Kila kitu anachofanya Mungu kimepangiliwa kwa uhakika. Anapoona jambo au hali ikitokea, kutakuwa na kiwango cha kulipima jambo hilo katika macho Yake, na kiwango hiki kitaamua kama Ataanza mpango wa kulishughulikia au namna ya kuchukulia jambo na hali hii. Yeye anajali na ana hisia kwa kila kitu. Kwa hakika ni kinyume kabisa cha mambo. Kunao mstari hapa ambao Mungu alimwambia Nuhu: “Mwisho wa wote walio na mwili umefika mbele zangu; kwa kuwa dunia imejawa na vurugu kupitia kwao; na, tazama, nitawaangamiza pamoja na dunia.” Katika maneno ya Mungu wakati huu, Alisema kwamba Angeangamiza binadamu tu? La! Mungu Alisema kwamba Angeangamiza viumbe wote hai wenye mwili. Kwa nini Mungu alitaka kuangamiza? Kunao ufunuo mwingine wa tabia ya Mungu hapa: Katika macho ya Mungu, kunayo mipaka ya subira yake kwa kupotoka kwa binadamu, kwa uchafu, vurugu, na kutotii kwa mwili wote. Mipaka Yake ni ipi? Ni kama vile alivyosema Mungu: “Mungu akaiangalia dunia, na, tazama, ilikuwa imepotoka; kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani.” Kauli hii “kwa sababu kila aliye na mwili alikuwa amejipotoshea njia yake duniani” inamaanisha nini? Inamaanisha kiumbe yeyote hai, wakiwemo wale waliofuata Mungu, wale walioita jina la Mungu, wale waliowahi kutoa sadaka za kuteketezwa kwa Mungu, wale waliomtambua Mungu kwa vinywa vyao na hata kumsifia Mungu—pindi tabia yao ilipojaa upotovu na kufikia macho ya Mungu, basi ingemlazimu kuwaangamiza. Hiyo ndiyo ilikuwa mipaka ya Mungu. Hivyo basi ni hadi kiwango kipi Mungu alibakia kuwa mwenye subira kwa binadamu na upotovu wa mwili wote? Hadi katika kiwango ambacho watu wote, wawe wafuasi wa Mungu au wasioamini, walikuwa hawatembelei njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu alikuwa hajapotoshwa tu katika maadili na mwenye wingi wa maovu, lakini pia pale ambapo hakukuwa na mtu aliyesadiki uwepo wa Mungu, tupilia mbali yeyote aliyesadiki kuwa ulimwengu unatawaliwa na Mungu na kwamba Mungu anaweza kuwaletea watu nuru na njia sahihi. Hadi kiwango ambacho binadamu aliudharau uwepo wa Mungu, na hakumruhusu Mungu kuwepo. Pindi upotovu wa mwanadamu ulipofikia kiwango hiki, Mungu asingeweza tena kuwa na subira Ni nini kingechukua nafasi yake? Kuja kwa hasira ya Mungu na adhabu ya Mungu. Huu haukuwa ufunuo kiasi wa tabia ya Mungu? Katika enzi hii ya sasa, yupo bado binadamu mwenye haki katika macho ya Mungu? Yupo bado binadamu mtimilifu katika macho ya Mungu? Enzi hii ndiyo ile ambayo tabia ya miili yote duniani imepotoka mbele ya macho ya Mungu? Katika siku na enzi hii, mbali na wale Mungu anataka kuwafanya kuwa kamili, wale wanaoweza kumfuata Mungu na kuukubali wokovu Wake, huoni kwamba watu wote wa mwili wanapatia changamoto ile mipaka ya subira ya Mungu? Si kila kitu kinachofanyika kando yenu, kila mnachoona kwa macho yenu, na kusikia kwa masikio yenu, na kupitia ninyi binafsi kila siku katika ulimwengu huu kimejaa vurugu? Katika macho ya Mungu, si ulimwengu kama huu, enzi kama hii, inafaa kukomeshwa? Ingawaje usuli wa enzi ya sasa ni tofauti kabisa na usuli wa enzi ya Nuhu, hisia na hasira Alizo nazo Mungu kwa kupotoka kwa binadamu inabakia ileile sawa na ilivyokuwa wakati huo. Mungu anaweza kuwa mwenye subira kwa sababu ya kazi Yake, lakini kulingana na hali na masharti ya aina yote, ulimwengu huu unafaa kuwa uliangamizwa kitambo katika macho ya Mungu. Hali imepita na kupitiliza ile iliyokuwa hapo nyuma wakati ulimwengu uliangamizwa na gharika.
Kimetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I”
Katika upana mkubwa wa dunia hii, mabadiliko yasiyohesabika yamefanyika, bahari kujaa hadi kuziba mashamba, mashamba kufurika hadi baharini, tena na tena. Isipokuwa Yule ambaye anatawala kila kitu katika ulimwengu, Hakuna anayeweza kuongoza na kuelekeza jamii hii ya wanadamu. Hakuna yeyote hodari kufanya kazi au kufanya maandalizi kwa ajili ya jamii hii ya binadamu, sembuse yule anayeweza kuiongoza jamii hii ya wanadamu hadi hatima ya mwanga na kuikomboa kutokana na udhalimu wa duniani. Mungu hulalamikia wakati ujao wa wanadamu, huhuzunishwa na kuanguka kwa mwanadamu na anaumizwa kwamba binadamu wanatembea, hatua baada ya nyingine hadi kuoza na katika njia ambayo hawawezi kurudi. Wanadamu ambao wameuvunja moyo wa Mungu na wakamkana kumfuata yule mwovu: je, kuna yeyote ambaye amewahi kuwaza kuhusu mwelekeo ambao wanadamu wa aina hii huenda wanafuata? Ni kwa sababu hii haswa kwamba hakuna anayehisi hasira ya Mungu, hakuna anayetafuta njia ya kumpendeza Mungu au kujaribu kuja karibu na Mungu na isitoshe, hakuna anayetafuta kufahamu huzuni na maumivu ya Mungu. Hata baada ya kusikia sauti ya Mungu, binadamu anaendelea tu kwenye njia yake mwenyewe, anazidi kwenda mbali na Mungu, kukwepa neema na huduma ya Mungu, na kuepuka ukweli Wake, akiona heri kujiuza kwa Shetani, adui wa Mungu. Na ni nani amefikiri—iwapo mwanadamu ataendelea kuwa mkaidi—jinsi Mungu atakavyowatendea wanadamu hawa ambao wamempuuza bila kusita? Hakuna anayejua kwamba maana ya ukumbusho wa mara kwa mara na kusihi kwa Mungu ni kwa sababu Yeye anayo katika mikono yake maafa yasiyokuwa ya kawaida ambayo ameandaa, maafa ambayo yatakuwa magumu kwa mwili na nafsi ya mwanadamu kustahimili. Maafa haya siyo tu adhabu ya mwili bali pia ya roho. Unafaa kujua hili: Mpango wa Mungu utakaposhindikana na wakati makumbusho Yake na kusihi Kwake hakutapata majibu yoyote, atatoa hasira ya aina gani? Hii itakuwa kama kitu ambacho hakijawahi kushuhudiwa hapo awali au hata kusikika na viumbe vyovyote. Na hivyo Nasema, majanga haya hayana mengine ya kulinganishwa nalo awali na kamwe hayatawahi kurudiwa. Hii ni kwa sababu ni mpango wa Mungu kuumba wanadamu mara hii moja tu na kuwaokoa wanadamu mara hii moja tu. Hii ndiyo mara ya kwanza na pia ni ya mwisho. Kwa hivyo, hakuna anayeweza kuelewa nia za bidii na hamu ya ari ambazo kwazo Mungu huokoa wanadamu wakati huu.
Kimetoholewa kutoka katika “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu”
Siku za mwisho zimefika na nchi nyingi ulimwenguni ziko katika machafuko. Vurugu ya kisiasa, njaa, ndwele, mafuriko, na ukame unaonekana kila mahali. Kuna maangamizi katika ulimwengu wa mwanadamu; Mbingu pia imetuma msiba hapa chini. Hizi ni ishara za siku za mwisho. Lakini kwa watu, unaonekana kama ulimwengu wa uchangamfu na fahari, ambao unaendelea kuwa hivyo zaidi na zaidi. Mioyo ya watu yote inavutiwa nao, na watu wengi wananaswa na hawawezi kujinasua kutoka kwa ulimwengu; idadi kubwa itadanganywa na wale wanaoshiriki katika hila na uchawi.
Kimetoholewa kutoka katika “Utendaji (2)”
Maafa yote yatatokea moja baada ya nyingine; mataifa yote na maeneo yote yatapitia maafa—tauni, njaa, mafuriko, ukame na matetemeko ya ardhi yatakuwa kila mahali. Maafa haya hayatokei tu sehemu moja au mbili, wala hayataisha kwa siku moja au mbili, lakini badala yake yataeneza juu ya eneo kubwa zaidi na zaidi, na maafa yatakuwa makali zaidi na zaidi. Wakati huu kila namna ya wadudu tauni watatokea kwa mfululizo, na tukio la watu kuwala watu litatokea kila mahali. Hii ni hukumu Yangu juu ya mataifa yote na watu.
Kimetoholewa kutoka katika “Sura ya 65” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni
Fungueni macho yenu na muangalie, na mnaweza kuona nguvu Zangu kuu kila mahali! Mnaweza kuwa na uhakika na Mimi kila mahali. Ulimwengu na anga vinaeneza nguvu Zangu kuu. Maneno ambayo Nimenena yametimia katika ongezeko la joto la hali ya hewa, katika mabadiliko ya hali ya hewa, katika ukosefu wa ukawaida ndani ya watu, katika ulemavu wa elimumwendo ya kijamii, na katika udanganyifu ulio mioyoni mwa watu. Jua linakuwa jeupe na mwezi unakuwa mwekundu; vyote haviko katika usawa. Je, kweli bado hamuoni mambo haya?
Nguvu kuu ya Mungu inafichuliwa katika haya. Ni bila shaka, Yeye ni Mungu mmoja wa kweli—Mwenyezi—ambaye watu wamemwandama kwa miaka mingi! Nani anayeweza kufanya vitu viwepo kwa kunena maneno tu? Mwenyezi Mungu wetu pekee. Punde Anapozungumza, ukweli huonekana. Unawezaje kukosa kusema kwamba Yeye ni Mungu wa kweli?
Kimetoholewa kutoka katika “Sura ya 39” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni
Leo hii, Sishuki tu juu ya taifa la joka kuu jekundu, Mimi pia Nageuza uso Wangu kuelekea ulimwengu mzima, mpaka kila kitu cha mbingu kinatetemeka. Kunayo sehemu hata moja isiyopitia hukumu Yangu? Kunayo sehemu isiyo chini ya mateso Ninayovurumisha kuelekea chini? Kila Ninapoenda Nimesambaza “mbegu za maafa” ya kila aina. Hii ni mojawapo ya njia ambazo Nafanya kazi, na bila shaka ni kitendo cha ukombozi kwa ajili ya mwanadamu, na kile Ninachompa bado ni aina ya upendo. Nataka kufanya hata watu zaidi wapate kunijua Mimi, waweze kuniona Mimi, na kwa njia hii wapate kumcha Mungu ambaye wao hawajamwona kwa miaka mingi sana lakini ambaye, leo hii, ni halisi.
Kimetoholewa kutoka katika “Sura ya 10” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima
Lakini ulimwengu wa kitambo ukiendelea kuwepo, Nitavurumisha hasira Yangu kwa mataifa yake, Nikieneza amri Zangu za utawala katika ulimwengu mzima, na kuleta kuadibu kwa yeyote anayezikiuka:
Ninapougeuza uso Wangu kwa ulimwengu kuzungumza, binadamu wote wanasikia sauti Yangu, na hapo kuona kazi yote ambayo Nimefanya katika ulimwengu. Wale wanaoenda kinyume na mapenzi Yangu, hivyo ni kusema, wanaonipinga kwa matendo ya mwanadamu, watapitia kuadibu Kwangu. Nitachukua nyota nyingi mbinguni na kuzitengeneza upya, na kwa mujibu Wangu jua na mwezi vitafanywa upya—anga hazitakuwa tena jinsi zilivyokuwa hapo awali; vitu visivyohesabika duniani vitafanywa kuwa vipya. Yote yatakuwa kamili kupitia maneno Yangu. Mataifa mengi katika ulimwengu yatagawanishwa upya na kubadilishwa kuwa taifa Langu, ili kwamba mataifa yote yaliyomo duniani yatatoweka milele na kuwa taifa linaloniabudu Mimi; mataifa yote ya dunia yataangamizwa, na hayatakuwepo tena. Kati ya binadamu walio ulimwenguni, wale wote walio wa Shetani wataangamizwa; wale wote wanaomwabudu Shetani watalazwa chini na moto Wangu unaochoma—yaani, isipokuwa wale walio ndani ya mkondo, waliobaki watabadilishwa kuwa jivu. Nitakapoadibu watu wengi, wale walio katika dunia ya kidini, kwa kiasi tofauti, watarudi kwa ufalme Wangu, wakiwa wameshindwa na kazi Yangu, kwani watakuwa wameona kufika kwa Aliye Mtakatifu akiwa amebebwa juu ya wingu jeupe. Wanadamu wote watafuata aina yao, na watapokea kuadibu kunakotofautiana kulingana na kile walichofanya. Wale ambao wamesimama kinyume na Mimi wataangamia; na kwa wale ambao matendo yao duniani hayakunihusisha, kwa sababu ya vile wamejiweka huru wenyewe, wataendelea kuwa duniani chini ya uongozi wa wana Wangu na watu Wangu. Nitajionyesha kwa mataifa mengi yasiyohesabika, Nikipaza sauti Yangu kote duniani Nikitangaza kukamilika kwa kazi Yangu kuu ili wanadamu wote waone kwa macho yao.
Kimetoholewa kutoka katika “Sura ya 26” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima