01Kwa kuwa Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi, hiyo inamaanisha kuwa kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu imekamilika?

Watu wengi huamini kwamba wakati Bwana Yesu alisema “Imekwisha” Alipokuwa msalabani, hiyo ilimaanisha kuwa kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu ilikuwa imekamilika. Lakini, je, hivyo ndivyo ilivyo kweli? Ukweli ni kwamba, Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi, ambayo ilihusisha tu kuwasamehe watu dhambi zao. Hakuondoa asili yao ya dhambi au tabia zao za kishetani. Wakiwa wamefungwa na dhambi zao, watu bado hawawezi kujizuia kutenda dhambi na kumpinga Mungu. Sote tunaishi katika hali ya kutenda dhambi na kukiri, tusiweze kabisa kuepuka minyororo ya dhambi. Ili kuwaokoa wanadamu kutoka katika dhambi kabisa, Mungu anahitaji kufanya hatua nyingine ya kazi katika siku za mwisho, kazi ambayo ni mpya zaidi na ya juu zaidi kuliko ile iliyotangulia.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34–35).

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” ( Waebrania 9:28).

“Ninyi mnaohifadhiwa na nguvu zake Mungu kupitia imani hadi kwa wokovu ambao uko tayari kufichuliwa katika muda wa mwisho” (1 Petro 1:5 ).

“Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

“Na nikamwona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, akiwa na injili ya daima kuwahubiria hao wanaoishi katika ulimwengu, na kwa kila taifa, na ukoo, na lugha, na watu, Akisema kwa sauti kuu, Mwogopeni Mungu, na kumpa utukufu; kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja: na mumsujudie yule aliyeziumba mbingu, na ulimwengu, na bahari, na chemchemi za maji” (Ufunuo 14:6-7).

02Hatua tatu za kazi kwa pamoja ndizo kazi kamili ya Mungu kuwaokoa wanadamu

Baada ya wanadamu kupotoshwa na Shetani, Mungu alitoa sheria Yake ili kuwaongoza watu katika maisha yao na ili waweze kujua dhambi ilikuwa nini. Kufikia mwishoni mwa Enzi ya Sheria, wanadamu walikuwa wanazidi kupotoka kwa kina zaidi hadi kufikia hatua kwamba hakuna mtu aliyeweza kufuata sheria, na wote walikuwa katika hatari ya kuuawa. Bwana Yesu Mwenyewe alipata mwili na kufanya kazi ya kuwakomboa wanadamu, Akiwaruhusu watu waokolewe kwa imani yao na kuepuka shutuma na kulaaniwa chini ya sheria. Licha ya ukombozi huu, asili ya watu ya kishetani bado imekita mizizi na hawawezi kujizuia ila kuendelea kutenda dhambi. Ili kuwaokoa wanadamu kikamilifu kutoka dhambini, Mungu bado anahitaji kutekeleza kazi ya hukumu katika siku za mwisho, kwa kuwa ni baada ya hapo tu ndipo watu wataokolewa kutoka katika dhambi na kutakaswa kabisa. Hii ndiyo maana mpango mzima wa usimamizi wa Mungu unajumuisha hatua tatu za kazi.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Na akaniambia, Imekwisha. Mimi ndiye Alfa na Omega, mwanzo na pia mwisho. Nitampa yeye aliye na kiu ya chechichemi ya maji ya uhai bila malipo. Yeye anayeshinda atavirithi vitu vyote; nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwana Wangu” (Ufunuo 21:6–7 ).

03Mpango wa Mungu wa wokovu unakuaje wa kina katika kila moja ya hatua tatu?

Kila moja ya hatua tatu za Mungu za kuwaokoa wanadamu ni ya juu na ya kina zaidi kuliko ya awali. Zina uhusiano wa karibu sana, kila hatua ikifanywa juu ya msingi wa hatua iliyotangulia. Katika Enzi ya Neema, kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu ilifanywa juu ya msingi wa kazi ya Enzi ya Sheria, na pia iliweka msingi wa kazi ya Mungu ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho. Bila kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, tusingeweza kusamehewa dhambi zetu kamwe. Bila kazi ya Mungu ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho, wale ambao wamekombolewa na Mungu hawataweza kamwe kuepuka dhambi zao na kupata wokovu kamili. Hatua tatu za kazi ya Mungu za kuwaokoa wanadamu zinatekelezwa ili kuwaokoa watu kabisa kutoka katika ushawishi wa Shetani, na hatua hizi tatu kwa pamoja pekee ndizo zinakamilisha mpango mzima wa usimamizi wa Mungu.

Mchakato Mzima wa Wokovu wa Mungu wa Wanadamu: Hatua Tatu za Kazi

Tovuti Rasmi