Madhumuni ya hatua tatu za kazi ya usimamizi wa Mungu wa wanadamu
Lengo la hatua tatu za kazi ni wokovu wa wanadamu wote—ambayo inamaanisha wokovu kamili wa mwanadamu kutoka kwa miliki ya Shetani. Ingawa kila moja ya hatua ya kazi ina madhumuni na umuhimu, kila moja ni sehemu ya kazi ya kumwokoa mwanadamu, na ni kazi tofauti ya wokovu inayotekelezwa kulingana na matakwa ya mwanadamu.
Madhumuni na Umuhimu wa Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Wakati huu, umuhimu, kusudi na awamu za kazi ya Yehova huko Israeli zilikuwa kuanzisha kazi Yake katika dunia nzima, ambayo, ikichukua Israeli kama kituo chake, ilienea polepole hadi kwa mataifa yasiyo ya Kiyahudi. Hii ni kanuni ambayo kwayo Anafanya kazi katika ulimwengu mzima—kuunda mfano na kisha kuupanua hadi watu wote ulimwenguni watakuwa wamepokea injili Yake.
Uhusiano Kati ya Kila Moja ya Hatua Tatu za Kazi ya Mungu
Hatua tatu za kazi zilifanywa na Mungu mmoja; haya ndiyo maono makubwa zaidi, na ndiyo njia ya pekee ya kumjua Mungu. Hatua tatu za kazi zingefanywa tu na Mungu Mwenyewe, na hapana mwanadamu yeyote ambaye angeweza kufanya kazi kama hii kwa niaba Yake—ambayo ni kusema kuwa ni Mungu Mwenyewe pekee ambaye angeifanya kazi Yake toka mwanzo hadi leo.
Ni jinsi gani hatua tatu za kazi ya Mungu kwa pole pole huongeza uketo ili watu waokolewe na kukamilishwa?
Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na kwa njia hii mahitaji ya mwanadamu huwa ya juu hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huwa ya juu hata zaidi.