Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV

Utakatifu wa Mungu (I) (Sehemu ya Pili)

Hebu sasa tuangalie maneno na maonyesho mengine ya Shetani yanayomruhusu mwanadamu kuona uso wake wenye sura mbaya. Hebu tuendelee kusoma baadhi ya maandiko.

Mazungumzo kati ya Shetani na Yehova Mungu

Ayubu 1:6-11 Sasa kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Basi Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Kisha Shetani akamjibu Yehova, na kusema, je, Ayubu anamcha Mungu bure? Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo? Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.

Ayubu 2:1-5 Tena kulikuweko na siku ambapo wana wa Mungu walikuja kujidhihirisha mbele za Yehova, naye Shetani akaja pia kati yao ili kujidhihirisha mbele za Yehova. Naye Yehova akasema kwa Shetani, Ni wapi umetoka? Na Shetani akamjibu Yehova, na kunena, Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo. Naye Yehova akasema kwa Shetani, je, umemfikiria mtumishi wangu Ayubu, kwamba hakuna hata mtu kama yeye duniani, mtu mtimilifu na mwaminifu, ambaye anamcha Mungu, na kuepuka maovu? Na bado anashikilia ukamilifu wake, ingawa ulinichochea dhidi yake, ili mimi nimwangamize bila sababu. Naye Shetani akamjibu Yehova, na akasema, Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.

Vifungu hivi viwili ni mazungumzo kati ya Mungu na Shetani, na vinarekodi kile alichosema Mungu na kile alichosema Shetani. Je, Mungu alisema mengi sana? (La.) Hakuzungumza sana, na Aliongea kwa urahisi sana. Tunaweza kuona utakatifu wa Mungu katika maneno rahisi ya Mungu? Wengine watasema “hii si rahisi. Hivyo tunaweza kuona ubaya wa shetani katika majibu yake?” (Ndiyo.) Kwanza wacha tuangalie ni aina gani ya swali ambalo Yehova Mungu alimwuliza Shetani. (“Ni wapi umetoka?”) Hili ni swali linaloeleweka kwa urahisi? (Ndiyo.) Kuna maana iliyofichwa? (La.) Ni swali tu, safi, bila madhumuni mengine. Kama Ningekuuliza: “Unatoka wapi wewe?” mngejibu vipi? Ni swali gumu kujibu? Mngesema: “Natoka katika kuzungukazunguka, na katika kutembea huku na huku”? (La.) Hamngejibu namna hii, kwa hivyo mnahisi aje mnapomwona Shetani akijibu kwa njia hii? (Tunahisi kwamba Shetani ni mpumbavu na mjanja.) Mnahisi hivi? Unaweza kusema ni nini Ninachohisi? Kila wakati Ninapoona maneno haya Nahisi kuchukizwa. Kwa sababu anazungumza bila kusema lolote! Alijibu swali la Mungu? (La.) Mbona? Maneno yake hayakuwa jibu, hakukuwa na matokeo yoyote. Hayakuwa jibu lililoelekezwa kwa swali la Mungu. “Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo.” Unayaelewa maneno haya? Unayaelewa? Shetani ametoka wapi duniani? Mmepata jibu? (La.) Hii ndiyo “akili” ya ujanja wa Shetani, kutomwacha yeyote kujua anachosema. Baada ya kuyasikia maneno haya, bado huwezi kutambua ni nini amesema, ilhali amemaliza kujibu. Anaamini kwamba amejibu vizuri sana. Basi unahisi vipi? (Kuchukizwa.) Kuchukizwa; sasa unaanza kuchukizwa na maneno haya, Shetani haongei moja kwa moja, hivyo kukuacha ukikuna kichwa chako na kutoweza kutambua chanzo cha maneno yake. Anazungumza kimakusudi, kwa ujanja, na anatawaliwa na kiini chake mwenyewe, asili yake. Maneno haya yalitoka moja kwa moja kinywani mwa Shetani. Hayakuzingatiwa kwa muda mrefu na kisha kuzungumzwa na Shetani, akijifikiri mwenyewe mwerevu; aliyaeleza kiasili. “Ametoka wapi duniani?” Unahisi kuchanganyikiwa, bila kujua ametoka wapi. Kuna wowote kati yenu wanaozungumza hivi? (Ndiyo.) Hii ni njia ya aina gani ya kuzungumza? (Si dhahiri na haina jibu la uhakika.) Tunapaswa kutumia aina gani ya maneno kuelezea namna hii ya kuzungumza? Ni ya kupotosha na kudanganya, siyo? Tuseme mtu hataki wengine wajue alipoenda jana. Unawauliza: “Nilikuona jana. Ulikuwa unaelekea wapi?” Hawakujibu moja kwa moja kusema mahali walienda jana. Wanasema “Jana ilikuwa siku kweli. Nimechoka sana!” Je, walijibu swali lako? Walijibu, lakini hilo si jibu ulilokuwa unataka. Hii ni “akili” ya ujanja wa mwanadamu. Huwezi kugundua wanachomaanisha ama kutambua chanzo ama nia nyuma ya maneno yao. Hujui ni nini wanachojaribu kuepuka kwa sababu ndani ya mioyo yao wanayo hadithi yao wenyewe—hii ni yenye kudhuru kwa siri. Je, ninyi pia huongea hivi mara nyingi? (Ndiyo.) Basi madhumuni yenu ni yapi? Je, huwa ni kulinda maslahi yenu wakati mwingine, kudumisha nafasi yenu wakati mwingine, taswira yenu, kuweka siri za maisha yenu ya kibinafsi, kuokoa sifa zenu binafsi? Licha ya madhumuni, hayatenganishwi na maslahi yenu, yanahusiana na maslahi yenu. Hii sio asili ya mwanadamu? Si kila mtu aliye na asili ya aina hii ni kama Shetani? Tunaweza kusema hivi, sivyo? Kuzungumza kwa ujumla, huu udhihirisho ni wenye makuruhu na wa kusinya. Mnahisi pia sasa kuchukizwa, sivyo? (Ndiyo.)

Tukiangalia tena kifungu cha kwanza, Shetani anamjibu tena Yehova Mungu, akisema: “Je, Ayubu anamcha Mungu bure?” Anaanza kushambulia tathmini ya Yehova Mungu ya Ayubu, na shambulio hili linapakwa rangi na uhasama. “Wewe hujamzunguka kila upande na ukingo, na kila upande wa nyumba yake, na kila upande wa yote aliyo nayo?” Huu ndio uelewa na tathmini ya Shetani ya kazi ya Yehova Mungu kwa Ayubu. Shetani anaitathmini hivi, akisema: “Umebariki kazi ya mikono yake, na mali yake inaongezeka nchini. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse yote aliyo nayo, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.” Shetani huongea kwa utata kila mara, lakini hapa anaongea kwa uhakika. Hata hivyo, maneno haya yaliyozungumzwa kwa uhakika ni shambulio, ni kufuru na ni upinzani kwa Yehova Mungu, kwa Mungu Mwenyewe. Mnahisi vipi mnapomsikia? Mnahisi chuki? Mnaweza kuona nia zake? Kwanza kabisa, anakataa kabisa tathmini ya Yehova Mungu ya Ayubu—yule anayemwogopa Mungu na kuepuka maovu. Kisha anakataa kabisa kila kitu anachosema na kufanya Ayubu kwa kumcha Yehova Mungu. Je, yeye anashitaki? Shetani anashitaki, anakataa na anashuku kila anachofanya na kusema Yehova Mungu. Haamini, akisema, “Ukisema mambo yako namna hii, mbona sijaiona? Umempa baraka nyingi, anawezaje kukosa kukucha?” Je, huku si kukataa kabisa kila anachofanya Mungu? Kushitaki, kukataa, kufuru—maneno yake si ya ugomvi? Si ni maonyesho ya ukweli ya kile anachofikiria Shetani ndani ya moyo wake? Haya maneno hakika si sawa na maneno tuliyoyasoma hivi sasa: “Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo.” Ni tofauti sana na hayo. Kupitia maneno haya, Shetani anaweka wazi mtazamo wake kwa Mungu na kuchukizwa na kumcha Mungu kwa Ayubu ambako kuko katika moyo wake. Haya yakifanyika, ubaya wake na asili yake mbovu inafichuliwa kabisa. Anawachukia wale wanaomcha Mungu, anawachukia wale wanaoepukana na maovu, na hata zaidi anamchukia Yehova Mungu kwa sababu ya kumpa mwanadamu baraka. Anataka kutumia fursa hii kumwangamiza Ayubu ambaye Mungu alimwinua na mkono Wake mwenyewe, kumwangamiza, akisema: “Unasema Ayubu anakuogopa na kuepukana na maovu. Naiona vingine.” Anatumia mbinu mbalimbali kumchochea na kumjaribu Yehova Mungu, na kutumia mbinu mbalimbali ili Yehova Mungu amkabidhi Ayubu kwa Shetani ili atawaliwe, adhuriwe na ashughulikiwe kwa ukatili. Anataka kutumia fursa hii ili kumwangamiza mtu huyu ambaye ni mwenye haki na mtimilifu katika macho ya Mungu. Yeye kuwa na moyo wa aina hii ni msukumo wa muda mfupi? La, siyo. Imekuwa ikiundwa kwa muda mrefu. Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini? Hataki Mungu awe na mtu yeyote; anataka wale wote ambao Mungu anataka, kuwamiliki, kuwatawala, kuwaelekeza ili wamwabudu, ili watende maovu pamoja naye. Je, hii siyo nia ya husuda ya Shetani? Kwa kawaida, ninyi husema mara nyingi kwamba Shetani ni mwovu sana, mbaya sana, lakini umemwona? Mnaweza kuona tu jinsi ambavyo mwanadamu ni mbaya na hamjaona kwa uhakika jinsi ambavyo Shetani ni mbaya sana. Lakini mmemwona kwa hili swala linalohusiana na Ayubu? (Ndiyo.) Swala hili limeufanya uso wenye sura mbaya wa Shetani na kiini chake kuwa wazi kabisa. Shetani yuko vitani na Mungu, akifuata nyuma Yake. Lengo lake ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka Kufanya, kuwamiliki na kudhibiti wale wote ambao Mungu anawataka, kuwafisha kabisa wale ambao Mungu anataka. Kama hawajafishwa, basi wanakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake. Na Mungu anafanya nini? Mungu anasema tu sentensi rahisi katika kifungu hiki; hakuna rekodi ya chochote zaidi ambacho Mungu anafanya, lakini tunaona kwamba kuna rekodi nyingi zaidi za kile ambacho Shetani anafanya na kusema. Katika kifungu cha maandishi hapa chini, Yehova Mungu alimwuliza Shetani, “Ni wapi umetoka?” Jibu la Shetani ni nini? (Bado ni “Natoka katika kuenda hapa na pale duniani, na katika kutembea juu chini humo.”) Bado ni sentensi hiyo. Imekuwaje wito wa Shetani, kazi ya Shetani ya ujuzi wa juu? Si Shetani ni wa kuchukia? Kusema sentensi hii inayochafua moyo mara moja inatosha. Kwa nini Shetani daima anarejelea Sentensi hii? Hii inadhihirisha kitu kimoja: asili ya Shetani haibadiliki. Uso wake wenye sura mbaya si kitu anachoweza kuficha kwa muda mrefu. Mungu anamwuliza swali na anajibu kwa njia kama hiyo, sembuse anavyotendea watu! Hamwogopi Mungu, hamchi Mungu, na hamtii Mungu. Hivyo anathubutu kuwa na kiburi isiyo na maadili mbele ya Mungu, kutumia haya maneno ili kujaribu kuficha kwa maswali ya Mungu, kutumia jibu hili moja kujibu swali la Mungu, kujaribu kutumia jibu hili kumshangaza Mungu—huu ndio uso usiopendeza wa Shetani. Haamini uweza wa Mungu, haamini mamlaka ya Mungu, na hakika hayuko tayari kutii kutawaliwa na Mungu. Daima anampinga Mungu, daima anashambulia yote anayofanya Mungu, akijaribu kuharibu yote anayofanya Mungu—hili ndilo lengo lake ovu.

Katika mpango wa Mungu wa usimamizi wa miaka elfu sita, vifungu hivi viwili ambavyo Shetani anasema na mambo ambayo Shetani anafanya katika kitabu cha Ayubu yanawakilisha upinzani wake kwa Mungu, na hivi ndivyo Shetani akidhihirisha alivyo kwa kweli. Umeyaona maneno na matendo ya Shetani katika maisha halisi? Utakapoyaona, unaweza kutoyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na Shetani, lakini badala yake kuyafikiria kuwa vitu vilivyoongelewa na mwanadamu, siyo? Kipi kilichowakilishwa, wakati mambo kama hayo yanazungumzwa na mwanadamu? Shetani anawakilishwa? Hata kama utamtambua, bado huwezi kuona kwamba ukweli unazungumzwa na Shetani. Lakini hapa na sasa umeona bila shaka kile ambacho Shetani mwenyewe amesema. Sasa una uelewa usio na shaka na ulio wazi kabisa wa uso wenye sura mbaya na uovu wa Shetani. Hivyo hivi vifungu viwili vilivyozungumzwa na Shetani ni vya thamani kwa watu wa leo kuweza kujua asili ya Shetani? Hivi vifungu viwili vinastahili kukusanywa ili binadamu leo aweze kutambua uso wenye sura mbaya wa Shetani, kutambua uso wa asili na wa kweli wa Shetani? Ingawa kusema jambo hili hakuonekani kufaa sana, kulieleza kwa njia hii bado kunaweza kuchukuliwa kuwa sahihi. Naweza tu kuliweka kwa njia hii na iwapo mnalielewa, basi imetosha. Tena na tena, Shetani anayashambulia mambo ambayo Yehova Mungu anafanya, akitoa mashtaka kuhusu kumcha Yehova Mungu kwa Ayubu. Anajaribu kumchochea Yehova Mungu kwa kutumia mbinu mbalimbali, kumfanya Yehova Mungu kumkubali kumjaribu Ayubu. Maneno yake basi yanachochea sana. Basi Niambieni, baada ya Shetani kuzungumza maneno haya, Mungu anaweza kuona wazi kile ambacho Shetani anataka kufanya? (Ndiyo.) Je, Mungu anaelewa kile anataka kufanya? (Ndiyo.) Katika moyo wa Mungu, huyu mtu Ayubu ambaye Mungu anamwangalia—huyu mtumishi wa Mungu, ambaye Mungu anamchukulia kuwa mwenye haki, mtu mtimilifu—anaweza kuyahimili majaribio ya aina hii? (Ndiyo.) Kwa nini Mungu anasema “ndiyo” kwa uhakika kama huo? Mungu huchunguza moyo wa binadamu daima? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anaweza kuchunguza moyo wa binadamu? (La.) Shetani hawezi. Hata kama Shetani anaweza kuona moyo wa mwanadamu, asili yake mbovu haiwezi kuamini kwamba utakatifu ni utakatifu, ama kwamba uchafu ni uchafu. Shetani mwovu hawezi kuthamini chochote kilicho takatifu, chenye haki ama chenye kung’aa. Shetani hawezi kuepuka kuumiza kwa kutenda kupitia asili yake, uovu wake, na kupitia mbinu hizi anazotumia. Hata kwa hatari ya yeye kuadhibiwa na kuangamizwa na Mungu, hasiti kumpinga Mungu kwa ukaidi—huu ni uovu, hii ni asili ya Shetani. Kwa hivyo katika kifungu hiki, Shetani anasema: “Ngozi kwa ngozi, ndiyo, yote ambayo mtu anayo atayatoa kwa sababu ya uhai wake. Lakini nyosha mbele mkono wako sasa, na uguse mfupa wake na nyama yake, na yeye atakulaani mbele ya uso wako.” Shetani anafikiri kwamba kumcha Mungu kwa mwanadamu ni kwa sababu mwanadamu amepata manufaa mengi kutoka kwa Mungu. Mwanadamu hupata manufaa mengi kutoka kwa Mungu, kwa hivyo anasema Mungu ni mwema. Lakini si kwa sababu Mungu ni mwema, ni kwa sababu tu mwanadamu amepata manufaa mengi na hivyo anaweza kumcha Mungu kwa njia hii: Punde Mungu anapomnyima manufaa haya, basi anaachana na Mungu. Katika asili yake mbovu, Shetani haamini kwamba moyo wa mwanadamu kwa kweli unaweza kumcha Mungu. Kwa sababu ya asili yake mbovu hajui utakatifu ni nini, na hata chini zaidi hajui heshima ya kuogopa ni nini. Hajui ni nini kumtii Mungu ama ni nini kumcha Mungu. Kwa sababu yeye mwenyewe hamchi Mungu, anafikiri mwanadamu hawezi kumcha Mungu pia haiwezekani. Niambieni, si Shetani ni mwovu? (Ndiyo!) Shetani ni mwovu. Isipokuwa kanisa letu, yawe ni makundi ya kidini na madhehebu mbalimbali, ama makundi ya kidini na ya kijamii, hakuna kati yao yanayoamini uwepo wa Mungu ama kuamini kwamba Mungu anaweza kufanya kazi hivyo wanafikiri, kwamba kile unachoamini si Mungu pia. Mfano wa mwanamume mzinzi, anaangalia na kuona kila mtu mwingine akiwa mzinzi, kama alivyo yeye. Mwanadamu anayedanganya kila wakati anaangalia na kuona hakuna mtu mwaminifu, anawaona wote wakidanganya. Mtu mwovu anawaona watu wote wakiwa waovu na anataka kupigana na kila mtu anayemwona. Wakati wale watu ambao walio na uaminifu kwa kulinganisha wanawaona wote kuwa waaminifu, na hivyo daima wanalaghaiwa, wanadanganywa, na hakuna wanachoweza kufanya kuhusu hilo. Nasema mifano hii michache ili kuwafanya kuwa na uhakika zaidi: asili mbovu ya Shetani si msukumo wa muda mfupi ama kitu kinachosababishwa na mazingira yake, wala si udhihirisho wa muda ulioletwa na sababu yoyote ama usuli wowote. Sivyo kabisa! Hana namna ila kuwa hivyo! Hawezi kufanya chochote chema! Hata anaposema kitu kinachofurahisha kusikia, anakushawishi tu. Kadiri maneno yake yanavyofurahisha, yenye busara zaidi, uungwana zaidi, ndivyo nia zake za husuda zinakuwa za kijicho zaidi nyuma ya maneno haya. Shetani anaonyesha uso na asili ya aina gani katika vifungu hivi viwili? (Ya kudhuru kwa siri, yenye kijicho, na mbovu.) Tabia yake ya msingi ni mbovu, hasa mbovu na yenye kijicho.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?