Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu (Sehemu ya Kwanza)

Kwa vile sasa mmesikiliza ushirika uliopita kuhusu mamlaka ya Mungu, Ninao ujasiri kwamba mmejihami vilivyo na mseto wa maneno kuhusu suala hili. Kiwango unachoweza kukubali, kufahamu, na kuelewa vyote hivi vinategemea na jitihada zipi utakazotumia. Ni tumaini Langu kwamba utaweza kutazamia suala hili kwa dhati; kwa vyovyote vile hufai kulishughulikia shingo upande! Sasa, je, kujua mamlaka ya Mungu ni sawa na kujua Mungu kwa uzima wake? Mtu anaweza kusema kwamba kujua mamlaka ya Mungu ndiyo mwanzo wa kumjua Mungu mwenyewe kwa upekee wake, na mtu anaweza kusema pia kwamba kuyajua mamlaka ya Mungu kunamaanisha kwamba mtu tayari ameingia kwenye lango kuu la kujua hali halisi ya ule upekee wa Mungu Mwenyewe. Ufahamu huu ni sehemu moja ya kumjua Mungu. Sehemu ile nyingine ni nini, hivyo basi? Hii ndiyo mada ambayo Ningependa tuweze kushiriki pamoja leo—tabia ya haki ya Mungu.

Nimeteua sehemu mbili kutoka kwenye Biblia ambazo ningependa tushiriki pamoja kuhusu mada ya leo: Jambo la kwanza linahusu kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu, ambalo linaweza kupatikana kwenye Mwanzo 19:1-11 na Mwanzo 19:24-25; jambo la pili linahusu ukombozi wa Ninawi na Mungu, ambalo linaweza kupatikana kwenye kitabu cha Yona 1:1-2, kuongezea sura zile za tatu na nne za kitabu hiki. Ninashuku kwamba nyinyi nyote mnasubiri kusikia kile Nilicho nacho kuhusu sehemu hizi mbili. Kile Ninachosema hakiwezi kwenda kando na mada ya kutaka kumjua Mungu Mwenyewe na kujua hali Yake halisi, lakini ni nini kitakachokuwa zingatio la ushirika wa leo? Je, yupo yeyote kati yenu anayejua? Ni sehemu zipi za ushirika Wangu kuhusu “Mamlaka ya Mungu” ziliweza kuwavutia? Kwa nini Nilisema kwamba yule tu anayemiliki mamlaka na nguvu kama hizo ndiye Mungu mwenyewe? Ni nini Nilichotaka kuelezea kwa kusema hivyo? Ni nini ambacho Nilipenda kukufahamisha kuhusu? Je, mamlaka na nguvu za Mungu ni mtazamo mmoja unaoelezea kuhusu hadhi Yake halisi na inavyoonyeshwa? Je, mamlaka na nguvu hizi ni sehemu ya hali Yake halisi ambayo inathibitisha utambulisho Wake na hadhi? Je, maswali haya yamekufahamisha kile Ninachoenda kusema? Ni nini Ninachotaka uelewe? Fikiria hili kwa makini.

Kwa Kupinga Mungu kwa Ukaidi, Binadamu Anaangamizwa na Hasira za Mungu

Kwanza, hebu tuweze kuangalia mafungu mbalimbali ya maandiko yanayofafanua “kuangamizwa kwa Sodoma na Mungu.”

Mwa 19:1-11 Na jioni malaika wawili walikuja Sodoma; naye Lutu aliketi katika lango la Sodoma: na baada ya Lutu kuwaona aliinuka kwenda kuwakaribisha; na akasujudu; Naye akasema, Tazama saa hii, bwana zangu, ingieni ndani, nawaomba, ndani ya nyumba ya mtumishi wenu, na mbaki usiku mzima, na msafishe miguu yenu, na mtaamka mapema, na mshike njia zenu. Nao wakasema, La; lakini tutaketi katika uwanja usiku mzima. Na akawaomba sana; na wakamjia na kuingia katika nyumba yake; na akawaandalia karamu, na kupika mikate bila chachu, na hawakula. Lakini kabla ya wao kujilaza, watu kutoka mjini, hata wenyeji wa Sodoma, waliizunguka nyumba hiyo, wazee na pia vijana, watu wote kutoka kila sehemu: Na wakamwita Lutu, na kumwambia, Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua. Naye Lutu akatoka mlangoni mahali walipokuwa, na akafunga mlango nyuma yake, Na kusema, nawaomba, ndugu, msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu. Na walisema. Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango. Lakini watu wale wakanyosha mbele mkono wao, na kumvuta Lutu katika nyumba walikokuwa, na kuufunga mlango. Na wakawagonga wale watu waliokuwa katika mlango wa nyumba na upofu, wakubwa na wadogo: kiasi kwamba walijichosha kuutafuta mlango.

Mwa 19:24-25 Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka Yehova kutoka mbinguni; Na akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.

Kutoka kwenye mafungu haya, si vigumu kuona kwamba dhambi ya Sodoma na kupotoka kwake tayari vilikuwa vimefikia kiwango kilichochukiza binadamu na Mungu, na kwamba kwa macho ya Mungu mji ulifaa kuangamizwa. Lakini nini kilichofanyikia mji huu hapo awali kabla haujaangamizwa? Ni nini tunachoweza kujifunza kutoka kwenye matukio haya? Je, mtazamo wa Mungu katika matukio haya unatuonyesha nini kuhusu tabia yake? Ili kuelewa hadithi nzima, hebu na tuweze kusoma kwa makini kile kilichorekodiwa katika Maandiko …

Kupotoka kwa Sodoma: Kunakasirisha Binadamu, Kunaghadhibisha Mungu

Kwenye usiku huo, Lutu alipokea wajumbe wawili kutoka kwa Mungu na akawatayarishia karamu. Baada ya chajio, kabla hawajalala, watu kutoka kila pahali kwenye mji walizunguka makazi ya Lutu na kumwita nje Lutu. Maandiko yanawarekodi wakisema, “Wako wapi wale wanaume waliokuja kwako leo usiku? Walete kwetu, ili tupate kuwajua.” Ni nani aliyesema maneno haya? Alikuwa akiwaambia kina nani? Haya yalikuwa maneno ya watu wa Sodoma, walipiga mayowe nje ya makazi ya Lutu wakinuia kumwita Lutu. Je, unahisi vipi ukiyasikia maneno haya? Unaghadhibishwa? Je, maneno haya yanakuhuzunisha? Je, unabubujikwa na hasira kali? Je, Huoni kwamba maneno haya yananuka Shetani? Kupitia kwa maneno haya, unaweza kuhisi uovu na giza vilivyomo kwenye mji huu? Je, unaweza kuhisi ukatili na ushamba wa tabia za watu hawa kupitia kwa maneno yao? Je, unaweza kuhisi kina cha kupotoka kwao kupitia kwa tabia yao? Kupitia kwa maudhui ya hotuba yao, si vigumu kuona kwamba asili yao ya dhambi na tabia yao iliyopotoka ilikuwa imefikia kiwango kilichokuwa zaidi ya wao kuidhibiti. Isipokuwa Lutu, kila mtu katika mji huu hakuwa tofauti na Shetani; ule mtazamo tu wa mtu mwingine uliwafanya watu hawa kutaka kudhuru na kuwapotosha wao…. Mambo haya hayampatii tu mtu hisia ya asili potovu na ya kutisha ya mji huu, lakini pia yanamwonyesha harufu ya kifo iliyouzunguka mji huu; yanampa pia mtu hisia za dhambi na umwagikaji wa damu.

Alipojipata uso kwa uso na genge la majambazi waliojaa ukatili, watu waliokuwa wamejaa na maono ya kupotosha nafsi, Lutu aliitikia vipi? Kulingana na Maandiko: “Nawaomba … msitende maovu hivyo. Tazameni sasa, ninao mabinti wawili ambao ni mabikira; mniruhusu, nawaomba, niwalete nje kwenu, na mwafanyie mwonavyo kuwa vizuri katika macho yenu: ila kwa hawa wanaume msifanye chochote: kwani wamekuja chini ya kivuli cha paa langu.” Lutu alimaanisha yafuatayo katika maneno yake: Alikuwa radhi kuwatoa binti zake wawili ili kuwalinda wale wajumbe. Kutokana na akili razini, watu hawa wangekubali masharti ya Lutu na kuwaacha wale wajumbe wawili pekee; kwani hata hivyo, wajumbe hao walikuwa watu wageni kabisa kwao, watu ambao hawakuwa na chochote katu kuhusiana na wao; wajumbe hawa wawili walikuwa hawajawahi kudhuru masilahi yao. Hata hivyo, wakiwa na motisha ya asili yao ya dhambi, hawakuliwachia suala hili hapo. Badala yake, walizidisha tu jitihada zao. Hapa mojawapo ya mabishano yao yanaweza bila shaka kumpatia mtu maono zaidi kuhusu asili ya kweli na potovu ya watu hawa; wakati uo huo yanatujuza na kutufanya tuelewe sababu ya Mungu kutaka kuuangamiza mji huu.

Kwa hivyo walisema nini baadaye? Kama vile Biblia inavyosoma: “Toka. Na wakasema tena, Mtu huyu mmoja aliingia kwetu kukaa kwa muda, naye anatamani kuhukumu: sasa tutakushughulikia kwa njia mbaya zaidi, kuliko wao. Na wakamshinikiza sana mtu huyo, hadi Lutu, na wakawa karibu kuuvunja mlango.” Kwa nini walitaka kuuvunja mlango? Sababu ni kwamba walikuwa na hamu kubwa zaidi ya kuwadhuru wale wajumbe wawili. Wale wajumbe walikuwa wakifanya nini Sodoma? Kusudio lao la kuja hapo lilikuwa ni kumwokoa Lutu na familia yake; hata hivyo, watu wa mji huo walifikiri kimakosa kwamba walikuwa wamekuja kuchukua nyadhifa zao rasmi. Bila ya kuulizia kusudio lao, ilikuwa tu hali ya kujiamulia kufanya mambo kabla ya kujua ukweli wake, iliyoufanya mji huo kutaka kuwadhuru vibaya wajumbe hawa wawili; walitaka kuwadhuru watu wawili ambao hawakuhusiana kwa vyovyote vile na wao. Ni wazi kwamba watu wa mji huu walikuwa wamepoteza kabisa ubinadamu na akili zao razini. Kiwango cha wendawazimu wao na kukosa ustaarabu kwao kilikuwa tayari si tofauti na asili potovu ya Shetani ya kudhuru na kudanganya binadamu.

Walipowaamuru watu hawa watoke kwa Lutu, Lutu alifanya nini? Kutoka kwenye maandishi yanayofuata tunajua kwamba Lutu hakuwakabidhi wajumbe hawa kwa watu hawa. Je, Lutu aliwajua wajumbe hawa wawili wa Mungu? Bila shaka la! Lakini kwa nini aliweza kuwaokoa watu hawa wawili? Je, alijua ni nini walichokuwa wamekuja kufanya? Ingawaje hakujua kuhusu sababu yao ya kuja, alijua kwamba walikuwa ni watumishi wa Mungu, na kwa hivyo aliwapokea. Kwamba aliweza kuwaita watumishi hawa wa Mungu mabwana yaonyesha kwamba Lutu kwa kawaida alikuwa ni mfuasi wa Mungu, tofauti na wale wengine waliokuwa ndani ya Sodoma. Kwa hivyo, wakati wajumbe wa Mungu walipomjia, alihatarisha maisha yake binafsi ili kuwapokea watumishi hao wawili; aidha, aliwakabidhi binti zake wawili badala ya watumishi hao wawili ili kuwalinda watumishi hao. Hiki ndicho kitendo cha haki ya Lutu; vilevile ni onyesho linaloonekana waziwazi kuhusu asili na hali halisi ya Lutu, na ndiyo pia sababu ya Mungu kuwatuma watumishi Wake ili kumwokoa Lutu. Wakati alipokabiliwa na changamoto, Lutu aliwalinda watumishi hawa wawili bila kujali chochote kingine; alijaribu hata kufanya biashara ya kuwabadilisha binti zake wawili mradi tu watumishi hawa wapate usalama. Mbali na Lutu, kulikuwa na mtu yeyote mwingine ndani ya mji ambaye angefanya jambo kama hili? Kama vile hoja zinavyothibitisha—la! Kwa hivyo, ni wazi kabisa kwamba kila mtu katika Sodoma, isipokuwa Lutu, alikuwa mlengwa wa kuangamizwa pamoja na mlengwa aliyestahili kuangamizwa.

Sodoma Yaangamizwa kwa Kukosea Hasira za Mungu

Wakati watu wa Sodoma walipowaona watu hawa wawili, hawakuuliza sababu ya wao kuja wala hakuna yule aliyeuliza kama walikuwa wamekuja kueneza mapenzi ya Mungu. Kinyume cha mambo, walikusanyika na kuwa umati wa watu na, bila kusubiri ufafanuzi wowote, walikuja kuwakamata watumishi hawa wawili ni kana kwamba walikuwa mbwa koko au mbwa mwitu. Je, Mungu aliyatazama mambo haya wakati yalipokuwa yakifanyika? Mungu alikuwa akifikiria nini katika moyo Wake kuhusiana na tabia hii ya binadamu, aina ya jambo hili? Mungu aliamua kuangamiza mji huu; Asingesita wala kusubiri, wala Asingeendelea kuonyesha subira yake. Siku yake ilikuwa imetimia, na kwa hivyo Aliweza kuweka wazi kazi Aliyopenda kufanya. Hivyo basi, Mwanzo 19:24-25 inasema, “Kisha Yehova alinyesha kwa Sodoma na Gomora kibiriti na moto kutoka Yehova kutoka mbinguni; Na akaiangusha hiyo miji, na mabonde yote, na wenyeji wote wa miji hiyo, na kile kilichomea kutoka ardhini.” Mistari hii miwili inawaambia watu mbinu ambayo kwayo Mungu aliuangamiza mji huu; pia inawaambia watu kile ambacho Mungu aliangamiza. Kwanza, Biblia inasimulia kwamba Mungu aliunguza mji kwa moto, na kwamba kiwango cha moto kilikuwa tosha kuangamiza watu wote na kila kitu kilichomea kwenye ardhi. Hii ni kusema kwamba, moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji; uliangamiza pia watu wote na vitu vilivyo hai ndani yake, vyote bila kuacha chochote nyuma. Baada ya mji kuangamizwa, ardhi ilikuwa tupu bila kitu chochote kilicho hai. Hakukuwa tena na maisha, wala dalili zozote za maisha. Mji ulikuwa umebadilika na kuwa ardhi iliyoharibiwa, mahali patupu palipojaa kimya cha kutisha. Kusingekuwa na matendo maovu zaidi dhidi ya Mungu mahali hapa; kusingekuwa na uchinjaji zaidi au umwagikaji wa damu.

Kwa nini Mungu alitaka kuuchoma mji huu kabisa? Ni nini unachoweza kuona hapa? Je, Mungu angevumilia kumwona mwanadamu na asili, viumbe Vyake mwenyewe, vikiangamia hivi? Kama unaweza kutambua ghadhabu ya Yehova Mungu kutokana na moto ule ambao uliangushwa kutoka mbinguni, basi si vigumu sana kuona kiwango Chake cha hasira kali kutoka kwenye lengo la maangamizo Yake pamoja na kiwango ambacho mji huo uliweza kuangamizwa. Wakati Mungu anadharau mji, Ataweza kutekeleza adhabu Yake juu ya mji huo. Wakati Mungu anachukizwa na mji, Ataweza kutoa maonyo mbalimbali akifahamisha watu kuhusu ghadhabu Yake. Hata hivyo, wakati Mungu anaamua kukomesha na kuangamiza mji—yaani, wakati hasira Yake na adhama vimekosewa—Hataweza kutoa maonyo au adhabu nyingine. Badala yake, Ataweza kuuangamiza moja kwa moja. Ataufanya kutoweka kabisa. Hii ndiyo tabia ya haki ya Mungu.

Baada ya Ukinzani wa Mara kwa Mara wa Sodoma na Ukatili Wao Dhidi Yake, Mungu Anaufuta Kabisa

Mara tu tunapokuwa na ufahamu wa jumla kuhusu tabia ya haki ya Mungu, tunaweza kurejesha umakinifu wetu kwenye mji wa Sodoma—kile ambacho Mungu aliona kuwa mji wa dhambi. Kwa kuelewa hali halisi ya mji huu, tunaweza kuelewa ni kwa nini Mungu alitaka kuuangamiza na ni kwa nini Aliuangamiza kabisa. Kutokana na haya, tunaweza kujua tabia ya haki ya Mungu.

Kutoka katika mtazamo wa binadamu, Sodoma ulikuwa ni mji ulioweza kutosheleza kikamilifu matamanio ya binadamu na maovu ya binadamu. Ulivutia na uliduwaza, kwa muziki na densi usiku baada ya usiku, ufanisi wake uliwasukuma wanaume kufurahia na kuruka kichwa. Maovu yake yalidhuru mioyo ya watu na yakawaduwaza hadi kuzoroteka. Huu ulikuwa mji uliokuwa na roho chafu na roho za Shetani zilicharuka hewani; ulijaa dhambi na mauaji na harufu ya damu iliyovunda. Ulikuwa mji ambao ulitisha watu kabisa, mji ambao mtu angejitoa kwake kwa hofu. Hakuna mtu katika mji huu—awe wa kiume au wa kike, awe mchanga au mzee—aliyetafuta njia ya kweli; hakuna aliyetamani mwangaza au kutaka kuachana na dhambi. Kila mmoja aliishi chini ya udhibiti wa Shetani, upotovu na uwongo. Kila mmoja alikuwa ameupoteza ubinadamu wake; walikuwa wamepoteza hisia zao, na walikuwa wamepoteza shabaha asilia ya kuweko kwa binadamu. Walitenda dhambi zisizohesabika za ukinzani dhidi ya Mungu; walikataa mwongozo wake na kupinga mapenzi Yake. Yalikuwa matendo yao maovu ambayo yaliwapeleka watu hawa, mji na kila kiumbe kilichokuwa ndani ya mji huu, hatua kwa hatua, kwenye njia ya maangamizo.

Ingawaje mafungu haya mawili hayarekodi maelezo yanayofafanua kiwango cha kupotoka cha watu wa Sodoma, badala yake yanarekodi mwenendo wao kwa watumishi wawili wa Mungu kufuatia kuwasili kwao mjini, ukweli mtupu unaweza kufichua kiwango ambacho watu wa Sodoma walikuwa wamepotoka, walijaa maovu na walimpinga Mungu. Kwa mujibu wa haya, ukweli wa mambo na hali halisi ya watu wa mji huu vinafichuliwa pia. Mbali na kutokubali maonyo ya Mungu, hawakuogopa pia adhabu Yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, walifanyia mzaha ghadhabu ya Mungu. Walimpinga Mungu bila sababu. Haijalishi ni nini Alichofanya au ni vipi Alivyokifanya, asili yao ya tamaa ilizidi kuongezeka, na wakampinga Mungu mara kwa mara. Watu wa Sodoma walikuwa wakatili kwa uwepo wa Mungu, kuja Kwake, adhabu Yake, na hata zaidi, maonyo Yake. Hawakuona chochote kingine chenye thamani karibu nao. Waliwapotosha na kuwadhuru watu wote walioweza kupotoshwa na kupata madhara, na wakawatendea watumishi wa Mungu vivyo hivyo. Kuhusiana na matendo yote ya uovu yaliyotendwa na watu hawa wa Sodoma, kuwadhuru watumishi wa Mungu kulikuwa mfano tu wa tone baharini ya kile walichokuwa wakifanya, na asili yao ya uovu uliofichuliwa kwa kweli ulionekana tu kuwa mdogo zaidi kuliko hata tone moja ndani ya bahari kubwa. Kwa hivyo, Mungu alichagua kuwaangamiza kwa moto. Mungu hakutumia gharika, wala Hakutumia zilizala, mtetemeko wa ardhi, sunami au mbinu yoyote nyingine ya kuuangamiza mji huu. Kule kutumia moto na Mungu kuangamiza mji huu kulimaanisha nini? Kulimaanisha uangamizaji kamili wa mji huo; kulimaanisha kwamba mji huu ulitoweka kabisa kutoka ulimwenguni na kutoka katika kuwepo kwake. Hapa, “kuangamiza” hakurejelei tu kule kutoweka kwa umbo na muundo au sura ya nje ya mji huo; kunamaanisha pia kwamba nafsi za watu ndani ya mji huo zilisita kuwepo, baada ya kufutwa kabisa. Kwa ufupi, watu wote, matukio na mambo yote yaliyohusiana na mji huu yaliangamizwa. Kusingekuwa na maisha baada ya kifo au roho kuwa mwilini mwao; Mungu alikuwa amewafuta kabisa kutoka katika binadamu, uumbaji Wake, mara moja na tena milele. Yale “matumizi ya moto” yalimaanisha kusitisha dhambi, na yalimaanisha mwisho wa dhambi; dhambi hii ingesita kuwepo na kuenea. Yalimaanisha kwamba uovu wa Shetani ulikuwa umepoteza mahali pake pa kunawiri pamoja na eneo la kaburi ambalo liliupatia mji huo mahali pa kukaa na kuishi. Kwenye vita kati ya Mungu na Shetani, matumizi ya moto na Mungu ni alama ya ushindi Wake ambayo Shetani anatajiwa. Kuangamizwa kwa Sodoma ni hatua kubwa ya kuzuia maono ya Shetani ya kupinga Mungu kwa kupotosha na kudanganya binadamu, na vilevile ni ishara ya kudhalilishwa kwa muda kwenye maendeleo ya binadamu ambapo binadamu alikataa mwongozo wa Mungu na akajiachilia kutenda maovu. Aidha, ni rekodi ya ufunuo wa kweli wa tabia ya haki ya Mungu.

Wakati ule moto ambao Mungu alituma kutoka mbinguni ulikuwa umeteketeza kabisa Sodoma hata zaidi ya majivu, ilimaanisha kwamba mji huu ulioitwa “Sodoma” ungesita kuwepo, na vilevile kila kitu ndani ya mji wenyewe. Uliangamizwa kwa ghadhabu ya Mungu; ulitoweka kutokana na hasira na adhama ya Mungu. Kwa sababu ya tabia ya haki ya Mungu Sodoma ilipokea adhabu yake ya haki; kutokana na tabia ya haki ya Mungu, ilipokea mwisho wake wa haki. Mwisho wa kuwepo kwa Sodoma ulitokana na maovu yake, na ulitokana pia na tamanio la Mungu kutowahi kuutazamia mji huu tena, pamoja na watu wote walioishi ndani ya mji huo au maisha yoyote yaliyowahi kukua ndani ya mji huo. “Tamanio la kutowahi kuutazamia mji huo tena” la Mungu ni hasira Yake, pamoja na adhama Yake. Mungu aliuteketeza mji kwa sababu maovu na dhambi zake vilimsababisha Yeye kuhisi ghadhabu, maudhi na chuki katika mji huu na tamanio lake la kutowahi kuuona au watu wowote wa mji huo na viumbe vyote vilivyo hai vilivyokuwa ndani ya mji huo tena. Baada ya mji huo kuacha kuchomeka, huku ukiwa umeacha nyuma jivu pekee, ulikuwa kwa kweli umesita kuwepo mbele ya macho ya Mungu; hata kumbukumbu za Mungu kuuhusu ziliondolewa, zilifutwa. Hii inamaanisha kwamba moto ulioangushwa kutoka mbinguni haukuangamiza tu mji wote wa Sodoma kwa jumla na watu waliokuwa wamejaa dhambi ndani yake, wala kuangamiza tu vitu vyote vilivyokuwa ndani ya mji uliokuwa umepatwa na dosari ya dhambi; hata zaidi, moto huu uliangamiza kumbukumbu za maovu na ukinzani wa binadamu dhidi ya Mungu. Hili ndilo lilikuwa kusudio la Mungu kwa kuuchoma ule mji.

Binadamu ulikuwa umepotoka kupindukia. Watu hawa hawakujua Mungu alikuwa nani au kule walikokuwa wametokea. Kama ungemtaja Mungu, watu hawa wangekushambulia, kukutukana na kukufuru. Hata wakati watumishi wa Mungu walikuwa wamekuja kueneza onyo Lake, watu hawa waliopotoka hawakuweza kuonyesha ishara zozote za toba; vilevile hawakuacha mwenendo wao wa maovu. Kinyume cha mambo ni kwamba, waliweza bila ya haya, kuwadhuru watumishi wa Mungu. Kile walichoonyesha na kufichua kilikuwa asili na hali yao halisi ya uadui mkubwa kwa Mungu. Tunaweza kuona kwamba ukinzani wa watu hawa waliopotoka dhidi ya Mungu ulikuwa zaidi ya ufunuo wa tabia yao potovu, kama vile tu ilivyokuwa zaidi ya tukio la matusi au kejeli iliyotokana na ukosefu wa ufahamu wa ukweli. Ujinga wala kutojua havikusababisha mwenendo huu wa maovu; haikuwa kwa sababu watu hawa walikuwa wamedanganywa, na bila shaka si kwa sababu walikuwa wamepotoshwa. Mwenendo wao ulikuwa umefikia kiwango cha uhasama wa wazi wa kupinga na kuasi dhidi ya Mungu. Bila shaka, aina hii ya tabia ya binadamu ingempa hasira kali Mungu, na ingeongeza hasira kali kwenye tabia Yake—tabia ambayo haifai kukosewa. Kwa hivyo, Mungu aliachilia kwa njia ya moja kwa moja na kwa uwazi hasira Yake na adhama Yake; huu ni ufunuo wa kweli wa tabia Yake ya haki. Akiwa amekabiliwa na mji uliotiririka na dhambi, Mungu alitamani kuuangamiza kwa njia ya haraka zaidi iliyowezekana; Alipenda kuwaondoa watu waliokuwa ndani yake na uzima wa dhambi zao kwa njia kamilifu zaidi, kuwafanya watu hawa wa mji kusita kuwepo na kukomesha dhambi ndani ya mahali hapa kuongezeka. Njia ya haraka zaidi na kamilifu zaidi ya kufanya hivyo ilikuwa ni kuuteketeza kwa moto. Mtazamo wa Mungu kwa watu wa Sodoma haukuwa ule wa kuwaacha au kutowajali; bali, Alitumia hasira Yake, adhama na mamlaka kuwaadhibu, kuwaweka chini na kuwaangamiza kabisa watu hawa. Mtazamo wake kwao haukuwa tu ule wa kuwaangamiza kimwili bali pia kuwaangamiza kinafsi, ukomeshaji wa milele. Hii ndiyo athari ya kweli ya tamanio la Mungu kwao “kuweza kusita kuwepo.”

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp