01Je, kukubali njia ya toba ya Enzi ya Neema kweli inamaanisha kupata njia ya uzima wa milele?

Kwa kuamini katika Bwana na kukiri dhambi zetu Kwake, tunasamehewa dhambi zetu na tunaweza kufurahia neema na baraka za Mungu. Hili linatupa tumaini la uzima wa milele, na wengi wanaamini kwamba huku ndiko kupata njia ya uzima wa milele. Lakini, je, hiyo ni kweli? Sote tunajua kuwa Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema, akiwafundisha wanadamu kukiri na kutubu kwa Mungu, kuwa na unyenyekevu na uvumilivu katika kila kitu, kila mtu kubeba msalaba wake, na kadhalika. Haya yote yanazingira ukweli ulioonyeshwa wakati wa kazi ya ukombozi, na ukweli huu ndio njia ya toba. Kwa kukubali njia ya toba, tumesamehewa dhambi zetu na tunaona mabadiliko fulani chanya katika tabia zetu. Hata hivyo, bado tunakosa ufahamu wa kweli wa asili yetu ya dhambi na vile vile ukweli wa jinsi watu wanavyoweza kuwekwa huru kutoka dhambini na kutakaswa. Asili yetu ya dhambi bado imekita mizizi, na bado hatuwezi kujizuia kutenda dhambi, kumpinga Mungu, na kuasi dhidi Yake. Je, huku kunawezaje kuwa ndiko kupata njia ya uzima wa milele?

Aya za Biblia za Kurejelea

“Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17).

“Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele” (Yohana 8:34-35).

“Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu” (Waebrania 9:28).

02Njia ya uzima wa milele ni nini?

Njia ya uzima wa milele siyo rahisi kama tu sisi kukiri na kutubu, na kisha kuwa na tabia nzuri za nje. Badala yake, ni njia ya ukweli inayotuwezesha kuishi milele. Hiyo inamaanisha kusuluhisha kabisa asili yetu ya dhambi, kutuokoa kutoka katika ushawishi wa Shetani, na kutupilia mbali tabia zetu potovu za Shetani ili tuweze kutakaswa na kuokolewa kabisa na Mungu. Kisha ukweli unakuwa maisha yetu, tunakuwa na uwezo wa kumtii Mungu kweli, kumcha na kumpenda, tunakuwa wenye kupatana na Mungu, na tunapatwa kikamilifu na Mungu. Njia hii tu ndiyo njia ya uzima wa milele.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo” (Yohana 16:12-13).

“Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:48).

“Na nikamwona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, akiwa na injili ya daima kuwahubiria hao wanaoishi katika ulimwengu, na kwa kila taifa, na ukoo, na lugha, na watu, Akisema kwa sauti kuu, Mwogopeni Mungu, na kumpa utukufu; kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja: na mumsujudie yule aliyeziumba mbingu, na ulimwengu, na bahari, na chemchemi za maji” (Ufunuo 14:6-7).

“Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo. Na vinywani mwao hakukuwa na hila: kwani hawana hatia mbele ya Kiti cha Mungu cha enzi” (Ufunuo 14:4-5).

03Tunawezaje kupata njia ya uzima wa milele?

Kuna mpango na kuna hatua katika Mungu kuonyesha ukweli kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi katika Enzi ya Neema; Alionyesha njia ya toba, akasamehe dhambi za mwanadamu na akatukomboa kutoka katika mfumbato wa Shetani. Kazi inayofanywa na Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ni kazi ya hukumu, na ukweli Anaoonyesha unaweza kututakasa na kuwaokoa watu kabisa. Hili linatuwezesha kuepuka minyororo ya dhambi, tutakasike, na kupatwa na Mungu. Ukweli huu ndio njia ya uzima wa milele ambao Mungu huwapa wanadamu. Hii ndiyo sababu lazima tukubali ukweli wote unaoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ili tupate njia ya uzima wa milele.

Aya za Biblia za Kurejelea

“Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi” (Ufunuo 3:20).

“Yeye aliye na sikio, na alisikie neno ambalo Roho aliyaambia makanisa. Kwa yule ambaye anashinda, nitampa matunda ya mti wa uzima ale, ambao uko katikati ya bustani ya Mungu” (Ufunuo 2:7).

“Naye Roho na Bibi harusi wanasema, Kuja. Na Yule anayesikia na aseme, Kuja. Na Yule aliye na kiu na akuje. Na yeyote anayetaka, na anywe maji ya uzima kwa uhuru” (Ufunuo 22:17).

“Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata. Na ninawapa uzima wa daima; na wao hawataangamia kamwe, wala hakuna mtu ambaye atawapokonya kutoka mkononi Mwangu” (Yohana 10:27-28).

“Wamebarikiwa wale wanaofanya amri zake, ili wawe na haki ya mti wa uzima, na waweze kuingia mjini humo kupitia malango yake” (Ufunuo 22:14).

Makala ya Marejeo

Je, Kauli “Yule Amwaminiye Mwana Ana Uzima wa Milele” Inamaanisha Nini Hasa?

Je, Kauli “Yule Amwaminiye Mwana Ana Uzima wa Milele” Inamaanisha Nini Hasa?

Video za Marejeo

Mada Zaidi

Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Mchakato Mzima wa Wokovu wa Mungu wa Wanadamu: Hatua Tatu za Kazi
Kuokolewa dhidi ya Kupata Wokovu Kamili
Kuokolewa dhidi ya Kupata Wokovu Kamili
Hukumu ya Kiti Kikuu Cheupe cha Enzi Ilianza Zamani
Hukumu ya Kiti Kikuu Cheupe cha Enzi Ilianza Zamani
Jinsi Mwanadamu Anaweza Kutakaswa Upotovu
Jinsi Mwanadamu Anaweza Kutakaswa Upotovu