Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II

Tabia ya Haki ya Mungu (Sehemu ya Pili)

Ingawaje Hasira ya Mungu ni Fiche na Haijulikani kwa Binadamu, Haivumilii Kosa Lolote

Namna Mungu alivyoshughulikia binadamu wote wa ujinga na kutojua ulitokana kimsingi na huruma na uvumilivu. Hasira yake, kwa upande mwingine, imefichwa kwenye wingi mkubwa mno wa muda na wa mambo; haijulikani kwa binadamu. Kutokana na hayo, ni vigumu sana kwa binadamu kumwona Mungu akionyesha hasira Yake, na ni vigumu pia kuelewa hasira Yake. Kwa hivyo, binadamu huchukulia hasira ya Mungu kuwa ndogo. Wakati binadamu anakabiliwa na kazi ya mwisho ya Mungu na hatua ya kuvumilia na kusamehe binadamu—yaani, wakati onyesho la mwisho la Mungu la huruma na onyo Lake la mwisho linapowafikia—kama bado wangali wanatumia mbinu zile kumpinga Mungu na hawafanyi jitihada zozote za kutubu, kurekebisha njia zao au kukubali huruma Yake, Mungu hataweza tena kuwapatia uvumilivu na subira yake. Kinyume cha mambo ni kwamba, ni katika wakati huu ambapo Mungu atafuta huruma Yake. Kufuatia hili, Atatuma tu hasira Yake. Anaweza kuonyesha hasira Yake kwa njia tofauti, kama vile tu Anavyoweza kutumia mbinu tofauti kuwaadhibu na kuwaangamiza watu.

Matumizi ya Mungu ya moto kuuangamiza mji wa Sodoma ndio mbinu Yake ya haraka zaidi ya kuondoa kabisa binadamu au kitu. Kuwachoma watu wa Sodoma kuliangamiza zaidi ya miili yao ya kimwili; kuliangamiza uzima wa roho zao, nafsi zao na miili yao, na kuhakikisha kwamba watu waliokuwa ndani ya mji wangesita kuwepo kwenye ulimwengu wa anasa na hata ulimwengu usioonekana na mwanadamu. Hii ni njia moja ambayo Mungu hufichua na kuonyesha hasira Yake. Mfano huu wa ufunuo na maonyesho ni dhana moja ya hali halisi ya hasira ya Mungu, kama vile ilivyo kwa kawaida pia ufunuo wa hali halisi ya tabia ya haki ya Mungu. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, Yeye husita kufichua huruma au upole wa upendo wowote, na wala haonyeshi tena uvumilivu au subira Yake; hakuna mtu, kitu au sababu inayoweza kumshawishi kuendelea kuwa na subira, kutoa huruma Yake tena, na kumpa binadamu uvumilivu wake kwa mara nyingine. Badala ya mambo haya, bila kusita hata kwa muda mfupi, Mungu atashusha hasira Yake na adhama, kufanya kile Anachotamani, na Atafanya mambo haya kwa haraka na kwa njia safi kulingana na matamanio Yake binafsi. Hii ndiyo njia ambayo Mungu hushusha hasira Yake na adhama, ambayo binadamu hafai kukosea, na pia ni maonyesho ya dhana moja ya tabia Yake ya haki. Wakati watu wanashuhudia Mungu akionyesha wasiwasi na upendo kwa binadamu, hawawezi kugundua hasira Yake, kuiona adhama Yake au kuhisi kutovumilia Kwake kwa kosa. Mambo haya siku zote yamewaongoza watu kusadiki kwamba tabia ya haki ya Mungu ni ile ya huruma, uvumilivu na upendo tu. Hata hivyo, wakati mtu anapoona Mungu akiuangamiza mji au akichukia binadamu, hasira Yake katika kuangamiza binadamu na adhama Yake huruhusu watu kuona picha ya upande ule mwingine wa tabia Yake ya haki. Huyu ni Mungu asiyevumilia kosa. Tabia ya Mungu isiyovumilia kosa inazidi yale mawazo ya kiumbe chochote kilichoumbwa, na miongoni mwa viumbe ambavyo havikuumbwa, hakuna kati ya hivyo kinachoweza kuhitilafiana na kingine au kuathiri kingine; lakini hata zaidi, hakiwezi kughushiwa au kuigwa. Kwa hivyo, dhana hii ya tabia ya Mungu ndiyo ambayo binadamu anafaa kujua zaidi. Mungu Mwenyewe Pekee ndiye aliye na aina hii ya tabia, na Mungu Mwenyewe pekee ndiye anayemiliki aina hii ya tabia. Mungu anamiliki aina hii ya tabia kwa sababu Anachukia maovu, giza, maasi na vitendo vya uovu vya Shetani—vya kutosha na kudanganya wanadamu—kwa sababu Anachukia vitendo vyote vya dhambi vinavyompinga Yeye na kwa sababu ya hali Yake halisi takatifu na isiyo na doa. Ni kwa sababu ya haya ndiposa Hataacha viumbe vyovyote kati ya vile vilivyoumba au ambavyo havikuumbwa vimpinge waziwazi au kushindana na Yeye. Hata mtu binafsi ambaye Aliwahi kumwonyesha huruma au kuchagua anahitaji tu kuchochea tabia Yake na kukiuka kanuni Yake ya subira na uvumilivu, na Ataachilia na kufichua tabia Yake ya haki bila ya huruma hata kidogo au kusitasita kokote—tabia isiyovumilia kosa lolote.

Hasira ya Mungu Ni Usalama wa Nguvu Zote za Haki na Mambo Yote Mazuri

Kwa kuielewa mifano hii ya hotuba, fikira na vitendo vya Mungu, je, unaweza kuielewa tabia ya haki ya Mungu, tabia isiyoweza kukosewa? Mwishowe, hii ni dhana ya tabia ya kipekee kwa Mungu Mwenyewe, bila ya kujali ni kiwango kipi ambacho binadamu anaweza kuelewa. Kutoweza kuvumilia kosa kwa Mungu ndicho kiini Chake cha kipekee; hasira ya Mungu ndiyo tabia Yake ya kipekee; adhama ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya kipekee. Kanuni inayoelezea ghadhabu ya Mungu inaonyesha utambulisho na hadhi ambayo Yeye tu ndiye anayemiliki. Mtu hana haja kutaja kwamba ni ishara pia ya hali halisi ya Mungu Mwenyewe wa kipekee. Tabia ya Mungu ndiyo hali Yake halisi ya asili. Haibadiliki kamwe na kupita kwa muda, wala haibadiliki kila wakati mahali panapobadilika. Tabia Yake ya asili ndiyo kiini Chake halisi cha kweli. Haijalishi ni nani anayetekelezea kazi Yake, hali Yake halisi haibadiliki, na wala tabia ya haki Yake pia. Wakati mtu anapomghadhibisha Mungu, kile Anachomshushia ni tabia Yake ya asili; wakati huu kanuni inayoelezea ghadhabu Yake haibadiliki, wala utambulisho na hadhi Yake ya kipekee. Haghadhibishwi kwa sababu ya mabadiliko katika hali Yake halisi au kwa sababu ya tabia Yake kusababisha dalili tofauti, lakini kwa sababu upinzani wa binadamu dhidi Yake hukosea tabia Yake. Uchochezi waziwazi wa binadamu kwa Mungu ni changamoto kubwa katika utambulisho na hadhi binafsi ya Mungu. Kwa mtazamo wa Mungu, wakati binadamu anapompinga Yeye, binadamu huyo anashindana na Yeye na anampima ghadhabu Yake. Wakati binadamu anapompinga Mungu, wakati binadamu anaposhindana na Mungu, wakati binadamu anapojaribu kila mara ghadhabu ya Mungu—na ndio maana pia dhambi huongezeka—hasira ya Mungu itaweza kufichuka kwa kawaida na kujitokeza yenyewe. Kwa hivyo, maonyesho ya Mungu ya hasira Yake yanaashiria kwamba nguvu zote za maovu zitasita kuwepo; yanaashiria kwamba nguvu zote katili zitaangamizwa. Huu ndio upekee wa tabia ya haki ya Mungu, na ndio upekee wa hasira ya Mungu. Wakati heshima na utakatifu wa Mungu vinapopata changamoto, wakati nguvu za haki zinapata kuzuiliwa na kutoonekana na binadamu, Mungu atashusha hasira Yake. Kwa sababu ya hali halisi ya Mungu, nguvu hizo zote ulimwenguni zinazoshindana na Mungu, zinazompinga Yeye na kushindana na Yeye ni za maovu, kupotoka na kutokuwa na dhalimu; zinatoka Kwake na zinamilikiwa na Shetani. Kwa sababu Mungu ni wa haki, wa nuru na mtakatifu bila dosari, vitu vyote viovu, vilivyopotoka na vinavyomilikiwa na Shetani vitatoweka baada ya kuachiliwa kwa hasira ya Mungu.

Ingawaje kumwagwa kwa hasira ya Mungu ni dhana ya maonyesho ya tabia ya haki Yake, hasira ya Mungu kwa vyovyote vile haibagui walengwa wake au haina kanuni. Kinyume cha mambo ni kwamba, Mungu si mwepesi wa ghadhabu, wala Hakimbilii kufichua hasira Yake na adhama Yake. Aidha, hasira ya Mungu inadhibitiwa na kupimwa kwa kiwango fulani; hailinganishwi kamwe na namna ambavyo binadamu atakavyowaka kwa hasira kali au kutoa ghadhabu zake. Mazungumzo mengi kati ya binadamu na Mungu yamerekodiwa kwenye Biblia. Maneno ya baadhi ya watu hawa binafsi yalikuwa ya juujuu, yasiyo na ujuzi na yasiyofaa, lakini Mungu hakuwaangusha chini, wala Hakuwashutumu. Hususan, wakati wa majaribio ya Ayubu, je, Yehova Mungu aliwachukuliaje marafiki watatu wa Ayubu na wale wengine baada ya kusikia maneno waliyomzungumzia Ayubu? Je, Aliwashutumu? Je, Aligeuka na kushikwa na hasira kali kwao? Hakufanya kitu kama hicho! Badala yake Alimwambia Ayubu kuwasihi, kuwaombea; Mungu, kwa mkono mwingine, hakuchukua lawama zao na kutia moyoni. Matukio haya yote yanawakilisha mtazamo mkuu ambao Mungu anashughulikia binadamu waliopotoka, na wasiojua. Kwa hivyo, kushushwa kwa hasira ya Mungu si kwa vyovyote vile maonyesho au hali ya kutoa nje hali Yake ya moyo. Hasira ya Mungu si mlipuko mkubwa wa hasira kali kama vile binadamu anavyoielewa. Mungu hawachilii hasira Yake kwa sababu hawezi kuidhibiti hali ya moyo Wake binafsi au kwa sababu ghadhabu Yake imefikia kilele na lazima itolewe. Kinyume cha mambo ni kwamba, hasira Yake ni maonyesho ya tabia ya haki Yake na maonyesho halisi ya tabia ya haki Yake; ni ufunuo wa ishara ya hali Yake halisi takatifu. Mungu ni hasira, asiyevumilia kosa—hivi si kusema kwamba ghadhabu ya Mungu haitofautishi sababu za kufanya hivyo au haifuati kanuni; ni binadamu waliopotoka ambao unafuata mkondo wa kipekee wa kutokuwa na kanuni, mlipuko wa hasira kali bila mpango usiotofautisha hali hii miongoni mwa sababu mbalimbali. Mara tu binadamu anapokuwa na hadhi, mara nyingi atapata ugumu wa kudhibiti hali ya moyo wake, na kwa hivyo atafurahia kutumia nafasi mbalimbali kueleza kutotosheka kwake na kutoa nje hisia zake; mara nyingi atawaka kwa hasira kali bila sababu yoyote, ili kuonyesha uwezo wake na kuwafanya wengine kujua kwamba hadhi yake na utambulisho wake ni tofauti na ule wa watu wa kawaida. Bila shaka, watu waliopotoka wasiokuwa na hadhi yoyote mara kwa mara pia watapoteza udhibiti wao. Ghadhabu yao mara nyingi husababishwa na uharibifu wa manufaa yao ya kibinafsi. Ili kulinda hadhi yake binafsi na heshima, mwanadamu aliyepotoka mara kwa mara atatoa nje hisia zake na kufichua asili yake yenye kiburi. Binadamu atalipuka kwa ghadhabu na kutoa nje hisia zake ili kutetea uwepo wa dhambi, na matendo haya ndiyo njia ambayo binadamu anaonyesha kutotosheka kwake. Matendo haya yamejaa hadi pomoni kwa kuchafuliwa; yamejaa kwa mifumo na mbinu mbalimbali; yamejaa kupotoka na maovu ya binadamu; zaidi ya hayo, yanajaa kwa malengo na matamanio ya binadamu. Wakati haki inaposhindana na maovu, binadamu hataruka juu kwa ghadhabu ili kutetea uwepo wa haki; kinyume ni kwamba, wakati nguvu za haki zinatishwa, zinateswa na kushambuliwa, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutotilia maanani, kukwepa, au kushtuka. Hata hivyo, wakati anapokabiliwa na nguvu za maovu, mtazamo wa binadamu ni ule wa kutunza, na kunyenyekea mno. Hivyo basi, kutoa nje ghadhabu kwa binadamu ni kimbilio la nguvu za maovu, maonyesho ya mwenendo wa maovu uliokithiri na usiositishwa wa binadamu wa kimwili. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake, hata hivyo, nguvu zote za maovu zitasitishwa; dhambi zote za kudhuru binadamu zitasitishwa; nguvu zote katili zinazozuia kazi ya Mungu zitawekwa wazi, zitatenganishwa na kulaaniwa; washirika wote wa Shetani ambao wanampinga Mungu wataadhibiwa, na kuondolewa. Badala yake, kazi ya Mungu itaendelea huru bila vizuizi vyovyote; mpango wa usimamizi wa Mungu utaendelea kuimarika hatua kwa hatua kulingana na utaratibu uliopo; watu walioteuliwa na Mungu watakuwa huru dhidi ya kusumbuliwa na Shetani na kudanganywa; wale wanaomfuata Mungu watafurahia uongozi na ujazo wa Mungu miongoni mwa mazingira yenye utulivu na amani. Hasira ya Mungu ni usalama unaozuia nguvu zote za maovu dhidi ya kuzidishwa na kutapakaa kwa nguvu, na pia ni usalama unaolinda kuwepo na kuenea kwa mambo yote ya haki na mazuri na daima dawamu unayalinda mambo haya dhidi ya kukandamizwa na kuangamizwa.

Unaweza kuona hali halisi ya hasira ya Mungu katika kuangamiza Kwake kwa Sodoma? Je, kuna jambo lolote lililochanganyika kwenye hasira Yake kali? Je, hasira kali ya Mungu ni safi? Ili kutumia maneno ya binadamu, je, hasira kali ya Mungu imetiwa najisi? Je, kunayo hila yoyote katika hasira Yake? Je, kunayo njama yoyote? Je, zipo siri zozote zisizotamkika? Ninaweza kukwambia wazi na kwa makini: Hakuna sehemu ya hasira ya Mungu inayoweza kumwongoza mtu kwa shaka. Ghadhabu yake haina kasoro, ni hasira ambayo haijatiwa najisi na haijasheheni nia au shabaha zozote zingine. Sababu ya ghadhabu Yake ni safi, haina lawama na haipingiki. Ni ufunuo wa kawaida na onyesho la hali Yake halisi ya utakatifu; ni kitu ambacho hakuna kiumbe chochote kinamiliki. Hii ni sehemu ya tabia ya kipekee ya haki ya Mungu, na ni utofauti wa wazi kati ya hali halisi husika ya Muumba na uumbaji Wake.

Haijalishi kama mtu anakuwa na ghadhabu akiwa mbele ya wengine au wakiwa hawako naye, kila mtu anayo nia na kusudi tofauti. Pengine wanajenga heshima zao, au pengine wanatetea masilahi yao binafsi, na kuendeleza taswira yao au kulinda sura yao. Baadhi yao huendeleza hali ya kuzuia ghadhabu yao, huku nao wengine wanakimbilia na wanapandwa na hasira kali kila wanapopenda bila ya hata kiwango kidogo zaidi cha kujizuia. Kwa ufupi, ghadhabu ya binadamu inatokana na tabia yake iliyopotoka. Haijalishi kusudi lake, ni la mwili na ni la asili; halina uhusiano wowote na haki au ukiukaji wa haki kwa sababu hakuna kitu katika asili ya binadamu na hali halisi vinavyolingana na ukweli. Kwa hivyo, hasira ya binadamu wapotovu na hasira ya Mungu vyote havifai kutajwa kwa kiwango sawa. Bila ubaguzi, tabia ya mwanadamu aliyepotoshwa na Shetani huanza na tamanio la kulinda upotovu, na ina msingi katika upotovu; hivyo basi, hasira ya mwanadamu haiwezi kutajwa kwa kiwango sawa na ghadhabu ya Mungu, haijalishi ni bora namna gani kinadharia. Wakati Mungu anaposhusha hasira Yake kali, nguvu za giza zinakaguliwa, mambo ya giza yanaangamizwa, huku mambo ya haki na mazuri yakifurahia utunzaji wa Mungu, ulinzi, na yote yanaruhusiwa kuendelea. Mungu hushusha hasira Yake kwa sababu ya mambo dhalimu, mabaya na ya giza, yanayozuia, yanayotatiza au kuangamiza shughuli na maendeleo ya kawaida ya mambo ya haki na mazuri. Shabaha ya ghadhabu ya Mungu si kusalimisha hadhi na utambulisho Wake binafsi, lakini kusalimisha uwepo wa mambo ya haki, mazuri, ya kupendeza na kuvutia, kusalimisha sheria na mpangilio wa kuwepo kwa kawaida kwa binadamu. Hiki ndicho chanzo asilia cha hasira ya Mungu. Hasira kali ya Mungu ni bora sana, ya kiasili na ufunuo wa kweli wa tabia Yake. Hakuna makusudi yoyote katika hasira Yake kali, wala hakuna udanganyifu au njama yoyote; au hata zaidi, hasira Yake kali haina tamanio lolote, ujanja, mambo ya kijicho, udhalimu, maovu, au kitu kingine ambacho binadamu wote waliopotoka huwa navyo. Kabla ya Mungu kushusha hasira Yake kali, huwa tayari Ametambua hali halisi ya kila suala kwa uwazi na ukamilifu zaidi, na huwa tayari Amepangilia ufafanuzi na hitimisho sahihi na zilizo wazi. Hivyo basi, lengo la Mungu katika kila suala Analofanya ni wazi kabisa, vile ulivyo mtazamo Wake. Yeye si mtu aliyechanganyikiwa; Yeye si kipofu; Yeye si mtu wa kuamua ghafla; Yeye si mzembe; na zaidi, Yeye si mtu asiyefuata kanuni. Hii ndiyo dhana ya kimatendo ya hasira ya Mungu, na ni kwa sababu ya dhana hii ya kimatendo ya hasira ya Mungu kwamba binadamu wamefikia uwepo wao wa kawaida. Bila ya hasira ya Mungu, binadamu wangeishia kuishi katika mazingira yasiyo ya kawaida; viumbe vyote vyenye haki, virembo na vizuri vingeangamizwa na kusita kuwepo. Bila ya hasira ya Mungu, sheria na mpangilio unaotawala uumbaji vingekiukwa au hata kupinduliwa kabisa. Tangu uumbwaji wa binadamu, Mungu ametumia bila kusita, tabia Yake ya haki kusalimisha na kuendeleza uwepo wa kawaida wa binadamu. Kwa sababu tabia Yake ya haki inayo hasira na adhama, watu wote waovu, vitu, vifaa na vitu vyote vinavyotatiza na kuharibu uwepo wa kawaida wa binadamu vinaadhibiwa, vinadhibitiwa na kuangamizwa kwa sababu ya hasira Yake. Kwenye milenia mbalimbali zilizopita, Mungu ameendelea kutumia tabia Yake ya haki kuangusha na kuangamiza kila aina za roho chafu na za giza ambazo zinampinga Mungu na kuchukua nafasi ya wasaidizi wa Shetani na kusaidia katika kazi Yake ya kuwasimamia binadamu. Hivyo basi, kazi ya Mungu ya wokovu wa binadamu siku zote imeimarika kulingana na mpango Wake. Hivi ni kusema kwamba kwa sababu ya uwepo wa hasira ya Mungu, sababu ya haki zaidi miongoni mwa binadamu haijawahi kuangamizwa.

Sasa kwa vile unao ufahamu wa hali halisi ya hasira ya Mungu, bila shaka lazima utakuwa na ufahamu bora zaidi wa namna ya kutofautisha maovu ya Shetani!

Ingawa Shetani Anaonekana Mwenye Utu, Haki na Maadili, Ni Mkatili na Mwovu katika Kiini Chake

Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ushenzi wake; tamanio lake la kudhuru na kudanganya watu ndipo litazidi zaidi. Hii ni kwa sababu anapandwa na hasira kali kwa kuzindukana kwa binadamu; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka wa jela yake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kishenzi.

Katika kila suala, tabia ya Shetani hufichua asili yake maovu. Kati ya vitendo vyote vya maovu ambavyo Shetani ametekeleza kwa binadamu—tangu jitihada zake za mapema za kudanganya binadamu ili aweze kumfuata, hadi unyonyaji wake wa binadamu, ambapo anamkokota binadamu hadi kwenye matendo maovu, na ulipizaji wa kisasi wa Shetani kwa binadamu baada ya sifa zake za kweli kuweza kufichuliwa na binadamu kuweza kutambua na kumwacha—hakuna hata kimoja kati ya vitendo hivi kinachoshindwa kufichua hali halisi ya uovu wa Shetani; hakuna hata moja inayoshindwa kuthibitisha hoja kwamba Shetani hana uhusiano na mambo mazuri; hakuna hata moja hushindwa kuthibitisha kwamba Shetani ndiye chanzo cha mambo yote maovu. Kila mojawapo ya matendo yake inasalimisha maovu yake, inadumisha maendelezo ya vitendo vyake vya maovu, inaenda kinyume cha haki na mambo mazuri, inaharibu sheria na mpangilio wa uwepo wa kawaida wa binadamu. Wao ni katili kwa Mungu, na ndio wale ambao hasira ya Mungu itaangamiza. Ingawaje Shetani anayo hasira yake kali, hasira yake kali ni mbinu ya kutoa nje asili yake mbovu. Sababu inayomfanya Shetani kukereka na kuwa mkali ni: Kwa sababu njama zake zisizotamkika zimefichuliwa; mipango yake haikwepeki kwa urahisi; malengo yake yasiyo na mipaka na tamanio la kubadilisha Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa. Kuitisha kwa Mungu hasira Yake mara kwa mara ndiko kumesitisha mipango ya Shetani dhidi ya kukamilika na kukatiza kuenea na kusambaa kwa maovu ya Shetani; kwa hivyo, Shetani anaogopa na kuchukia hasira ya Mungu. Kila matumizi ya hasira ya Mungu huwa yanafichua sura halisi ya aibu ya Shetani; na pia kufichua na kuweka kwenye nuru matamanio ya maovu ya Shetani. Wakati uo huo, sababu za hasira kali ya Shetani dhidi ya binadamu zinafichuliwa kabisa. Kule kulipuka kwa hasira kali ya Shetani ni ufunuo wa kweli wa asili yake mbovu, ufichuzi wa njama zake. Bila shaka, kila wakati Shetani anapopandwa na hasira kali, huwa ni dalili ya maangamizo ya mambo maovu; huwa ni ishara ya ulinzi na maendelezo ya mambo mazuri, na huwa ni ishara ya asili ya hasira ya Mungu—ile ambayo haiwezi kukosewa!

Mtu Hafai Kutegemea Uzoefu na Fikira Ili Kujua Tabia ya Haki ya Mungu

Ukijipata unakabiliwa na hukumu na kuadibiwa na Mungu, je, utasema kwamba neno la Mungu limetiwa najisi? Je, utasema kwamba kunayo hadithi inayoelezea hasira kali ya Mungu, na kwamba hasira Yake kali imetiwa najisi? Je, utamchafulia Mungu jina, ukisema kwamba tabia Yake si ya haki kwa ujumla? Wakati unaposhughulikia kila mojawapo ya vitendo vya Mungu, lazima uwe na hakika kwamba tabia ya haki ya Mungu iko huru dhidi ya vipengele vingine vyovyote, kwamba ni takatifu na haina dosari; vitendo hivi vinajumuisha binadamu kuweza kuangushwa chini, kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu. Bila kuacha, kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu kinatekelezwa kulingana na tabia yake ya asili na mpango Wake—hii haijumuishi maarifa ya binadamu, mila na falsafa—na kila kimojawapo cha vitendo vya Mungu ni maonyesho ya tabia Yake na hali halisi, isiyohusiana na chochote kinachomilikiwa na binadamu aliyepotoka. Katika dhana za binadamu, ni upendo, huruma na uvumilivu wa Mungu tu kwa binadamu ndivyo visivyokuwa na dosari, ambavyo havijatiwa najisi na vilivyo vitakatifu. Hata hivyo, hakuna anayejua kwamba ghadhabu ya Mungu na hasira Yake vilevile vyote havijatiwa najisi; aidha, hakuna yule aliyefikiria maswali kama vile: kwa nini Mungu havumilii kosa lolote au kwa nini ghadhabu Yake ni kubwa mno. Kinyume ni kwamba, baadhi ya watu hukosa kuelewa hasira ya Mungu na kudhania kuwa ni hasira kali ya binadamu waliopotoka: wanaelewa ghadhabu ya Mungu kuwa hasira kali ya binadamu waliopotoka; wao hata hudhania kimakosa kwamba hasira kali ya Mungu ni sawa tu na ufunuo wa kiasili wa tabia potovu ya binadamu. Wanasadiki kimakosa kwamba utoaji wa hasira ya Mungu ni sawa tu na ghadhabu ya binadamu waliopotoka, jambo linalotokana na kutoridhika; wanasadiki hata kwamba utoaji wa hasira ya Mungu ni maonyesho ya hali Yake ya moyo. Baada ya kikao hiki cha ushirika, Ninatumai kwamba kila mmoja wenu aliye hapa hatakuwa tena na dhana potovu, fikira au kukisia kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na Natumai baada ya kusikiliza maneno Yangu mnaweza kuwa na utambuzi wa kweli wa hasira ya tabia ya haki ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba mnaweza kuweka pembeni kuelewa kokote kwa awali kulikofikiriwa vinginevyo kuhusiana na hasira ya Mungu, kwamba mnaweza kubadilisha imani zenu binafsi zilizopotoka na mitazamo ya hali halisi ya hasira ya Mungu. Vilevile, Natumai kwamba mnaweza kuwa na ufafanuzi sahihi wa tabia ya Mungu katika mioyo yenu, kwamba hamtakuwa tena na mashaka yoyote kuhusiana na tabia ya haki ya Mungu, na kwamba hamtatumia kuwaza kokote kwa binadamu au kufikiria kuhusu tabia ya kweli ya Mungu. Tabia ya haki ya Mungu ni hali halisi ya kweli ya Mungu mwenyewe. Si kitu kilichotungwa au kuandikwa na binadamu. Tabia Yake ni tabia Yake ya haki na haina uhusiano au miunganisho yoyote na uumbaji wowote ule. Mungu Mwenyewe ni Mungu Mwenyewe. Hatawahi kuwa sehemu ya uumbaji, na hata kama Atakuwa mwanachama miongoni mwa viumbe vilivyoumbwa, tabia Yake ya asili na hali halisi Yake havitabadilika. Hivyo basi, kumjua Mungu si kujua kifaa; si kuchunguza kitu, wala si kuelewa mtu. Kama utatumia dhana yako au mbinu yako ya kujua kifaa au kuelewa mtu ili kumjua Mungu, basi hutawahi kuweza kutimiza maarifa ya Mungu. Kumjua Mungu hakutegemei uzoefu au kufikiria kwako, na hivyo basi hufai kulazimisha uzoefu wako au kufikiria kwako kwa Mungu. Haijalishi uzoefu au kufikiria kwako ni kwa kipekee namna gani, huko kote bado ni finyu; na hata zaidi, kufikiria kwako hakulingani na hoja, isitoshe hakulingani na ukweli, na pia hakulingani na tabia na hali halisi ya kweli ya Mungu. Hutawahi kufanikiwa kama utategemea kufikiria kwako ili kuelewa hali halisi ya Mungu. Njia ya pekee ni hivi: kukubali yote yanayotoka kwa Mungu, kisha kwa utaratibu uweze kuyapitia na kuyaelewa. Kutakuwa na siku ambayo Mungu atakupa nuru ili uweze kuelewa kwa kweli na kumjua Yeye kwa sababu ya ushirikiano wako na kwa sababu ya hamu yako ya kutaka ukweli. Na kwa haya, hebu na tuhitimishe sehemu hii ya mazungumzo yetu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp