Mtu anawezaje kwa kweli kuwa na hakika kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Bwana Yesu aliyerudi? Kutofautisha kati ya Njia ya Kweli na Njia ya Uongo
Kwa wale ambao wamemwamini Bwana Yesu kwa miaka mingi na wamejitumia kwa bidii na kufanya kazi bila kuchoka, wameteseka sana kwa ajili ya Bwana. Inawezekana kuwa kwamba kwa kutokubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho watanyimwa wokovu na uingiaji katika ufalme wa mbinguni? Masharti ya Kuingia katika Ufalme wa Mbinguni
Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa mara nyingi huwahubiria waumini kwamba mahubiri yoyote yanayosema kwamba Bwana amekuja katika mwili ni uongo. Wao hutegemeza hili aya za Biblia: “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24:23-24). Sasa hatuna habari tunavyofaa kumtambua Kristo wa kweli kutoka kwa wale wa uongo, hivyo tafadhali jibu swali hili. Kutofautisha kati ya Kristo wa kweli na Makristo wa Uongo
Kwa nini kazi ya Mungu katika siku za mwisho haifanywi kupitia njia ya Roho? Kwa nini Mungu amekuja kufanya kazi Yake katika mwili?
Kwa nini kurudi kwa Bwana kunahusisha kupata mwili—kushuka kwa siri—na pia kushuka hadharani kutoka mawinguni?
Unashuhudia kwamba Mungu amekuwa mwili na kuwa Mwana wa Adamu ili kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na bado wengi wa wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanakiri kwamba Bwana atarudi akija na mawingu, na wanategemeza hili hasa aya za Biblia: “Huyu Yesu … atakuja kwa namna hiyo hiyo ambayo mmemuona akienda mbinguni” (Matendo 1:11). “Tazama, anakuja na mawingu; nalo kila jicho litamwona yeye” (Ufunuo 1:7). Na zaidi ya hayo, wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa pia hutufundisha kwamba Bwana Yesu yeyote asiyekuja na mawingu ni wa uongo na lazima aachwe. Kwa hiyo hatuna uhakika kama mtazamo huu unakubaliana na Biblia; ni sahihi kuchukua huu kama ukweli au la?
Unasema kwamba Bwana Yesu amerudi, kwa nini hatujamwona? Kuona ni kuamini. Kama hatujamwona, basi hilo lazima limaanishe kuwa Yeye hajarudi bado; nitaamini hilo nitakapomwona. Unasema kwamba Bwana Yesu amerudi, kwa hiyo Yuko wapi sasa? Anafanya kazi gani? Bwana Amesema maneno gani? Nitaliamini ukishuhudia kwa dhahiri mambo haya.
Sisi hufuata mfano wa Paulo na hufanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Bwana, tukieneza injili na kumshuhudia Bwana, na tukiyalisha makanisa ya Bwana, kama vile Paulo tu: “Nimepigana vita vizuri, nimeutimiza mwendo wangu, nimeihifadhi imani” (2 Timotheo 4:7). Si huku ni kufuata mapenzi ya Mungu? Kutenda kwa njia hii kunamaanisha kuwa tunastahili kunyakuliwa na kuingia katika ufalme wa mbinguni, hivyo kwa nini tunapaswa kuikubali kazi ya Mungu ya hukumu na utakaso katika siku za mwisho kabla tuweze kuletwa katika ufalme wa mbinguni?
Watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanaamini kuwa Bwana Yesu kusema “Imekwisha” (Yohana 19:30) msalabani ni ushahidi kwamba kazi ya Mungu ya wokovu tayari imekamilika kabisa. Na bado unashuhudia kwamba Bwana amerejea katika mwili kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu ili kuwaokoa wanadamu kabisa. Kwa hiyo ni kwa njia gani hasa mtu anafaa kuelewa kazi ya Mungu ya kuwaokoa wanadamu? Hatuko dhahiri juu ya kipengele hiki cha ukweli, kwa hiyo tafadhali shiriki hili kwa ajili yetu.
Bibilia inasema: “Kwani mwanadamu husadiki moyoni ili kupata haki; na kwa mdomo hukubali hadi apate wokovu” (Warumi 10:10). Tunaamini kwamba Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wenye haki kupitia imani. Aidha, tunaamini kwamba mtu akiokolewa mara moja, basi ameokolewa milele, na Bwana atakaporudi tutanyakuliwa na tutaingia katika katika ufalme wa mbinguni. Hivyo kwa nini unashuhudia kuwa tunapaswa kukubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho kabla ya kuweza kuokolewa na kuletwa katika ufalme wa mbinguni?
Watu wengine husema: Bwana Yesu aliposema msalabani, “Imekwisha,” si hiyo ilionyesha kuwa kazi ya wokovu ya Mungu ilikuwa imekamilika? Kwa hiyo ni kwa nini Mungu anahitaji kufanya kazi ya hukumu akianza na nyumba ya Mungu atakaporudi katika siku za mwisho?
Katika Enzi ya Neema, Mungu alipata mwili ili kutumika kama sadaka ya dhambi kwa wanadamu, akiwaokoa kutoka kwa dhambi. Katika siku za mwisho Mungu amepata mwili tena ili kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake ya hukumu ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa. Kwa nini Mungu anahitaji kuwa mwili mara mbili ili kufanya kazi ya kumwokoa wanadamu? Na kuna umuhimu gani wa Mungu kuwa mwili mara mbili?
Mungu alimtumia Musa kufanya kazi ya Enzi ya Sheria, hivyo kwa nini Mungu hawatumii watu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, lakini badala yake Analazimika kupata mwili ili kuifanya Mwenyewe? Kuna tofauti gani muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na watu ambao Mungu huwatumia?
Kwa miaka elfu mbili, imani ya mwanadamu katika Bwana imekuwa imetegemezwa Biblia, na kuja kwa Bwana Yesu hakukuikanusha Biblia ya Agano la Kale. Baada ya Mwenyezi Mungu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, kila mtu anayemkubali Mwenyezi Mungu atalenga kula na kunywa maneno ya Mwenyezi Mungu na aitasoma Biblia mara chache tena. Kile ninachopenda kufuatilia ni, baada ya mtu kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, ni mtazamo gani sahihi hasa mtu anafaa kuwa nao kwa Biblia, na mtu anafaa kuitumia kwa jinsi gani? Imani ya mtu katika Mungu inafaa itegemezwe nini ili mtu aitembee njia ya imani katika Mungu na kupata wokovu wa Mungu?
Biblia ni ushahidi wa kazi ya Mungu; ni kwa kusoma Biblia pekee ndiyo wale wanaomwamini Bwana wanaweza kutambua kwamba Mungu aliumba mbingu na dunia na vitu vyote na kuona matendo ya ajabu ya Mungu, ukuu Wake na uweza. Katika Biblia kuna maneno mengi ya Mungu na ushuhuda mwingi wa uzoefu wa mwanadamu; inaweza kuyakimu maisha ya mwanadamu na kuwa na manufaa sana kwa mwanadamu, hivyo kile ninachopenda kufuatilia ni, kwa kweli tunaweza kupata uzima wa milele kwa kusoma Biblia? Kweli hakuna njia ya uzima wa milele katika Biblia?
Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanashikilia maneno ya Paulo katika Biblia: “Andiko lote limetolewa kwa msukumo wa Mungu” (2 Timotheo 3:16), wakiamini kwamba kila kitu katika Biblia ni maneno ya Mungu. Lakini unasema kwamba maneno ya Biblia si maneno ya Mungu kabisa, kwa hiyo haya yote yanamaanisha nini?