Ishara 6 za kurudi kwa Bwana Yesu Zimeonekana

11/06/2020

Na Xinjie

Miaka elfu mbili iliyopita, Bwana Yesu alituahidi: “Tazama, Naja upesi(Ufunuo 22:12). Sasa, kila aina ya ishara za kurudi Kwake zimeonekana, na ndugu wengi wamekuwa na maono kwamba siku ya Bwana iko karibu. Je, Bwana tayari Amerudi? Je, tunaweza kufanya nini ili kumkaribisha Bwana? Hebu tujadili hili sasa kwa kuchunguza unabii ulio katika Biblia.

Ishara ya Kwanza ya Kurudi kwa Bwana: Matetemeko ya Ardhi, Njaa, Mapigo na Vita

Mathayo 24:6-8 kinasema: “Na ninyi mtasikia kuhusu vita na uvumi juu ya vita: hakikisheni msihangaike: kwani mambo haya yote lazima yafanyike, lakini mwisho bado hujafika Kwani taifa litainuka dhidi ya taifa, na ufalme dhidi ya ufalme: na kutakuweko na njaa, na ndwele, na ardhi kutetemeka katika sehemu mbalimbali. Yote haya ndiyo asili ya huzuni.” Vita vimeibuka mara kwa mara katika miaka ya hivi karibuni, matukio kama vile kupinduliwa kwa serikali ya Kitalibani nchini Afghanistani, mzozo kati ya India na Pakistani, uvamizi wa Iraki na Marekani, na vita vinavyoendelea kati ya Israeli na Palestina. Mapigo, mioto, mafuriko, na matetemeko ya ardhi pia yanaonekana kila mahali. Tukio la kutajika zaidi ni “virusi vipya vya korona”, vilivyolipuka huko Wuhan, Uchina mnamo 2019 na kufikia sasa vimeenea ulimwenguni kote. Kulikuwa pia na mioto mikali ya nyikani huko Australia mnamo Septemba 2019, wakati mlipuko mkubwa wa nzige ulitokea Afrika Mashariki huko upande mwingine wa sayari, nchi nyingi sasa zikikabiliwa na baa la njaa. Mnamo Januari 2020, Indonesia ilikumbwa na mafuriko, na Newfoundland huko Kanada ilipigwa na dhoruba ya theluji ambayo haijaoneka kwa karne moja. Matetemeko ya ardhi yametokea huko Elazigi, Uturuki, Kusini mwa Kuba katika Karibiani, na kwingineko. Kutoka kwa ishara hizi, inaweza kuonekana kuwa unabii huu umetimia.

Ishara ya Pili ya Kurudi kwa Bwana: Kuonekana kwa Mambo ya Mbingu Yasiyo Kawaida

Ufunuo 6:12 kinasema, “Na nikaona wakati ambapo alikuwa ameufungua muhuri wa sita, na, tazama, kulikuwa na tetemeko kubwa la ardhi; na jua likageuka kuwa jeusi kama gunia la nywele, na mwezi ukageuka kuwa kama damu.” Yoeli 2:30–31 kinasema, “Na nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani, damu, na moto, na miimo ya moshi. Jua litageuzwa kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja kwa siku kuu na ya kutisha ya Yehova.” Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na visa vingi vya mwezi kubadilika kuwa mwekundu kama damu. Kwa mfano, katika kipindi cha miaka miwili ya 2014 na 2015, mfululizo wa “miezi ya damu” ilitokea, na mnamo Januari 31, 2018, kulikuwa na “mwezi mkubwa wa damu wa bluu,” ambao huonekana mara moja tu kila baada ya miaka 150. Kisha, “mwezi mkuu wa damu wa mbwa mwitu” ulionekana mnamo Januari 2019. Tukio lililotabiriwa la jua kugeuka kuwa nyeusi pia limeonekana, na hakika, kumekuwa na kupatwa kamilifu kwa jua, kama vile kupatwa kwa huko Singapore mnamo Desemba 26, 2019 na huko Chile mnamo Julai 2 ya mwaka huo huo. Kutimia kwa unabii huu kunaonekana wazi katika matukio haya.

