01Tunawezaje kushuhudia kuonekana kwa Mungu na kukaribisha kurudi kwa Bwana?

Linapokuja suala la kumkaribisha Bwana, watu wengi wanatarajia kumwona Bwana Yesu akiwaonekania wanadamu katika Roho. Lakini, je, hii ndiyo njia sahihi ya kumlaki Bwana? Sote tunajua kuwa Ayubu alisema “Nimesikia kukuhusu kwa kusikia na masikio: lakini sasa jicho langu lakuona.” kwa sababu alisikia sauti ya Yehova katika upepo wa kimbunga. Petro pia aliisikia sauti ya Bwana Yesu, ambavyo ndivyo alivyomtambua Yesu kama Kristo. Tunaweza kuona hapa kwamba haijalishi jinsi Mungu anavyowaonekania watu, wanaweza tu kubaini kwamba kweli ni kuonekana kwa Mungu kwa kusikia sauti ya Mungu. Ni wazi kuwa kuweza kuisikia sauti ya Mungu ndiyo njia pekee ya kushuhudia kuonekana Kwake na kumpokea Bwana aliyerejea.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).

“Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua wao, nao hunifuata” (Yohana 10:27).

“Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa” (Ufunuo 2:7).

02Sauti ya Mungu ni nini? Tunawezaje kuwa na uhakika kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni sauti ya Mungu?

Sauti ya Mungu inarejelea matamko Yake—inarejelea ukweli. Iwe Mungu anaongea katika umbo Lake la mwili au la Roho Wake, Yeye amesimama mahali pa juu akizungumza na wanadamu wote. Hii ndiyo sauti na sifa bainifu ya maneno ya Mungu, na njia ya kipekee ya kunena ya Bwana wa uumbaji. Yeyote aliye na moyo na roho atahisi kuwa maneno ya Mungu ni ukweli, kwamba ni yenye mamlaka na yenye nguvu mara tu atakapoyasikia. Atayajua kuwa sauti ya Mungu! Bwana Yesu tayari amerudi—Yeye ni Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Anaonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu. Kwa hivyo tunawezaje kuthibitisha kwamba maneno ya Mwenyezi Mungu ni sauti ya Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea

“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana1:1).

“Yesu akanena kwake, Mimi ndiye njia, ukweli, na uzima: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu” (Yohana 14:6).

“Ni Roho anayetia uhai, mwili haufai kitu; maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai” (Yohana 6:63).

“Kwa kuwa neno la Mungu ni la haraka na lenye nguvu, na ni kali kuliko upanga wowote ukatao kuwili, likiuchoma hata kuzigawanya roho na nafsi, na viungo na uboho, na linatambua fikira na nia za moyo” (Waebrania 4:12).

“Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17).

“Na mtajua ukweli, na ukweli huo utawaweka huru” (Yohana 8:32).

1)Maneno ya Mungu ndiyo njia, ukweli na uzima.

2)Maneno ya Mungu ni onyesho la tabia ya Mungu. Hayo ni yenye nguvu na mamlaka.

3)Mungu huonyesha ukweli na kuleta kazi Yake ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho.

03Matokeo ya kufuata yale tunayoweza kuona pekee wakati wa kumkaribisha Bwana ni yapi?

Ukweli unaoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, umekuwa ukipatikana wazi mtandaoni kwa muda fulani ili watu kutoka ulimwenguni kote watafute na kuchunguza. Waumini wengi wa kweli wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu wameona kwamba maneno yote yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, kwamba ni yenye nguvu na yenye mamlaka. Wameyatambua kama sauti ya Mungu na wamgeukia Mwenyezi Mungu, mmoja baada ya mwingine. Hata hivyo, kuna wale ambao husisitiza kwamba Bwana atakuja Akiwa juu ya wingu na hukataa kuisikiliza sauti ya Mungu. Wengine hata wameisikia sauti ya Mungu lakini hawatakubali kuwa huku ni kuonekana kwa Mungu, na wanapinga na kushutumu kurudi kwa Bwana. Matokeo ya jambo hili yatakuwa yapi?

Aya za Biblia za Kurejelea

“Yule ambaye ni wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu: nyinyi kwa hivyo hamyasikii, kwa kuwa nyinyi si wa Mungu” (Yohana 8:47).

“Kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini” (Yohana 20:29).

“Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye. Hata hivyo, Amina” (Ufunuo 1:7).

Je, Umeisikia Sauti ya Mungu?

Tovuti Rasmi