Ishara za Nyakati za Mwisho Zimeonekana na Bwana Yesu Atarudije?

17/05/2020

Siku za Nuhu Zimeonekana: Je, Hili Linaashiria Nini?

Tunapozungumza juu ya wanadamu katika wakati wa Nuhu, kila mtu anajua kwamba mauaji na uchomaji, unyang’anyi na wizi, na uzinzi ulikuwa maisha ya kawaida kwa watu wa wakati huo. Walimwepa Mungu na hawakusikiza maneno ya Mungu, na mwishowe Mungu aliwaangamiza kwa mafuriko makubwa. Kisha tunawaangalia watu wa ulimwengu wa leo: Wao huucha uovu, na mtu anaweza kuona maeneo kama vile mikahawa ya karaoke, sehemu za kukanda misuli ya miguu, vilabu vya pombe na vilabu vya densi kwenye mitaa na barabara katika kila jiji; watu hula, kunywa na kufurahia, wakijiendekeza katika raha za mwili; watu wengi hushindana kwa ajili ya umaarufu, faida, na hadhi, wakipigana, kuliana njama, na kudanganyana, jamaa na marafiki hawaachwi nyuma. Watu wote hawapendi ukweli, wanapenda dhulma, na wanaishi katika dhambi; hakuna mtu anayechukua hatua ya kutafuta ukweli au kutafuta njia ya kweli, na hata wanamkana na kumpinga Mungu waziwazi. Wanadamu wote wanamilikiwa na Shetani, na hata wale wanaomwamini Bwana hujishusha hadhi na kufuata mienendo ya ulimwengu. Wanatamani raha za dhambi, kila wakati wakiishi katika mzunguko wa kutenda dhambi na kisha kukiri, na hawaweki mafundisho ya Bwana katika vitendo ingawa wanayajua vizuri. Matukio kama haya yanakumbusha unabii uliofanywa na Bwana Yesu miaka elfu mbili iliyopita: “Na jinsi ilivyokuwa katika siku za Nuhu, hivyo ndivyo itakavyokuwa pia katika siku za Mwana wa Adamu. Walikula, walikunywa, walioa, waliolewa, mpaka siku ambayo Nuhu aliingia ndani ya safina, na gharika ikaja, na kuwaangamiza wote. … Hivyo ndivyo itakavyokuwa katika siku ambapo Mwanadamu atafunuliwa(Luka 17:26-30). Tunaweza kuona kutoka katika unabii huu kwamba watu wa siku za mwisho wanapokuwa wapotovu na waovu kama watu wa wakati wa Nuhu, Bwana atakuja tena. Lakini Bwana ataonekana kwa namna gani? Na tunapaswa kumlaki vipi?

Bwana Atakuja Vipi Katika Siku za Mwisho?

Watu wengi huzungumza kuhusu mstari huu katika Biblia: “Na wao watamwona yule Mwana wa Adamu akifika kwa mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mkubwa(Mathayo 24:30). Wao huamini kuwa Bwana atakaporudi, Atafanya hivyo waziwazi juu ya wingu, na kwamba Atatuinua moja kwa moja hadi katika ufalme wa mbinguni na kila mtu Atamwona, na kwa hivyo wanamngojea Bwana aje juu ya wingu bila wao kufanya lolote. Hata hivyo, ukweli ni kwamba tumepuuza unabii wa biblia ambao unasema kuna njia moja zaidi ambayo kwayo Bwana atarudi, kama vile “Tazama, mimi nakuja kama mwizi(Ufunuo 16:15), “Iwapo basi hutakesha, nitakujia kama mwizi….(Ufunuo 3:3), “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20), “Kwa kuwa kama umeme unavyotokea mashariki, na kumulika pia magharibi; ujio wa Mwana wa Adamu utakawa hivyo pia(Mathayo 24:27), na “Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu(Mathayo 24:44). Unabii huu unataja Bwana kurudi “kama mwizi,” na kwamba “nimesimama mlangoni na kupiga hodi.” Hili linathibitisha kuwa Bwana atakuja kimya kimya na kwa siri, na kwamba hili litatokea bila ufahamu wa mtu yeyote. Mistari hii pia inataja “ujio wa Mwana wa Adamu” na “atakapokuja Mwana wa Adamu” na marejeleo yoyote ya “Mwana wa Adamu” yanamaanisha Mungu mwenye mwili. Ni Yule tu aliyezaliwa kutoka kwa mwanadamu na aliye na ubinadamu wa kawaida ndiye anayeweza kuitwa “Mwana wa Adamu”; Bwana angekuja katika umbo la mwili Wake wa kiroho baada ya kufufuka Kwake, basi asingeitwa “Mwana wa Adamu.” Kwa hivyo, hili linaonyesha kuwa katika siku za mwisho, Bwana anarudi katika mwili kufanya kazi miongoni mwa wanadamu kwa siri.

Kwa wakati huu, wengine wanaweza kuhisi kuchanganyikiwa na wanaweza kuwaza, “Biblia inatabiri ya kwamba Bwana atakuja na mawingu na kwamba macho yote yatamwona, lakini pia kwamba Bwana atakuja katika mwili kwa siri. Je, huu sio utata?” Kwa kweli, hakuna utata katika maneno ya Mungu. Kuja kwa Bwana kunafanyika kwa njia mbili: Njia moja ni kwamba Anakuja kwa wazi na mawingu, huku nyingine ni kwamba Anakuja kwa siri kama mwizi. Kila kitu ambacho Mungu alitabiri kitatimizwa na kufanikishwa, lakini Mungu hufanya kazi kwa hatua, na kuna mpango katika kazi Yake. Kwanza Mungu anapata mwili na kuja kwa siri kufanya kazi Yake kumwokoa mwanadamu, na kisha Anaonekana wazi kwa wote, Akiwa juu ya wingu, kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu.

Bwana Anakuja Kufanya Kazi Gani katika Siku za Mwisho?

Kwa nini Mungu anakuja kwa siri kwanza? Hili linahusu kazi ambayo Mungu anafanya Anapoonekana katika siku ya mwisho. Hebu tusome vifungu hivi kutoka katika Biblia: “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). “Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12: 48). “Akisema kwa sauti kuu, Mwogopeni Mungu, na kumpa utukufu; kwa kuwa saa ya hukumu yake imekuja: na mumsujudie yule aliyeziumba mbingu, na ulimwengu, na bahari, na chemchemi za maji(Ufunuo 14:7). “Yule ambaye anashinda nitamfanya awe nguzo katika hekalu lake Mungu wangu, na hatatoka nje tena(Ufunuo 3:12). “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana hatazungumza juu yake mwenyewe; bali chochote atakachosikia, atakinena: na atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12-13). Na neno la Mungu linasema, “Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani. Na kwa hivyo, baada ya mwanadamu kusamehewa dhambi zake, Mungu Amerudi katika mwili kumwongoza mwanadamu katika enzi mpya, na kuanza kazi ya kuadibu na hukumu, na kazi hii imemleta mwanadamu katika ulimwengu wa juu zaidi(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Dibaji).

Tunaweza kuona kutoka katika maneno haya kwamba Bwana atakaporudi katika siku za mwisho, Ataonyesha ukweli zaidi na kutekeleza kazi ya hukumu. Atatumia “neno ambalo [Amenena]” kuhukumu na kufunua upotovu wetu, ili tuweze kutafakari kujihusu, tufanikishe toba na mabadiliko ya kweli, mwishowe tuweze kutakaswa na Mungu na kuwa washindi, ambao wanaongozwa kuingia katika ufalme Wake. Hii ni kwa sababu, ingawa tumekombolewa na Bwana Yesu na dhambi zetu zimesamehewa, kiini cha dhambi zetu, yaani, asili yetu ya dhambi inabaki ndani yetu kwa kina na, tukidhibitiwa nayo, hatuna budi ila kutenda dhambi mara kwa mara. Hapa kuna mifano michache tu: Watu wengine wanapofanya mambo ambayo yanakwenda kinyume na masilahi yetu, tunaweza kuwachukia na hata kukasirika; kwa kawaida, tunasema tutakuwa waaminifu kwa Mungu na kumtii, lakini wakati kitu kitatokea ambacho hatupendi, hatueleweki na kumlaumu Mungu na, katika kesi kali, tunamwelewa Mungu visivyo. Hili linaonyesha kuwa hatujaondokana na minyororo na vizuizi vya dhambi, kwamba bado tunaishi katika hali ya kutenda dhambi na kisha kukiri, na kwamba tunamhitaji Mungu mwenye mwili Atekeleze kazi ya hukumu ili kutakasa upotovu wetu mara moja. Tunaposikia sauti ya Mungu, kuinuliwa mbele za Mungu, na kupitia hukumu na kuadibu kwa maneno ya Mungu, tabia zetu potovu zinapotakaswa, na tunaweza kumtii Mungu, kumwabudu Mungu na kumpenda Mungu katika hali yoyote, hapo ndipo tunapofanywa kuwa washindi na Mungu. Hawa ndio washindi 144,000 kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo, na linatimiza kikamilifu Sura ya 14, Mstari wa 4 katika Ufunuo: “Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo.” Kama Bwana angerudi kwanza juu ya wingu na utukufu mkubwa, basi watu wote wangesujudu ili kumwabudu. Haingewezekana basi kuufunua uasi na upinzani kwa Mungu ulio katika asili ya mwanadamu, na hakungekuwa na msingi wa Mungu kuonyesha ukweli unaolenga kuonyesha kwetu upotovu ili kutuhukumu. Hata kama Mungu angefichua asili yetu potovu, hatungeikubali, na hatungetakaswa na kubadilishwa. Hali ingekuwa hivyo, Mungu hangeweza kutekeleza kazi Yake ya kufanya washindi.

Aidha, katika siku za mwisho, Mungu pia atafichua kila aina ya mtu, amtenganishe kila mmoja kulingana na aina yao, na kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu. Bwana angerudi juu ya wingu na utukufu mkubwa, basi wote wangemwona na kusujudu ardhini kumpokea na kujisalimisha Kwake. Hakuna yeyote, awe alimwamini Mungu au ni wa Shetani, awe alipenda ukweli au la, awe alimtii Mungu au kumpinga, angeweza kufunuliwa na Mungu. Basi, uvunaji na upepetaji kama ilivyotabiriwa katika Biblia na kazi ya kutenganisha kila kulingana na aina yao, kutenganisha kondoo na mbuzi, ngano na magugu, na kadhalika, havingetendeka. Ingawa Mungu anajua ni nani mwema na ni nani mwovu, watu wasipofichuliwa, basi hawatakubali hali hiyo, sembuse kushawishiwa kuihusu. Kwa hivyo ni wazi kuwa Mungu anafanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho ili kumwokoa mwanadamu mara moja, kufanya kikundi cha washindi, na kutenga kila mmoja kulingana na aina yake. Ili kufanya hivi, lazima kwanza Awe mwili na kuja kwa siri. Mara kikundi cha washindi kinapofanywa, kipindi cha kazi ya siri ya Mungu kitakamilika, na ni hapo tu ndipo Mungu atakapokuja waziwazi na mawingu, Akionekana kwa mataifa na watu wote ili kuanza kuwatuza wema na kuwaadhibu waovu. Wote ambao wamekubali kazi ya Mungu ya hukumu na wametakaswa hatimaye wataongozwa kuingia katika ufalme wa Mungu, huku wale ambao hawajakubali kazi ya Mungu mwenye mwili, na ambao wanapinga, kumkashifu, na kumkufuru Mungu, wote watafichuliwa kama watumishi waovu na magugu. Watu kama hao watafagiliwa katika maafa wakilia sana na kusaga meno. Hapo tu ndipo utabiri huu kutoka katika Kitabu cha Ufunuo utatimia: “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye, na pia wale waliomdunga: na makabila yote ya ulimwengu yatalia kwa huzuni kwa sababu ya yeye(Ufunuo 1:7).

Tunapaswa Kulaki Kuonekana na Kazi ya Bwana Vipi?

Tunapaswa Kulaki Kuonekana na Kazi ya Bwana Vipi?

Wakati Mungu mwenye anafanya kazi kwa siri, tunaweza kufanya nini ili kuweza kumlaki Bwana? Ufunuo 3:20 kinasema: “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi.” Mathayo 25:6 kinasema: “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha.” Tunaweza kuona kutoka katika mistari hii kwamba katika siku za mwisho, Mungu atatumia matamko Yake kubisha kwenye milango yetu, na Atawatumia watu kutupigia mayowe na habari kwamba bwana harusi amerudi. Kwa hivyo, mtu anapotuhubiria injili, tunapaswa kutafuta kwa moyo wa kutaka kujifunza na kuzingatia kusikiliza sauti ya Mungu. Mradi tunaitambua kuwa ni sauti ya Mungu, lazima basi tuharakishe kukubali na kutii, na kuenda sambamba na kazi ya Mungu katika siku za mwisho. Hii ndiyo maana ya kulaki kurudi kwa Bwana.

Siku hizi, Kanisa la Mwenyezi Mungu pekee ndilo linaloshuhudia wazi kwamba Bwana amekuja kwa siri katika mwili na kwamba yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho. Mwenyezi Mungu ameonyesha mamilioni ya maneno na Yeye hutekeleza kazi ya hukumu Akianza na nyumba ya Mungu, Akiwatakasa na kuwaokoa wote wanaokuja mbele Yake. Mwenyezi Mungu alionekana na Amekuwa akitekeleza kazi Yake kwa takribani miaka 30, na tayari amefanya kikundi cha walishindi—kazi ya hukumu ya Mungu sasa inakaribia mwisho wake. Maafa yanatokea moja baada ya nyingine ulimwenguni kote; siku za Nuhu zinakaribia. Lazima tuwe mabikira wenye busara na tuharakishe kuichunguza kazi ya Mwenyezi Mungu ya siku za mwisho, kwani kwa kufanya hivyo tutapata nafasi ya kumlaki Bwana na kupatwa kabla maafa hayajafika. Tukishikilia wazo la Bwana kuja na mawingu, tukikataa kutafuta na kuichunguza kazi ya Mungu mwenye mwili, basi tutaachwa na kuondolewa na Bwana, na tutaangamia katika maafa na kuadhibiwa. Ni kama vile Mwenyezi Mungu asemavyo: “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayedaiwa kuwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki. Pengine huo utakuwa wakati wa furaha kubwa kwako, ilhali lazima ujue kuwa wakati utakaposhuhudia Yesu Akishuka kutoka mbinguni ndio pia wakati ambapo utaenda chini kuzimu kuadhibiwa. Huo ndio utakuwa wakati wa mwisho wa mpango wa Mungu wa usimamizi na ndio utakuwa wakati ambapo Mungu atawatunukia wazuri na kuwaadhibu waovu. Kwani hukumu ya Mungu itakuwa imeisha kabla ya mwanadamu kuona ishara, wakati kuna onyesho la ukweli tu(“Kufikia Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu, Mungu Atakuwa Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia” katika Neno Laonekana katika Mwili).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kusadiki Uvumi Kunamaanisha Kupoteza Wokovu wa Mungu wa Siku za Mwisho

Mafarisayo walieneza uongo na kumkashifu na kumkufuru Mungu, na sote tunaweza kukisia mwisho waliokumbana nao, lakini, je, wale watu wa Kiyahudi waliochukulia uongo na kashfa hizo kuwa ukweli—je, mwisho wao haukuwa wa huzuni hivyo? Walipitia maangamizi yasiyo ya kifani ya taifa na watu wa Kiyahudi walitawanyika pande zote. Hawakuwa na nyumbani pa kurudia kwa miaka 2,000. Je, haya siyo matokeo ya kuchukulia uongo wa Mafarisayo kuwa ukweli na kumpinga Mungu?

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp