01Ulimwengu umezongwa na maafa—Bwana tayari amewasili sirini

Tauni, njaa, matetemeko ya ardhi, mafuriko na maafa mengine yamekuwa matukio ya kawaida kote ulimwenguni mara nyingi, na yanazidi kuwa mabaya. Matukio ya ajabu ya mbinguni pia yameonekana. Unabii wa kurudi kwa Bwana umetimia kwa kiasi kikubwa. Bwana Yesu tayari amewasili kwa siri; Ameonyesha ukweli na kutekeleza kazi ya hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu.

Aya za Biblia za Kurejelea

Kwani taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme: na kutakuweko na njaa, na ndwele, na ardhi kutetemeka katika sehemu mbalimbali. Yote haya ndiyo asili ya huzuni(Mathayo 24:7–8).

Na nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani, damu, na moto, na miimo ya moshi. Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja kwa siku kuu na ya kutisha ya Yehova(Yoeli 2:30–31).

Na nikaona wakati ambapo alikuwa ameufungua muhuri wa sita, na, tazama, kulikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; na jua likageuka kuwa jeusi kama gunia la nywele, na mwezi ukageuka kuwa kama damu. Na nyota za angani zikaanguka duniani, jinsi vile mtini unavyopukuta matini yake kwa wakati usiofaa unapotikiswa na upepo mkali(Ufunuo 6:12-13).

Na ninyi pia muwe tayari: maana katika saa kama hii msiyofikiria kuwa Mwana wa Adamu atakuja(Luka 12:40).

Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, atawaongoza hadi kwenye ukweli wote(Yohana 16:12–13).

Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48).

Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17).

02Nafasi ya pekee ya kuokolewa na kuingia katika ufalme wa mbinguni ni kunyakuliwa kabla ya dhiki kuu

Unyakuo kabla ya dhiki kuu ni matamanio ya pamoja ya kila mtu ambaye anatamani sana kuonekana kwa Bwana. Wote wanaofuata nyayo za Mungu na kuja mbele Yake, ambao wanakubali kazi ya Mungu ya hukumu ya siku za mwisho, wote watanyakuliwa hadi mbele ya kiti cha enzi cha Mungu kabla ya dhiki kuu. Ni wao pekee watakaoweza kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo na kufanywa kuwa washindi na Mungu. Dhiki kuu itakapokuja, watalindwa na kuhifadhiwa na Mungu, na kuletwa ndani ya ufalme wa Mungu.

Aya za Biblia za Kurejelea

Na akaniambia, Andika, Wamebarikiwa wale wanaoitwa katika karamu ya arusi ya Mwanakondoo(Ufunuo 19:9).

Na nikamwona malaika mwingine akipaa kutoka mashariki, akiwa na muhuri ya Mungu mwenye uhai; na akawapigia wale malaika wanne walioagizwa kuidhuru dunia na bahari kelele, akisema kwa sauti kubwa, Msiidhuru dunia, wala bahari, wala miti, hadi tutie muhuri kwenye vipaji vya nyuso za watumishi wa Mungu wetu. Na nikasikia idadi ya wao waliotiwa muhuri; na waliotiwa muhuri walikuwa mia moja na arobaini na elfu nne ya makabila yote ya Waisraeli(Ufunuo 7:2-4).

Na nikaangalia, na ona, Mwanakondoo alikuwa amesimama juu ya mlima Sayuni, na pamoja na yeye watu elfu mia moja arobaini na nne, waliokuwa na jina la Baba yake limeandikwa katika mapaji ya nyuso zao. … Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo. Na vinywani mwao hakukuwa na hila: kwani hawana hatia mbele ya Kiti cha Mungu cha enzi(Ufunuo 14:1, 4–5).

Wamebarikiwa wale wanaofanya amri zake, ili wawe na haki ya mti wa uzima, na waweze kuingia mjini humo kupitia malango yake(Ufunuo 22:14).

Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao. Na Mungu atayafuta machozi yote kutoka kwa macho yao, na hakutakuwa na kifo tena, wala huzuni, wala kilio, wala hakutakuwa na uchungu tena; maana yale mambo ya kale yamepita(Ufunuo 21:3–4).

03Jinsi ya kumkaribisha Bwana kabla ya dhiki kuu na kunyakuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu

Kitabu cha Ufunuo chatabiri, “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). Tunaweza kuona kutoka kwa aya hii kwamba jambo la muhimu zaidi katika kukaribisha kuja kwa Bwana ni kuweza kusikia sauti ya Mungu. Kukubali, kutii na kufuata mara tu unapobaini kuwa hii ni sauti ya Mungu ndiyo njia pekee ya kumkaribisha Bwana kabla ya dhiki na kuinuliwa mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.

Aya za Biblia za Kurejelea

Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20).

Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6).

Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua wao, nao hunifuata(Yohana 10:27).

Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo Roho alisema kwa makanisa(Ufunuo 2:11).

Yesu akanena kwake, Mimi ndiye njia, ukweli na uhai(Yohana 14:6).

04Athari za kupoteza nafasi ya kunyakuliwa kabla ya dhiki kuu

Bwana anaporudi katika siku za mwisho kuzungumza, kuonekana na kufanya kazi, wale ambao hawatafuti kusikia sauti ya Mungu—hasa wale wanaosikia sauti ya Mungu lakini bado wanampinga na kumlaumu Mungu mno, ambao wanakataa kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho—watapoteza nafasi yao kwenye unyakuo kabla ya dhiki. Kazi ya Mungu itakapokamilika na dhiki kubwa ishushwe, watu wema watakapoanza kutuzwa na waovu kuadhibiwa, wote ambao hawatakuwa wamenyakuliwa kabla ya dhiki watatumbukizwa kwenye maafa, wakilia na kusaga meno yao.

Aya za Biblia za Kurejelea

"Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha. Kisha hao mabikira wote wakaamka na kutayarisha taa zao. Nao wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, Tugawieni mafuta yenu kiasi; kwani taa zetu zimezimika. Lakini wenye busara wakajibu, wakisema, Hatuwezi; yasije yakakosa kututosha sisi na ninyi: lakini ni heri muende kwa wale wanaouza na mkajinunulie. Na wakati walienda kununua, bwana harusi alikuja; na wale waliokuwa tayari wakaingia ndani na yeye kwa harusi: nao mlango ukafungwa. Baadaye wale wanawali wengine pia wakaja, wakisema, Bwana, Bwana tufungulie. Lakini akajibu na kusema, Kweli nawambieni, Siwajui" (Mathayo 25:6-12).

Wengi watasema kwangu siku hiyo, Bwana, Bwana, hatujatabiri kupitia jina lako? Na kutoa mapepo kupitia jina lako? Na kutenda miujiza mingi kupitia jina lako? Na hapo ndipo nitasema wazi kwao, Sikuwahi kuwajua: tokeni kwangu, ninyi ambao hutenda udhalimu(Mathayo 7:22–23).

Naye malaika wa tano akapiga baragumu, na nikaona nyota ikianguka kutoka mbinguni hadi duniani: naye akapewa ufunguo wa shimo la kuzimu. Na akafungua hilo shimo la kuzimu; na moshi ukapaa kutoka kwa shimo hilo, kama moshi wa tanuu kubwa; na jua na anga vikatiwa kivuli kwa ajili ya moshi wa ule shimo. Na nzige wakatoka kwa ule moshi hadi duniani: na wakapewa nguvu, kama nguvu ya nge wa duniani. Na wakaamriwa kwamba wasiharibu nyasi ya duniani, wala kitu chochote cha kijani, wala mti wowote; bali wale watu wasio na muhuri wa Mungu kwenye vipaji vyao vya uso pekee. Na wakaamriwa kwamba wasiwaue, bali wawatese kwa miezi tano: na mateso yao yalikuwa kama mateso ya nge anapomuuma mwanadamu. Na katika siku hizo wanadamu watatafuta kifo, na hawatakipata; na watatamani kufa, na kifo kitawatoroka(Ufunuo 9:1-6).

Jinsi ya Kunyakuliwa Kabla ya Dhiki

Tovuti Rasmi