Maneno Juu ya Kuonekana na Kazi ya Mungu Mwenye Mwili

Zaidi

Maneno Husika ya Mungu

Kwa nini Mungu hamtumii mwanadamu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho lakini badala yake Yeye ni lazima apate mwili na kuifanya Mwenyewe?

Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

Kupata Mwili Ni Nini? Ni Nini Kiini cha Kupata Mwili?

Maana ya kupata mwili ni kwamba Mungu Anajionyesha katika mwili, na Anakuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu wa uumbaji Wake katika umbo la mwili. Hivyo, ili Mungu kuwa mwili, ni lazima kwanza Apate umbo la mwili, mwili wenye ubinadamu wa kawaida; hili ndilo hitaji la kimsingi zaidi. Kwa kweli, maana ya kupata mwili kwa Mungu ni kwamba Mungu Anaishi na kufanya kazi katika mwili, Mungu katika kiini Chake Anakuwa mwili, Anakuwa mwanadamu.

Tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu

Mungu mwenye mwili Anaitwa Kristo, na Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.

Video za Marejeo

Tazama zaidi

Maneno Juu ya Kazi ya Mungu ya Hukumu katika Siku za Mwisho

Zaidi

Maneno Husika ya Mungu

Mungu aliwakomboa wanadamu katika Enzi ya Neema, hivyo kwa nini bado anahitaji kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho?

Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani.

Umuhimu wa hukumu ya Mungu katika siku za mwisho unaweza kuonekana katika matokeo yaliyofanikishwa na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho

Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.

Video za Marejeo

Tazama zaidi

Maneno Juu ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu ya Wokovu kwa Wanadamu

Zaidi

Maneno Husika ya Mungu

Madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu

Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu.

Madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Wakati huu, umuhimu, kusudi na awamu za kazi ya Yehova huko Israeli zilikuwa kuanzisha kazi Yake katika dunia nzima, ambayo, ikichukua Israeli kama kituo chake, ilienea polepole hadi kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hii ni kanuni ambayo kwayo Anafanya kazi katika ulimwengu mzima—kuunda mfano na kisha kuupanua hadi watu wote ulimwenguni watakuwa wamepokea injili Yake.

Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu

Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo.

Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?

Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na kwa njia hii mahitaji ya mwanadamu huwa ya juu hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huwa ya juu hata zaidi.

Video za Marejeo

Tazama zaidi

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp