Utabiri wa Nyakati za Mwisho Umetimia: Jinsi ya Kukaribisha Ujio wa Pili wa Bwana

07/03/2020

Na Anyuan, Ufilipino

Miaka elfu mbili iliyopita, wafuasi wa Bwana walimuuliza Yesu, “Ishara ya kuwasili Kwako, na ya mwisho wa ulimwengu itakuwa ipi?” (Mathayo 24:3). Bwana Yesu alijibu, “Na ninyi mtasikia kuhusu vita na uvumi juu ya vita: hakikisheni msihangaike: kwani mambo haya yote lazima yafanyike, lakini mwisho bado hujafika. Kwani taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme: na kutakuweko na njaa, na ndwele, na ardhi kutetemeka katika sehemu mbalimbali. Yote haya ndiyo asili ya huzuni(Mathayo 24:6-8).Leo, majanga yanatokea zaidi na zaidi kote duniani. Matetemeko ya ardhi, milipuko, njaa, vita na mafuriko yanafanyika moja baada ya lingine. Mwishoni mwa mwaka wa 2019, aina mpya ya kirusi aina ya coronavirus iliibuka mkoani Wuhan, Uchina. Kiwango cha maambukizi yake ni cha kutisha; kwa muda wa miezi michache tu, visa vilitokea kote nchini, na mara moja China ilitumbukia katika machafuko. Mikoa, manispaa na vijiji vingi vinaendelea kutengwa moja baada ya nyingine huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka. Virusi hivyo pia vimeenea hadi katika nchi zingine zaidi ya ishirini kote ulimwenguni. Zaidi ya hayo, kati ya Septemba 2019 na Januari 2020, mioto ya nyikani isambaayo haraka huko Australia iliharibu zaidi ya majengo 5,900 na kuua wanyama zaidi ya bilioni moja. Mnamo Januari 2020, bara hilo hilo lilipigwa na mvua nyingi ya mara moja kwa karne, ikisababisha mafuriko ambayo yaliwaua viumbe wengi wa maji safi. Mwezi huo huo, makumi ya maelfu ya watu waliachwa bila makao kwa sababu ya mafuriko nchini Indonesia. Kulikuwa pia na mlipuko wa volkano huko Ufilipino, kutapakaa kubaya zaidi kwa nzige ndani ya miaka 25 barani Afrika, tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.4 huko Xinjiang. … Orodha hiyo inaendelea. Unabii wa Biblia wa kuja kwa Bwana umetimia. Ni jambo lililo wazi kwamba Bwana amerudi—hivyo kwa nini bado hatujakaribisha kuwasili Kwake? Je, hatutatumbukia katika dhiki kuu ikiwa hili litaendelea? Na tunapaswa kufanya nini hasa ili kukaribisha kuja kwa Bwana?

Utabiri wa Nyakati za Mwisho Umetimia: Jinsi ya Kukaribisha Ujio wa Pili wa Bwana

Bwana Atakuja kwa Namna Gani?

Watu wengi wamesoma maneno haya katika Biblia: “Tazama, anakuja na mawingu” (Ufunuo 1:7). “Na wao watamwona yule Mwana wa Adamu akifika kwa mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mkubwa(Mathayo 24:30). Wana hakika kuwa Bwana atakuja na mawingu. Hata hivyo, kwa nini bado hatujaona tukio kama hilo? Je, hii ndiyo njia ya pekee ambayo Bwana atakuja? Kwa kweli kuna jambo moja kuu ambalo tumelipuuza kuhusu kuja kwa Bwana. Katika maandiko, kuna pia unabii kuhusu Mungu kuja kwa siri, kama vile: “Tazama, mimi nakuja kama mwizi(Ufunuo 16:15). “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). “Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu(Mathayo 24:44). “Kwani kama umeme, unavyomulika chini ya mbingu kutoka sehemu moja, huangaza hadi sehemu nyingine chini ya mbingu; vivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakuwa katika siku yake. Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki(Luka 17:24-25).

Marejeleo ya maandiko “kama mwizi” and “kukawa na kelele sasa sita ya usiku” yanaonyesha kuwa Bwana atakaporudi wakati wa siku za mwisho, Atafanya hivyo kimya kimya, kwa siri. Na “Mwana wa Adamu” linarejelea nini? “Mwana wa Adamu” hakika anazaliwa kutoka kwa mtu, ana mama na baba, na ni mwenye mwili na damu. Chukua Bwana Yesu kwa mfano, Alipata mwili katika mfano wa mtu wa kawaida anayeishi kati ya wanadamu. Kwa hivyo tunaweza kuona kuwa “Mwana wa Adamu” linarejelea Mungu mwenye mwili; Roho hawezi kuitwa Mwana wa Adamu. Aidha, Maandiko pia yanasema, “Bali kwanza lazima apitie mambo mengi, na akataliwe na kizazi hiki.” Kifungu hiki cha Maandiko kinasema wazi kuwa Bwana atakaporudi, Atavumilia mateso mengi na kukataliwa na kizazi hiki. Sote tunajua kuwa Mungu angeweza kukataliwa tu Akiwa katika mwili kama Mwana wa Adamu, kwa maana Mungu katika mwili ni wa kawaida sana na watu hawamjui; wanamchukulia kama mtu wa kawaida, na Anapitia shida nyingi sana kwa sababu hiyo. Hata hivyo, Bwana angemwonekania mwanadamu kama Roho, basi wawe wazuri au wabaya, waumini au wasioamini, au hata wale wanaompinga Mungu, wote wangesujudu mbele ya Mungu katika ibada—kwa kuwa ni nani angeweza kumkataa Mungu hivyo? Na kisha Angeteseka vipi? Hii inaonyesha kuwa Bwana wa siku za mwisho anawaonekania binadamu kama Mwana wa Adamu mwenye mwili.

Bwana Atafanya Kazi Gani Atakaporejea?

Kwa wakati huu, ndugu wengine wanaweza kuchanganyikiwa: Bwana akija kufanya kazi kati ya mwanadamu kwa siri katika siku za mwisho, unabii wa kuja Kwake ndani ya wingu unatimizwaje? Kuna hatua na mpango katika kazi ya Mungu. Kwanza, Mungu anakuwa mwili na kuwasili kwa siri kutekeleza kazi Yake ya kumwokoa mwanadamu, kisha Anamwonekania mwanadamu waziwazi katika wingu. Ili kuelewa swali hili, lazima tujifunze zaidi kuhusu ni kazi gani ambayo Bwana anafanya Anaporudi katika siku za mwisho. Bwana Yesu alisema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). “Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12: 48). “Kwa kuwa Baba hamhukumu mwanadamu yeyote, ila amekabidhi hukumu yote kwa Mwana(Yohana 5:22). Biblia pia inasema, “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Vifungu hivi vya maandiko vinatuambia kuwa Mungu wa siku za mwisho Anakuja kimsingi kunena maneno, kutekeleza kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Kwa sababu hiyo, wale wanaokubali kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho wanakaribisha kuwasili kwa Bwana, na wanainuliwa mbele za Mungu! Leo, Mwenyezi Mungu mwenye mwili Ametamka mamilioni ya maneno yote ambayo yamerekodiwa katika kitabu Neno Laonekana katika Mwili. Katika kitabu hiki, maneno ya Mwenyezi Mungu yanafunua siri nyingi ambazo hapo awali hatungezielewa, kama vile historia ya maendeleo ya wanadamu, jinsi Shetani anavyowaangamiza wanadamu, jinsi Mungu anavyomwokoa mwanadamu, ni watu wa aina gani wanaopendwa na Mungu, ni watu wagani wanaochukiwa na Yeye, matokeo na hatima za watu wa aina mbalimbali, na kadhalika. Si hili tu, bali Mungu pia ameonyesha maneno ya hukumu na kuadibu, Akifunua tabia zetu potovu. Wote wanaokubali maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu watasafishwa na kubadilishwa tabia zao potovu; watafanywa kuwa washindi kabla ya maafa makuu, na mwishowe wataingia katika ufalme wa Mungu ili wafurahie furaha kamili ya milele. Wale wasiofanya jitihada yoyote kuisikia sauti ya Mungu katika kipindi ambacho Mungu yuko katika mwili na Anafanya kazi kwa siri, wasiokubali kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho, wanaomshutumu na kumkufuru Mungu mwenye mwili kulingana na fikira na mawazo yao wenyewe, watafunuliwa na kuondolewa na Mungu. Kwa hivyo, ngano na magugu, kondoo na mbuzi, wanawali wenye busara na wanawali wapumbavu, watumishi wazuri na watumishi wabaya, wale wanaopenda ukweli na wale wanaochukia ukweli—kila mmoja atafunuliwa na kuainishwa kulingana na aina yake. Baada ya hapo, Mungu atakuja na mawingu, Akionekana wazi kwa mataifa yote na watu wote wa dunia, na kuanza kuyazawadi mema na kuadhibu maovu, na hivyo kutimiza unabii wa biblia: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye. Hata hivyo, Amina(Ufunuo 1:7). “Na kisha itatokea ishara yake Mwana wa Adamu huko mbinguni: na kisha makabila yote ya dunia yataomboleza, na wao watamwona yule Mwana wa Adamu akifika kwa mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mkubwa(Mathayo 24:30). Wakati huo, wote wanaompinga, kumkataa na kumshutumu Mungu watajipiga vifua vyao na kujawa na majuto kwa sababu ya matendo yao maovu. Kutoka kwa kazi ya Mungu tunaona jinsi Mungu alivyo mwenye haki, mwenye nguvu na mwenye busara!

Jinsi ya Kukaribisha Kurejea kwa Bwana

Leo, Mwenyezi Mungu mwenye mwili tayari ameshinda na kuliokoa kundi la watu. Pia washindi hao wamekamilishwa. Kazi ya Mungu kwa siri itakamilika hivi karibuni, na baada ya hapo kila aina ya dhiki kuu itaikumba dunia. Tuna kazi ya dharura mbele yetu: Tunapaswa kukaribishaje kurudi kwa Bwana Yesu na kuikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho? Bwana Yesu alisema, “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, na mimi Ninawajua, nao hunifuata(Yohana 10:27). Unabii huu pia unaonekana katika Biblia: “Yeye ambaye ana sikio, hebu asikize lile ambalo Roho huambia makanisa(Ufunuo 2:7). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). Na Mwenyezi Mungu anasema: “Kazi ya Mungu ni kama mawimbi yanayotapakaa kwa nguvu. Hakuna anayeweza kumweka kizuizini, na hakuna anayeweza kusimamisha nyayo Zake. Wale tu wanaosikiza maneno Yake kwa makini, na wanaomtafuta na kuwa na kiu naye, wanaweza kufuata nyayo Zake na kupokea ahadi Zake. Wasiofanya hivyo watakabiliwa na maafa makuu na adhabu inayostahili(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 2: Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote). Je, ungependa kufuata nyayo za Mwanakondoo? Je, ungependa kumkaribisha Bwana? Je, ungependa kunyakuliwa kabla ya dhiki kuu? Maneno ya Mungu yanatuambia kwamba ikiwa tunatarajia kumkaribisha Bwana, ni muhimu kwamba tujifunze jinsi ya kuisikia sauti ya Mungu kwa kuangalia iwapo maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu ni ukweli, iwapo hayo ni maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa. Ninaamini kwamba tukiwa na mioyo minyenyekevu ya kutafuta na kutamani sana ukweli, Mungu atatuongoza katika kumkaribisha Bwana hivi karibuni!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Je, Maafa Yatakapofika, Utakuwa Umetimiza Toba ya Kweli?

Siku, maangamizi ya ulimwengu yanapokua makali zaidi, unabii wa kuja kwa Bwana umetimia. Bwana Yesu alisema, “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17). Toba ya kweli ni nini hasa? Na tunawezaje kutimiza toba ya kweli? Makala haya yatakuambia majibu.

Ishara 6 za kurudi kwa Bwana Yesu Zimeonekana

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alituahidi: “Tazama, Naja upesi” (Ufunuo 22:12). Sasa, kila aina ya ishara za kurudi Kwake zimeonekana, na ndugu wengi wamekuwa na maono kwamba siku ya Bwana iko karibu. Je, Bwana tayari Amerudi? Je, tunaweza kufanya nini ili kumkaribisha Bwana? Hebu tujadili hili sasa kwa kuchunguza unabii ulio katika Biblia.

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp