Nimepata Njia ya Kuingia Katika Ufalme wa Mbinguni

13/08/2020

Mwenyezi Mungu anasema, “Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima(Neno Laonekana katika Mwili). Maneno ya Mungu ni bayana sana. Bwana Yesu alifanya kazi ya ukombozi, ambayo ilikuwa tu kusamehe dhambi za wanadamu. Yeye hakutondolea asili zetu za dhambi. Bado tunahitaji Bwana arudi katika siku za mwisho kufanya kazi ya hukumu na utakaso, kutupa ukweli zaidi na kutatua asili yetu ya dhambi ili tuweze kuondokana na utumwa wa dhambi kikamilifu. Kisha hatutafanya dhambi tena au kumpinga Mungu, na tutakuwa watu wanaomtii na kumcha Mungu. Hivyo pekee ndivyo tutakavyostahili kuingia katika ufalme wa Mungu. Sikuelewa kazi ya Mungu hapo awali. Nilidhani kwamba Bwana alikuwa Amesamehe dhambi zetu, kwa hivyo tumehesabiwa haki kwa imani na tunaweza kuingia mbinguni. Lakini baada ya zaidi ya miaka 10 ya imani, bado nilifanya dhambi wakati wote na sikuweza kutenda maneno ya Bwana. Mungu ni mtakatifu, na hakuna mtu asiye mtakatifu anayeweza kumwona Mungu, kwa hivyo mtu anayeishi katika dhambi kama mimi anaweza kweli kunyakuliwa na kuingia katika ufalme wa Mungu Bwana atakapokuja? Nilikanganyikiwa. Sikuweza kubaini jambo hilo. Ni baada tu ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu ndipo nilielewa kwamba sikuwa na uzoefu wa hatua muhimu zaidi ya kazi ya Mungu— kazi ya hukumu katika siku za mwisho inayoanza na nyumba ya Mungu. Katika imani yetu, lazima tupitie hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ili tabia zetu potovu ziweze kutakaswa. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuokolewa na kuingia katika ufalme. Ningependa kushiriki uzoefu wangu kuhusu hili.

Nimekuwa nikienda kanisani pamoja na wazazi wangu tangu nilipokuwa mdogo. Nilipenda kuwasikiza kina ndugu wakifanya ushirika juu ya maneno ya Bwana. Baada ya kufunga ndoa, mimi na mume wangu bado tuliipa kazi ya kanisa kipaumbele. Tulikuwa tukihusika kikamilifu katika huduma za kanisa, kubwa na ndogo. Lakini baada ya muda, niligundua kwamba mahubiri ya mchungaji yalikuwa makavu sana, na kwamba alizungumza tu mambo ya kawaida, na alikuwa akituhimiza kila wakati tuote sadaka. Alijishughulisha sana na fedha kuliko maisha yetu. Wachungaji na wazee waligombania jukwaa na vyeo vyao na waliliana njama. Ndugu waliohudhuria ibada walizidi kuwa wachache, na walipohudhuria, walipiga domo, au kuzungumza juu ya starehe za mwili, na walilala wakati wa mahubiri. Mimi mwenyewe sikuweza kuhisi mwongozo wa Bwana, na kushiriki katika huduma za kanisa kulichosha sana. Sikuweza kutenda maneno ya Bwana, na nilikuwa nikiishi katika hali ya kufanya dhambi na kisha kukiri. Na nilipomwona mume wangu akija kutoka kazini, na kisha kujitosa katika michezo ya mtandaoni bila kufanya kitu kingine chochote, sikuweza kujizuia kumsumbua na kumkaripia, nikimwambia afanye hivi au vile kwa sauti ya kuamuru. Hakunisikiza, na nilighadhabika hata zaidi. Sikuvumilia hata kumwona akifanya mambo polepole, na nilimkosoa kwa kufanya mambo kwa uzembe. Alikuwa akinikosoa pia kila mara, akisema, “Hujabadilika kamwe hata baada ya miaka mingi ya kuwa muumini.” Nilihisi hatia, na nilifikiria maneno ya Bwana Yesu: “Na kwa nini unaiona chembe ambayo iko ndani ya jicho lake ndugu yako, lakini huoni boriti ambayo iko ndani ya jicho lako mwenyewe? Ama utamwambia vipi ndugu yako, Hebu nitoe chembe kutoka jicho lako; nawe una boriti katika jicho lako mwenyewe?(Mathayo 7:3-4). Bwana alitufundisha kwamba hatupaswi kuangalia kasoro ya watu wengine kila mara, bali tuchunguze kasoro zetu wenyewe. Lakini mume wangu aliposema au kufanya kitu ambacho sikupenda, sikumvumilia. Nilikuwa nikighadhabika kila wakati na kugombana naye. Uhusiano wetu ulizidi kuharibika, na nilikuwa nikiteseka sana. Mungu alisema: “Mtakuwa watakatifu; kwani mimi ni mtakatifu” (Walawi 11:44). Mungu ni mtakatifu, na mtu yeyote asiye mtakatifu hawezi kumwona Bwana. Lakini sikuweza kufuata mafundisho ya Bwana au kutenda maneno Yake. Nilikuwa nikitenda dhambi kila wakati, na sikuweza kuepuka utumwa wa dhambi. Je, mtu kama mimi anawezaje kuingia katika ufalme wa mbinguni? Wazo hili liliniacha nikiwa na wasiwasi.

Wakati mmoja baada ya ibada, nilimuuliza mchungaji kuhusu shaka zangu. Alisema, “Usijali. Ijapokuwa tunatenda dhambi mara kwa mara, Bwana Yesu ametusamehe dhambi zetu zote. Almradi tuendelee kumwomba Bwana na kukiri Kwake, Atakapokuja, atatuleta katika ufalme wa mbinguni.” Alichosema hakikutatua mkanganyiko wangu. Inasema katika Biblia, “Fuata amani na watu wote, na utakatifu, bila huu hakuna mwanadamu atakayemwona Bwana” (Waebrania 12:14). “Kwa sababu tukitenda dhambi makusudi baada ya sisi kupokea maarifa ya ukweli, hakuna tena dhabihu ya dhambi” (Waebrania 10:26). Imeandikwa waziwazi kwamba tusipotenda maneno ya Bwana, tukifanya dhambi kwa makusudi, hakutakuwa na dhabihu nyingine ya dhambi. Kwa hivyo, je, watu wanaofanya dhambi kila wakati wanaweza kweli kunyakuliwa na kuingia mbinguni? Sikujua jinsi ya kuacha kufanya dhambi, kwa hivyo nilijitahidi kuwa na uvumilivu na msamaha ambao Bwana alifundisha, lakini sikuweza kabisa kuviweka katika vitendo. Katika uchungu wangu, nilimtafuta mchungaji tena. Alitikisa kichwa bila msaada na kusema, “Mimi pia sina suluhisho la tatizo la kutenda dhambi na kisha kukiri. Hata Paulo alisema, ‘Kwa sababu kutaka kumo ndani yangu, lakini jinsi ya kutenda lililo jema sipati. Kwani sitendi wema niupendao: ila natenda uovu ambao siupendi’ (Warumi 7:18-19). Hatuwezi kujizuia kutenda dhambi, kwa hivyo tubu tu na ukiri kwa Bwana zaidi, na nitakuombea zaidi pia.” Kusikia haya kutoka kwa mchungaji kulinikatisha tamaa sana. Katika uchungu wangu, nilimwomba Bwana: “Ee Bwana! Sitaki kufanya dhambi, lakini kwa kweli siwezi kujizuia. Kuishi katika dhambi kunanihuzunisha sana lakini sijui jinsi ya kuepuka. Naogopa kwamba Utaniacha haya yakiendelea. Bwana naomba Uniokoe.”

Mwisho wa mwanadamu ndio mwanzo wa Mungu. Nilikutana na Dada Susan mtandaoni siku moja mnamo Mei 2018. Tulishiriki juu ya Biblia sana. Alikuwa na utambuzi wa kipekee kuhusu Biblia na ushirika wake ulitia nuru sana, kwa hivyo nilishiriki naye wasiwasi na shaka yangu katika kutafuta. Nilisema, “Nimemwamini Bwana kwa miaka mingi, lakini siwezi hata kutenda msamaha na uvumilivu. Mimi hufanya dhambi wakati wote. Nina wasiwasi kuwa sitaingia katika ufalme wa mbinguni. Mchungaji wetu husema kwamba Bwana Yesu ametusamehe dhambi zetu zote, na mradi tuombe na kukiri kwa Bwana mara nyingi, Atatupeleka mbinguni Atakapokuja. Lakini bado nimechanganyikiwa moyoni. Je, una maoni gani kuhusu haya?” Dada Susan alisema, “Ni kweli kwamba Bwana Yesu ametusamehe dhambi zetu, lakini hiyo haimaanishi kwamba tumetakaswa, au kwamba hatuwezi kutenda dhambi. Bwana Yesu alisema, ‘Hakika nawaambieni, Yeyote ambaye hutenda dhambi ni mtumishi wa dhambi. Na mtumishi haishi katika nyumba milele: lakini Mwana huishi milele(Yohana 8:34-35). ‘Siye kila mmoja ambaye aliniambia, Bwana, Bwana, ataingia ufalme wa mbinguni, ila yeye atendaye mapenzi ya Baba yangu ambaye yuko mbinguni(Mathayo 7:21). Bwana Yesu hakuwahi kusema tutaingia mbinguni kwa sababu tu dhambi zetu zimesamehewa, na Alituambia waziwazi kuwa ni wale tu ambao hufanya mapenzi ya Baba ndio wanaoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni.” “Tunaweza kuona kwamba kuingia katika ufalme wa Mungu kwa sababu dhambi zetu zimesamehewa ni fikira na mawazo ya kibinadamu. Hayana msingi wowote katika maneno ya Mungu. Tumeona jambo moja la hakika katika miaka yetu ya kuamini: Baada ya watu kupata imani na kusamehewa dhambi, wanaendelea kuishi katika hali ya kufanya dhambi kisha kukiri, kukiri kisha kutenda dhambi. Hii inaonyesha kwamba kumwamini Bwana na kusamehewa dhambi si sawa na kuondokana na utumwa na shutuma za dhambi, na bila shaka haimaanishi kuwa tumetakaswa. Mungu ni mtakatifu. Hawezi kamwe kumruhusu mtu yeyote ambaye bado hufanya dhambi na kumpinga aingie katika ufalme Wake. Ni wale tu ambao wanaweza kumtii Mungu na kufanya mapenzi Yake ndio wanaoweza kuingia katika ufalme wa mbinguni.” Niliposikia ushirika wake, niliwaza, “Hivyo ndivyo ilivyo. Mungu akituruhusu, sisi ambao hutenda dhambi kila wakati, tuingie katika ufalme wa mbinguni, utakatifu Wake unawezaje kuonyeshwa?”

Aliendelea na ushirika wake. “Hata ingawa tunaomba na kukiri kwa Bwana na kujaribu kwa bidii kutenda mafundisho Yake, bila kujali tunajaribu kwa bidii kiasi gani, bado tunazuiliwa na dhambi. Sababu ya hilo hasa ni ipi?” Kisha akasoma vifungu fulani vya maneno ya Mungu. “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi. Wote wanaonyenyekea chini ya utawala Wake watapata kufurahia ukweli wa juu na kupata baraka nyingi mno. Wataishi katika mwanga kwa kweli, na watapata ukweli, njia na uzima.” “Ingawa mwanadamu amekombolewa na kusamehewa dhambi zake, inachukuliwa kuwa Mungu hakumbuki makosa ya mwanadamu na kutomtendea mwanadamu kulingana na makosa yake. Hata hivyo, mwanadamu anapoishi katika mwili na hajaachiliwa huru kutoka kwa dhambi, ataendelea tu kutenda dhambi, akiendelea kufunua tabia yake potovu ya kishetani. Haya ndiyo maisha ambayo mwanadamu anaishi, mzunguko usiokoma wa dhambi na msamaha. Wengi wa wanadamu wanatenda dhambi mchana kisha wanakiri jioni. Hivi, hata ingawa sadaka ya dhambi ni ya manufaa kwa binadamu milele, haitaweza kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye dhambi. Ni nusu tu ya kazi ya wokovu ndiyo imemalizika, kwani mwanadamu bado yuko na tabia potovu. … Sio rahisi kwa mwanadamu kuzifahamu dhambi zake; mwanadamu hawezi kufahamu asili yake iliyokita mizizi. Ni kupitia tu katika hukumu na neno ndipo mabadiliko haya yatatokea. Hapo tu ndipo mwanadamu ataendelea kubadilika kutoka hatua hiyo kuendelea.” “Kupitia kazi hii ya kuadibu na hukumu, mwanadamu atakuja kujua hali yake kamili ya uchafu na upotovu ndani Yake, na ataweza kubadilika kabisa na kuwa msafi. Ni hivi tu ndivyo mwanadamu ataweza kustahili kurudi katika kiti cha enzi cha Mungu. Kazi yote ifanywayo siku hii ya leo ni ili mwanadamu afanywe msafi na kubadilika; kupitia hukumu na kuadibiwa na neno, na pia kutakaswa, mwanadamu anaweza kuacha nje upotovu wake na kufanywa safi. Badala ya kuichukua hatua hii ya kazi kuwa ile ya wokovu, itafaa zaidi kusema kuwa ni kazi ya utakaso(Neno Laonekana katika Mwili).

Dada Susan aliendelea kushiriki baada ya kusoma haya. “Hata ingawa tumepokea ukombozi wa Bwana Yesu na dhambi zetu zimesamehewa, asili zetu za kishetani zinazotusababisha tufanye dhambi hazijatatuliwa. Ndio maana hatuwezi kujizuia kutenda dhambi na kumpinga Mungu wakati wote, na hatuwezi kutenda maneno ya Bwana. Katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya tu kazi ya ukombozi ili kutukomboa kutoka katika dhambi zetu ili tuweze kuepuka kuhukumiwa na kufungwa na sheria, tustahili kuja mbele za Mungu na kufurahia neema na furaha Anayotupa. Hata ingawa Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu, tabia na asili zetu za kishetani hazikutatuliwa. Bado tuna kiburi sana, tunajikweza, tumepotoka, tuna ubinafsi, na tunastahili dharau. Sisi hujifikiria sana, na kutaka kuwa na kauli ya mwisho kila wakati na kuwalazimisha wengine wafanye mambo kwa njia yetu. Mtu anapofanya mambo tusiyoyapenda, tunamkaripia na kumzuia. Pia, tunasema uwongo na kudanganya kila wakati, na sala zetu kwa Mungu ni maneno matupu na ahadi tupu. Sisi huzungumza juu ya kumtii na kumpenda Mungu, lakini katika hali halisi, sisi hufanya kila kitu kwa ajili ya manufaa yetu. Sisi hujitumia na kujitolea kwa ajili ya Mungu ili tubarikiwe na tuingie katika ufalme Wake. Tunafurahia tunapopata neema ya Bwana, lakini tunapokabili dhiki au majaribio, tunakuwa hasi na kulalamika. Tunaweza hata kumkana au kumsaliti Mungu. Tabia hizi za kishetani ni mbaya zaidi na zimekita mizizi zaidi kuliko dhambi. Zisipotatuliwa, tuna uwezekano wa kufanya maovu na kumpinga Mungu wakati wowote. Sisi ni wa namna ya Shetani. Tunawezaje kustahili ufalme wa Mungu? Hii ndiyo maana Bwana Yesu aliahidi kwamba Atarudi. Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, ndiye Bwana Yesu aliyerudi. Ameonyesha ukweli wote ili kuwasafisha na kuwaokoa wanadamu kabisa. Yeye hufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu. Hii hasa ni ili kutatua tabia na asili potovu na za kishetani za wanadamu, kuondoa kabisa tatizo letu la kutenda dhambi na kumpinga Mungu kila wakati, na kututakasa na kutuokoa kabisa, na kutuleta katika ufalme wa mbinguni.” “Kazi na maneno ya Mwenyezi Mungu yanatimiza unabii huu wa Bwana Yesu: ‘Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12-13). ‘Kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho’(Yohana 12:47-48). Na kitabu cha Petro 1 kinasema: ‘Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Kwa kukubali hukumu ya maneno ya Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, tunaweza kupata ukweli. Tabia zetu za kishetani zinaweza kutakaswa, na ni wakati huo tu ndipo tunaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.

Niliona kwamba ushirika wa Dada Susan ulikuwa umejaa nuru na ulilingana na Biblia kabisa. Niliridhika kabisa. Niligundua kuwa katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya tu kazi ya ukombozi, lakini hiyo haikuwa kazi ya kutatua asili ya wanadamu ya dhambi. Imani yetu katika Bwana inaweza tu kutuletea msamaha wa dhambi zetu, na lazima tupitie kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho ili kutatua chanzo cha kutenda dhambi kwetu, kuepukana na dhambi, na kutakaswa. Macho yangu yalifunguliwa. Niliona kwamba kulikuwa na hatua ya kazi ya Mungu ambayo sikuwa nimepitia katika imani yangu. Nilimsikia dada huyu akishiriki kwamba Bwana Yesu tayari alikuwa Amerudi na kuonyesha ukweli mwingi ili kufanya kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu na mwishowe kutuleta katika ufalme wa Mungu. Nilifurahi sana, nilimuuliza Dada Susan papo hapo katika kutafuta, “Je, Mwenyezi Mungu anafanyaje kazi Yake ya hukumu ili kutusafisha?”

Alinisomea vifungu kadhaa vya maneno ya Mwenyezi Mungu. “Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu. Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme.” “Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu(Neno Laonekana katika Mwili).

Dada Susan kisha aliendeleza ushirika wake. “Katika siku za mwisho, Mwenyezi Mungu anaonyesha ukweli ili kufanya kazi ya hukumu. Ameonyesha ukweli wote ili kuwatakasa na kuwaokoa wanadamu kikamilifu, na kufunua siri za kazi ya Mungu ya usimamizi. Amefichua kiini na ukweli wa upotovu wa Shetani kwa wanadamu, na kufunua na kuchambua asili yetu ya kishetani ya kumpinga Mungu, Ametuambia ni tabia na sumu zipi za kishetani zimo katika asili zetu, na sumu hizi za kishetani husababisha hali na mawazo gani yaliyopotoka, na jinsi ya kutatua mambo haya. Maneno ya Mungu pia yanafafanua waziwazi kila kipengele cha ukweli, pamoja na kumtii Mungu ni nini, upendo wa kweli kwa Mungu ni nini, na jinsi ya kuwa mtu mwaminifu. Yanatuonyesha njia ya kuacha tabia zetu potovu na kupata wokovu kamili. Pia yanamfichulia mwanadamu tabia ya Mungu takatifu, ya haki, na isiyokosewa. Kwa kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, tunaweza kuelewa ukweli polepole, na kuelewa kiini na ukweli wa kupotoshwa kwetu na Shetani. Kisha tunakuja kuchukia jinsi ambavyo Shetani ametupotosha sana, tunasujudu mbele ya Mungu na kutubu, na kuzingatia kutenda ukweli. Tabia zetu potovu zinaweza kutakaswa na kubadilishwa polepole, na tunaweza kupata kumcha na kumtii Mungu kiasi. Kisha hatutendi dhambi na kumpinga Mungu sana.” Dada Susan alishiriki nami uzoefu wake wa kibinafsi pia. Alisema kwamba alidhani kila wakati kwamba alikuwa bora zaidi kuliko watu wengine, kwamba alikuwa akijifikiria tu katika kila kitu na aliwashinikiza watu wakubali maoni yake. Alimtenga na kumkaripia yeyote ambaye hakukubaliana naye. Alimdhuru na kumzuia kila mtu. Kupitia hukumu na ufunuo katika maneno ya Mungu, alitambua kwamba alikuwa akiishi kulingana na sheria na mantiki ya Shetani ya “Mimi pekee ndiye ninayetawala” na “Kila kitu kinanihusu.” Alikuwa mwenye kiburi sana na hakukubali kutawaliwa na yeyote, kila wakati akitaka wengine watii na kukubaliana na mawazo yake kana kwamba yalikuwa ukweli. Hakumcha Mungu kabisa na hakuwa na mantiki kabisa. Hii ilimchukiza Mungu na kuwachukiza watu. Aliwataka watu wengine wamsikilize kila mara, na hiyo ni tabia halisi ya kishetani. Shetani ana kiburi na majivuno sana, na yeye hutaka kuwa sawa na Mungu kila wakati. Anataka kuwadhibiti watu, kuwafanya watu wamsikilize na wamche, na kwa hivyo amelaaniwa na Mungu. Alihisi hofu mara alipotambua asili na matokeo ya tatizo hilo, kisha alianza kujichukia na kuzingatia kutenda ukweli. Alianza kuwa mnyenyekevu katika maingiliano yake na wengine. Hakuwadharau tena wala kuwazuia kama hapo awali. Mara nyingi, aliweza kukubali watu wengine walipokuwa sahihi, wakati ambapo maoni yao yalikubaliana na ukweli, na alielewana vyema zaidi na watu. Moyo wangu ulichangamka niliposikia ushirika wake juu ya maneno ya Mwenyezi Mungu na uzoefu wake. Niligundua kuwa Mungu ananena maneno ili kuhukumu na kutakasa tabia zetu potovu. Kufanya kazi kwa Mungu kwa njia hii ili kutuokoa ni kwa vitendo sana! Nilikuwa nimeamini kwa miaka mingi, lakini sikuweza kuepuka utumwa wa dhambi. Nilikuwa nikiishi kwa uchungu mbaya, lakini hatimaye nilikuwa nimepata njia!

Baada ya hapo, nilianza kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, kutazama filamu za injili, na kusikiliza nyimbo kutoka kwa Kanisa la Mwenyezi Mungu kwenye programu ya simu kila siku. Pia nilijiunga na mikutano pamoja na kina ndugu ili kushiriki juu ya maneno ya Mungu. Kwa kweli niliweza kuhisi kazi na mwongozo wa Roho Mtakatifu. Nilielewa siri nyingi na ukweli ambao sikujua katika miaka mingi ya kuwa muumini. Nilikuwa nikifurahia sana. Nilijua moyoni mwangu kuwa Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi!

Nilisoma maneno mengi zaidi ya Mwenyezi Mungu baada ya hapo na nilipata ufahamu kuhusu tabia yangu ya majivuno. Niliona kwamba nilijiona kuwa bora na niliwakaripia wengine na nilikuwa nikifichua tabia yangu ya kishetani. Hicho ni kitu ambacho Mungu anachukia. Nilimwomba Mungu ili kutubu. Sikutaka tena kutenda kulingana na tabia yangu ya kishetani au kuzingatia kila wakati matatizo ya watu wengine. Huko ni kukosa busara. Nilipoona mume wangu akicheza michezo au akifanya kitu kingine ambacho sikupenda, nilimwomba Mungu autulize moyo wangu ili niweze kuzungumza naye kwa utulivu. Siku moja, mume wangu aliniambia ghafla, “Umebadilika! Umekuwa tofauti tangu ulipoanza kumwamini Mwenyezi Mungu. Hukasiriki au kunikemea kama hapo zamani, na unaweza kufanya majadiliano jambo linapotokea.” Nilimshukuru Mungu ndani ya moyo wangu tena na tena. Nilijua kwamba yote hayo yalikuwa yamefanikishwa ndani yangu kupitia maneno ya Mungu. Kilichonishangaza sana ni kwamba mume wangu alipoona mabadiliko yaliyotokea ndani yangu, alianza pia kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, na alikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Mume wangu baadaye alitambua kupitia maneno ya Mungu kwamba michezo ya mtandaoni ni mojawapo ya njia za Shetani za kuwashawishi, kuwadhibiti, na kuwapotosha watu. Alianza kuelewa kiini na hatari ya kucheza michezo ya mtandaoni, na hakufadhaishwa tena nayo. Hatubishani tena. Sisi husoma maneno ya Mungu pamoja, na kufanya ushirika pamoja. Tunapokabiliwa na tatizo au shida, sisi hutafuta ukweli kutoka katika maneno ya Mungu ili kupata suluhisho. Nahisi kweli kuwa kazi ya Mwenyezi Mungu ya hukumu ni kile ninachohitaji kabisa, na kwamba ni muhimu sana ili kututakasa na kutuokoa kikamilifu. Hatimaye nimepata njia ya kutakaswa na kuingia katika ufalme wa mbinguni. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Sauti Hii Yatoka Wapi?

Na Shiyin, ChinaNilizaliwa katika familia ya Kikristo, na jamaa wangu wengi ni wahubiri. Nilimwamini Bwana pamoja na wazazi wangu tangu...

Upendo wa Aina Tofauti

Na Chengxin, BrazilNafasi ya bahati mnamo mwaka wa 2011 iliniruhusu nije Brazili kutoka China. Nilipokuwa nimewasili tu, nilizidiwa na...

Niliupata Mwanga wa Kweli

Qiuhe, Japani Nilizaliwa katika familia ya Kikatoliki. Tangu nilipokuwa mdogo, nilihudhuria Misa kanisani na babu na bibi yangu. Kutokana...

Neno La Mungu Ni Nguvu Yangu

Na Jingnian, KanadaNimefuata imani ya familia yangu katika Bwana tangu nilipokuwa mtoto, nikisoma Bibilia mara nyingi na kuhudhuria ibada....

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp