01Mungu kurudi akiwa katika mwili katika siku za mwisho kunatimiza kikamilifu unabii wa Bwana

Waumini wengi wanamngojea Bwana ashuke akiwa juu ya wingu na aonekane kwa wanadamu. Hata hivyo, unabii unaohusu kurudi Kwake tayari umetimia, hivyo kwa nini hatujamwona Akishuka akiwa juu ya wingu? Kwa kweli, unabii unaohusu kurudi kwa Bwana hauzuiliwi tu kwa Yeye kushuka akiwa juu ya wingu, kwa kuwa pia kuna unabii kuhusu Yeye kuja kwa siri, kama vile “Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja” (Luka 12:40). “Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa” (Mathayo 24:37), na zaidi. Bwana tayari Amekuja akiwa katika mwili kama Mwana wa Adamu, akitembea kimya kimya miongoni mwetu, na hivyo kutimiza unabii wa “kuja kwa Mwana wa Adamu.”

Aya za Biblia za Kurejelea

“Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja” (Luka 12:40).

“Lakini kama jinsi zilivyokuwa zile siku za Nuhu, ndivyo pia kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa” (Mathayo 24:37).

“Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24–25).

“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).

02Kwa nini Mungu katika siku za mwisho Awe mwili tena ili Aonekane na kufanya kazi?

Aya za Biblia za Kurejelea

“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” (Waebrania 9:28).

“Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

“Kwa kuwa ameiteua siku, ambayo atauhukumu ulimwengu kwa haki, kupitia kwa yule mtu ambaye ameteua” (Matendo 17:31).

“Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana” (Yohana 5:22).

“Na yeye amempa mamlaka ya kuhukumu pia, kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu” (Yohana 5:27).

03Matokeo ya kutokubali ukweli wa Mungu kurudi akiwa katika mwili ni yapi?

Mungu amerudi akiwa katika mwili kama Mwana wa Adamu ili aonekane na kufanya kazi Yake katika siku za mwisho, na Anafanya hili kwa ajili ya kuwaokoa wanadamu wapotovu kutoka dhambini kabisa, ili watu waweze kutakaswa na kupata wokovu kamili wa Mungu. Baada ya kazi ya wokovu ya Mungu mwenye mwili kufika tamati, Atashusha majanga makubwa na Ataanza kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu. Baadaye, Atashuka akiwa juu ya wingu na kujifichua waziwazi kwa watu wote. Kisha Mungu atawaongoza wale wote ambao wametakaswa na kuokolewa kikamilifu hadi katika ufalme Wake, huku wale ambao wamekataa na kupinga kupata mwili kwa mara ya pili kwa Mungu watakumbwa na majanga hayo makubwa, nao watalia na kusaga meno yao.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha. Kisha hao mabikira wote wakaamka na kutayarisha taa zao. Nao wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, Tugawieni mafuta yenu kiasi; kwani taa zetu zimezimika. Lakini wenye busara wakajibu, wakisema, Hatuwezi; yasije yakakosa kututosha sisi na ninyi: lakini ni heri muende kwa wale wanaouza na mkajinunulie. Na wakati walienda kununua, bwana harusi alikuja; na wale waliokuwa tayari wakaingia ndani na yeye kwa harusi: nao mlango ukafungwa. Baadaye wale wanawali wengine pia wakaja, wakisema, Bwana, Bwana tufungulie. Lakini akajibu na kusema, Kweli nawambieni, Siwajui” (Mathayo 25:6–12).

“Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye. Hata hivyo, Amina” (Ufunuo 1:7).

“Lakini wenye woga, na wasiosadiki, na wa kuchukiza mno, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na wanaoabudu sanamu, na waongo wote, watakuwa na sehemu yao katika ziwa linalochoma kwa moto na kiberiti: ambacho ni kifo cha pili” (Ufunuo 21:8).

Bwana Alisharudi Kitambo Akiwa Katika Mwili ili Aonekane na Kufanya Kazi

Tovuti Rasmi