Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Utakatifu wa Mungu (II) Sehemu ya Kwanza

Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu "Upendo Safi Bila dosari.")

1. "Upendo" unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna umbali na hakuna chochote kichafu. Iwapo una upendo, basi hautadanganya, kulalamika, kusaliti, kuasi, kushurutisha, au kutafuta kupata kitu au kupata kiasi fulani.

2. "Upendo" unarejelea hisia ambayo ni safi na bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna umbali na hakuna chochote kichafu. Iwapo una upendo, basi utajitolea na kuvumilia magumu kwa furaha, na utalingana na Mungu. Utapeana vyote ulivyo navyo kwa sababu ya Mungu: familia zako, siku zako za baadaye, ujana wako, na ndoa yako. Vinginevyo, upendo wenu haungekuwa upendo hata kidogo, lakini badala yake udanganyifu na usaliti!

Huu ulikuwa wimbo mzuri kuchagua. Mnapenda kuimba wimbo huu? (Ndiyo.) Mnahisi nini baada ya kuimba wimbo huu? Mnaweza kuhisi upendo wa aina hii ndani yenu? (Siyo vile bado.) Ni maneno gani kutoka ndani ya wimbo huu yanakugusa kwa kina? ("Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna umbali na hakuna chochote kichafu." Lakini ndani yangu bado naona uchafu mwingi na pia naona wapi najaribu kufanya mipango na Mungu, maeneo niliyo na upungufu, kwa hivyo ninapofikiria kuhusu mimi leo kwa kweli sijafikia aina ya upendo ulio safi na bila dosari.) Kama hujafikia aina ya upendo ambao ni safi na bila dosari, una upendo wa aina gani? Una kiwango kipi cha upendo ndani yako? (Niko tu katika hatua ambapo niko tayari kutafuta na nina hamu.) Kulingana na kimo chako mwenyewe na kutumia maneno yako mwenyewe kutoka kwa uzoefu wako mwenyewe, umefikia kiwango kipi? Je, una udanganyifu, una malalamiko? Je, una madai ndani ya moyo wako, kuna vitu ambavyo unataka na kutamani kutoka kwa Mungu? (Ndiyo, kuna hivi vitu vilivyo na doa.) Vinajitokeza katika hali gani? (Wakati hali ambayo Mungu amenipangia hailingani na fikira zangu ya vile inapaswa kuwa, ama wakati matakwa yangu hayajatimizwa, nitaonyesha aina hii ya tabia potovu.) Nyinyi huimba wimbo huu mara nyingi? Mnaweza kujadili vile mnaelewa "upendo safi bila dosari"? Na mbona Mungu anafafanua upendo namna hii? (Naupenda wimbo huu sana kwa sababu kwa kweli naweza kuona kwamba upendo huu ni upendo kamili. Hata hivyo, nahisi umbali kiasi na kiwango hicho. Sasa niko tu katika hatua ambapo mimi kutoa mambo fulani na kuvumilia gharama kiasi katika kufuatilia ukweli, lakini punde tu kitu kinaathiri siku zangu za usoni na kudura yangu, ninahisi kuchanganyikiwa ndani yangu. Naona kwamba nina imani kidogo kwa Mungu.) (Sasa nahisi kwamba bado niko mbali sana kufikia upendo wa kweli. Kuna baadhi ya mambo ambapo nimeweza kuendelea mbele kuufikia, njia moja nafanya hivi ni kupitia nguvu ambayo maneno ya Mungu yananipatia na njia nyingine ni kwamba katika hali hizi nashiriki na Mungu kupitia maombi. Hata hivyo, inapohusiana maoni yangu ya uwepo, wakati mwingine siwezi kuyashinda.) Umewahi kufikiria kuhusu vitu ambavyo vinaweza kuwa vinakuzuia nyakati hizo huwezi kuyashinda? Umewahi kuchunguza maswala haya? (Ndiyo, nimekuwa nikichunguza na kwa sehemu kubwa ni kiburi changu na majivuno na pia matarajio yangu ya siku zangu za baadaye na kudura yangu ambavyo ni kizuizi kikubwa.) Wakati siku zako za baadaye na kudura zinakuwa kizuizi kikubwa kwako, umewahi kufikiria kuhusu mbona hili liwe hivi? Unataka nini kutoka kwa siku zako za baadaye na kudura yako? (Siko wazi sana kuhusu suala hili, wakati mwingine nakumbana na hali fulani ambapo nahisi sina siku za baadaye au kudura, ama wakati mwingine nahisi hata kwamba sina hatima ninapofunuliwa na Mungu. Katika nyakati hizi nahisi mnyonge sana na nahisi kwamba hii imekuwa kizuizi kikubwa kwa mimi mwenyewe. Baada ya kipindi cha uzoefu na kupitia maombi, hii hali yangu inaweza kufika kipindi muhimu, lakini bado nahisi mara nyingi kusumbuliwa na suala hili.) Unarejelea nini kwa kweli unaposema "siku za baadaye na kudura"? Kuna kitu mnachoweza kuashiria? Ni picha ama kitu mlichofikiria ama ni kitu mnaweza kweli kuona? Ni kitu halisi? Katika kila mioyo yenu mnapaswa kufikiri, wasiwasi mlio nayo katika mioyo yenu kuhusu siku zenu za baadaye na kudura zenu inarejelea nini? (Ni kuokolewa na kusalimika, na matumaini ya kufaa polepole ili kutumiwa na Mungu na kutekeleza wajibu wangu hadi katika kiwango cha juu kupitia njia ya kufanya wajibu wangu. Hata hivyo, mara nyingi ninafichuliwa na Mungu katika mambo haya, na nahisi kwamba nina upungufu, kana kwamba sina siku za baadaye.) Kaka na dada wengine wanapaswa kujadili, unaelewaje "upendo safi bila dosari"? (Hakuna chochote kichafu kutoka kwa mtu binafsi na hadhibitiwi na siku zake za baadaye na kudura zao. Licha ya vile Mungu anamtunza, anaweza kutii kikamilifu kazi ya Mungu, na pia kutii mipango ya Mungu na kumfuata Yeye hadi mwisho kabisa. Upendo wa aina hii tu kwa Mungu ni upendo safi bila dosari. Ni wakati tu ninapojilinganisha na hilo ndipo ninapogundua kwamba katika miaka michache ambayo nimemwamini Mungu, nimeweza, juujuu, kutoa vitu fulani ama kuvumilia baadhi ya gharama, lakini sijawahi kuweza kweli kumpa Mungu moyo wangu. Wakati Mungu ananifichua, nahisi kana kwamba nimeainishwa kama mtu ambaye hawezi kuokolewa, na nakaa katika hali hii hasi. Najiona nikifanya wajibu wangu, lakini wakati huo huo nikijaribu kutekeleza mipango na Mungu, na kutoweza kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, na kwamba hatima yangu, siku zangu za baadaye, na kudura yangu yote daima yako kwa akili yangu.)

Inaonekana kwamba mmeimba wimbo huu mara nyingi na mna baadhi ya uelewa kuuhusu na kwamba kuna uhusiano fulani na uzoefu wako halisi. Hata hivyo, karibu kila mtu ana viwango tofauti vya kukubali kila kirai katika wimbo "Upendo Safi bila Dosari." Watu wengine wako radhi, watu wengine wanatafuta kuweka kando siku zao za baadaye, watu wengine wanatafuta kuweka kando familia zao, watu wengine hawatafuti kupokea chochote. Bado wengine wanajihitaji kuwa bila udanganyifu, bila malalamiko, na kutoasi dhidi ya Mungu. Kwa nini Mungu angetaka kupendekeza aina hii ya upendo na kuhitaji kwamba watu wampende namna hii? Hii ni aina ya upendo ambao watu wanaweza kuufikia? Hiyo ni kusema, watu wanaweza kupenda namna hii? Watu wanaweza kuona kwamba hawawezi, kwa sababu hawamiliki kamwe upendo wa aina hii. Wakati hawaumiliki, na kimsingi hawajui kuhusu upendo, Mungu anazungumza maneno haya, ambayo ni mageni kwao. Kwa sababu watu wanaishi katika dunia hii, wanaishi katika tabia yao potovu, iwapo watu wangekuwa na aina hii ya upendo ama iwapo mtu angeweza kumiliki aina hii ya upendo, bila kuwa na maombi na madai, kuwa radhi kujitoa wenyewe na kuwa radhi kustahimili mateso na kuacha vyote vilivyo vyao, mtu anayemiliki aina hii ya upendo angewezaje kuonekana katika macho ya watu wengine? Si angekuwa mtu kamili? (Ndiyo.) Mtu kamili kama huyo yupo katika dunia hii? Hayupo, yupo? Mtu wa aina hii hayupo kabisa katika dunia hii, ila angeweza kuishi katika utupu, siyo? Hivyo, watu wengine—kupitia uzoefu wao—wanatumia juhudi nyingi kuwa kama kile ambacho maneno haya yalielezea. Wanajishughulikia, wanajizuia, na hata daima wanajitupa: Wanastahimili mateso na wanaacha dhana ambazo si sahihi walizokuwa nazo. Wanaacha njia walivyokuwa wakiasi Mungu, wanaacha tamaa zao na matakwa. Lakini mwishowe bado hawawezi kufikia mahitaji hayo. Kwa nini hayo yanafanyika? Mungu anasema mambo haya ili kupeana kiwango cha watu kufuata, ili watu wajue kiwango wanachodaiwa na Mungu. Lakini Mungu huwahi kusema kwamba watu lazima wafikie hiki mara moja? Je, Mungu huwahi kusema ni katika wakati upi watu wanapaswa kufikia hiki? (La.) Je, Mungu huwahi kusema kwamba watu lazima wampende namna hii? Kifungu hiki kinasema hivi? La, hakisemi hivi. Mungu anawaambia watu tu kuhusu "upendo" Aliokuwa akirejelea. Kuhusiana na watu kuweza kumpenda Mungu namna hii na kumtendea Mungu namna hii, mahitaji ya Mungu ni yapi? Si muhimu kuyafikia mara moja, ama papo hapo kwa sababu watu hawawezi kufanya hivyo. Mmewahi kufikiria kuhusu masharti ambayo watu wanapaswa kutimiza ili kupenda namna hii? Iwapo watu wangeyasoma maneno haya mara nyingi watakuwa na upendo huu polepole? (La.) Masharti ni yapi basi? Kwanza, watu wanawezaje kuwa huru kutokana na tuhuma kumhusu Mungu? (Ni watu waaminifu tu wanaoweza kufikia jambo hilo.) Je, kuwa huru kutokana na udanganyifu? (Pia wanapaswa kuwa watu waaminifu.) Kuwa mmoja asiyetaka kufanya mipango na Mungu? Huyo pia lazima awe mtu mwaminifu, Je, kutokuwa na ujanja? Kunarejelea nini kusema hakuna chaguo katika upendo? Yote yanarejelea kuwa mtu mwaminifu? Kuna maelezo mengi hapo; uwezo wa Mungu kutaja upendo wa aina hii ama uwezo wa Mungu kufafanua aina hii ya upendo, kuisema namna hii, hii inathibitisha nini? Tunaweza kusema kwamba Mungu anamiliki upendo wa aina hii? (Ndiyo.) Mnaona hii wapi? (Kwa upendo Mungu alio nao kwa mwanadamu.) Upendo wa Mungu kwa mwanadamu una sharti? (La.) Kuna vizuizi ama umbali kati ya Mungu na mwanadamu? (La.) Mungu ana tuhuma kumhusu mwanadamu? (La.) Mungu humwangalia mwanadamu na kwa kweli anamwelewa mwanadamu. Je, Mungu ni mdanganyifu kwa mwanadamu? (La.) Kwa sababu Mungu anaongea kikamilifu kuhusu upendo huu, moyo Wake ama kiini Chake kinaweza kuwa kamili sana? (Ndiyo.) Watu wamewahi kufafanua upendo kwa njia hii? Mwanadamu amefafanua upendo katika hali gani? Mwanadamu anazungumza vipi kuhusu upendo? Si ni kupeana ama kutoa? (Ndiyo.) Ufafanuzi wa mwanadamu wa upendo ni rahisi, na hauna kiini.

Ufafanuzi wa Mungu wa upendo na namna Mungu anazungumza kuhusu upendo inahusiana na kipengele cha kiini Chake, lakini kipengele kipi cha kiini Chake? Wakati uliopita Tulishiriki kuhusu mada muhimu sana, ni mada ambayo watu wamezungumzia mara nyingi na kutaja awali, na ni neno ambalo linatajwa mara nyingi katika kipindi cha kumwamini Mungu, lakini ni neno linalojulikana na pia ni geni kwa watu, lakini mbona hivyo? Ni neno linalotoka kwa lugha za mwanadamu, na miongoni mwa mwanadamu ufafanuzi wake ni dhahiri na pia ni usio dhahiri. Neno hili ni nini? (Utakatifu.) Utakatifu: hiyo ndiyo ilikuwa mada ya wakati wa mwisho tuliposhiriki. Tulishiriki kiasi kuhusu mada hii, lakini kushiriki kwetu hakukuwa kamili. Kulingana na sehemu tuliyoshiriki wakati uliopita, kila mtu alipata uelewa mpya kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Mnafikiri uelewa mpya ulikuwa nini? Yaani, nini katika uelewa huo ama maneno hayo yaliwafanya kuhisi kwamba uelewa wenu wa utakatifu wa Mungu ulikuwa tofauti ama uliobadilishwa na kile Nilichoshiriki kuhusu utakatifu wa Mungu? Je, uliacha maono? (Mungu anasema Anachohisi katika moyo Wake; ni safi. Hiki ni kipengele kimoja cha utakatifu.) Hii ni sehemu moja yake, kuna chochote kingine cha kuongezea? (Kuna utakatifu wakati Mungu ana ghadhabu kwa mwanadamu, hakuna dosari.) (Naona katika mamlaka ya Mungu ukamilifu Wake, uaminifu Wake, hekima Yake na utawala Wake juu ya vitu vyote. Naelewa mambo haya.) "Utawala juu ya vitu vyote," ambao ni kuhusu mamlaka ya Mungu, sasa tunazungumza kuhusu utakatifu wa Mungu. (Kuhusu utakatifu wa Mungu, naelewa kwamba kuna ghadhabu ya Mungu na huruma ya Mungu katika tabia Yake ya haki, hili liliacha maono yenye nguvu kwangu. tabia ya Mungu ya haki ni ya kipekee, ambayo zamani sikuwa na uelewa kama huo wa ama ufafanuzi kama huo wake. Lakini katika ushirika Wako Ulijadili kwamba ghadhabu ya Mungu ni tofauti na hasira ya mwanadamu. Ni kitu ambacho hakuna kiumbe anamiliki. Ghadhabu ya Mungu ni kitu chema na kina kanuni; inatolewa kwa sababu ya kiini kiasilia cha Mungu. Ni kwa sababu Anaona kitu hasi na hivyo Mungu anaachilia ghadhabu Yake. Huruma ya Mungu, pia ni kitu ambacho hakuna kiumbe anamiliki. Ingawa mwanadamu ana matendo mazuri ama vitendo vya haki ambavyo vinachukuliwa kuwa sawa na huruma, ni vichafu na kuna nia nyuma yavyo. Aina zingine zinazoitwa huruma hata ni bandia na tupu. Lakini nimeuona wokovu wa Mungu wakati anaonyesha huruma kwa watu, na huruma hii inamweka mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya kuokolewa. Inawaweka watu kwa njia sahihi ya kumwamini Mungu ili wapokee hatima yao mazuri. Kwa hivyo huruma ya Mungu inamilikiwa na kiini Chake. Hata ingawa Mungu angeharibu mji kwa sababu ya ghadhabu Yake, kwa sababu ana kiini cha huruma, Angeweza kwa wakati wowote ama pahali popote kuonyesha huruma kuwaokoa na kuwalinda watu wa mji huo. Huu ni uelewa wangu.) Una baadhi ya uelewa kuhusu tabia ya haki ya Mungu.

Mada yetu ya sasa, ni maarifa ya utakatifu wa Mungu. Mara nyingi watu huhusisha tabia ya haki ya Mungu na utakatifu Wake na wote wamesikia kuhusu tabia Yake ya haki. Zaidi, watu wengi mara nyingi wanaongea kuhusu utakatifu wa Mungu pamoja na tabia ya haki, wakisema kwamba tabia ya Mungu ya haki ni takatifu. Kila mtu anajua neno "takatifu" na ni neno linalotumika sana, lakini kuhusiana na kidokezo cha neno hilo, maonyesho gani ya utakatifu wa Mungu ambayo watu wanaweza kuona? Ni nini Mungu amefichua ambacho watu wanaweza kutambua? Ninahofia kwamba hiki ni kitu ambacho hakuna anayejua. Tunasema kwamba tabia ya Mungu ni ya haki, lakini basi ukichukua tabia ya haki ya Mungu na kuisema kuwa takatifu, hiyo inaonekana isiyo dhahiri kiasi, ya kuchanganya kiasi; mbona hivi? Unasema tabia ya Mungu ni ya haki, ama unasema tabia Yake ya haki ni takatifu, hivyo katika mioyo yenu mnauainisha utakatifu wa Mungu vipi? Mnauelewa vipi? Hivyo ni kusema, ni nini Mungu amefichua ama ni nini kuhusu kile Mungu anacho na alicho ambacho watu wanaweza kutambua kama takatifu? Umefikiria hili hapo awali? Kile Nilichoona ni kwamba watu mara nyingi husema maneno yanayotumika sana ama wana virai ambavyo vimesemwa mara kwa mara, lakini hawajui wanachosema. Hivi tu ni vile kila mtu anavyosema, na wanasema hivi mara nyingi, hivyo inakuwa kirai kilichowekwa. Hata hivyo, iwapo wangechunguza na kutafiti kwa kina maelezo, wangepata kwamba hawajui maana halisi ni nini ama inachorejelea. Kama tu neno "takatifu," hakuna anayejua kabisa ni kipengele kipi cha kiini cha Mungu kinarejelewa kuhusiana na utakatifu Wake ambao watu wanaongelea kuhusu. Kuhusu kupatanisha neno "takatifu" na Mungu, hakuna anayejua na mioyo ya watu imechanganyikiwa, na ni pana jinsi wanavyotambua Mungu ni mtakatifu. Lakini Mungu ni mtakatifu vipi? Kuna anayejua? Hakuna aliye wazi kabisa kuhusu suala hili. Leo tutashiriki kuhusu mada kupatanisha neno "takatifu" na Mungu ili watu waweze kuona maudhui ya kweli ya kiini cha utakatifu wa Mungu, na hili litazuia watu wengine kulitumia neno hilo kimazoea ovyo ovyo na kusema vitu kwa nasibu wakati hawajui maana yake, ama hata kama wako sawa na sahihi ama la. Watu daima wameisema hivi: umeisema, nimeisema, na imekuwa jinsi ya kuongea na watu hivyo wameliharibu neno "takatifu" bila kusudi.

Kuhusu neno "takatifu," juujuu linaonekana rahisi sana kuelewa, siyo? Kwa kiwango cha chini kabisa watu wanaamini neno "takatifu" linamaanisha nadhifu, isiyo na doa, tukufu, na safi, au kuna watu wengine ambao huhusisha "takatifu" na "upendo" katika wimbo "Upendo Safi Bila dosari," tulioimba hivi karibuni, ambayo ni sahihi; hii ni sehemu yake, upendo wa Mungu ni sehemu ya kiini Chake, lakini si kiini chote. Hata hivyo, katika mitazamo ya watu, wanaona neno na kulishirikisha na vitu ambavyo wao wenyewe wanaviona kuwa nadhifu na safi, ama na vitu ambavyo wao binafsi wanafikiri havina doa wala havina dosari. Kwa mfano, watu wengine walisema kwamba ua la yungiyungi ni safi, ni vipi watu walikuja kufafanua ua la yungiyungi kwa njia hii? (Ua la yungiyungi linamea kwa matope lakini linatoa maua bila dosari.) Linatoa maua bila dosari kutoka kwa maji machafu, hivyo watu wakaanza kutumia neno "takatifu" kwa ua la yungiyungi. Watu wengine walichukulia hadithi za mapenzi zilizobuniwa na wengine kuwa takatifu, ama wangemchukulia mhusika mkuu anayestahili upaa kuwa mtakatifu. Zaidi, wengine walifikiria watu kutoka kwa Biblia, ama wengine walioandikwa katika vitabu vya kiroho—kama watakatifu, mitume, au wengine ambao walimfuata Mungu awali Alipokuwa akifanya kazi Yake—kama waliokuwa na uzoefu wa kiroho ambao ulikuwa takatifu. Haya yote ni mambo yaliyofikiriwa na watu na hizi ni dhana zinazoshikiliwa na watu. Mbona watu wanashikilia dhana kama hizi? Kuna sababu moja na ni rahisi sana: Ni kwa sababu watu wanaishi miongoni mwa tabia potovu na wanaishi katika dunia ya uovu na uchafu. Kila kitu wanachoona, kila kitu wanachogusa, kila kitu wanachopitia ni uovu wa Shetani na upotovu wa Shetani na pia kufanya mipango, kupigana wenyewe kwa wenyewe, na vita vinavyotokea miongoni mwa watu walio chini ya ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, hata wakati Mungu anafanya kazi Yake kwa watu, na hata wakati Anazungumza nao na kufichua tabia na kiini Chake hawawezi kuona ama kujua utakatifu na kiini cha Mungu ni nini. Watu mara nyingi husema kwamba Mungu ni mtakatifu, lakini hawana uelewa wowote wa kweli; wao husema tu maneno matupu. Kwa sababu watu wanaishi miongoni mwa uchafu na upotovu na wanamilikiwa na Shetani, hawaoni mwangaza, hawajui chochote kuhusu masuala mema na zaidi, hawajui ukweli. Kwa hivyo, hakuna anayejua maana ya takatifu. Baada ya kusema hayo, kuna vitu vitakatifu ama watu watakatifu miongoni mwa binadamu hawa potovu? (La.) Tunaweza kusema kwa uhakika La, hakuna, kwa sababu kiini cha Mungu tu ndicho kitakatifu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana