kumridhisha Mungu huku akitimiza wajibu wake, ni mwenye maadili katika maneno ya matendo yake, na anaweza kuingia katika uhalisi a vipengele vya ukweli, basi huyu ni mtu ambaye anakamilishwa na Mungu. Inaweza kusemekana kuwa kazi na maneno ya Mungu yamekuwa ya kufaa kabisa kwa watu kama hao, kwamba maneno ya Mungu yamekuwa maisha yao, wamepata ukweli, na wanaweza kuishi kulingana na maneno ya Mungu. Baada ya hili, asili ya mwili wao—yaani, msingi maalum wa uwepo wao wa kwanza—itatikisika na kuanguka. Baada ya watu kuwa na maneno ya Mungu kama maisha yao, watakuwa watu wapya. Maneno ya Mungu yakiwa maisha yao, maono ya kazi ya Mungu, matakwa Yake kwa wanadamu, ufunuo Wake kwa wanadamu, na viwango vya maisha ya kweli ambayo Mungu anawahitaji watimize vikiwa maisha yao, wakiishi kulingana na maneno haya na ukweli huu, basi wanakamilishwa na Mungu. Watu kama hawa wanazaliwa tena, na wamekuwa watu wapya kupitia maneno ya Mungu.
Kimetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kuishika Njia ya Petro”
Umuhimu wa kumwamini Mungu ni kuokolewa, kwa hiyo kuokolewa kunamaanisha nini? “Kuokolewa,” “kujitenga na ushawishi mwovu wa Shetani”—watu huzungumza juu ya mada hizi mara nyingi, lakini hawajui kuokolewa kunamaanisha nini. Je, kuokolewa kunamaanisha nini? Hii inahusiana na mapenzi ya Mungu. Ili kuokolewa, kuzungumza kwa lugha ya wenyeji, kunamaanisha unaweza kuendelea kuishi, na kwamba unafufuliwa. Kwa hiyo kabla ya hayo, je, umekufa? Unaweza kuzungumza, na unaweza kupumua, kwa hivyo unawezaje kusemekana kwamba umekufa? (Roho imekufa.) Kwa nini inasemekana kwamba watu wamekufa ikiwa roho yao imekufa? Msingi wa msemo huu ni upi? Kabla ya kuokolewa, wako wapi? (Wanamilikiwa na Shetani.) Watu wanaishi chini ya ushawishi wa Shetani. Wanategemea nini ili kuishi? (Falsafa na sumu za Shetani.) Wanategemea asili yao ya kishetani na asili potovu ili kuishi. Mtu anapoishi kwa kufuata mambo haya, nafsi yake nzima—mwili wake, na vipengele vingine vyote kama vile roho na mawazo yao—wako hai au wamekufa? Kutoka katika mtazamo wa Mungu, wao ni wafu. Kwa juu juu, unaonekana kuwa unapumua na kufikiria, lakini kila kitu unachokifikiria daima ni kiovu; unafikiria kuhusu vitu ambavyo vinamwasi Mungu na vya ukaidi dhidi ya Mungu, vitu ambavyo Mungu huchukia, hukirihi, na kushutumu. Machoni pa Mungu, mambo haya yote si ya mwili tu, bali pia ni ya Shetani na ya pepo kikamilifu. Kwa hiyo watu ni nini machoni pa Mungu? Je, wao ni wanadamu? La, wao si wanadamu. Mungu huwaona kama pepo, kama wanyama, na kama Shetani, Shetani waishio! Watu wanaishi kulingana na vitu na asili ya Shetani, na machoni pa Mungu, wao ni Shetani waishio waliovalia miili ya binadamu. Mungu huwafafanua watu kama hao kama maiti zinazotembea; kama wafu. Mungu anafanya kazi Yake ya sasa ya wokovu kuwachukua watu kama hawa—maiti hizi zinazotembea zinazoishi kwa kufuata tabia zao za kishetani na kwa kufuata viini vyao vipotovu vya kishetani—Anawachukua hawa wanaodaiwa kuwa wafu na kuwageuza kuwa walio hai. Hii ndiyo maana ya kuokolewa.
Sababu ya kumwamini Mungu ni kupata wokovu. Kuokolewa kunamaanisha kuwa unageuka kutoka kuwa mtu aliyekufa hadi kuwa mtu aliye hai. Maana ya hili ni kwamba pumzi yako inafufuliwa, na wewe unakuwa hai; unaweza kumwona Mungu, unaweza kumtambua, na unaweza kusujudu ili umwabudu Yeye. Moyoni mwako huna upinzani zaidi dhidi ya Mungu; humkatai tena, humshambulii tena, au kumuasi tena. Watu kama hawa tu ndio walio hai kwa kweli machoni pa Mungu. Mtu akisema tu kwamba anamkubali Mungu na anaamini moyoni mwake kwamba kuna Mungu, basi ni mmoja wa walio hai au la? (La, sio.) Kwa hiyo watu walio hai ni wa aina gani? Je, walio hai wana uhalisi wa aina gani? Angalau, walio hai wanaweza kuzungumza lugha ya binadamu. Hiyo ni nini? Inamaanisha kwamba maneno wanayotamka yanahusu mawazo, fikira, na utambuzi. Watu walio hai hufikiri na kufanya nini mara nyingi? Wanaweza kujihusisha na shughuli za binadamu, na kutimiza wajibu wao. Asili ya kile wanachofanya na kusema ni ipi? Ni kwamba kila kitu wanachofichua, kila kitu wanachofikiria, na kila kitu wanachofanya kinafanywa na asili ya kumcha Mungu na kuepuka uovu. Ili kuliweka kwa usahihi zaidi, kila tendo na kila wazo lako hakihukumiwi na Mungu au kuchukiwa na kukataliwa na Mungu; badala yake, yanaidhinishwa na kusifiwa na Mungu. Hiki ndicho watu walio hai hufanya, na pia ndicho ambacho watu walio hai wanapaswa kufanya.
Kimetoholewa kutoka katika “Kuwa Mtiifu Kwa Kweli Pekee Ndiyo Imani ya Kweli”
Ikiwa watu wanatamani kuwa viumbe hai, na kuwa na ushuhuda wa Mungu, na kuthibitishwa na Mungu, wanapaswa kukubali wokovu wa Mungu, wanapaswa kuwa watiifu katika hukumu na kuadibu Kwake, na wanapaswa kukubali kwa furaha kushughulikiwa na kupogolewa na Mungu. Ni hapo tu ndipo wataweza kuweka katika matendo ukweli wote unaohitajika na Mungu, na baada ya hapo ndipo wataweza kupata wokovu wa Mungu, na kuwa viumbe hai kabisa. Walio hai wanaokolewa na Mungu, wamehukumiwa na kuadibiwa na Mungu, wapo tayari kujitoa wenyewe na wana furaha kutoa maisha yao kwa Mungu, na wapo tayari kujitoa maisha yao yote kwa Mungu. Pale ambapo walio hai watachukua ushuhuda wa Mungu ndipo Shetani ataweza kuaibishwa, ni walio hai tu ndio wanaweza kueneza kazi ya injili ya Mungu, ni walio hai tu ndio wanaoupendeza moyo wa Mungu, ni walio hai tu ndio watu halisi. Mwanadamu wa asili aliyeumbwa na Mungu alikuwa hai, lakini kwa sababu ya uharibifu wa Shetani mwanadamu anaishi katikati ya kifo, na anaishi chini ya ushawishi wa Shetani, na hivyo watu hawa wamekuwa wafu ambao hawana roho, wamekuwa ni maadui ambao wanampinga Mungu, wamekuwa nyenzo ya Shetani, na wamekuwa mateka wa Shetani. Watu wote walio hai ambao wameumbwa na Mungu wamekuwa wafu, na hivyo Mungu amepoteza ushuhuda wake, na Amempoteza mwanadamu, ambaye Alimuumba na ndiye kiumbe pekee aliye na pumzi Yake. Ikiwa Mungu ataamua kurejesha ushuhuda Wake, na kuwarejesha wale ambao waliumbwa kwa mkono wake lakini ambao wamechukuliwa mateka na Shetani, basi ni lazima awafufue ili waweze kuwa viumbe hai, na ni lazima awaongoe ili kwamba waweze kuishi katika nuru Yake. Wafu ni wale ambao hawana roho, wale ambao ni mbumbumbu kupita kiasi, na wale ambao wanampinga Mungu. Aidha, ni wale ambao hawamjui Mungu. Watu hawa hawana nia hata ndogo ya kumtii Mungu, kazi yao ni kumpinga na kuasi dhidi Yake, na hawana hata chembe ya utii. Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake.
Kimetoholewa kutoka katika “Je, Wewe ni Mtu Ambaye Amepata Uzima?”