Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I

Mamlaka ya Mungu (I) (Sehemu ya Kwanza)

Vikao vyangu mbalimbali vya ushirika vilivyopita vilikuwa vinahusu kazi ya Mungu, tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe. Baada ya kuvisikiliza vikao hivi vya ushirika, je, unahisi kuwa umefaidi na kupata ufahamu na maarifa kuhusu tabia ya Mungu? Ufahamu wako na maarifa ni mkubwa kiwango gani? Je, unaweza kuweka nambari katika kiwango hicho? Je, vikao hivi vya ushirika vilikupa ufahamu wa kina kuhusu Mungu? Inaweza kusemwa ufahamu huu ni maarifa ya kweli ya Mungu? Inaweza kusemwa kwamba maarifa na ufahamu huu wa Mungu ni maarifa ya hali halisi nzima ya Mungu, na kila kitu Anacho na alicho? La, bila shaka haiwezi kusemwa hivyo! Hii ni kwa sababu vikao hivi vya ushirika vilitupa tu ufahamu wa sehemu ya tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho—na wala si kila kitu, au uzima Wake wote. Vikao hivi vya ushirika vilikuwezesha wewe kuelewa sehemu ya kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na kupitia kwa hayo uliweza kuielewa tabia ya Mungu, na kile Anacho, na alicho, pamoja na mtazamo na kufikiria kuliko kila kitu ambacho Amefanya. Hata hivyo huu ni ufahamu tu wa moja kwa moja, wa matamshi, na katika moyo wako, unabakia kutojua ni kiwango kipi haswa ambacho ni kweli. Ni nini hasa huamua kama kunao uhalisia wowote katika ufahamu wako wa mambo kama haya? Yanaamuliwa na kiwango kipi cha maneno na tabia ya Mungu ambayo kwa kweli umepitia kwenye yale yote ya kweli ambayo wewe umepitia, na kiwango kipi ambacho umeweza kuona na kujua kwenye hali hizi halisi ambazo ulipitia. “Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vilituruhusu kuelewa mambo yanayofanywa na Mungu, fikira za Mungu, na, zaidi ya yote, mtazamo wa Mungu kwa mwanadamu na msingi wa hatua Zake, pamoja na kanuni za vitendo Vyake. Na kwa hivyo tumekuja kuelewa tabia ya Mungu, na kujua Mungu kwa uzima Wake.” Je, kunaye aliyesema maneno haya? Ni sahihi kusema hivi? Kwa kweli ni wazi kwamba si sahihi. Na kwa nini Nasema kwamba si sahihi? Tabia ya Mungu, na kile Anacho na alicho, vyote vinaonyeshwa katika mambo ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ametamka. Binadamu anaweza kuelewa kile Anacho na alicho kupitia kwa kazi ambayo Yeye amefanya na maneno ambayo Yeye ameongea, lakini hii ni kusema tu kwamba ile kazi na maneno humwezesha binadamu kuelewa sehemu ya tabia ya Mungu, na sehemu ya kile Anacho na alicho. Kama binadamu atataka kufaidi ufahamu mwingi zaidi na ulio wazi kuhusu Mungu, basi binadamu lazima apitie maneno na kazi nyingi zaidi za Mungu. Ingawaje binadamu hufaidi tu ufahamu kiasi wa Mungu wakati anapokuwa akipitia sehemu ya maneno au kazi ya Mungu, je, ufahamu huu wa kiasi unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu? Je, unawakilisha hali halisi ya Mungu? Bila shaka unawakilisha tabia ya kweli ya Mungu, na hali halisi ya Mungu, hapo hapana shaka. Haijalishi ni lini au wapi, au ni kwa njia gani ambayo Mungu hufanya kazi Yake, au ni umbo gani ambalo humwonekania binadamu, au ni kwa njia gani Anaonyesha mapenzi Yake, kila kitu Anachofichua na kuonyesha huwakilisha Mungu Mwenyewe, hali halisi ya Mungu na kile Anacho na alicho. Mungu hutekeleza kazi Yake na kile Anacho na alicho, na katika utambulisho Wake wa kweli; Huu ni ukweli mtupu. Ilhali, leo, watu wanao ufahamu kiasi tu wa Mungu kupitia maneno Yake, na kupitia kile wanachosikia wanaposikiliza mahubiri, na kwa hivyo hadi kufikia kiwango fulani, ufahamu huu unaweza kusemwa tu kuwa maarifa ya kinadharia. Kwa mtazamo wa hali zenu halisi, mnaweza kuthibitisha tu ufahamu au maarifa ya Mungu ambayo mmesikia, kuona, au kujua na kuelewa katika moyo wako leo kama kila mmoja wenu atashuhudia haya kupitia kwa yale yote halisi aliyoyapitia, na anakuja kuyajua kidogokidogo. Kama Singeweza kushiriki maneno haya na wewe, je, ungeweza kutimiza maarifa ya kweli ya Mungu ukiwa pekee kupitia kwa yale yote uliyoyapitia? Kufanya hivyo, Naogopa, kunaweza kuwa vigumu sana. Hiyo ni kwa sababu lazima watu wawe kwanza na maneno ya Mungu ili kujua namna ya kuyapitia. Hata hivyo wingi wa maneno ya Mungu ambayo watu hushiriki, hicho ndicho kiwango wanachoweza kupitia. Maneno ya Mungu huongoza njia iliyo mbele, na humpa binadamu mwongozo katika yale yote anayoyapitia. Kwa ufupi, kwa wale walio na baadhi ya mambo ya kweli waliyoyapitia, vikao hivi mbalimbali vya mwisho vitawasaidia kutimiza ufahamu wa kina wa kweli, na hali yenye uhalisia zaidi kuhusu maarifa ya Mungu. Lakini kwa wale wasiokuwa na hali yoyote ya kweli ya waliyoipitia, au ambao wameanza tu hali yao wanayopitia, au wameanza tu kugusia uhalisia wa mambo, huu ni mtihani mkubwa.

Yale maudhui makuu ya vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika yalihusu “tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe.” Ni nini ulichoona kwenye sehemu zile muhimu na kuu kati ya kila kitu Nilichoongea? Kupitia kwenye vikao hivi vya ushirika, unaweza kutambua kwamba Yule aliyefanya kazi, na Akaweza kufichua tabia hizi, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye na ukuu juu ya mambo yote? Kama jibu lako ni ndiyo, basi ni nini kinachokuongoza katika hitimisho kama hilo? Ni katika dhana zipi uliweza kufikia hitimisho hili? Je, kunaye yeyote anayeweza kuniambia Mimi? Ninajua kwamba vikao vya mwisho vya ushirika vilikuathiri kwa undani, na vilikupa mwanzo mpya katika moyo wako kwa minajili ya maarifa yako kwa Mungu, jambo ambalo ni kuu. Lakini ingawaje umeweza kuchukua hatua kubwa katika ufahamu wako wa Mungu ukilinganishwa na awali, ufafanuzi wako wa utambulisho wa Mungu bado unahitaji hatua zaidi ya majina ya Yehova Mungu wa Enzi ya Sheria, Bwana Yesu wa Enzi ya Neema, na Mwenyezi Mungu wa Enzi ya Ufalme. Hivi ni kusema kwamba, ingawaje vikao hivi vya ushirika kuhusu “tabia ya Mungu, kazi ya Mungu, na Mungu Mwenyewe” viliweza kukupa ufahamu fulani wa maneno yaliyowahi kuzungumzwa na Mungu, na kazi iliyowahi kufanywa na Mungu, na uwepo na vinavyomilikiwa vilivyowahi kufichuliwa na Mungu, huwezi kutoa ufafanuzi wa ukweli na mpangilio sahihi wa neno “Mungu.” Na wala huna mpangilio wa kweli na sahihi na maarifa ya hali na utambulisho wa Mungu Mwenyewe, hii ni kusema, katika hadhi ya Mungu miongoni mwa mambo yote na kotekote kwenye ulimwengu mzima. Hii ni kwa sababu, kwenye vikao vya ushirika vya awali kuhusu Mungu Mwenyewe na tabia ya Mungu, maudhui yote yalitokana na maonyesho na ufunuo mbalimbali wa awali kuhusu Mungu uliorekodiwa kwenye Biblia. Ilhali ni vigumu kwa binadamu kugundua uwepo na miliki ambazo zinamilikiwa na kuonyeshwa na Mungu wakati wa, au nje ya, usimamizi na wokovu Wake kwa mwanadamu. Kwa hivyo, hata kama utaelewa nafsi na miliki za Mungu ambazo zilifichuliwa kwenye kazi Aliyowahi kufanya, ufafanuzi wako wa utambulisho na hadhi ya Mungu ungali mbali sana na ule wa Mungu wa kipekee, Yule anayeshikilia ukuu juu ya viumbe vyote, na ni tofauti na ule wa Muumba. Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vilifanya kila mmoja kuhisi kwa njia moja: Binadamu angejuaje fikira za Mungu? Kama kweli mtu angejua, basi mtu huyo bila shaka angekuwa Mungu, kwa maana Mungu Mwenyewe ndiye anayejua fikira Zake, na Mungu Mwenyewe tu ndiye anayejua msingi na mtazamo wa kila kitu Anachofanya. Yaonekana ya kueleweka na ya mantiki kwako wewe kutambua utambulisho wa Mungu kwa njia kama hiyo, lakini ni nani anayeweza kujua kutoka kwenye tabia na kazi ya Mungu kwamba kwa kweli hii ni kazi ya Mungu Mwenyewe, na wala si kazi ya binadamu, kazi ambayo haiwezi kufanywa kwa niaba ya Mungu na binadamu? Nani anayeweza kuona kwamba kazi hii inapatikana katika uongozi wa ukuu wa Yule aliye na hali halisi na nguvu za Mungu? Hii ni kusema kwamba, kupitia sifa au hali halisi gani ndipo unapotambua kwamba Yeye ni Mungu Mwenyewe, aliye na utambulisho wa Mungu, na Ndiye aliye na ukuu juu ya viumbe vyote? Umewahi kufikiria hivi? Kama hujawahi, basi hii inathibitisha hoja moja: Vikao mbalimbali vya mwisho vya ushirika vimeweza kukupa tu ufahamu fulani wa kipande cha historia ambapo Mungu alifanya kazi Yake, na mtazamo, maonyesho, na ufunuo wa Mungu kwenye kipindi cha kufanyika kwa kazi hiyo. Ingawaje ufahamu kama huo unafanya kila mmoja wenu kutambua bila ya shaka yoyote kwamba Yule aliyetekeleza awamu hizi mbili za kazi ni Mungu Mwenyewe ambaye tunamsadiki na kumfuata, na Ndiye lazima siku zote tumfuate, tungali hatuna uwezo wa kutambua kwamba Yeye ni Mungu aliyekuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu, na Atakayeendelea kuwepo milele hadi milele, na wala hatuwezi kutambua kwamba Yeye Ndiye anayetuongoza na Anayeshikilia utawala juu ya wanadamu wote. Kwa kweli hujawahi kufikiria kuhusu tatizo hili. Awe ni Yehova Mungu au Bwana Yesu, ni kupitia kwa dhana zipi za hali halisi na maonyesho husika ndipo unaweza kutambua kwamba Yeye si Mungu tu ambaye lazima umfuate, lakini pia Ndiye anayeamuru mwanadamu na Anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu, ambaye, vilevile, ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee anayeshikilia ukuu dhidi ya mbingu na ardhi na viumbe vyote? Ni kupitia kwenye njia gani ndipo unapotambua kwamba Yule unayemsadiki na kumfuata ni Mungu Mwenyewe anayeshikilia ukuu juu ya viumbe vyote? Ni kupitia kwenye njia gani ndipo unapounganisha Mungu unayemsadiki na Mungu anayeshikilia ukuu juu ya hatima ya mwanadamu? Ni nini kinachokuruhusu kutambua kwamba Mungu unayemsadiki ndiye yule Mungu Mwenyewe wa kipekee, aliye mbinguni na ulimwenguni, na miongoni mwa viumbe vyote? Hili ndilo tatizo ambalo Nitatatua kwenye sehemu ijayo.

Matatizo ambayo hujawahi kufikiria kuhusu au huwezi kufikiria kuhusu ndiyo yayo hayo ambayo yanaweza kuwa muhimu zaidi kwa kumjua Mungu, na ambayo kwayo unaweza kutafuta ukweli usioweza kufikirika kwa mwanadamu. Wakati matatizo haya yanapokukumba, na lazima wewe ndiwe unayefaa kuyakabili, na unahitajika kufanya uamuzi, kama hutaweza kuyatatua kikamilifu kwa sababu ya ujinga au kutojua kwako, au kwa sababu yale yote uliyopitia wewe ni ya juujuu sana na unakosa maarifa ya kweli ya Mungu, basi yatakuwa kizuizi kikubwa zaidi na changamoto kubwa zaidi kwenye njia yako ya kumsadiki Mungu. Na kwa hivyo Nahisi kwamba tunahitajika kabisa kushiriki pamoja nanyi mada hii. Je, unajua tatizo lako ni nini sasa? Je, unatambua matatizo Ninayoyazungumzia? Je, matatizo haya ndiyo utakayokabiliana nayo? Je, haya ndiyo matatizo usiyoyaelewa? Je, haya ndiyo matatizo ambayo hayajawahi kukutokea? Je, matatizo haya ni muhimu kwako? Je, ni matatizo kweli? Suala hili ni chanzo cha mkanganyo mkuu kwako, na hivyo inaonekana kwamba huna ufahamu wa kweli wa Mungu unayemsadiki, na kwamba humchukulii Yeye kwa umakinifu. Baadhi ya watu husema, “Ninajua Yeye ni Mungu, na kwa hivyo ninamfuata Yeye kwa sababu maneno Yake ni maonyesho ya Mungu. Hayo yanatosha. Thibitisho lipi zaidi linahitajika? Kwa kweli hatuhitaji kuibua shaka kuhusu Mungu? Kwa kweli hatupaswi kumjaribu Mungu? Kwa kweli hatuhitaji kuulizia hali halisi ya Mungu na utambulisho wa Mungu Mwenyewe?” Bila kujali kama unafikiria kwa njia hii, huwa Siyaulizi maswali fulani ili kukukanganya kuhusu Mungu, au kukufanya umjaribu Mungu, na isitoshe ili kukupa shaka kuhusu utambulisho na hali halisi ya Mungu. Badala yake, Ninafanya hivi ili kuhimiza ndani yenu ufahamu mkubwa zaidi wa hali halisi ya Mungu, na uhakika na imani kubwa zaidi kuhusu hadhi ya Mungu, ili Mungu awe Ndiye wa pekee katika mioyo ya wale wote wanaomfuata Mungu, na ili ile hadhi ya asili ya Mungu—kama Muumba, Kiongozi wa viumbe vyote, Mungu Mwenyewe wa kipekee—iweze kurejeshwa katika mioyo ya kila kiumbe. Hii pia ndiyo mada itakayohusu ushirika wetu.

Sasa hebu na tuanze kusoma maandiko yafuatayo kutoka kwenye Biblia.

1. Mungu Hutumia Maneno ili Kuumba Viumbe Vyote

Mwa 1:3-5 Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza.

Mwa 1:6-7 Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:9-11 Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane; na kukawa vivyo hivyo. Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema. Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.

Mwa 1:14-15 Naye Mungu akasema, Kuwe na mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kutenga mchana na usiku; na uwe ndio ishara; na majira, na siku na miaka: Na tena uwe ndio mwangaza katika anga la mbingu kwa minajili ya kupa nchi nuru; na ikawa vile.

Mwa 1:20-21 Na Mungu akasema, Na maji yalete kwa wingi kiumbe asongaye aliye na uhai, na ndege wanaoweza kuruka juu ya nchi katika anga wazi la mbingu. Naye Mungu akaumba nyangumi wakubwa, na viumbe wote walio na uhai wasongao, ambao maji yalileta kwa wingi, kwa aina yao, na kila ndege anayeruka kwa aina yake: na Mungu akaona kuwa ilikuwa vizuri.

Mwa 1:24-25 Naye Mungu aksema, Dunia na ilete kiumbe kilicho hai kwa namna yake, mifugo, na kitu kinachotambaa, na wanyama wa mwituni kwa namna yake: na ikafanyika. Naye Mungu akaumba wanyawa wa mwituni kwa namna yake, na mifugo kwa namna yake, na chote kinachotambaa duniani kwa namna yake: na Mungu akaona kwamba ni vizuri.

Kwenye Siku ya Kwanza, Mchana na Usiku wa Mwanadamu Vinazaliwa na Kujitokeza Waziwazi kwa Msaada wa Mamlaka ya Mungu

Hebu na tuweze kuangalia fungu la kwanza: “Na Mungu akasema, Na kuwe na mwanga; kukawa na mwanga. Mungu akauona mwanga, na kuwa ulikuwa mzuri: na Mungu akautenga mwanga na kiza. Naye Mungu akauita mwanga Mchana, na kiza akaliita Usiku. Na jioni na asubuhi yalikuwa siku ya kwanza” (Mwa 1:3-5). Fungu hili linafafanua kitendo cha kwanza cha Mungu wakati wa mwanzo wa uumbaji, na siku ya kwanza ambayo Mungu alipitisha ambapo kulikuwa na jioni na asubuhi. Lakini ilikuwa siku ya kipekee: Mungu alianza kutayarisha nuru ya viumbe vyote, na, vilevile, Akagawa nuru kutoka kwa giza. Kwenye siku hii, Mungu alianza kunena, na matamshi na mamlaka Yake vyote vilikuwa pamoja. Mamlaka Yake yalianza kujitokeza miongoni mwa viumbe vyote, na nguvu Zake zikaenea miongoni mwa viumbe vyote kutokana na maneno Yake. Kuanzia siku hii kuendelea mbele, viumbe vyote viliumbwa na vikawa viko tayari kwa sababu ya maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu, na vikaanza kufanya kazi kwa msaada wa maneno ya Mungu, mamlaka ya Mungu na nguvu za Mungu. Wakati Mungu aliposema maneno haya “Na kuwe na mwanga,” kulikuwepo na nuru. Mungu hakuanza kushughulikia shughuli yoyote; nuru ilikuwa imeonekana kama matokeo ya maneno Yake. Hii ilikuwa nuru ambayo Mungu aliita mchana, na ambayo binadamu angali anaitegemea kwa minajili ya kuwepo kwake leo. Kwa amri ya Mungu, hali yake halisi na thamani havijawahi kubadilika na havijawahi kutoweka. Uwepo wake unaonyesha mamlaka na nguvu za Mungu, na unatangaza uwepo wa Mungu, na unathibitisha, tena na tena, utambulisho na hadhi ya Muumba. Haiwezi kushikika, au kuonekana, lakini ni nuru halisi inayoweza kuonekana na binadamu. Kuanzia wakati huo kusonga mbele, kwenye ulimwengu huu mtupu ambao “nchi ilikuwa ya ukiwa na tupu; na kulikuwa na giza sehemu ya juu ya vilindi,” kulikuwepo kiumbe kile cha kwanza cha kushikika. Kiumbe hiki kilitokana na maneno ya kinywa cha Mungu na kikaonekana kwenye tukio la kwanza la kuumbwa kwa viumbe vyote kwa sababu ya mamlaka na matamshi ya Mungu. Muda mfupi baadaye, Mungu aliamuru nuru na giza kutengana…. Kila kitu kilibadilika na kilikamilishwa kwa sababu ya maneno ya Mungu…. Mungu akaiita nuru hii “Mchana,” na giza hili Akaliita “Usiku.” Kuanzia wakati huo, jioni ya kwanza na asubuhi ya kwanza ziliweza kuumbwa katika ulimwengu ambao Mungu alinuia kuumba, na Mungu akasema hii ndiyo iliyokuwa siku ya kwanza. Siku hii ilikuwa siku ya kwanza ya vile vilivyoumbwa na Muumba wa viumbe vyote, na ilikuwa mwanzo wa kuumbwa kwa viumbe vyote, na ndio wakati wa kwanza ambao mamlaka na nguvu za Muumba vilikuwa vimeonyeshwa katika ulimwengu huu ambao Alikuwa ameumba.

Kupitia maneno haya, binadamu anaweza kutazama mamlaka ya Mungu, na mamlaka ya maneno ya Mungu, na nguvu za Mungu. Kwa sababu Mungu tu ndiye anayemiliki nguvu kama hizo, na kwa hivyo Mungu pekee ndiye aliye na mamlaka, na kwa sababu Mungu ndiye anayemiliki mamlaka kama hayo, kwa hivyo Mungu pekee ndiye aliye na nguvu kama hizo. Je, binadamu au kifaa chochote kingeweza kumiliki mamlaka na nguvu kama hizi? Je, kunalo jibu katika moyo wako? Mbali na Mungu, je, kuna kiumbe chochote kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa kinachomiliki mamlaka kama hayo? Umewahi kuona mfano wa kiumbe kama hiki kwenye vitabu vingine vyovyote au machapisho? Kunayo rekodi yoyote kwamba mtu aliumba mbingu na ulimwengu na viumbe vyote? Jambo hili halionekani katika vitabu au rekodi nyingine zozote; haya ndiyo, bila shaka, maneno ya kipekee yenye mamlaka na nguvu kuhusu uumbaji wa kupendeza wa Mungu wa ulimwengu, yaliyorekodiwa kwenye Biblia, na maneno haya yanazungumzia mamlaka ya kipekee ya Mungu, na utambulisho wa kipekee wa Mungu. Je, mamlaka na nguvu kama hizi zinaweza kusemekana kuwa zinaashiria utambulisho wa kipekee wa Mungu? Yanaweza kusemwa yanamilikiwa na Mungu, na Mungu pekee? Bila shaka, Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizi! Mamlaka na nguvu hizi vyote haviwezi kumilikiwa au kubadilishwa na kiumbe chochote kingine kilichoumbwa au kile ambacho hakikuumbwa! Je, hii ni mojawapo ya sifa za Mungu Mwenyewe wa kipekee? Je, umewahi kuishuhudia? Maneno haya yanaruhusu watu kuelewa kwa haraka na waziwazi hoja hii kwamba Mungu anamiliki mamlaka ya kipekee, na nguvu za kipekee, na Anamiliki utambulisho na hadhi isiyo ya kawaida. Kutokana na ushirika wa hapa juu, je, unaweza kusema kwamba Mungu unayemsadiki ndiye Mungu Mwenyewe wa kipekee?

Kwenye Siku ya Pili, Mamlaka ya Mungu Yalipangilia Maji, na Kufanya Mbingu, na Anga za Mbinu za Kimsingi Zaidi za Kuishi kwa Binadamu Kuonekana

Hebu na tusome fungu la pili la Biblia: “Na Mungu alisema, Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji. Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu: na kukawa vivyo hivyo” (Mwa 1:6-7). Ni mabadiliko gani yaliyofanyika baada ya Mungu kusema “Na kuwe na mbingu katikati ya maji, na uigawanye maji kutoka kwa maji”? Maandiko yanasema: “Na Mungu akaitengeneza mbingu, na akayagawanya yale maji yaliyokuwa chini ya mbingu kutoka kwa yale maji yaliyokuwa juu ya mbingu.” Ni nini kilichokuwa matokeo baada ya Mungu kutamka hivi na kufanya hivyo? Jibu linapatikana kwenye sehemu ya mwisho ya fungu hili: “na kukawa vivyo hivyo.”

Sentensi hizi fupi mbili zinarekodi tukio la kupendeza, na zinafafanua mazingira mazuri—utekelezaji wa kipekee ambapo Mungu aliyatawala maji, na kuunda anga ambayo binadamu angeishi …

Katika picha hii, maji na anga vinaonekana mbele ya macho ya Mungu papo hapo, na vyote vinagawanywa kwa mamlaka ya matamshi ya Mungu, na kugawanywa kwa sehemu ya juu na ya chini kwa njia ambayo iliteuliwa na Mungu. Hivi ni kusema, anga iliyoumbwa na Mungu haikufunika tu maji yaliyo chini, lakini pia ilishikilia maji yaliyo juu…. Katika haya, binadamu hawezi kufanya chochote ila kukodoa macho, kushangaa, na kutweta kwa kuvutiwa na maajabu ya onyesho hilo ambalo Muumba aliyahamisha maji, na kuyaamuru maji, na kuumba anga, na yote haya Alifanya kupitia kwa nguvu za mamlaka Yake. Kupitia kwa matamshi ya Mungu, na nguvu za Mungu, na mamlaka ya Mungu, Mungu aliweza kutimiza tendo jingine kubwa. Je, hizi si nguvu za mamlaka ya Muumba? Hebu na tutumie maandiko haya katika kufafanua vitendo vya Mungu: Mungu aliyatamka matamshi Yake na kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu kulikuwa na anga katikati ya maji. Wakati uo huo, badiliko la ajabu lilitokea kwenye nafasi hii kwa sababu ya matamshi haya ya Mungu, na halikuwa badiliko katika hali ya kawaida, lakini aina fulani ya kibadala ambapo kitu kisichokuwepo kiligeuka na kuwa kitu kilichopo. Yote haya yalizaliwa kwenye fikira za Muumba, na yakawa kitu kilichopo kutoka kwenye kitu kisichokuwepo kwa sababu ya matamshi yaliyotamkwa na Muumba, na, vilevile, kuanzia sasa kwenda mbele yangekuwepo na kuwa imara, kwa minajili ya Muumba, na yangesonga, kubadilika, na kupata nguvu kulingana na fikira za Muumba. Ufahamu huu unafafanua kitendo cha pili cha Muumba katika viumbe Vyake vya ulimwengu mzima. Yalikuwa maonyesho mengine ya mamlaka na nguvu za Muumba, na ulikuwa utekelezaji mwingine anzilishi uliofanywa na Muumba. Siku hii ndiyo iliyokuwa siku ya pili ambayo Muumba alikuwa amepitisha tangu kuwekwa msingi kwa ulimwengu, na ilikuwa siku nyingine nzuri Kwake: Alitembea miongoni mwa nuru, Aliileta anga, Aliyapangilia na kuyatawala maji, na vitendo Vyake, mamlaka Yake, na nguvu Zake vyote viliweza kuanza kazi kwenye siku hiyo mpya …

Je, kulikuwepo na anga katikati ya maji kabla ya Mungu kutamka matamshi Yake? Bila shaka la! Na je, baada ya Mungu kusema “Na kuwe na mbingu katikati ya maji”? Viumbe vilivyonuiwa na Mungu vilionekana; kulikuwa na anga katikati ya maji, na maji yaligawanywa kwa sababu Mungu alisema hivyo “na uigawanye maji kutoka kwa maji.” Kwa njia hii, kufuatia maneno ya Mungu, viumbe vipya viwili, viumbe viwili vilivyozaliwa na vilivyokuwa vipya vilionekana miongoni mwa viumbe vyote kutokana na mamlaka na nguvu za Mungu. Na unahisi vipi kuhusu kujitokeza kwa viumbe hivi viwili vipya? Je, unahisi ukubwa wa nguvu za Muumba? Unahisi ile nguvu ya kipekee na isiyo ya kawaida ya Muumba? Ukubwa wa msukumo na nguvu kama hizo unatokana na mamlaka ya Mungu na mamlaka haya ni kiwakilishi cha Mungu Mwenyewe, na sifa ya kipekee ya Mungu Mwenyewe.

Je, ufahamu huu umekupa mtazamo mwingine kamilifu wa upekee wa Mungu? Lakini haya ni machache tu kati ya mengi; mamlaka na nguvu za Muumba vinazidi haya yote. Upekee wake hauko hivyo tu kwa sababu Anamiliki hali halisi isiyo kama ya viumbe vingine, lakini pia kwa sababu ya mamlaka na nguvu Zake kuwa zisizo za kawaida, zisizo na mipaka, bora kabisa kuliko vyote, na inapita vitu vyote, na vilevile, kwa sababu mamlaka Yake na kile Anacho na alicho kinaweza kuumba maisha, na kufanya miujiza, na Anaweza kuumba kila mojawapo ya dakika na sekunde iliyo ya kustaajabisha na isiyo ya kawaida, na wakati uo huo, Anaweza kutawala maisha Anayoyaumba na kushikilia ukuu Wake juu ya miujiza na kila mojawapo ya dakika na sekunde Anazoumba.

Kwenye Siku ya Tatu, Matamshi ya Mungu Yazaa Ardhi na Bahari, na Mamlaka ya Mungu Yasababisha Ulimwengu Kujaa Maisha

Sasa, hebu na tusome sentensi ya kwanza ya Mwanzo 1:9-11: “Naye Mungu akasema, Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ni mabadiliko gani yaliyotokea baada ya Mungu kusema tu, “Nayo maji yaliyo chini ya mbingu yakonge pahali pamoja, na ardhi kavu ionekane”? Na hii nafasi iliyokuwa katikati ya nuru na anga ilikuwa nini? Katika Maandiko, imeandikwa: “Naye Mungu akaiita nchi kavu Dunia: na kukonga kwa maji akakuita Bahari: naye Mungu akaona kwamba ni vyema.” Hivi ni kusema, kulikuwepo sasa na ardhi na bahari kwenye anga hii, nayo ardhi na bahari viliweza kutenganishwa. Kujitokeza kwa vitu hivi vipya kulifuata amri kutoka kwenye kinywa cha Mungu, “na kukawa vivyo hivyo.” Je, Maandiko yanafafanua Mungu akiwa ameshughulika kila pahali wakati Akifanya haya? Je, yanafafanua Mungu akiwa anajihusisha katika kazi ngumu? Kwa hivyo, haya yote yaliwezaje kufanywa na Mungu? Mungu aliwezaje kusababisha vitu hivi vipya kuumbwa? Tunaelewa wenyewe bila kuelezewa, kwamba Mungu alitumia matamshi kutimiza mambo haya yote, kuumba uzima wa haya yote.

Kwenye mafungu matatu yaliyo hapo juu, tumejifunza kunatokea matukio matatu makubwa. Matukio haya matatu makubwa yalionekana, na yakaumbwa kuwa hivyo, kupitia kwa matamshi ya Mungu, na ni kwa sababu ya matamshi Yake ndipo, moja baada ya lengine, yaliweza kujitokeza mbele ya macho ya Mungu. Kwa hivyo inaweza kuonekana kwamba “Mungu huongea, na ikatimizwa; huamuru, na ikawa imara” haya si maneno matupu. Hali hii halisi ya Mungu inathibitishwa wakati ule ambao fikira Zake zinaeleweka, na wakati ambapo Mungu hufungua kinywa Chake kuongea, hali Yake halisi inajionyesha kikamilifu.

Hebu na tuendelee hadi kwenye sentensi ya mwisho ya fungu hili: “Naye Mungu akasema, Na dunia izae majani, mche ambao unatoa mbegu, na mti wa matunda ambao unazaa tunda kwa aina yake, ambao mbegu zake ziko ndani yake, juu ya dunia: na kukawa vivyo hivyo.” Huku Mungu akiongea, mambo haya yote yaliumbika kufuatia fikira za Mungu, na kwa muda mfupi tu, mseto wa viumbe vidogo vinyonge vyenye maisha vilikuwa vinachomoza vichwa vyao kwa kusita huku vichwa vyao vikiwa juu kupitia kwenye ardhi, na hata kabla ya kukung’uta chembechembe za uchafu kutoka kwenye miili yao vilikuwa vikipungiana mikono kusalimiana kwa hamu, kuitikia na kuufurahia ulimwengu. Vilishukuru Muumba kwa maisha aliyovipatia, na kuutangazia ulimwengu kwamba vilikuwa sehemu ya viumbe vyote, na kwamba kila kimojawapo kingejitolea katika maisha yavyo ili viwe vinaonyesha mamlaka ya Muumba. Kama vile matamshi ya Mungu yalivyotamkwa, ardhi ikawa yenye rutuba na kijani, aina zote za miti ambayo ingeweza kufurahiwa na binadamu iliweza kuota na kuchipuka kutoka kwenye ardhi, na milima na nchi tambarare vyote vikawa na idadi kubwa ya miti na misitu…. Ulimwengu huu tasa, ambao hakukuwahi kuwepo na chembechembe zozote za maisha, ulifunikwa mara moja na wingi wa nyasi, mimea ya msimu na miti na ilikuwa ikifurika kwa kijani kibichi kingi…. Harufu nzuri ya nyasi na mnukio wa mchanga uliosambazwa kupitia hewani, na mseto wa mimea vyote vilianza kupumua kulingana na mzunguko wa hewa, na vikaanza pia mchakato wa kukua. Wakati uo huo, kutokana na maneno ya Mungu na kufuatia fikira za Mungu, mimea yote ilianza mizunguko isiyoisha ya maisha ambapo inakua, inanawiri, inazaa matunda na kuzaana na kuongezeka. Ilianza kutii kwa umakinifu mikondo yao husika ya maisha, na kuanza kutekeleza wajibu wao husika miongoni mwa viumbe vyote…. Yote ilizaliwa na kuishi, kwa sababu ya matamshi ya Muumba. Ingepokea matoleo na ustawishi usiosita wa Muumba, na siku zote ingeendelea kuishi kwa shauku katika kila pembe ya ardhi ili kuonyesha mamlaka na nguvu za Muumba, na siku zote ingeonyesha nguvu za maisha walizopewa na Muumba …

Maisha ya Muumba ni yale yasiyo ya kawaida, fikira Zake ni zile zisizo za kawaida, na mamlaka Yake ni yale yasiyokuwa ya kawaida, na kwa hivyo, wakati matamshi Yake yalipotamkwa, yale matokeo ya mwisho yalikuwa “na ikawa hivyo.” Ni wazi kwamba, Mungu hahitaji kufanya kazi kwa mikono Yake wakati Anapofanya matendo; Anatumia tu fikira Zake kutoa amri, na matamshi Yake ili kuagizia, na kwa njia hii mambo yanatimizwa. Kwenye siku hii, Mungu aliyakusanya maji katika mahali pamoja, na Akaiacha ardhi kavu kujitokeza, baada ya hapo Mungu aliifanya nyasi kuota kutoka kwenye ardhi, na papo hapo palimea mimea ya msimu iliyozaa mbegu, na miti ya kuzaa matunda, na Mungu akaainisha kila mojawapo kulingana na aina, na kusababisha kila mmea kuwa na mbegu yake. Haya yote yaliwezekana kulingana na fikira za Mungu na amri za matamshi ya Mungu, na kila mmea ulijitokeza, mmoja baada ya mwingine, kwenye ulimwengu huu mpya.

Wakati Alikuwa aanze kazi Yake, Mungu tayari alikuwa na picha ya kile Alichonuia kutimiza katika akili Zake na wakati ambapo Mungu alianza kutimiza mambo haya, na ndio wakati ambao pia Mungu alikifungua kinywa Chake kuongea kuhusu maudhui ya picha hii, mabadiliko katika viumbe vyote yalianza kufanyika kutokana na mamlaka na nguvu za Mungu. Bila ya kujali namna Mungu alivyofanya, au Alivyoonyesha mamlaka Yake, kila kitu kilitimizwa hatua kwa hatua kulingana na mpango wa Mungu na kwa sababu ya matamshi ya Mungu, na mabadiliko ya hatua kwa hatua yalifanyika kati ya mbingu na ardhi kutokana na matamshi na mamlaka ya Mungu. Mabadiliko na matukio haya yote yalionyesha mamlaka ya Muumba, na nguvu za maisha ya Muumba zisizo za kawaida na zenye ukubwa. Fikira Zake si mawazo mepesi, au picha tupu, lakini mamlaka yanayomiliki nishati kuu na ile isiyo ya kawaida, na ndio nguvu zinazosababisha viumbe vyote kubadilika, kufufuka, kupata nguvu upya, na kuangamia. Na kwa sababu ya haya, viumbe vyote hufanya kazi kwa sababu ya fikira Zake, na, wakati uo huo, yote haya yanatimizwa kwa sababu ya matamshi kutoka kinywa Chake….

Kabla ya viumbe vyote kujitokeza, kwenye akili za Mungu mpango wa Mungu ulikuwa umeundwa kitambo, na ulimwengu mpya ulikuwa umetimizwa kitambo. Ingawaje kwenye siku ya tatu mimea aina yote ilijitokeza ardhini, Mungu hakuwa na sababu yoyote ya kusitisha hatua za uumbaji Wake kwa ulimwengu huu, Alinuia kuendelea kunena matamshi Yake, kuendelea kutimiza uumbaji wa kila kiumbe kipya. Angenena, angetoa amri Zake, na angeonyesha mamlaka Yake na kuendeleza nguvu Zake, na Alitayarisha kila kitu Alichokuwa amepanga ili kutayarishia viumbe vyote na mwanadamu ambaye Alinuia kuumba….

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp