01Maafa yanatokea moja baada ya nyingine na ishara za kurudi kwa Bwana zimeonekana—tayari amerudi

Tauni, njaa, matetemeko ya ardhi, mafuriko na maafa mengine yamekuwa matukio ya kawaida kote ulimwenguni mara nyingi, na yanazidi kuwa mabaya. Matukio ya ajabu ya mbinguni pia yameonekana. Unabii wa kurudi kwa Bwana umetimia kwa kiasi kikubwa. Bwana Yesu, ambaye tumekuwa tukimtamani kwa miaka mingi, alishuka kwa siri miongoni mwetu zamani.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Na jinsi ilivyokuwa katika siku za Nuhu, hivyo ndivyo itakavyokuwa pia katika siku za Mwana wa Adamu. Walikula, walikunywa, walioa, waliolewa, mpaka siku ambayo Nuhu aliingia ndani ya safina, na gharika ikaja, na kuwaangamiza wote. Vile vile pia ilivyokuwa siku za Loti: walikula, wakanywa, walinunua, waliuza, walipanda, walijenga; Lakini siku iyo hiyo ambayo Loti alitoka Sodoma kulinyesha moto na kiberiti kutoka mbinguni, na kuwaangamiza wote. Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika siku ambapo Mwanadamu atafunuliwa” (Luka 17:26–30).

“Na ninyi mtasikia kuhusu vita na uvumi juu ya vita: hakikisheni msihangaike: kwani mambo haya yote lazima yafanyike, lakini mwisho bado hujafika. Kwani taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme: na kutakuweko na njaa, na ndwele, na ardhi kutetemeka katika sehemu mbalimbali. Yote haya ndiyo asili ya huzuni” (Mathayo 24:6–8).

“Na nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani, damu, na moto, na miimo ya moshi. Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja kwa siku kuu na ya kutisha ya Yehova” (Yoeli 2:30–31).

“Na nikaona wakati ambapo alikuwa ameufungua muhuri wa sita, na, tazama, kulikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; na jua likageuka kuwa jeusi kama gunia la nywele, na mwezi ukageuka kuwa kama damu. Na nyota za angani zikaanguka duniani, jinsi vile mtini unavyopukuta matini yake kwa wakati usiofaa unapotikiswa na upepo mkali” (Ufunuo 6:12–13).

“Punde tu baada ya matata ya siku hizo ndipo jua litafifiza, nao mwezi hautatoa nuru yake, nazo nyota zitashuka chini kutoka mbinguni, nazo nguvu za mbinguni zitatetemeshwa” (Mathayo 24:29).

02Bwana anarudi kwa siri kabla ya maafa, kisha Atajidhihirisha wazi wazi baada ya maafa

Kuhusu suala la kumkaribisha Bwana, watu wengi hutilia maanani tu unabii wa Bwana kuja juu ya wingu huku wakipuuza unabii wa Bwana kuwa mwili na kuja kwa siri: “Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja(Luka 12:40). “Tazama, mimi nakuja kama mwizi(Ufunuo 16:15). Kwa kweli, Bwana anarudi kwa siri kabla ya maafa na kufanyiza kundi la washindi, kisha Atatokea waziwazi baada ya maafa kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu. Jambo hili linatimiza kabisa unabii wa kurudi kwa Bwana.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja” (Luka 12:40).

“Tazama, mimi nakuja kama mwizi. Amebarikiwa yeye anayekesha, na kuzihifadhi nguo zake, asije akatembea uchi, na wao waione haya yake” (Ufunuo 16:15).

“Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki” (Luka 17:24–25).

“Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno Yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47–48).

“Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu” (1 Petro 4:17).

“Na kisha itatokea ishara yake Mwana wa Adamu huko mbinguni: na kisha makabila yote ya dunia yataomboleza, na wao watamwona yule Mwana wa Adamu akifika kwa mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mkubwa” (Mathayo 24:30).

“Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye. Hata hivyo, Amina” (Ufunuo 1:7).

“Kwa sababu umeniona, umeamini, wamebarikiwa wale ambao hawajaona, lakini wameamini” (Yohana 20:29).

03Jinsi ya kumkaribisha Bwana anapokuwa hapa kwa siri

Kabla ya maafa, Bwana anakuja kwa siri, lakini Atajidhihirisha hadharani baada ya maafa. Kwa hivyo, tunawezaje kumkaribisha Bwana anapokuwa hapa kwa siri? Bwana Yesu alisema, “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). Bwana anaporudi duniani katika siku za mwisho, Ananena maneno ili kuwatafuta kondoo Wake. Wanawali wenye busara wanasikia sauti ya Mungu na wanaikubali na kuifuata. Hawa ndio watu wanaompokea Bwana na kuhudhuria karamu Yake kabla ya maafa makubwa.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote” (Yohana 16:12–13).

“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).

“Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha” (Mathayo 25:6).

“Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho” (Ufunuo 2:7).

“Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua wao, nao hunifuata” (Yohana 10:27).

Makala ya Marejeo

Utabiri wa Nyakati za Mwisho Umetimia: Jinsi ya Kukaribisha Ujio wa Pili wa Bwana

Utabiri wa Nyakati za Mwisho Umetimia: Jinsi ya Kukaribisha Ujio wa Pili wa Bwana

Ishara za Nyakati za Mwisho Zimeonekana na Bwana Yesu Atarudije?

Ishara za Nyakati za Mwisho Zimeonekana na Bwana Yesu Atarudije?

Video za Marejeo

Mada Zaidi

Bwana Amerudi
Mwokozi Amerudi Tayari Juu
Jinsi ya Kunyakuliwa Kabla ya Dhiki
Jinsi ya Kunyakuliwa Kabla ya Dhiki
Hukumu ya Kiti Kikuu Cheupe cha Enzi Ilianza Zamani
Hukumu ya Kiti Kikuu Cheupe cha Enzi Ilianza Zamani
Bwana Alisharudi Kitambo Akiwa Katika Mwili ili Aonekane na Kufanya Kazi
Bwana Alisharudi Kitambo Akiwa Katika Mwili ili Aonekane na Kufanya Kazi