Ishara ya Tatu ya Kurudi kwa Bwana: Makanisa Yana Ukiwa na Upendo wa Waumini ni Baridi

Mathayo 24:12 kinasema, “Na kwa kuwa uovu utaongezeka, mapenzi ya wengi yatakuwa baridi.” Katika ulimwengu mzima wa kidini, ukiwa unaenea. Mahubiri ya wachungaji na wazee wa kanisa yamechoka na ya istiari iliyochakaa, na yanashindwa kuwaruzuku waumini. Katika kupambania kwao hadhi, wachungaji wengine wanaunda vikundi na kutengeneza vikundi vidogo katika makanisa, na wengine wameingia katika biashara kwa kuanzisha viwanda vya kuwaelekeza waumini kwenye njia ya kidunia; wakati huo huo, kati ya waumini, kuna udhaifu wa jumla wa kujiamini na kusita kuachana na ulimwengu, na wanaishi katika matatizo yake ya kuchosha. Makanisa mengine yanaonekana kuwa yamejaa na ya kupendeza kutoka nje, lakini watu wengi huja kanisani ili kupanua mahusiano yao na kuuza bidhaa, wakitumia kanisa kama mahali pa biashara. Kuna tofauti gani kati ya kanisa leo na hekalu wakati wa mwisho wa Enzi ya Sheria? Katika mambo haya, kutimia kikamilifu kwa unabii huu wa kurudi kwa Bwana kunaonekana wazi.

Ishara ya Nne ya Kurudi kwa Bwana: Kuonekana kwa Makristo wa Uongo

Mathayo 24:4–5 kinasema “Na Yesu akajibu na kuwaambia, Kuweni waangalifu ili mtu asiwalaghai. Kwa kuwa wengi watafika kwa jina Langu, wakinena, Mimi ni Kristo; na watawalaghai wengi.” Kutoka katika unabii wa Bwana, tunaweza kuona kwamba Bwana atakaporudi, Makristo wa uwongo watatokea na kuwadanganya watu. Katika miaka ya hivi karibuni, Makristo wa uwongo wameonekana na kuwadanganya watu katika nchi kama Uchina, Korea Kusini na Japani. Makristo hawa wa uwongo hawana kiini cha Kristo, wala hawawezi kutangaza ukweli, lakini wanajidai kuwa wao ni Kristo. Hapa, kutimia kwa unabii huu ni dhahiri kabisa.

Ishara ya Tano ya Kurudi kwa Bwana: Urejesho wa Israeli

Mathayo 24:32-33 kinasema, “Sasa jifunzeni mfano wa mtini; Wakati tawi lake ni changa bado, na kuchipua majani, mnajua kwamba majira ya joto yanakaribia: Vivyo hivyo ninyi, mtakapoyaona haya mambo yote, jueni kwamba Amekaribia, yu mlangoni.” Wengi wanaomwamini Bwana wanajua ya kwamba matawi na majani mororo ya mtini hurejelea urejesho wa Israeli. Israeli inaporejeshwa, siku ya Bwana itakuwa karibu, na Israeli ilirejeshwa mnamo Mei 14, 1948. Bila shaka, unabii huu wa kurudi kwa Bwana umetimia kikamilifu.

Ishara ya Sita ya Kurudi kwa Bwana: Kuenea kwa Injili Hadi Miisho ya Dunia

Mathayo 24:14 kinasema: “Na injili hii ya ufalme itahubiriwa duniani kote kama ushuhuda kwa mataifa yote; na kisha mwisho utakuja.” Katika Marko 16:15, Bwana Yesu aliwaambia wafuasi Wake baada ya kufufuka Kwake, “Nendeni katika dunia nzima, na muihubiri injili kwa kila kiumbe.” Baada ya Yesu kufufuka na kupaa mbinguni, Roho Mtakatifu alianza kuwaongoza wale wanaomfuata Bwana Yesu kumshuhudia Bwana Yesu. Leo, Wakristo wameenea kote ulimwenguni na nchi nyingi za kidemokrasia zimeuchukua Ukristo kama dini yake ya kitaifa. Hata nchini China, ambapo chama kilicho madarakani ni kikana Mungu, makumi ya mamilioni ya watu wameikubali injili ya Bwana Yesu, na hivyo inaweza kuonekana kuwa injili ya ukombozi wa wanadamu kupitia kwa Bwana Yesu imeenea kote ulimwenguni. Katika hili, ni dhahiri kwamba unabii wa kurudi kwa Bwana umetimia.

Tunapaswa Kukaribishaje Kurudi kwa Bwana?

Kutoka katika ukweli ulioorodheshwa hapo juu, tunaweza kuona kwamba ishara sita za kurudi kwa Bwana tayari zimeonekana. Sasa ni wakati muhimu katika kukaribisha kuja kwa Bwana. Je, tunapaswa kufanya nini kabla tuweze kukaribisha kurudi kwa Bwana? Bwana Yesu alitupa jibu la swali hili muda mrefu uliopita.

Katika Yohana 16:12–13, Bwana Yesu alisema, “Bado ningali nayo mengi ya kuwaambieni, lakini hivi sasa hamwezi kuyavumilia. Hata hivyo, wakati Yeye, Roho wa ukweli, atakapokuja, Atawaongoza hadi kwenye ukweli wote: kwa maana Hatazungumza juu Yake Mwenyewe; bali chochote Atakachosikia, Atakinena: na Atawaonyesha mambo yajayo.” Ufunuo 3:20 kinasema, “Tazama, nimesimama mlangoni, na kupiga hodi: mtu yeyote akisikia sauti Yangu, na aufungue mlango, Mimi nitaingia kwake, na nitakula na yeye, na yeye na Mimi.” Pia kuna unabii mwingi katika sura ya 2 na 3 ya Ufunuo: “Yeye ambaye ana sikio, na asikie yale ambayo makanisa yaliambiwa na Roho.” Kama unavyoona kutoka kwa aya hizi, Bwana atakaporudi, Atatoa matamko na kuongea na makanisa, Akituambia ukweli wote ambao hatukuuelewa hapo awali. Wale ambao, baada ya kusikia hotuba ya Mungu na kuitambua sauti Yake, wanamkubali na kujisalimisha Kwake wataweza kumkaribisha Bwana na kuhudhuria karamu ya Mwanakondoo; kwa upande mwingine, wale wasioitambua sauti ya Mungu bila shaka hawatakuwa kondoo wa Mungu, na watafunuliwa na kuondolewa na Mungu. Katika hili, ni dhahiri kwamba tunapongojea kuja kwa Bwana, ni muhimu kwamba tupate maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa na tujifunze kuisikiliza sauti ya Mungu. Kama Mwenyezi Mungu asemavyo: “Kwa kuwa tunatafuta nyayo za Mungu, ni sharti tufuate mapenzi ya Mungu, maneno ya Mungu, matamshi ya Mungu—kwani palipo na maneno mapya ya Mungu, kuna sauti ya Mungu, na palipo na nyayo za Mungu, pana matendo ya Mungu. Palipo na maonyesho ya Mungu pana kuonekana kwa Mungu, na palipo na kuonekana kwa Mungu, pana ukweli, njia na uzima(Neno, Vol. 1. Kuonekana na Kazi ya Mungu. Kiambatisho 1: Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya).

Wanaposikia hili, watu wengine wanaweza kuuliza: “Kwa hivyo, tutaenda wapi ili kupata sauti ya Mungu?” Katika Mathayo 25:6, Bwana Yesu alisema, “Na kukawa na kelele saa sita ya usiku, Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha.” Kwa kuwa Bwana huwaita kondoo Wake kwa matamshi na usemi Wake, hakika kutakuwa na watu ambao wataisikia sauti ya Bwana kwanza na kufuata nyayo za Mwanakondoo, kisha watapiga ukelele kila mahali, “Bwana arusi yuaja,” ambalo ni kueneza habari ya kurudi kwa Bwana na maneno ya kuja kwa pili kwa Bwana, ili wote waweze kupata nafasi ya kuisikia sauti ya Mungu. Kwa hivyo inasemekana kwamba ikiwa tunaweza kwenda sambamba na nyayo za Mwanakondoo kunategemea na ikiwa tuna mioyo ambayo inatamani kumtafuta Yeye na ikiwa tunaweza kuitambua sauti ya Mungu. Kama tu wakati ambapo Bwana Yesu alionekana mara ya kwanza na kuanza kufanya kazi, Petro, Mariamu, na wengine walimtambua Bwana Yesu kama Masihi kutokana na kazi na usemi Wake, nao wakamfuata na kuanza kushuhudia injili Yake. Wale wanaosikia kazi na maneno ya Bwana Yesu na wanaweza kuitambua sauti ya Mungu ndio mabikira wenye busara, ilhali wale makuhani, waandishi, na Mafarisayo ambao hawakupenda ukweli walisikia mamlaka na nguvu ya maneno ya Bwana Yesu na bado hakuyachunguza. Badala yake, walifuata kwa ukaidi maoni yao na mawazo yao, wakidhani kwamba “mtu ambaye haitwi Masihi si Mungu” na kungojea Masihi awaonekanie. Hata waliishutumu na kuikufuru kazi ya Bwana Yesu, na, mwishowe, walipoteza wokovu wa Mungu. Kuna pia waumini wa Kiyahudi waliowafuata Mafarisayo na hawakuitambua sauti ya Mungu katika kazi na maneno ya Bwana Yesu, waliowasikiliza makuhani, waandishi, na Mafarisayo bila kufikiri, na wakaukataa wokovu wa Bwana. Watu kama hao huwa mabikira wapumbavu wanaoachwa na Bwana. Watu wengine wanaweza kuuliza: “Kwa hivyo sauti ya Mungu inaweza kutambuliwaje?” Wakati kwa kweli, hili si jambo gumu. Tamko na usemi wa Mungu lazima visiweze kusemwa na mwanadamu. Lazima viwe na mamlaka na nguvu hasa. Vitaweza kufunua siri za ufalme wa mbinguni na kufichua upotovu wa mwanadamu, na kadhalika. Maneno haya yote ni ukweli, na yote yanaweza kuwa uzima wa mwanadamu. Yeyote aliye na moyo na roho atahisi anapolisikia neno la Mungu, na kutakuwa na uthibitisho moyoni mwake kwamba Muumba anaongea na kutoa tamko Lake kwetu sisi wanadamu. Kondoo wa Mungu husikiliza sauti ya Mungu. Tukiwa na hakika kuwa maneno haya ni sauti ya Mungu, basi tunapaswa kuyakubali na kuyatii, bila kujali yanapatana na mawazo yetu kwa kiasi kidogo jinsi gani. Ni kwa njia hii tu ndiyo tunaweza kukaribisha kurudi kwa Bwana.

Ulimwenguni leo, Kanisa la Mwenyezi Mungu pekee ndilo linashuhudia kwamba Bwana—Mwenyezi Mungu mwenye mwili—tayari Amerudi. Mwenyezi Mungu ameonyesha mamilioni ya maneno, na maneno haya yamechapishwa Mtandaoni ili watu kutoka katika nchi zote na matabaka yote waweze kuyachunguza. Mmoja mmoja, watu wengi wa kila taifa wanaotamani sana ukweli huja kwa matumaini ya kusikia sauti ya Mungu na kumkaribisha Bwana. Kama isemavyo katika Biblia, “Tazama, anakuja bwana arusi; ondokeni nje ili kumkaribisha.” Tukisoma tu maneno zaidi yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, tukisikiliza kutambua ikiwa ni sauti ya Mungu, basi tutaweza kubaini kama Bwana amerudi au la. Kama Bwana Yesu alivyosema katika Yohana 10:27: “Kondoo wangu huisikia sauti yangu, nami nawajua wao, nao hunifuata.” Ninaamini kwamba mradi tuna moyo wa kutafuta kwa unyenyekevu, tunaweza kuitambua sauti ya Mungu na kukaribisha kurudi kwa Bwana.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Leave a Reply

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp