Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III

Mamlaka ya Mungu (II) (Sehemu ya Sita)

Kifo: Awamu ya Sita

4. Njoo Chini ya Utawala wa Muumba na Ukabiliane na Kifo kwa Utulivu

Wakati ule ambao mtu anazaliwa, nafsi ya mtu iliyo pweke inaanza kupitia maisha hapa duniani, inapitia mamlaka ya Muumba ambayo Muumba ameipangilia. Ni wazi kwamba, kwa mtu husika, ile nafsi, hii ni fursa nzuri kabisa ya kupata maarifa kuhusu ukuu wa Muumba, kujua mamlaka Yake na kuyapitia binafsi. Watu wanaishi maisha yao kulingana na sheria za hatima zilizowekwa wazi kwao na Muumba, na kwa mtu yeyote mwenye akili razini aliye na dhamiri, kuelewa ukuu wa Muumba na kutambua mamlaka yake kwenye mkondo wa miongo yao mbalimbali hapa nchini si jambo gumu kufanya. Kwa hivyo inafaa kuwa rahisi sana kwa kila mtu kutambua, kupitia kwa yale ambayo yeye mwenyewe amepitia maishani kwa kipindi cha miongo mbalimbali, kwamba hatima zote za binadamu zimeamuliwa kabla, na kung’amua au kujumlisha ni nini maana ya kuishi. Wakati uo huo ambao mtu anakumbatia mafunzo haya ya maisha, mtu ataelewa kwa utaratibu ni wapi maisha yanatokea, kunga’mua hasa ni nini ambacho moyo unahitaji kwa kweli, nini kitaongoza mtu kwenye njia ya kweli ya maisha, kazi maalum na shabaha ya maisha ya binadamu inafaa kuwa nini; na mtu ataanza kutambua kwa utaratibu kwamba kama mtu hataabudu Muumba, kama mtu hataingia kwenye utawala Wake, basi mtu anakabiliana na kifo—wakati nafsi iko karibu kukabiliana na Muumba kwa mara nyingine—moyo wa mtu utajazwa hofu na ugumu usio na mipaka. Kama mtu amekuwepo ulimwenguni kwa miongo kadhaa ilhali hajajua ni wapi maisha ya binadamu hutoka, angali hajatambua ni kwenye viganja vya mikono ya nani hatima ya binadamu huwa, basi si ajabu hataweza kukabiliana na kifo kwa utulivu. Mtu aliyepata maarifa ya ukuu wa Muumba baada ya kupitia miongo kadhaa ya maisha, ni mtu aliye na shukrani sahihi ya maana na thamani ya maisha; mtu aliye na kina cha maarifa kuhusu kusudi la maisha, aliye na hali halisi aliyopitia na anaelewa ukuu wa Muumba; na hata zaidi, mtu anayeweza kunyenyekea mbele ya mamlaka ya Muumba. Mtu kama huyo anaelewa maana ya uumbaji wa Mungu wa mwanadamu, anaelewa kwamba binadamu anafaa kumwabudu Muumba, kwamba kila kitu anachomiliki binadamu kinatoka kwa Muumba na kitarudi kwake siku fulani isiyo mbali sana kwenye siku za usoni; mtu kama huyo anaelewa kwamba Muumba hupangilia kuzaliwa kwa binadamu na ana ukuu juu ya kifo cha binadamu, na kwamba maisha na kifo vyote vimeamuliwa kabla na mamlaka ya Muumba. Kwa hiyo, wakati mtu anapong’amua mambo haya, mtu ataanza kuweza kukabiliana na kifo kwa utulivu na kwa kawaida, kuweka pembeni mali yake yote ya dunia kwa utulivu, kukubali na kunyenyekea kwa furaha kwa yote yatakayofuata, na kukaribisha awamu ya mwisho ya maisha iliyopangiliwa na Muumba badala ya kutishika vivyo hivyo tu na kung’ang’ana dhidi ya kifo. Ikiwa mtu anayaona maisha kama fursa ya kupitia ukuu wa Muumba na kujua mamlaka yake, ikiwa mtu anayaona maisha yake kama fursa nadra ya kutekeleza wajibu wake akiwa binadamu aliyeumbwa na kutimiza kazi yake maalum, basi mtu atakuwa ana mtazamo sahihi wa maisha, ataishi maisha yaliyobarikiwa na yanayoongozwa na Muumba, atatembea kwenye nuru ya Muumba, atajua ukuu wa Muumba, atakuwa katika utawala Wake, atakuwa shahidi wa matendo Yake ya kimiujiza na mamlaka Yake. Ni wazi kwamba, mtu kama huyo atahitajika kupendwa na kukubaliwa na Muumba, na mtu kama huyo ndiye anaweza kushikilia mtazamo mtulivu mbele ya kifo, na anayeweza kukaribisha awamu hii ya mwisho kwa furaha. Bila shaka Ayubu alikuwa na mtazamo kama huu kwa kifo; alikuwa katika nafasi ya kukubali kwa furaha awamu ya mwisho ya maisha, na baada ya kuhitimisha safari yake ya maisha vizuri, baada ya kukamilisha kazi yake maalum alirudi upande wa Muumba.

5. Bidii na Faida za Ayubu katika Maisha Zamruhusu Kukabiliana na Kifo kwa Utulivu

Katika Maandiko imeandikwa kuhusu Ayubu: “Kwa hivyo Ayubu akafariki, akiwa mzee na aliyejawa na siku” (Ayubu 42:17). Hii inamaanisha kwamba wakati Ayubu alipoaga dunia, hakuwa na majuto na hakuhisi maumivu, lakini aliondoka kimaumbile ulimwenguni. Kama vile kila mmoja anavyojua, Ayubu alikuwa mwanamume aliyemcha Mungu na aliyeambaa maovu alipokuwa hai; Mungu alimpongeza kwa matendo yake ya haki, watu waliyakumbuka, na maisha yake, zaidi ya yeyote yule mwengine, yalikuwa na thamani na umuhimu. Ayubu alifurahia baraka za Mungu na aliitwa mtakatifu na Yeye hapa duniani, na aliweza pia kujaribiwa na Mungu na kujaribiwa na Shetani; alisimama kuwa shahidi wa Mungu na alistahili kuwa mtu mtakatifu. Kwenye miongo mbalimbali baada ya kujaribiwa na Mungu, aliishi maisha ambayo yalikuwa yenye thamani zaidi, yenye maana zaidi, yaliyokita mizizi, na yenye amani zaidi kuliko hata awali. Kutokana na matendo yake ya haki, Mungu alimjaribu; kwa sababu ya matendo yake ya haki, Mungu alionekana kwake na kuongea naye moja kwa moja. Kwa hiyo, kwenye miaka yake baada ya kujaribiwa, Ayubu alielewa na kushukuru thamani ya maisha kwa njia thabiti zaidi, aliweza kutimiza ufahamu wa kina zaidi wa ukuu wa Muumba, na akapata maarifa yenye hakika na usahihi zaidi kuhusu namna ambavyo Muumba anavyotoa na kuzichukua baraka zake. Biblia inarekodi kwamba Yehovah Mungu alimpa hata baraka nyingi zaidi Ayubu kuliko hapo awali, Akimweka Ayubu katika nafasi bora zaidi ya kujua ukuu wa Muumba na kujua kukabiliana na kifo akiwa mtulivu. Kwa hiyo, Ayubu alipozeeka na kukabiliana na kifo, bila shaka asingekuwa na wasiwasi na mali yake. Hakuwa na wasiwasi wowote, hakuwa na chochote cha kujutia, na bila shaka hakuogopa kifo; kwani aliishi maisha yake akitembea ile njia ya kumcha Mungu, kuepuka maovu, na hakuwa na sababu yoyote ya kuwa na wasiwasi kuhusu mwisho wake mwenyewe. Ni watu wangapi leo wanaweza kuchukua hatua kwa njia zote hizo ambazo Ayubu alitumia alipokabiliwa na kifo chake mwenyewe? Kwa nini hakuna mtu anayeweza kuendeleza mwelekeo wa mtazamo rahisi kama huu? Kunayo sababu moja tu: Ayubu aliishi maisha kwenye harakati ya kutafuta kimsingi kusadiki, utambuzi, na unyenyekevu kwa ukuu wa Mungu, na ilikuwa katika kusadiki huku, utambuzi huu na unyenyekevu huu ambapo aliweza kupitia zile awamu muhimu za maisha, aliishi kwa kudhihirisha miaka yake ya mwisho na akajuliana hali na awamu yake ya mwisho ya maisha. Licha ya kile ambacho Ayubu alipitia, bidii zake na shabaha zake katika maisha zilikuwa za furaha na wala si zenye maumivu. Alikuwa na furaha si tu kwa sababu ya baraka au shukrani aliyopewa yeye na Muumba, lakini muhimu zaidi kwa sababu ya shughuli zake na shabaha za maisha, kwa sababu ya maarifa yaliyoongezeka kwa utaratibu na ufahamu wa kweli wa ukuu wa Muumba ambao alitimiza kupitia kwa kumcha Mungu na kwa kuepuka maovu, na zaidi, kwa sababu ya matendo Yake ya maajabu ambayo Ayubu alipitia kibinafsi wakati huu akiwa chini ya ukuu wa Muumba, na hali aliyopitia yenye uchangamfu na isiyosahaulika na kumbukumbu za kuwepo kwake, kuzoeana na wenzake, na kuzoeana kati yake yeye na Mungu; kwa sababu ya tulizo na furaha zilizotokana na kujua mapenzi ya Muumba; kwa sababu ya kustahi kulikotokea baada ya kuona kwamba Yeye ni mkubwa, ni wa ajabu, Anayependeka, na ni mwaminifu. Sababu ya Ayubu kuweza kukabiliana na kifo bila ya kuteseka ni kwamba alijua kwamba, kwa kufa, angerudi kwenye upande wa Muumba. Na zilikuwa shughuli zake katika maisha zilizomruhusu kukabiliana na kifo akiwa ametulia, kukabiliana na matarajio ya Muumba kuchukua tena maisha yake, kwa moyo mzuri, na zaidi ya yote, kusimama wima, kutotikisika na kuwa huru kutokana na mashaka mbele ya Muumba. Je, watu wanaweza siku hizi kutimiza aina ya furaha ambayo Ayubu alikuwa nayo? Je, nyinyi wenyewe mko katika hali ya kufanya hivyo? Kwa sababu watu siku hizi wako hivyo, kwa nini hawawezi kuishi kwa furaha, kama alivyofanya Ayubu? Kwa nini hawawezi kutoroka mateso yanayotokana na woga wa kifo? Wakati wanapokabiliwa na kifo, baadhi ya watu hujiendea haja ndogo; wengine hutetemeka, wakazirai, na wakalalamika dhidi ya Mbinguni na binadamu vilevile, wengine hata wakalia kwa huzuni na kutokwa machozi. Kwa vyovyote vile, hii ndiyo miitikio ya ghafla inayofanyika wakati kifo kinapokaribia. Watu huwa na tabia hii ya kuaibisha haswa kwa sababu, ndani ya mioyo yao, wanaogopa kifo, kwa sababu hawana maarifa yaliyo wazi na uwezo wa kushukuru ukuu wa Mungu na mipangilio yake, na isitoshe hata kujinyenyekeza mbele ya vitu hivi; kwa sababu watu hawataki chochote ila kupangilia na kutawala kila kitu wenyewe, kudhibiti hatima zao binafsi, maisha yao binafsi na hata kifo. Si ajabu, hivyo basi, kwamba watu hawajawahi kuweza kuacha woga wa kifo.

6. Ni kwa Kukubali tu Ukuu wa Muumba Ndipo Mtu Anaweza Kurejea Upande Wake

Wakati mtu hana maarifa yaliyo wazi na hajapitia ukuu wa Mungu na mipangilio Yake, maarifa ya mtu kuhusu hatima na yale ya kifo yatakuwa yale yasiyoeleweka. Watu hawawezi kuona waziwazi kwamba haya yote yamo kwenye kiganja cha mkono wa Mungu, hawatambui kwamba Mungu ameushika usukani na Anashikilia ukuu juu yao, hawatambui kwamba binadamu hawezi kutupa nje au kutoroka ukuu kama huo; na kwa hivyo wakati wanapokabiliwa na kifo hakuna mwisho wowote katika maneno yao ya mwisho, wasiwasi wao, na hata majuto. Wanalemewa sana na mambo mengi, wanajivuta ajabu, kunakuwa na mkanganyo mkubwa, na haya yote yanawafanya kuogopa kifo. Kwani mtu yeyote aliyezaliwa ulimwenguni humu, kuzaliwa kwake kunahitajika, na kuaga kwake hakuwezi kuepukika, na hakuna mtu anayeweza kuupiga chenga mkondo huu. Kama mtu atataka kuondoka ulimwenguni humu bila maumivu, kama mtu atataka kukabiliana na awamu ya mwisho ya maisha bila kusitasita au wasiwasi, njia pekee ni kutokuwa na majuto. Na njia pekee ya kuondoka bila majuto ni kujua ukuu wa Muumba, kujua mamlaka yake, na kunyenyekea mbele zake. Ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuwa mbali na mahangaiko ya binadamu, maovu, utumwa wa Shetani; ni kwa njia hii ndipo mtu anaweza kuishi maisha kama ya Ayubu, akiongozwa na akibarikiwa na Muumba, maisha yaliyo huru na yaliyokombolewa, maisha yenye thamani na maana, maisha yenye uaminifu na moyo wazi; ni kupitia kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kunyenyekea, kama Ayubu, kujaribiwa na kunyang’anywa na Muumba, kunyenyekeza katika mipango na mipangilio ya Muumba; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kumwabudu Muumba maisha yake yote na kuweza kupata pongezi Lake, kama Ayubu alivyopata, na kusikia sauti Yake, kumwona akionekana; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi na kufa kwa furaha, kama Ayubu, bila ya maumivu, bila wasiwasi, bila majuto; ni kwa njia hii tu ndipo mtu anaweza kuishi kwa nuru, kama Ayubu, kupita kila mojawapo ya awamu ya maisha kwa nuru, na kukamilisha vizuri safari yake kwa nuru, kutimiza kwa ufanisi kazi yake maalum—kupitia, kujifunza, na kujua ukuu wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa—na kuiaga dunia kwa nuru, na milele hadi milele kusimama upande wa Muumba kama kiumbe kilichoumbwa, kilichopongezwa na Yeye.

Usikose Fursa ya Kujua Ukuu wa Muumba

Awamu sita zilizofafanuliwa hapo juu ni awamu muhimu zilizowekwa wazi na Muumba ambazo kila mtu wa kawaida lazima apitie katika maisha yake. Kila mojawapo ya awamu hizi ni za kweli; hakuna mojawapo kati yazo ambayo inaweza kuepukwa, na zote zinasheheni uhusiano na kuamuliwa kabla kwa Muumba na ukuu Wake. Hivyo basi kwa binadamu, kila mojawapo ya awamu hizi ni sehemu muhimu ya kujikagua, na namna ya kupitia kila mojawapo vizuri ni suala muhimu sana ambalo nyinyi nyote mnakabiliwa nalo.

Mkusanyiko wa miongo ambayo inaunda maisha ya binadamu si mirefu sana wala mifupi sana. Miaka ishirini na kitu iliyopo katikati ya kuzaliwa na kukomaa hupita kwa muda mfupi tu wa kupepesa jicho, na ingawaje wakati huu katika maisha mtu anachukuliwa kuwa mtu mzima, watu katika kundi hili la umri wanajua machache sana kuhusu maisha ya binadamu na hatima ya binadamu. Wanapozidi kupata uzoefu zaidi, ndipo wanapopiga hatua kwa utaratibu hadi kwenye umri wa miaka ya kati. Watu katika miaka yao ya thelathini na arubaini huanza kuupata uzoefu unaoanza kuota wa maisha na hatima yake, lakini fikira zao kuhusu mambo haya zingali na ukungu mwingi sana akilini mwao. Si mpaka umri wa arubaini ndipo baadhi ya watu huanza kumwelewa binadamu na ulimwengu, vilivyoumbwa na Mungu, na kung’amua kwamba maisha ya binadamu yanahusu tu, kile ambacho hatima ya binadamu inahusu. Baadhi ya watu, ingawaje wamekuwa wafuasi wa muda mrefu wa Mungu na sasa wanao umri wa kati, bado hawamiliki maarifa na ufafanuzi sahihi wa ukuu wa Mungu, sikwambii hata unyenyekevu wa kweli. Baadhi ya watu hawajali chochote isipokuwa namna ya kupokea baraka, na ingawaje wameishi kwa miaka mingi, hawajui au hawaelewi hata kidogo hoja ya ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu, na kwa hivyo bado hawajaingia hata kwenye kipindi cha matendo halisi cha kunyenyekea katika mipango na mipangilio ya Mungu. Watu kama hao ni wajinga kabisa; watu kama hao wanaishi maisha yao bure bilashi.

Kama maisha ya binadamu yangegawanywa kulingana na kiwango cha mtu cha kile alichopitia maishani na maarifa yake kuhusu hatima ya binadamu, basi yangegawanywa kwa sura tatu. Sura ya kwanza ni ujana, miaka ile ya kati ya kuzaliwa na umri wa kati, au kuanzia kuzaliwa hadi kugonga miaka thelathini. Sura ya pili ni ya ukomavu, kuanzia umri wa miaka ya kati hadi umri wa uzee, au kuanzia thelathini hadi sitini. Na sura ya tatu ni kile kipindi cha uzee wa mtu, kuanzia umri wa uzee, kuanzia miaka sitini hivi, mpaka pale mtu anapoondoka ulimwenguni. Kwa maneno mengine, kuanzia kuzaliwa hadi umri wa miaka ya kati, maarifa ya watu wengi kuhusu hatima na maisha ni finyu na ni yale ya kuiga tu kama kasuku, fikira za wengine yanayokosa hali halisi iliyo ya kweli na ya matendo. Kwenye kipindi hiki, mtazamo wa mtu kuhusu maisha, na namna ambavyo mtu anapojipanga katika ulimwengu vyote ni vya juujuu na vinyonge sana. Hiki ndicho kipindi cha mtu cha utoto. Baada tu ya mtu kuonja furaha na huzuni zote za maisha ndipo anapofaidi na kupata ufahamu halisi wa hatima, ndipo mtu—kwa kufichika akilini, na ndani kabisa ya moyo wake—huanza kwa utaratibu kushukuru kutoweza kurudishwa nyuma kwa hatima, na kuanza kutambua polepole kwamba ukuu wa Muumba juu ya hatima ya binadamu kwa kweli upo. Kwa kweli hiki ndicho kipindi cha kuanza kukomaa kwa mtu. Baada ya mtu kusita kupambana dhidi ya hatima, na pale ambapo mtu hayuko radhi tena kuvutwa kwenye mabishano, lakini anajua msimamo wake, anajinyenyekeza kwa mapenzi ya Mbinguni, na kujumlisha mafanikio na makosa ya maisha ya mtu huyo, na anasubiria hukumu ya Muumba kwa maisha ya mtu—hiki ni kipindi cha ukomavu. Tukitilia maanani aina hizi tofauti za kile mtu amepitia na kufaidi ambako watu hupata kwenye vipindi hivi vitatu, katika hali za kawaida fursa ya mtu ya kujua ukuu wa Muumba si kubwa sana. Kama mtu ataishi kufikisha umri wa miaka sitini, mtu anayo miaka thelathini tu au karibu na hapo kuujua ukuu wa Mungu; kama mtu atataka kipindi kirefu zaidi cha muda, hilo linawezekana tu kama maisha ya mtu yatakuwa marefu zaidi, tuseme kama mtu ataweza kuishi karne moja. Kwa hivyo Ninasema, kulingana na kanuni za sheria za kawaida za uwepo wa binadamu, ingawaje ni mchakato mrefu sana kuanzia wakati ule mtu anakumbana na mada ya kujua ukuu wa Muumba hadi pale ambapo mtu anaweza kutambua hoja ya ukuu wa Muumba, na kutoka hapo mpaka pale ambapo mtu anaweza kujinyenyekeza kwa utawala huo, kama kwa hakika mtu atahesabu miaka hiyo, miaka hiyo haizidi thelathini au arubaini hivi ambapo mtu anayo fursa ya kufaidi haya yote. Na mara nyingi, watu hujisahau kutokana na matamanio yao na malengo yao ya kupokea baraka; hawawezi kutambua ni wapi ambapo kiini halisi cha maisha ya binadamu kipo, hawang’amui umuhimu wa kujua ukuu wa Muumba, na kwa hivyo hawafurahii fursa hii yenye thamani ya kuingia kwenye ulimwengu wa binadamu kuhusiana na maisha ya binadamu na kile alichopitia, kupitia ukuu wa Muumba, na hawatambui namna lilivyo jambo la thamani kwa kiumbe chochote kilichoumbwa kupokea mwongozo wa kibinafsi kutoka kwa Muumba. Kwa hivyo Ninasema, watu wale wanaotaka kazi ya Mungu kuisha haraka, wanaopenda Mungu angepangilia mwisho wa binadamu haraka iwezekanavyo, ili waweze mara moja kutazama hali Yake halisi na muda si muda kubarikiwa, wanayo hatia ya aina mbaya zaidi ya kutotii na ujinga wa kupindukia. Na kwa wale wanaotamani, kwenye muda wao finyu, kung’amua fursa hii ya kipekee ili kuujua ukuu wa Muumba, hao ni watu werevu, wenye akili zao. Matamanio haya mawili tofauti yanafichua mitazamo miwili tofauti na shughuli za kufuatilia: Wale wanaotafuta baraka ni wachoyo na waovu; hawatilii maanani mapenzi yoyote ya Mungu, wala hawatafuti kujua ukuu wa Mungu, wasiwahi kutamani kujinyenyekeza katika utawala huo, wanataka kuishi tu wanavyopenda. Wao ni watovu wa wema; wao ndio wanaofaa kuangamizwa. Wale wanaotafuta kumjua Mungu wanaweza kuweka pembeni matamanio yao, wako radhi kujinyenyekeza kwa ukuu wa Mungu na mipangilio ya Mungu; wanajaribu kuwa aina ya watu ambao wananyenyekea katika mamlaka ya Mungu na kutimiza tamanio la Mungu. Watu kama hao huishi kwa nuru, huishi katikati ya baraka za Mungu; kwa hakika wataweza kupongezwa na Mungu. Haijalishi ni nini, chaguo la binadamu halina manufaa, binadamu hawana kauli yoyote kuhusiana na muda gani ambao kazi ya Mungu itachukua. Ni bora zaidi kwa watu kujiweka katika udhibiti wa Mungu, kunyenyekea katika ukuu Wake. Usipojiweka katika huruma Yake, ni nini utakachofanya? Je, Mungu atakuwa na hasara yoyote? Usipojiweka katika huruma Yake, ukijaribu kuushika usukani, unafanya chaguo la kijinga, na wewe tu ndiwe utakayepata hasara hatimaye. Endapo tu watu watashirikiana na Mungu haraka iwezekanavyo, endapo tu watafanya hima kukubali mipango Yake, kujua mamlaka Yake, na kutambua yote ambayo Amewafanyia, ndipo watakuwa na tumaini, ndipo maisha yao yatapata maana na kuepuka kuwa hapo tu, ndipo watakapopata wokovu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp