Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

VITABU

 • Neno Laonekana katika Mwili

  Hii ilikuwa mara ya kwanza tangu uumbaji ambayo Mungu alikuwa amehutubia wanadamu wote. Matamshi haya yalikuwa maandiko ya kwanza yaliyoonyeshwa na Mungu akiwa miongoni mwa wanadamu ambayo kwayo Aliwafichua watu, Akawaongoza, Akawahukumu, na kuzungumza nao kwa dhati na kwa hiyo, pia, yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo kwayo Mungu aliwaruhusu watu kuzijua nyayo Zake, mahali ambamo Yeye huishi, tabia ya Mungu, kile Mungu anacho na alicho, fikira za Mungu, na masikitiko Yake kwa wanadamu. Inaweza kusemwa kwamba haya yalikuwa matamshi ya kwanza ambayo Mungu alikuwa amenena kwa wanadamu kutoka mbingu ya tatu tangu uumbaji, na mara ya kwanza ambayo Mungu alikuwa ametumia utambulisho Wake wa asili kuonekana na kuonyesha sauti Yake kwa wanadamu kati ya maneno.

  Soma Zaidi
 • Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

  Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, anaeleza maneno Yake ili kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu na kuwaongoza katika enzi mpya, Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaojisalimisha chini ya mamlaka Yake watafurahia ukweli wa juu zaidi na kupokea baraka nyingi zaidi. Kwa kweli wataishi kwenye mwanga, na wataupata ukweli, njia, na uzima.

  Soma Zaidi
 • Maneno Mashuhuri Kutoka kwa Mwenyezi Mungu, Kristo wa Siku za Mwisho

  Maneno bora zaidi yaliyoteuliwa kutoka katika maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, yamekusanywa katika kitabu hiki. Maneno haya ni mwongozo kwa wale wanaotamani sana kuonekana kwa Mungu kutafuta nyayo Zake. Yanaweza kukuongoza kupata mlango wa kuingia katika ufalme wa mbinguni.

  Soma Zaidi
 • Uchaguzi wa Maneno ya Mwenyezi Mungu

  Chaguzi kutoka kwa maneno bora zaidi ya Mwenyezi Mungu yaliyoshirikishwa katika kitabu hiki na zinazoshuhudia kwa wale wote wanaotumaini na kuomba kwa kuonekana kwa Mungu kwa kurudi kwa Mwokozi juu ya mawingu meupe zamani sana, na kushuhudia kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme. Hili huwasababisha wanadamu kutambua kwamba Mwenyezi Mungu na Bwana Yesu ni Mungu mmoja—Yeye ni Mwanakondoo aliyetabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo ambaye amekifungua kitabu na mihuri saba.

  Soma Zaidi
 • Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

  Kitabu hiki cha nyimbo kina sehemu mbili: Ya kwanza ni nyimbo ambazo zina matamshi bora ya Mwenyezi Mungu, na ya pili ni ushuhuda wa kweli wa watu wa Mungu walioteuliwa baada ya kupitia kazi Yake ya hukumu. Nyimbo hizi ni za msaada mkubwa sana kwa watu katika kufanya ibada zao za kiroho, kupitia maneno ya Mungu, na kujua kazi ya Mungu. Zinawasaidia watu kuelewa ukweli na kujiondolea tabia yao potovu ili kupata wokovu wa Mungu.

  Soma Zaidi
 • Ushuhuda kwa Kristo wa Siku za Mwisho

  Mwenyezi Mungu, Kristo wa siku za mwisho, ameonyesha namna nyingi za ukweli, amefunua kila ukweli na siri katika Biblia, na kuwafichulia wanadamu maelezo ya ndani ya hatua tatu za kazi ya Mungu, siri ya Mungu kupata mwili na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, n.k. Hili linathibitisha kwamba Mwenyezi Mungu ni kurudi kwa Bwana Yesu na kwamba Yeye ni kuonekana kwa Mungu katika siku za mwisho.

  Soma Zaidi
 • Kondoo wa Mungu Huisikia Sauti ya Mungu (Mambo Muhimu ya Muumini Mpya)

  Vilivyokusanywa katika kitabu hiki ni ukweli wenye uwezo wa kuona mbali wa hatua tatu za kazi ya Mungu, majina Yake, fumbo la kupata Kwake mwili, na jinsi ya kutofautisha kati ya njia ya kweli na njia za uongo, visomwe na kuzatitiwa na wale ambao wameikubali hivi karibuni kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na ili waweze kuweka misingi haraka iwezekanavyo kwa ukweli wenye uwezo wa kuona mbali wa kazi ya Mungu.

  Soma Zaidi
 • Sikiliza Sauti ya Mungu Tazama Kuonekana kwa Mungu

  Kitabu hiki ni mkusanyiko wa ukweli unaohusiana na kupata mwili kwa Mungu na vilevile hatua Zake tatu za kazi za kuwaokoa wanadamu. Ukweli huu huwaruhusu watu waone kuonekana kwa Kristo na kazi Yake katika siku za mwisho kupitia matamshi ya Mungu, na vilevile kupata kujua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye kurudi kwa Bwana Yesu, na kwamba Ameonyesha ukweli na hufanya kazi ya “hukumu Akianza katika nyumba ya Mungu” katika siku za mwisho, na hivyo kuwasababisha wanadamu warudi kwenye kiti cha enzi cha Mungu.

  Soma Zaidi
 • Ushuhuda wa Uzoefu Mbele ya Kiti cha Hukumu cha Kristo

  Hukumu mbele ya enzi kubwa nyeupe ya siku za mwisho imeanza. Kristo wa Mwisho—Mwenyezi Mungu—ameeleza ukweli ili kufanya kazi yake ya kuwahukumu na kuwatakasa wanadamu. Kupitia ufunuo na hukumu ya neno la Mungu, polepole watu wateule wa Mungu wanatambua upotoshwaji wao na Shetani na wanapata njia ya kuutoroka ushawishi wa Shetani, wakisaidia maisha yao kupata mabadiliko ya asteaste. Tajriba hizi halisi zinathibitisha kwamba kazi ya hukumu inayofanywa na Mwenyezi Mungu ni kazi ya kumwokoa mwanadamu kikamilifu.

  Soma Zaidi
 • Ushuhuda wa Washindi

  Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameanzisha kazi yake ya hukumu ya siku za siku mwisho nchini China, ingawa watu walioteuliwa wa Mungu wamepitia mateso makali, ya ukatili yakifanywa na serikali ya Kichina, wamekuwa watu wasioshindika na waaminifu kwa udhabiti chini ya mwongozo wa maneno ya Mungu, wakiunda shahidi mkubwa wa ushindi juu ya Shetani. Ukweli unaonyeshwa kikamilifu kwamba Mwenyezi Mungu kwa hakika ametengeneza kikundi cha washindi katika Enzi ya Ufalme, akifanikisha mpango wa usimamizi wa Mungu wa miaka elfu sita.

  Soma Zaidi
 • Jinsi Nilivyomgeukia Mwenyezi Mungu Tena

  Kila mmoja ambaye humwamini Mungu na kumgeukia Yeye tena hupitia safari isiyo ya kawaida ya moyo, na uzoefu wa kila mtu ni tofauti. Kitabu hiki ni mkusanyiko wa uzoefu wa kweli wa wateule wa Mungu kumgeukia Mwenyezi Mungu tena. Uzoefu huu unasimulia wateule wa Mungu kulegeza mawazo yao na vizuizi vya dini chini ya mwongozo wa maneno ya Mwenyezi Mungu, na kujiweka huru dhidi ya nguvu zinazompinga Kristo za dunia ya dini na vilevile vurugu na hali ya kushurutisha ya nguvu za shetani za CCP. Pia unasimulia safari zao za kuguza hisi za kupata uhakika kamili wa njia ya kweli na kugeukia tena kiti cha Mungu cha enzi katikati ya vita vyao vya kiroho. Vita hivi vikali vya kiroho vinasisitiza ubaya na uovu wa Shetani, na hasa vinasisitiza mamlaka na nguvu ya maneno ya Mungu. Wale wote ambao kwa kweli humwamini Mungu bila shaka watarudi mbele ya kiti cha Mungu cha enzi!

  Soma Zaidi
 • Maneno ya Mungu ya Kila Siku

  Kitabu hiki kina vifungu vilivyoteuliwa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili. Ili kwamba wateule wa Mungu waweze kupata ukweli na riziki ya kila siku ya uzima kutoka katika maneno Yake, maneno haya yaliyo bora kabisa ya Mwenyezi Mungu, ambayo yanaadilisha sana kwa kuingia kwa watu katika uzima, hapa yameteuliwa kwa njia maalumu ili watu wafurahie, na hivyo kuwaruhusu wale wanaopenda ukweli waweze kuuelewa, waweze kuishi mbele za Mungu, na kuokolewa na kukamilishwa na Mungu. Maneno haya yaliyo bora kabisa ya Mungu ni maonyesho ya ukweli; aidha, haya ndiyo kanuni zilizo bora kabisa zaidi za maisha, na hakuna maneno yanayowaadilisha na kuwanufaisha watu zaidi ya haya. Ukiweza kweli kufurahia kifungu kimoja cha maneno haya kila siku, basi hii ndiyo neema yako kubwa kabisa, na umebarikiwa na Mungu.

  Soma Zaidi
Gawa
Pakua