Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu (Sehemu ya Nne)

Kutubu kwa Kweli Ndani ya Mioyo ya Waninawi Kunawapa Rehema ya Mungu na Kwabadilisha Hatima Zao Wenyewe

Je, kulikuwa na kuhitilafiana kokote kati ya mabadiliko ya moyo wa Mungu na hasira Yake? Bila shaka la! Hii ni kwa sababu uvumilivu wa Mungu kwa wakati ule ulikuwa na sababu yake. Je, sababu yake yaweza kuwa nini? Ni ile iliyotajwa kwenye Biblia: “Kila mtu aligeuka kutoka kwenye njia yake ya maovu” na “kuacha udhalimu uliokuwa mikononi mwake.”

Hii “Njia ya maovu” hairejelei kusanyiko la vitendo vya maovu, lakini inarejelea chanzo cha maovu katika tabia ya watu. “Kugeuka kutoka njia yake ya maovu” kunamaanisha kwamba wale wanaozungumziwa hawatawahi kutekeleza vitendo hivi tena. Kwa maneno mengine, hawatawahi kuwa na tabia inayoonyesha njia hii ya maovu tena; mbinu, chanzo, kusudio, nia na kanuni za vitendo vyao vyote vimebadilika; hawatawahi tena kutumia mbinu na kanuni hizi kuleta nafuu na furaha mioyoni mwao. Kule “kuacha” katika “kuacha udhalimu ulio mikononi mwao” kunamaanisha kuweka chini au kuweka pembeni, kujitenga kabisa na mambo ya kale na kutorudi nyuma tena. Wakati watu wa Ninawi walipoacha udhalimu uliokuwa mikononi mwao, hii ilithibitisha na vilevile iliwakilisha kutubu kwao kwa kweli. Mungu huangalia kwa makini sehemu ya nje na vilevile ndani ya mioyo ya watu. Wakati Mungu alipoangalia kwa makini kutubu kwa kweli katika mioyo ya Waninawi bila kuuliza swali na pia kutambua kwamba walikuwa wameacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu uliokuwa mikononi mwao, Alibadilisha moyo Wake. Hivi ni kusema kwamba mwenendo na tabia ya watu hawa na njia mbalimbali za kufanya mambo, pamoja na kuungama na kutubu kwa kweli kwa dhambi zilizokuwa mioyoni mwao, kulisababisha Mungu kubadilisha Moyo Wake, kubadilisha nia Zake, kufuta uamuzi wake na kutowaadhibu wala kuwaangamiza. Kwa hivyo, watu wa Ninawi waliweza kufikia hatima tofauti. Waliyakomboa maisha yao binafsi na wakati uo huo wakapata kibali cha huruma na uvumilivu wa Mungu, na wakati uo huo Mungu akawa pia amefuta hasira Yake.

Huruma na Uvumilivu wa Mungu si Nadra—Kutubu kwa Kweli kwa Binadamu Ni Nadra

Licha ya vile ambavyo Mungu alikuwa na ghadhabu kwa Waninawi, mara tu walipotangaza kufunga na kuvalia nguo ya gunia pamoja na jivu, moyo Wake ulianza kutulia taratibu, na Akaanza kubadilisha moyo Wake. Wakati Alipowatangazia kwamba Angeangamiza mji wao—ule muda kabla ya kuungama na kutubu kwa dhambi zao—Mungu alikuwa angali na ghadhabu na wao. Baada ya wao kupitia misururu ya vitendo vya kutubu, ghadhabu ya Mungu kwa watu wa Ninawi ikaanza kubadilika kwa utaratibu na Akaanza kuwaonea huruma na uvumilivu. Hakuna kitu kinachohitilafiana kuhusu ufunuo wenye ulinganifu katika dhana hizi mbili za tabia ya Mungu kwenye tukio lilo hilo. Ni vipi ambavyo mtu anafaa kuelewa na kujua ukosefu huu wa kuhitilafiana? Mungu aliweza kuonyesha kwa ufanisi na kufichua vipengele hivi viwili tofauti kabisa wakati watu wa Ninawi walipokuwa wakitubu, na Akawaruhusu watu kuona uhalisi na hali halisi ya kutokosewa kwa Mungu. Mungu alitumia mtazamo Wake kuambia watu yafuatayo: Si kwamba Mungu havumilii watu, au hataki kuwaonyesha huruma; ni kwamba wao hutubu kwa kweli mara nadra sana kwa Mungu, na ni nadra sana kwa watu kuweza kugeuka kwa kweli na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio mikononi mwao. Kwa maneno mengine, wakati Mungu ana ghadhabu kwa binadamu, Anatumaini kwamba binadamu ataweza kutubu kwa kweli na Anatumaini kumwona binadamu akitubu kwa kweli, ambapo Ataendelea kwa haki kumpa binadamu huyo huruma na uvumilivu. Hivi ni kusema kwamba mwenendo wa maovu ya mwanadamu ndio husababisha hasira ya Mungu, huku nazo rehema na uvumilivu wa Mungu zikipewa wale wanaomsikiliza Mungu na kutubu mbele yake, kwa wale wanaoweza kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuacha udhalimu ulio kwenye mikono yao. Mtazamo wa Mungu uliweza kufichuliwa waziwazi kuhusiana na vile Alivyowashughulikia Waninawi: Huruma na uvumilivu wa Mungu kwa kweli si vigumu kuvipokea; Anahitaji mtu kuwa na kutubu kwa kweli. Mradi tu watu waweze kugeuka na kuacha njia zao za maovu na kuuacha udhalimu ulio mikononi mwao, Mungu atabadilisha moyo Wake na kubadilisha mtazamo Wake kwao.

Tabia ya Haki ya Muumba ni ya Kweli na Wazi

Wakati Mungu alibadilisha moyo Wake kwa minajili ya watu wa Ninawi, je, huruma na uvumilivu Wake ulikuwa wa bandia? Bila shaka la! Basi mabadiliko haya kati ya dhana hizi mbili za tabia ya Mungu kwenye suala lili hili yalikuruhusu kuweza kuona nini? Tabia ya Mungu ni kamili na wazi; haijagawanywa hata kidogo. Licha ya kama Anaonyesha ghadhabu au huruma na uvumilivu kwa watu, haya yote ni maonyesho ya tabia Yake ya haki. Tabia ya Mungu ni kweli na wazi. Yeye hubadilisha fikira na mitazamo Yake kulingana na maendeleo ya mambo. Mabadiliko ya mtazamo Wake kwa Waninawi yanawaambia binadamu kwamba Anazo fikira na mawazo Yake mwenyewe; Yeye si roboti au chombo kilichofinyangwa kwa udongo, bali Yeye ni Mungu Mwenyewe mwenye uhai. Angeweza kuwa na ghadhabu kwa sababu ya watu wa Ninawi, sawa tu na vile ambavyo Aliweza kusamehe dhambi zao za kale kulingana na mitazamo yao; Angeweza kuamua kuwaletea Waninawi mkosi na Angeweza kubadilisha uamuzi Wake kwa sababu ya kutubu kwao. Watu hupendelea kutumia sheria bila kumakinika na wanapendelea kutumia sheria ili kuthibitisha na kufafanua Mungu, sawa tu na vile watu wanavyopendelea kutumia fomula ili kujua tabia ya Mungu. Kwa hivyo, kulingana na himaya ya fikira za binadamu, Mungu hafikirii wala Yeye hana mawazo yoyote halisi. Kwa uhalisi, fikira za Mungu zinabadilika mara moja kulingana na mabadiliko katika mambo, na mazingira; huku fikira hizi zikiwa zinabadilika, dhana tofauti za hali halisi ya Mungu zitaweza kufichuliwa. Kwenye kipindi hiki cha mabadiliko, wakati ule Mungu hubadilisha moyo Wake, Yeye hufichulia mwanadamu ukweli wa uwepo wa maisha Yake na kufichua kwamba tabia Yake ya haki ni halisi na wazi. Aidha, Mungu hutumia ufunuo Wake wa kweli kuthibitisha kwa mwanadamu ukweli wa uwepo wa hasira Yake, huruma Yake, upole wa upendo Wake na uvumilivu Wake. Hali hii halisi Yake itafichuliwa wakati wowote na mahali popote kulingana na maendeleo ya mambo. Anamiliki hasira ya simba na huruma na uvumilivu wa mama. Tabia yake ya haki hairuhusiwi kushukiwa, kukiukwa, kubadilishwa au kuharibiwa na mtu yeyote. Miongoni mwa masuala yote na mambo yote, tabia ya haki ya Mungu, yaani, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, vyote vinaweza kufichuliwa wakati wowote na mahali popote. Anaonyesha waziwazi dhana hizi katika kila elementi ya asili na kuzitekeleza kila wakati. Tabia ya haki ya Mungu haiwekewi mipaka ya muda au nafasi, au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Mungu haionyeshwi bila kufikiri au kufichuliwa kama inavyoongozwa na mipaka ya muda au nafasi. Badala yake, tabia ya haki ya Mungu inaonyeshwa kwa njia huru na kufichuliwa mahali popote na wakati wowote. Unapoona Mungu akibadilisha moyo Wake na kusita kuonyesha hasira Yake na kujizuia dhidi ya kuuangamiza mji wa Ninawi, je, unaweza kusema kwamba Mungu ni mwenye huruma na upendo tu? Je, unaweza kusema kwamba hasira ya Mungu inayo maneno matupu tu. Wakati Mungu anapoonyesha hasira Yake na kuiondoa huruma Yake, je, unaweza kusema kwamba Hana hisia zozote za upendo wa kweli kwa binadamu? Mungu huonyesha hasira kutokana na vitendo viovu vya watu, hasira Yake haina kosa. Moyo wa Mungu unavutiwa na kutubu kwa watu, na ni kutubu huku ambako hubadilisha moyo Wake. Kuvutiwa kwake, mabadiliko katika moyo Wake pamoja na huruma na uvumilivu Wake kwa binadamu, vyote kwa kweli havina kosa kamwe; ni safi, havina kasoro, havina doa na havijachafuliwa. Uvumilivu wa Mungu kwa kweli ni uvumilivu; Huruma Yake ni huruma bila kasoro. Tabia yake itafichua hasira, pamoja na huruma na uvumilivu, kulingana na kutubu kwa binadamu na mwenendo wake tofauti. Haijalishi kile ambacho Anafichua na kuonyesha, yote hayo hayana kasoro; yote ni ya moja kwa moja; hali Yake halisi ni tofauti na chochote kile katika uumbaji. Kanuni za matendo ambayo Mungu anaonyesha, fikira na mawazo Yake, au uamuzi wowote ule, pamoja na kitendo chochote kimoja, vyote havina dosari wala doa. Kama vile Mungu alivyoamua, ndivyo Atakavyotenda, na katika njia hii, Yeye hukamilisha shughuli Zake. Aina hizi za matokeo ni sahihi na hazina dosari kwa sababu chanzo chake hakina dosari na doa lolote. Hasira ya Mungu haina dosari. Vilevile, huruma na uvumilivu wa Mungu, ambazo hazimilikiwi na kiumbe chochote ni takatifu na hazina kosa, na zinaweza kujitokeza na kuendeleza utekelezaji na uzoefu.

Baada ya kuelewa hadithi ya Ninawi, je, unauona upande ule mwingine wa hali halisi ya tabia ya haki ya Mungu? Je, unauona upande ule mwingine wa tabia ya haki na ya kipekee ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote miongoni mwenu anayemiliki aina hii ya tabia? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki aina hii ya hasira kama ile ya Mungu? Je, kunaye mtu yeyote anayemiliki huruma na uvumilivu kama ule wa Mungu? Ni nani miongoni mwa viumbe anayeweza kuitisha hasira nyingi na kuamua kuangamiza au kuleta maafa kwa mwanadamu? Na ni nani amefuzu kutoa huruma, na kuvumilia na kumsamehe binadamu na hivyo basi kubadilisha uamuzi wake dhidi ya kuangamiza binadamu? Muumba huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni Zake za binafsi za kipekee; Hategemei kudhibitiwa au kuzuiliwa na watu, matukio au mambo yoyote. Akiwa na tabia Yake ya kipekee, hakuna mtu anayeweza kubadilisha fikira na mawazo Yake, wala hakuna yule anayeweza kumshawishi yeye na kubadilisha uamuzi wowote Wake. Uzima wa tabia na fikira za uumbaji upo katika hukumu ya tabia Yake ya haki. Hakuna anayeweza kudhibiti kama ataendeleza hasira au huruma; ni hali halisi tu ya Muumba—au kwa maneno mengine, tabia ya haki ya Muumba—inaweza kuamua hivi. Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!

Baada ya kuchambua na kuelewa mabadiliko katika mtazamo wa Mungu kwa watu wa Ninawi, je, unaweza kutumia neno “upekee” kufafanua huruma inayopatikana katika tabia ya haki ya Mungu? Hapo awali tulisema kwamba hasira ya Mungu ni dhana ya hali halisi ya tabia Yake ya haki na ya kipekee. Sasa Nitafafanua dhana mbili, hasira ya Mungu na huruma ya Mungu, kama tabia Yake ya haki. Tabia ya haki ya Mungu ni takatifu; haiwezi kukosewa na vilevile kushukiwa; ni kitu kisichomilikiwa na yeyote miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa. Ni ya kipekee na maalum kwa Mungu pekee. Hivi ni kusema kwamba hasira ya Mungu ni takatifu na isiyokosewa; wakati uo huo, kipengele kile kingine cha tabia ya haki ya Mungu—huruma ya Mungu—ni takatifu na haiwezi kukosewa. Hakuna yeyote kati ya viumbe vile vilivyoumbwa au vile ambavyo havikuumbwa, vinavyoweza kubadilisha au kuwakilisha Mungu katika vitendo Vyake, wala hakuna yeyote anayeweza kubadilisha au kumwakilisha Yeye katika kuangamiza Sodoma au wokovu wa Ninawi. Haya ndiyo maonyesho ya kweli ya tabia ya haki ya kipekee ya Mungu.

Hisia za Dhati za Muumba kwa Wanadamu

Watu mara nyingi husema kwamba si jambo rahisi kumjua Mungu. Mimi, hata hivyo, nasema kwamba kumjua Mungu si jambo gumu kamwe, kwani Mungu mara kwa mara huruhusu binadamu kushuhudia matendo Yake. Mungu hajawahi kusitisha mazungumzo Yake na mwanadamu; Yeye hajawahi kujificha kutoka kwa binadamu, wala Yeye hajajificha. Fikira Zake, mawazo Yake, maneno Yake na matendo Yake vyote vimefichuliwa kwa mwanadamu. Kwa hivyo, mradi tu mwanadamu angependa kumjua Mungu, anaweza kumwelewa hatimaye na kumjua Yeye kupitia aina zote za mambo na mbinu. Sababu inayomfanya binadamu kufikiria kwa kutojua kwamba Mungu amemwepuka kimakusudi, kwamba Mungu amejificha kimakusudi kutoka kwa binadamu, kwamba Mungu hana nia yoyote ya kumruhusu mwanadamu kuelewa na kumjua Yeye, ni kwamba hajui Mungu ni nani, wala asingependa kujua Mungu; na hata zaidi, hajali kuhusu fikira, matamshi au matendo ya Muumba…. Kusema kweli, kama mtu atatumia tu muda wake wa ziada vizuri katika kuzingatia na kuelewa matamshi au matendo ya Muumba na kuuweka umakinifu mchache kwa fikira za Muumba na sauti ya moyo Wake, haitakuwa vigumu kwa wao kutambua ya kwamba fikira, maneno na matendo ya Muumba, vyote vinaonekana na viko wazi. Vilevile, itachukua jitihada kidogo kutambua kwamba Muumba yuko miongoni mwa binadamu siku zote, kwamba siku zote Anazungumza na binadamu na uumbaji mzima, na kwamba Anatekeleza matendo mapya, kila siku. Hali Yake halisi na tabia vyote vimeelezewa katika mazungumzo Yake na binadamu; fikira na mawazo Yake vyote vinafichuliwa kabisa kwenye matendo Yake haya; Anaandamana na kufuatilia mwanadamu siku zote. Anaongea kimyakimya kwa mwanadamu na uumbaji wote kwa maneno Yake ya kimyakimya: Mimi niko juu ya ulimwengu, na Mimi nimo miongoni mwa uumbaji Wangu. Ninawaangalia, Ninawasubiri; Niko kando yenu…. Mikono yake ni yenye joto na thabiti; nyayo Zake ni nuru; sauti Yake ni laini na yenye neema, umbo Lake linapita na kugeuka, linakumbatia binadamu wote; uso Wake ni mzuri na mtulivu. Hajawahi kuondoka, wala Hajatoweka. Usiku na mchana, Yeye ndiye rafiki wa karibu na wa siku zote wa mwanadamu. Utunzaji wake wa kujitolea na huba maalum kwa binadamu, pamoja na kujali Kwake kwa kweli na upendo kwa binadamu, vyote vilionyeshwa kwa utaratibu wakati Alipookoa mji wa Ninawi. Haswa, mabadilishano ya mazungumzo kati ya Yehova Mungu na Yona yaliweza kuweka msingi wa huruma ya Muumba kwa mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe Aliumba. Kupitia kwa maneno haya, unaweza kupata ufahamu wa kina wa hisia za dhati za Mungu kwa binadamu …

Yafuatayo yamerekodiwa kwenye kitabu cha Yona 4:10-11: “Kisha Yehova akasema, Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?” Haya ni maneno halisi ya Yehova Mungu, mazungumzo kati Yake na Yona. Huku mabadilishano ya mazungumzo haya yakiwa mafupi, yamejaa utunzaji wa Muumba kwa mwanadamu na kutotaka Kwake kukata tamaa. Matamshi haya yanaonyesha mtazamo na hisia za kweli ambazo Mungu anashikilia ndani ya moyo Wake kuhusu uumbaji Wake, na kupitia kwa maneno haya yaliyowekwa wazi, ambayo yanasikizwa kwa nadra sana na binadamu, Mungu anakariri nia Zake za kweli kwa binadamu. Mabadilishano ya mazungumzo haya yanawakilisha mtazamo ambao Mungu alishikilia kwa watu wa Ninawi—lakini mtazamo aina hii ni upi? Ni mtazamo Alioshikilia kuhusu watu wa Ninawi kabla na baada ya kutubu kwao. Mungu huchukulia binadamu kwa njia sawa. Ndani ya maneno haya mtu anaweza kupata fikira Zake, pamoja na tabia Yake.

Je, ni fikira zipi za Mungu zinafichuliwa katika maneno haya? Usomaji wa makini unafichua mara moja kwamba Anatumia neno “huruma”; matumizi ya neno hili yanaonyesha mtazamo wa kweli wa Mungu kwa binadamu.

Kutokana na mtazamo wa kisemantiki, mtu anaweza kufasiri neno “huruma” kwa njia tofauti: kwanza, kupenda na kulinda, kuhisi huruma kuhusu kitu fulani; pili, kupenda kwa dhati; hatimaye, kutokuwa radhi kukiumiza na vilevile kutoweza kuvumilia kufanya hivyo. Kwa ufupi, unaashiria yale mahaba na upendo wa dhati, pamoja na kutokuwa radhi kukata tamaa na kumwacha mtu au kitu; unamaanisha huruma ya Mungu na uvumilivu kwa mwanadamu. Ingawaje Mungu alitumia neno linalotamkwa mara nyingi miongoni mwa binadamu, matumizi ya neno hili yanaweka wazi sauti ya moyo wa Mungu na mtazamo Wake kwa mwanadamu.

Huku mji wa Ninawi ukiwa umejaa watu waliopotoka, walio waovu, na wenye udhalimu kama wale wa Sodoma, kutubu kwao kulisababisha Mungu kubadilisha moyo Wake na kuamua kutowaangamiza. Kwa sababu mwitikio wao kwa maneno na maagizo ya Mungu ulionyesha mtazamo uliokuwa na utofauti mkavu na ule wa wananchi wa Sodoma, na kwa sababu ya utiifu wao wa dhati kwa Mungu na kutubu kwa uaminifu dhambi zao, pamoja na tabia yao ya kweli na dhati kwa hali zote, Mungu kwa mara nyingine alionyesha huruma Yake ya moyoni naye akaweza kuwapa. Tuzo ya Mungu na huruma Yake kwa binadamu haiwezekani kwa yeyote yule kurudufu; hakuna mtu anayeweza kumiliki huruma au uvumilivu wa Mungu, wala hisia Zake za dhati kwa binadamu. Je, yupo yeyote unayemwona kuwa mwanamume au mwanamke mkuu, au hata mwanamume mkuu zaidi, ambaye angeweza, kutoka katika mtazamo mkuu, akiongea kama mwanamume au mwanamke mkuu au kwenye sehemu ya mamlaka ya juu, kutoa aina hii ya kauli kwa mwanadamu au viumbe? Ni nani miongoni mwa wanadamu anaweza kujua masharti ya kuishi ya binadamu kama viganja vya mkono wake? Ni nani anayeweza kuvumilia mzigo na jukumu la kuwepo kwa binadamu? Nani anaweza kutangaza kuangamizwa kwa mji? Na ni nani anaweza kusamehe mji? Ni nani wanaoweza kusema wanafurahia uumbaji wao binafsi? Muumba Pekee! Muumba pekee ndiye aliye na huruma kwa wanadamu hawa. Muumba pekee ndiye anayeonyesha mwanadamu huyu huruma na huba. Muumba pekee ndiye anayeshikilia huba ya kweli, isiyovunjika kwa mwanadamu huyu. Vilevile, Muumba pekee ndiye anayeweza kumpa huruma mwanadamu huyu na kufurahia viumbe vyake vyote. Moyo wake waruka na kuumia kwa kila matendo ya mwanadamu: Ameghadhibishwa, dhikishwa, na kuhuzunishwa juu ya maovu na kupotoka kwa binadamu; Ameshukuru, amefurahia, amekuwa mwenye kusamehe na mwenye kushangilia kutokana na kutubu na kuamini kwa binadamu; kila mojawapo ya fikira na mawazo Yake vyote vipo juu ya na vinazungukia mwanadamu; kile Alicho na anacho vyote vinaonyeshwa kwa uzima au kwa minajili ya mwanadamu; uzima wa hisia Zake vyote vimeingiliana na uwepo wa mwanadamu. Kwa minajili ya mwanadamu, Anasafiri na kuzungukazunguka; kwa utaratibu Anatoa kila sehemu ya maisha Yake; Anajitolea kila dakika na sekunde ya maisha Yake…. Hajawahi kujua namna ya kuyahurumia maisha Yake, ilhali siku zote Amehurumia na kufurahia mwanadamu ambaye Yeye Mwenyewe aliumba…. Anatoa kila kitu Alichonacho kwa binadamu hawa…. Yeye anatoa huruma na uvumilivu Wake bila masharti na bila matarajio ya kufidiwa. Anafanya hivi tu ili mwanadamu aweze kuendelea kuwepo mbele ya macho Yake, kupokea toleo Lake la maisha; Anafanya hivi tu ili mwanadamu siku moja aweze kunyenyekea mbele Yake na kutambua kwamba Yeye ni yule anayetosheleza kuwepo kwa binadamu na kuruzuku maisha ya viumbe vyote.

Muumba Aonyesha Hisia Zake za Kweli Kwa Binadamu

Mazungumzo haya kati ya Yehova Mungu na Yona bila shaka ni onyesho la hisia za kweli za Muumba juu ya binadamu. Kwa upande mmoja yanafahamisha watu kuhusu ufahamu wa Muumba wa asili yote yaliyo katika amri Yake; kama vile Yehova Mungu alivyosema, “Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu, ulio na zaidi ya watu elfu mia na ishirini ndani yake ambao hawawezi kutambua kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; na pia mifugo wengi?” Kwa maneno mengine, ufahamu wa Ninawi na Mungu haukuwa hata karibu na ule wa laana. Hakujua tu idadi ya viumbe vilivyo hai ndani ya mji (wakiwemo watu na mifugo), bali Alijua pia ni wangapi wasingeweza kutambua kati ya mikono yao ya kulia na kushoto—yaani, ni watoto na vijana wangapi walikuwepo. Hii ni ithibati thabiti ya ufahamu bora kuhusu mwanadamu. Kwa upande mwingine mazungumzo haya yanafahamisha watu kuhusu mtazamo wa Muumba kwa binadamu, ambako ni kusema kwamba uzito wa binadamu katika moyo wa Muumba. Ni vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Umeuonea mtango huruma, ambao hujafanyia kazi, wala kuukuza; ambao ulimea kwa usiku mmoja, na kufa kwa usiku mmoja: Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma, mji ule mkuu…?” Haya ndiyo maneno ya Yehova Mungu kuhusu lawama kwa Yona lakini yote ni kweli.

Ingawaje Yona alikuwa ameaminiwa kutangaza matamshi ya Yehova Mungu kwa watu wa Ninawi, hakuelewa nia za Yehova Mungu, wala hakuelewa wasiwasi na matarajio Yake kwa watu wa mji huu. Kupitia kwa kemeo hili Mungu alinuia kumwambia kwamba binadamu ulikuwa zao la mikono Yake mwenyewe, na kwamba Mungu alikuwa ametia jitihada za dhati kwa kila mtu; kila mtu alisheheni matumaini ya Mungu; kila mtu alifurahia ruzuku ya maisha ya Mungu; kwa kila mtu, Mungu alikuwa amelipia gharama ya dhati. Kemeo hili lilimfahamisha Yona kwamba Mungu aliufurahia binadamu, kazi ya mikono Yake mwenyewe, kama vile tu ambavyo Yona mwenyewe aliufurahia mtango. Mungu kwa vyovyote vile asingewaacha kwa urahisi kabla ya ule muda wa mwisho unaowezekana; vilevile, kulikuwa na watoto wengi na mifugo isiyo na hatia ndani ya mji. Wakati wa kushughulikia mazao haya machanga na yasiyojua uumbaji wa Mungu, ambayo yasingeweza hata kutofautisha mikono yao ya kulia na ile ya kushoto, Mungu hakuweza kamwe kukomesha maisha yao na kuamua matokeo yao kwa njia ya haraka hivyo. Mungu alitumai kuwaona wakikua; Alitumai kwamba wasingetembea njia ile ile kama wakubwa wao, kwamba wasingeweza kusikia tena onyo la Yehova Mungu, na kwamba wangeshuhudia mambo ya kale ya Ninawi. Na hata zaidi Mungu alitumai kuiona Ninawi baada ya kuweza kutubu, kuuona mustakabali wa Ninawi kufuatia kutubu kwake, na muhimu zaidi, kuiona Ninawi ikiishi katika huruma za Mungu kwa mara nyingine tena. Kwa hivyo, kwa macho ya Mungu, yale mazao ya uumbaji wake ambayo hayangeweza kutofautisha mikono yao ya kulia na kushoto yalikuwa mustakabali wa Ninawi. Wangeweza kubeba na kusimulia hadithi ya kale iliyostahili dharau, kama vile tu ambavyo wangeweza kusimulia wajibu muhimu wa kushuhudia hadithi ya kale ya Ninawi na mustakabali wake kupitia kwa mwongozo wa Yehova Mungu. Katika tangazo hili la hisia Zake za kweli, Yehova Mungu aliwasilisha huruma ya Muumba kuhusu binadamu kwa ukamilifu wake. Liliwaonyesha binadamu kwamba “ile huruma ya Muumba” si kauli tupu tu, wala si ahadi isiyotimizika; ilikuwa na kanuni, mbinu na majukumu ya kimsingi. Yeye ni kweli na halisi, na hatumii uwongo au utapeli wowote, na kwa njia ii hii huruma Yake inawekewa binadamu katika kila wakati na enzi. Hata hivyo, hadi siku hii, mabadilishano ya mazungumzo ya Muumba na Yona ndiyo kauli moja, na ya kipekee ya matamshi yanayoelezea ni kwa nini Anaonyesha huruma kwa binadamu, ni vipi Alivyo na uvumilivu kwa binadamu na hisia Zake za kweli kuhusu binadamu. Mazungumzo haya ya Yehova Mungu yenye uchache na uwazi yanaonyesha fikira Zake kamili kuhusu binadamu; ni maonyesho ya ukweli ya mtazamo wa moyo Wake kwa binadamu, na ni ushahidi thabiti wa kutoa Kwake kwingi kwa huruma juu ya binadamu. Huruma yake haipewi tu vizazi vya wazee wa binadamu; lakini pia imepewa wanachama wachanga zaidi wa binadamu, kama vile tu ambavyo imekuwa, kuanzia kizazi kimoja hadi kingine. Ingawaje hasira ya Mungu hushushwa mara kwa mara kwenye pembe fulani na enzi fulani za binadamu, huruma ya Mungu haijawahi kusita. Kupitia kwa huruma Yake, Yeye huongoza na kuelekeza kizazi kimoja cha uumbaji Wake hadi kingine, huruzuku na kukifaa kizazi kimoja cha uumbaji hadi kingine, kwa sababu hisia Zake za kweli kwa binadamu hazitawahi kubadilika. Vile tu Yehova Mungu alivyosema: “Nami sipaswi kuonea Ninawi huruma…?” Siku zote amefurahia uumbaji Wake mwenyewe. Hii ndiyo huruma ya tabia ya haki ya Muumba, na ndio pia upekee usio na kasoro wa Muumba!

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp