Kufichua Siri ya “Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua” katika Mathayo 24:36

17/05/2020

Na Xinjie

Miezi minne ya damu imeonekana, na majanga kama vile matetemeko ya ardhi, njaa, na magonjwa ya mlipuko yanazidi kuwa matukio ya kawaida. Unabii wa kurudi kwa Bwana umetimia kimsingi, na wengine wameshuhudia waziwazi mtandaoni kuwa Yeye tayari amekuja. Baadhi ya ndugu wamekanganywa, kwani imeandikwa waziwazi katika Biblia: “Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua, wala malaika wa mbinguni, isipokuwa Baba yangu tu(Matthew 24:36). Je, wanawezaje kujua kuwa Bwana amerudi? Amerudi kweli? Je, tunapaswa kufanya nini ili tuweze kumkaribisha? Hebu tushiriki pamoja juu ya swali hili.

Kufichua Siri ya “Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua” katika Mathayo 24:36

“Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua”—Je, Hii Inamaanisha Nini?

Baadhi ya ndugu wanaamini, kulingana na aya hii ya Biblia, “Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua,” kwamba Bwana atakaporudi, hakuna atakayejua. Hii ndiyo sababu hakuna yeyote kati yao anayeamini au kufikiria madai kutoka kwa watu wanaosambaza habari za kurudi kwa Bwana. Je, huu kweli ni uelewa sahihi, au la? Je, jambo hili linakubaliana na mapenzi ya Bwana? Bwana Yesu alitabiri wakati mmoja, “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha(Mathayo 25:6). “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi(Ufunuo 3:20). Tunaweza kuona kutoka katika mistari hii ya maandiko kwamba baada ya Bwana kurudi katika siku za mwisho, Atabisha mlangoni mwetu kwa maneno Yake, na hata kutufanya tutoke nje na kumpokea kwa njia ya kilio cha mwanadamu cha, “bwana arusi yuaja.” Kwa kuwa kuna watu wanaotuambia habari za kurudi kwa Bwana, hii inaonyesha kwamba Atakapokuja, hakika Atawajulisha watu. Bila shaka, kuelewa “Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua” kuwa hakuna yeyote atakayepata habari kuhusu kuja kwa Bwana baada ya Yeye kuja ni makosa kabisa.

Kwa hivyo tunapaswa kutafsiri kifungu hiki cha maandiko matakatifu vipi? Tunaweza kuunganisha aya hizi pamoja: “Sasa jifunzeni mfano wa mtini; Wakati tawi lake ni changa bado, na kuchipua majani, mnajua kwamba majira ya joto yanakaribia: Vivyo hivyo ninyi, mtakapoyaona haya mambo yote, jueni kwamba Amekaribia, yu mlangoni. Kweli ninawaambieni, Kizazi hiki hakitapita, kabla ya kutimia haya mambo yote. Mbingu na dunia vitapita lakini maneno Yangu hayatapita hata kidogo. Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua, wala malaika wa mbinguni, isipokuwa Baba yangu tu(Mathayo 24:32–36). “Nanyi jiwekeni tayari, kwa kuwa saa msiyodhani ndipo atakapokuja Mwana wa Adamu(Mathayo 24:44). Na Ufunuo 3:3 inasema, “Iwapo basi hutakesha, nitakujia kama mwizi, na hutajua saa ambayo nitakuja kwako.” Vifungu hivi vinatumia ishara za kurudi kwa Bwana kutuambia. Vinataja kwamba “Mwana wa Adamu aja” na “kama mwizi.” “Mwana wa Adamu” hakika inamaanisha Mungu mwenye mwili; mwili wa kiroho hauwezi kuitwa Mwana wa Adamu. Ni mtu tu kama Bwana Yesu—Roho wa Mungu aliyevikwa mwili, ambaye amekuja kati ya wanadamu kufanya kazi ya utendaji kabisa, ambaye ana ubinadamu wa kawaida—ndiye anayeweza kuitwa Mwana wa Adamu. “Kama mwizi” inamaanisha kuja kwa kunyemelea na kisirisiri. Kutokana na hili ni wazi kwamba kurudi kwa Bwana kunahusisha kushuka kisirisiri katika mwili kama Mwana wa Adamu. Kwa kuzingatia kwamba Yeye anashuka kisirisiri, hatutamtambua kwa urahisi, kwa sababu siku na saa ambayo Mungu anaonekana kama mwili hakuna anayejua. Yaani, “Lakini juu ya hiyo siku na saa hiyo hakuna mtu anayejua,” inamaanisha kwamba hakuna yeyote anayejua wakati kamili wa kurudi kwa Bwana. Hata hivyo, baada ya Yeye kuja kuzungumza na kufanya kazi, hakika kutakuwepo na baadhi ya watu ambao watajua kuhusu jambo hilo, na huu ndio wakati ambapo tunapaswa kuamka. Tunapowasikia watu wakieneza injili ya kurudi kwa Bwana, tunapaswa kutafuta na kuchunguza; ni wakati huo tu ndipo tutaweza kumkaribisha Bwana na kula pamoja na Yeye. Hata hivyo, hivi sasa, sio tu kwamba hatupo macho, lakini pia hatuendi kutafuta au kuchunguza tunapowasikia wengine wakieneza habari za kurudi kwa Bwana. Kwa hivyo, je, si tumeelewa mapenzi ya Bwana visivyo? Hebu tusome vifungu kadhaa zaidi vya maneno ya Mungu, na tutapata uelewa wa vifungu hivi vya maandiko matakatifu.

Mwenyezi Mungu amesema: “Wakati wa mapambazuko, bila kujulikana kwa mtu yeyote, Mungu Alikuja duniani na Akaanza maisha Yake katika mwili. Watu hawakujua kipindi hiki. Pengine wote walikuwa wamelala, pengine wengi waliokuwa wanakesha walikuwa wanasubiri, na pengine wengi walikuwa wanamwomba Mungu wa mbinguni kimyakimya. Lakini miongoni mwa watu hawa wote, hakuna hata mmoja aliyejua kuwa Mungu tayari Amekwishawasili duniani(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kazi na Kuingia (4)). “Mwanzoni, wakati Yesu alikuwa bado hajafanya rasmi huduma Yake, kama wanafunzi waliomfuata, wakati mwingine pia Yeye alihudhuria mikutano, na kuimba tenzi, Akasifu, na kusoma Agano la Kale kwa hekalu. Baada Yeye kubatizwa na kupanda, Roho alishuka rasmi juu yake na kuanza kufanya kazi, Akifichua utambulisho Wake na huduma Aliyokuwa afanye. Kabla ya haya, hakuna aliyejua utambulisho Wake, na mbali na Maria, hata Yohana hakujua. Yesu alikuwa 29 Alipobatizwa. Baada ya ubatizo wake kukamilika, mbingu zilifunguliwa, na sauti ikasema: ‘Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.’ Baada ya Yesu kubatizwa, Roho Mtakatifu alianza kumshuhudia kwa njia hii. Kabla ya kubatizwa Akiwa na umri wa 29, Alikuwa ameishi maisha ya ukawaida wa mtu, kula wakati Alipotakiwa kula, kulala na kuvaa kawaida, na hakuna chochote kumhusu kilikuwa tofauti. Bila shaka hii ilikuwa tu kwa nyama ya macho ya mwanadamu. … Biblia haijarekodi Alichofanya kabla ya kubatizwa kwa sababu Hakufanya kazi hii kabla ya kubatizwa. Alikuwa tu mtu wa kawaida, na Aliwakilisha mtu wa kawaida; kabla ya Yesu kuanza kufanya huduma Yake, Hakuwa na tofauti na watu wa wenye ukawaida, na wengine hawangeona tofauti yoyote na yeye. Ilikuwa tu baada ya Yeye kufikia 29 ndipo Yesu alijua kwamba Alikuwa amekuja kukamilisha hatua ya kazi ya Mungu; kabla; Yeye Mwenyewe hakujua, kwani kazi Aliyoifanya Mungu ilikuwa kawaida(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kuhusu Majina na Utambulisho).

Tunaweza kuona kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu kuwa hakuna yeyote anayejua wakati ambapo Mungu atashuka duniani kama mwili; hata Mwana wa Adamu hajui. Ni Roho aliye mbinguni tu ndiye anayelijua jambo hili. Hata hivyo, Mungu anapoanza kufanya kazi Yake, Roho Mtakatifu hushuhudia kazi ya Mungu mwenye mwili, na kisha kutumia wafuasi wa Mungu kueneza injili; kisha watu hupata habari kuhusu jambo hilo polepole. Ni kama tu hapo mwanzo, Yehova Mungu alitumia nabii kutabiri kuhusu kuja kwa Masihi, lakini kuhusiana na wakati au mahali ambapo Masihi angewasili, ni Yehova Mungu tu ndiye aliyejua. Bwana Yesu aliporudi katika mwili kufanya kazi, hata Yeye Mwenyewe hakujua mwanzoni kuwa Yeye ndiye aliyekuwa Masihi, kwamba Alikuwa amekuja kufanya kazi ya ukombozi. Aliishi maisha ya kawaida kama mwanadamu wa kawaida. Watu wengine hawakujua kwamba Bwana Yesu alikuwa Kristo, kwamba pia alikuwa Mungu Mwenyewe mwenye mwili. Baada ya Bwana Yesu kubatizwa, Roho Mtakatifu alianza kumshuhudia na Bwana Yesu alianza kuonyesha njia ya toba ya mwanadamu, Akionyesha ishara na maajabu ya Mungu, na kuwaponya wagonjwa na kuwafukuza pepo. Watu wengine walikuja kugundua polepole kuwa Bwana Yesu alikuwa Masihi. Wale waliokubali kwanza kazi ya ukombozi ya Bwana Yesu, kama vile Petro na Yohana, kisha wakaanza kusafiri kote, wakieneza injili ya Bwana. Kwa njia hiyo wokovu wa Bwana ulikuja kujulikana na watu wengi zaidi, na hii imepitishwa katika enzi zote hadi leo. Sasa kuna waumini katika kila sehemu ya ulimwengu.

Bwana Yesu pia alitoa utabiri huu wa siku za mwisho: “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo(Yohana 16:12–13). “Yeye ambaye ananikataa Mimi, na hayakubali maneno Yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho(Yohana 12:48). Na Biblia inasema: “Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli(Yohana 17:17). “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu(1 Petro 4:17). Bwana anaporudi, Anaonyesha ukweli ambao ni mwingi zaidi na wa juu zaidi kuliko ule wa Enzi ya Neema, kulingana na kimo chetu. Anatuhukumu na kututakasa kwa maneno Yake ili tujikomboe kutokana na minyororo ya dhambi na hivyo kutakaswa na kubadilishwa. Kwa hivyo, Bwana anaporudi katika siku za mwisho kuonekana na kufanya kazi, hakika kuna wengine wanaosikia sauti ya Mungu na kukubali kazi Yake, na kisha kusafiri kote ulimwenguni ili kueneza habari njema ya kurudi kwa Bwana. Hii ni sawa na tulipopata imani katika Bwana mara ya kwanza; tuliikubali tu baada ya kuwasikia wengine wakieneza injili ya kusulubiwa. Kama ilivyoandikwa katika Biblia, “Hivyo basi imani huja kupitia kusikia, na kusikia huja kupitia neno lake Mungu” (Warumi 10:17).

Kwa hivyo, tunapozisikia habari za kurudi kwa Bwana, lazima tusizikatae hata kidogo pasipo kufikiria; tunapaswa kutafuta tukiwa tayari kupokea mawazo mapya, tuwaulize wale wanaoeneza injili Bwana amefanya kazi gani tangu Aliporudi, na ni maneno gani ambayo Yeye ameyatamka. Ikiwa ushuhuda wao unalingana na unabii wa Bwana, basi hili ni thibitisho kwamba kweli Yeye amerudi kuonekana na kufanya kazi, na kwa kukubali na kutii tutakuwa tukimkaribisha Bwana. Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima. Mlipokuwa ukitafuta nyayo za Mungu, mliyapuuza maneno haya kuwa ‘Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.’ Kwa hivyo, watu wengi wanapoupokea ukweli, hawaamini kuwa wamepata nyayo za Mungu na hata zaidi hawasadiki kuonekana kwa Mungu. Kosa hilo ni kuu kiasi gani!(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya).

Kote ulimwenguni, kuna Kanisa la Mwenyezi Mungu pekee linaloshuhudia waziwazi kwamba Bwana amerudi–yaani, kuwa Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, Ameonyesha ukweli mwingi na kufanya kazi ya kuwahukumu na kuwatakasa watu. Idadi kubwa sana ya maneno ya Mwenyezi Mungu yameandikwa katika kitabu Neno Laonekana katika Mwili. Maneno ya Mungu yamefafanua kila kipengele cha ukweli. Yanazungumza waziwazi kuhusu siri za kupata mwili kwa Mungu, ukweli wa ndani wa Biblia, kusudi la mpango wa Mungu wa usimamizi wa wanadamu wa miaka elfu sita, tofauti kati ya kazi Yake na kazi ya mwanadamu, na vile vile jinsi Mungu anavyowahukumu na kuwatakasa watu, jinsi watu wanavyopaswa kumjua Mungu, jinsi Mungu anavyoamua matokeo na hatima ya kila mwanadamu, na kadhalika. Ukweli huu wote unahusiana na kazi ya Mungu mwenyewe; zote ni siri ambazo zinatuonyesha waziwazi njia ya wokovu. Tunapaswa kujishughulisha na kutafuta kuona ikiwa kweli huyu ni Roho Mtakatifu anayenenea makanisa, na ikiwa kweli ni Mungu wa siku za mwisho anayefanya kazi Yake ya hukumu Akianza na nyumba Yake. Hivi ndivyo tunavyoweza kuthibitisha ikiwa Mwenyezi Mungu kweli ndiye Yesu Kristo aliyerudi au la. Naamini kuwa mradi tuna hamu ya kutafuta, Mungu atatuongoza kukaribisha kurudi kwa Bwana! Hii ni kwa sababu, kama Bwana Yesu alivyosema “Wamebarikiwa wao walio maskini kiroho: kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao(Mathayo 5:3).

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Kusadiki Uvumi Kunamaanisha Kupoteza Wokovu wa Mungu wa Siku za Mwisho

Mafarisayo walieneza uongo na kumkashifu na kumkufuru Mungu, na sote tunaweza kukisia mwisho waliokumbana nao, lakini, je, wale watu wa Kiyahudi waliochukulia uongo na kashfa hizo kuwa ukweli—je, mwisho wao haukuwa wa huzuni hivyo? Walipitia maangamizi yasiyo ya kifani ya taifa na watu wa Kiyahudi walitawanyika pande zote. Hawakuwa na nyumbani pa kurudia kwa miaka 2,000. Je, haya siyo matokeo ya kuchukulia uongo wa Mafarisayo kuwa ukweli na kumpinga Mungu?

Ukweli Kuhusu Kunyakuliwa

Li Huan Kama tu ndugu Wakristo wengine wengi, natamani sana kuja kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu. Tunafuata fungu lifuatalo kutoka kwa...

Ishara 6 za kurudi kwa Bwana Yesu Zimeonekana

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alituahidi: “Tazama, Naja upesi” (Ufunuo 22:12). Sasa, kila aina ya ishara za kurudi Kwake zimeonekana, na ndugu wengi wamekuwa na maono kwamba siku ya Bwana iko karibu. Je, Bwana tayari Amerudi? Je, tunaweza kufanya nini ili kumkaribisha Bwana? Hebu tujadili hili sasa kwa kuchunguza unabii ulio katika Biblia.

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp