Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Utakatifu wa Mungu (II) (Sehemu ya Pili)

Kuhusu utakatifu wa kiini cha Mungu, wakati uliopita tulishiriki kidogo kuuhusu na huo ulikuwa msukumo wa maarifa ya watu ya utakatifu wa Mungu, lakini hautoshi. Hauwezi kutosha kusaidia watu kujua kikamilifu utakatifu wa Mungu, wala hautoshi kuwasaidia kuelewa kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee. Zaidi, hautoshi kuruhusu watu kuelewa kipengele cha maana ya ukweli ya utakatifu kwani imejumuishwa kabisa kwa Mungu. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba tuendelee na ushirika wetu katika mada hii. Hapo nyuma ushirika wetu ulijadili mada tatu, kwa hivyo sasa tunapaswa kujadili mada ya nne, na tutaanza kusoma maandiko.

Majaribu ya Shetani

Mat 4:1-4 Baada ya hapo Yesu akaongozwa mwituni na Roho Mtakatifu kwa minajili ya kujaribiwa na ibilisi. Na baada ya kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, alihisi njaa. Na aliyemjaribu alipokuja kwake, alimwambia, Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike mikate. Lakini akamjibu na kusema, imeandikwa, Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.

Haya ndiyo maneno ambayo ibilisi kwanza alijaribu kumjaribu Bwana Yesu. Ni nini maudhui ya aliyoyasema ibilisi? (“Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike mikate.”) Ibilisi alisema maneno haya, ambayo yalikuwa rahisi kiasi, lakini kuna shida na maudhui muhimu ya maneno haya? (Ndiyo.) Shida ni nini? Alisema, “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu,” lakini katika moyo wake, alijua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mwana wa Mungu? Alijua kwamba Alikuwa Kristo? (Ndiyo.) Basi kwa nini alisema “Iwapo wewe ni”? (Alikuwa akijaribu kumjaribu Mungu.) Hakika, alikuwa akijaribu kumjaribu Mungu, lakini ni nini madhumuni ya kufanya hivyo? Alisema, “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu.” Katika moyo wake alijua kwamba Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, haya yalikuwa wazi katika moyo wake, lakini licha ya haya, alinyenyekea Kwake au kumwabudu Yeye? (La.) Alitaka kufanya nini? Alitaka kufanya hivi na kusema maneno haya kumfanya Bwana Yesu kukasirika na kisha kumshawishi kuchukua chambo, na kumdanganya Bwana Yesu kufanya mambo kulingana na njia yake ya kufikiri na kuinuka kwa chango chake. Si alimaanisha hivi? Katika moyo wa Shetani alijua wazi kwamba huyu alikuwa Bwana Yesu Kristo, lakini alisema hivi hata hivyo. Hii si asili ya Shetani? Asili ya Shetani ni nini? (Kuwa mjanja, mwovu na kutokuwa na Heshima kwa Mungu.) Hamheshimu Mungu. Ni kitu kipi hasi alichokuwa akifanya hapa? Hakutaka kumshambulia Mungu? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, alisema: “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, yaamrishe mawe haya yabadilike mikate”; si hii ni nia ovu ya Shetani? (Ndiyo.) Alikuwa anajaribu kufanya nini kweli? Lengo lake ni wazi sana: Alikuwa anajaribu kutumia mbinu hii kukanusha nafasi na utambulisho wa Bwana Yesu Kristo. Alisema, “Iwapo wewe ni Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Usipo, basi wewe siwe Mwana wa Mungu na Hufanyi kazi hii.” Ni haya yaliyomaanishwa hapa? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, alitaka kuvunja na kuharibu kazi ya Mungu; huu ndio uovu wa Shetani. Uovu wake ni maonyesho ya kiasili ya asili yake. Ingawaje alijua Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, kupata mwili kwenyewe kwa Mungu Mwenyewe, hangeweza kuwacha kufanya kitu kama hiki, kumfuata Mungu nyuma na kuendelea kumshambulia na kujaribu sana kuvuruga na kuharibu kazi ya Mungu.

Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichotumia Shetani: “yaamrishe mawe haya yabadilike mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Iwapo kuna chakula, mbona usile? Mbona ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? (La.) Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? Je, Alikuwa na chakula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upuuzi wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Shetani anafanya idadi fulani ya mambo; unaona asili yake ovu na yenye kudhuru na unaona akiharibu kazi ya Mungu, na wa kuchukiza na kuudhi sana. Lakini kwa upande mwingine, unapata asili ya kitoto na ujinga nyuma ya maneno na vitendo vyake? (Ndiyo.) Huu ni ufunuo kuhusu asili ya Shetani; ana asili ya aina hii na atafanya kitu kama hiki. Kwa wanadamu, kirai hiki ni cha upuuzi na cha kuchekesha. Lakini maneno kama hayo kwa hakika yanaweza kutamkwa na Shetani. Tunaweza kusema kwamba ni asiyejua? Mjinga? Uovu wa Shetani uko kila mahali na daima unafichuliwa. Na Bwana Yesu anamjibu aje? (“Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee, lakini kwa kila neno linalotoka kinywani mwa Mungu.”) Maneno haya yana nguvu yoyote? (Yanayo.) Mbona tunasema kwamba yana nguvu? (Ni ya ukweli.) Sahihi. Maneno haya ni ukweli. Sasa, mtu anaishi kwa mkate tu? Bwana Yesu alifunga kwa siku na usiku 40. Alikufa kwa njaa? (La.) Hakufa kwa njaa, kwa hivyo Shetani alimkaribia, akimwambia abadili mawe yawe chakula kwa kusema kitu kama hiki: “Ukiyabadili mawe yawe chakula, Hutakuwa basi na vitu vya kula? Si basi Hutalazimika kufunga, Hutalazimika kuwa na njaa?” Lakini Bwana Yesu alisema, “Mwanadamu hatadumu kwa mkate pekee,” inayomaanisha kwamba, ingawa mwanadamu anaishi katika mwili, kile kinachompa uhai, kile kinachouruhusu mwili wake kuishi na kupumua, si chakula, ila maneno yote yaliyotamkwa na kinywa cha Mungu. Katika upande mmoja, mwanadamu anachukulia maneno haya kuwa ukweli. Maneno haya yanampa imani, yanamfanya ahisi kwamba anaweza kumtegemea Mungu, kwamba Mungu ni ukweli. Kwa upande mwingine, kuna kipengele cha vitendo katika maneno haya? (Kunacho.) Mbona? Kwa sababu Bwana Yesu amefunga kwa siku na usiku 40 na bado Anasimama hapo, bado yuko hai. Huu ni mfano? Hajakula chochote, chakula chochote kwa siku na usiku 40. Bado yuko hai. Huu ni ushahidi wa nguvu nyuma ya kirai Chake. Kirai hiki ni rahisi, lakini, kuhusiana na Bwana Yesu, kirai hiki kutoka kwa roho Yake Alifunzwa na mtu mwingine, ama Alikifikiria tu kwa sababu ya kile Shetani alimwambia? Fikiria jambo hili. Kuliweka kwa njia nyingine, Mungu ni ukweli, Mungu ni uhai, lakini je, ukweli na uhai wa Mungu uliongezwa kwa kuchelewa? Ulitokana na uzoefu? (La.) La, ni ya asili ndani ya Mungu, kumaanisha kwamba ukweli na uhai vipo ndani ya kiini cha Mungu. Licha ya kile kinachomfanyikia, Anachofichua ni ukweli. Ukweli huu, kirai hiki—iwapo maudhui yake ni mapama ama finyu—kinaweza kumwacha mwanadamu aishi, kimpe uhai; kinaweza kumwezesha mwanadamu kupata, ndani yake, ukweli, uwazi kuhusu njia ya maisha ya binadamu, na kumwezesha kuwa na imani kwa Mungu. Kwa maneno mengine, ndicho chanzo cha matumizi ya Mungu ya kirai hiki ni chema. Hivyo tunaweza kusema kitu hiki chema ni takatifu? (Ndiyo.) Kirai cha Shetani kinatoka kwa asili ya Shetani. Shetani anafichua asili yake ovu, asili yake yenye kijicho, kila mahali, daima. Sasa, ufunuo huu, Shetani anaufanya kiasili? (Ndiyo.) Kuna yeyote anayemchochea? Kuna yeyote anayemsaidia? Kuna yeyote anayemshurutisha? (La.) Anautoa kwa hiari yake mwenyewe. Hii ni asili ovu ya Shetani. Licha ya kile Mungu anafanya na jinsi Anavyokifanya, Shetani yuko nyuma Yake. Kiini na sura ya ukweli ya vitu hivi ambavyo Shetani anasema na kufanya ni kiini cha Shetani—kiini ovu, kiini cha kuonea kijicho. Sasa, kuendelea kusoma, ni nini tena Shetani anasema? Tuendelee kusoma hapa chini.

Mat 4:5-7 Kisha Ibilisi akamchukua hadi katika mji mtakatifu, na kumweka juu ya kinara cha hekalu, Naye akamwambia, Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jirushe chini: kwa kuwa imeandikwa, Atawaamuru malaika wake wakuchunge: na watakubeba mikononi mwao, usije ukaukwaa mguu wako kwenye jiwe wakati wowote. Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.

Hebu kwanza tuzungumze kuhusu kirai hiki cha Shetani. Alisema “Ikiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jirushe chini,” na kisha akadondoa kutoka kwa maandiko, “Atawaamuru malaika wake wakuchunge: na watakubeba mikononi mwao, usije ukaukwaa mguu wako kwenye jiwe wakati wowote.” Unahisi vipi unaposikia maneno ya Shetani? Si ni ya kitoto sana? Ni ya kitoto, upuuzi na kuchukiza. Mbona Nasema hivi? Daima Shetani hufanya kitu kijinga, anaamini kwamba ni mwerevu sana; na mara nyingi hutaja maandiko—hata neno la Mungu—anajaribu kuyabadili maneno haya dhidi ya Mungu kumshambulia na kumjaribu. Lengo lake la kufanya hivi ni kuharibu mpango wa kazi ya Mungu. Hata hivyo, unaona chochote kwa kile Shetani amesema? (Kuna nia ovu hapo.) Shetani daima amekuwa mjaribu; haongei kwa njia inayoeleweka rahisi, huongea kwa njia isiyo wazi akitumia majaribu, ulaghai na ushawishi. Shetani anamjaribu Mungu na pia mwanadamu: Anafikiri kwamba Mungu na mwanadamu wote hawajui, ni wajinga, na hawawezi kutofautisha kwa wazi vitu vilivyo. Shetani anafikiri kwamba Mungu na pia mwanadamu hawataona hadi kwa kiini chake na kwamba Mungu na mwanadamu wote hawataona udanganyifu wake na nia zake mbaya. Si hapa ndipo Shetani anapata ujinga wake? Zaidi, Shetani anataja maandiko wazi; anafikiria kwamba kufanya hivyo kunamfanya kuaminika, na kwamba hutaweza kuona dosari zozote kwa haya ama kuepuka kudanganywa na haya. Si hapa ndipo Shetani anakuwa mjinga na kama mtoto? (Ndiyo.) Hii ni kama wakati watu wengine wanaeneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, si wasioamini watasema kitu kama alichosema Shetani? Mmesikia watu wakisema kitu kama hiki? (Ndiyo.) Ni jinsi gani unahisi kuchukizwa unaposikia vitu kama hivyo? Unahisi kuchukizwa? (Ndiyo.) Unapohisi kuchukizwa, pia unahisi kutiwa kinyaa na kukirihishwa? (Ndiyo.) Unapokuwa na hisia hizi unaweza kutambua kwamba Shetani na tabia potovu ambayo Shetani anamfanyia mwanadamu ni ovu? Katika mioyo yenu mmewahi kuwa na utambuzi kama, “Mungu kamwe haongei namna hiyo. Maneno ya Shetani yanaleta mashambulizi na majaribu, maneno yake ni ya ujinga, ya kuchekesha, ya kitoto, na ya kuchukiza. Hata hivyo, katika matamshi ya Mungu na vitendo vya Mungu, Hangetumia mbinu kama hizi kuzungumza ama kufanya kazi Yake, na Hajawahi kufanya hivyo”? Bila shaka, katika hali hii watu wana tu kiasi kidogo cha kuhisi kuendelea na hawana utambuzi wa utakatifu wa Mungu, sivyo? Na kimo chenu cha sasa, mnahisi tu hivi: “Kila kitu Mungu anasema ni ukweli, ni cha manufaa kwetu, na lazima tukikubali”; bila kujali iwapo unaweza kukubali hili au la, bila ubaguzi unasema kwamba maneno ya Mungu ni ukweli na kwamba Mungu ni ukweli, lakini hujui kwamba ukweli ni utakatifu wenyewe na kwamba Mungu ni mtakatifu.

Hivyo, jibu la Bwana kwa maneno ya Shetani lilikuwa lipi? (Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.) Kuna ukweli katika kirai hiki ambacho Bwana Yesu alisema? (Ndiyo.) Kuna ukweli kwa kirai hicho. Juujuu inaonekana kama amri ya watu kufuata, ni kirai rahisi sana, lakini ni kimoja ambacho mwanadamu na Shetani wamekiuka mara nyingi. Hivyo, Bwana alimwambia, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” kwa sababu hiki ndicho kile Shetani alifanya mara nyingi na alifanya kila juhudi kufanya hivyo, unaweza hata kusema kwamba Shetani alifanya hivyo bila haya. Ni asili ya msingi ya Shetani kutomcha Mungu na kutomheshimu Mungu kwa moyo wake. Hivyo, hata wakati Shetani alikuwa kando ya Mungu na angeweza kumwona, Shetani hakuweza kuacha kumjaribu Mungu. Kwa hivyo, Bwana Yesu alimwambia Shetani, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Hiki ni kirai ambacho Mungu amemwambia Shetani mara nyingi. Si kutumia kirai hiki kunafaa hata leo? (Ndiyo.) Mbona? (Kwa sababu pia sisi humjaribu Mungu mara nyingi.) Watu mara nyingi humjaribu Mungu, lakini mbona watu hufanya hivyo mara nyingi? Je, ni kwa sababu watu wamejawa na tabia potovu ya kishetani? (Ndiyo.) Kwa hivyo kile Shetani alisema hapa juu ni kitu ambacho watu husema mara nyingi? (Ndiyo.) Katika hali gani? Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekuwa wakisema mambo kama haya licha ya wakati na mahali. Hii inadhihirisha kwamba tabia ya watu ni sawa kabisa na tabia potovu ya Shetani. Bwana Yesu alisema kirai rahisi, ambacho kinawakilisha ukweli na ambacho watu wanahitaji. Hata hivyo, katika hali hii Bwana Yesu alikuwa akigombana na Shetani? Kulikuwa na chochote cha kukabiliana kwa kile Alisema kwa Shetani? (La.) Bwana Yesu aliyachukulia vipi majaribu ya Shetani kwa moyo Wake? Je, Alihisi kuchukizwa na kutiwa kinyaa? (Ndiyo.) Bwana Yesu alihisi kutiwa kinyaa na kuchukizwa lakini Hakugombana na Shetani, wala hata chini zaidi Hakuzungumza kuhusu kanuni zozote kubwa, sivyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? (Bwana Yesu hakutaka kumkiri Shetani.) Kwa nini Hakutaka kumkiri Shetani? (Kwa sababu Shetani daima yuko hivyo, hawezi kubadilika.) Tunaweza kusema kwamba Shetani hana akili? (Ndiyo, tunaweza.) Je, Shetani anaweza kutambua kwamba Mungu ni ukweli? Shetani hatawahi kutambua kwamba Mungu ni ukweli na hatawahi kukubali kwamba Mungu ni ukweli; hii ni asili yake. Zaidi, kuna kitu kingine kuhusu asili ya Shetani kinachotia kinyaa, ni nini? Katika majaribio yake ya kumjaribu Bwana Yesu, Shetani alifikiri kwamba, hata kama alimjaribu Mungu na hangefaulu, bado angejaribu jambo hili tu. Hata kama angeadhibiwa, angeifanya tu. Hata kama hangepata chochote chema kutoka kwa kufanya hivyo, angeifanya tu, na kuendelea na kusimama dhidi ya Mungu hadi mwisho kabisa. Hii ni asili ya aina gani? Si huo ni uovu? (Ndiyo.) Yule anayekasirika sana wakati Mungu anatajwa, amemwona Mungu? Yule anayekuwa na hasira wakati Mungu anatajwa, anamjua Mungu? Hajui Mungu ni nani, hamwamini, na Mungu hajaongea naye. Mungu hajawahi kumsumbua, kwa hivyo mbona akuwe na hasira? Tunaweza kusema kwamba mtu huyu ni mwovu? Huyu anaweza kuwa mtu mwenye asili ovu? Haijalishi ni mienendo gani inafanyika duniani, iwe ya kufurahisha, chakula, watu maarufu, watu wenye sura nzuri, hakuna yoyote haya yanayomsumbua, lakini kutajwa mara moja kwa neno “Mungu” na anakasirika; huu si mfano wa asili ovu? Huu unatumika kama ushahidi wa kuridhisha wa asili ovu ya mwanadamu. Sasa, mkijizungumzia, kuna wakati ambapo ukweli unatajwa, ama wakati majaribio ya Mungu kwa mwanadamu yanatajwa ama wakati maneno ya Mungu ya hukumu dhidi ya mwanadamu yanatajwa, na mnahisi kusumbuliwa, kutiwa kinyaa, na hamtaki kusikia kuyahusu? Mioyo yenu inaweza kufikiri: Huu ni ukweli vipi? Si watu wote walisema kwamba Mungu ni ukweli? Huu si ukweli, haya bila shaka ni maneno ya Mungu ya maonyo kwa mwanadamu! Watu wengine hata wanaweza kuhisi kuchukizwa kwa mioyo yao: Haya yanatajwa kila siku, majaribio Yake kwetu daima yanatajwa kama hukumu Yake; haya yote yataisha lini? Tutapokea lini hatima njema? Haijulikani hasira hii isiyo na busara inatoka wapi. Hii ni asili ya aina gani? (Asili ovu.) Inasababishwa na asili ovu ya Shetani. Na kwa Mungu kuhusu asili ovu ya Shetani na tabia potovu ya mwanadamu, Hagombani kamwe wala kubishana na watu, na kamwe Halalamiki wakati watu wanatenda kutokana na ujinga. Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno ambalo amesema na kila kitendo amefanya kinahusiana na ukweli. Ukweli huu na maneno haya sio tu ndoto isiyo na msingi, lakini bali yake yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu Mungu amefanya ni ukweli, tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vizuri na uhalisi wa vitu hivyo vizuri, na kuwaruhusu kutembea njia njema. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake. Mmekiona, siyo? Tutaendelea kuyasoma maandiko.

Mat 4:8-11 Tena, Ibilisi akampeleka hadi kwenye mlima mrefu sana, na kumwonyesha falme zote za dunia, na fahari yao; Na akasema kwake, Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu. Kisha Yesu akamwambia, Ondoka uende zako, Shetani; kwa kuwa imeandikwa, Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia. Basi akawachwa na Ibilisi, na, tazama, malaika wakaja na wakamhudumia.

Shetani, ibilisi, baada ya kushindwa katika hila zake mbili za awali, alijaribu nyingine tena: Alionyesha falme zote duniani na utukufu wa falme hizi kwa Bwana Yesu na kumwambia amwabudu ibilisi. Unaona nini kuhusu sura za ukweli za ibilisi kutoka kwa hali hii? Si Shetani ibilisi hana haya kabisa? (Ndiyo.) Anaweza kukosa haya namna gani? Kila kitu kiliumbwa na Mungu, lakini Shetani anakigeuza na kumwonyesha Mungu akisema, “Angalia utajiri na utukufu wa falme hizi zote. Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu.” Je, si hili ni mabadiliko ya jukumu? Si Shetani hana haya? Mungu aliumba kila kitu, lakini kilikuwa cha raha Zake? Mungu alimpa mwanadamu kila kitu, lakini Shetani alitaka kunyakua vyote na baadaye akasema, “Niabudu! Niabudu na nitakupa Wewe haya yote.” Huu ni uso usiopendeza wa Shetani; hana haya kabisa, siyo? Shetani hata hajui maana ya neno “haya,” na huu ni mfano mwingine tu wa uovu wake. Hata hajui haya ni nini. Shetani anajua vyema kwamba Mungu aliumba kila kitu na kwamba Anavisimamia na Anavitawala. Kila kitu ni cha Mungu, si cha mwanadamu, sembuse Shetani, lakini Shetani ibilisi bila haya alisema kwamba angempa Mungu kila kitu. Si tena Shetani anafanya kitu cha ujinga na kisicho na aibu? Mungu anamchukia Shetani hata zaidi sasa, siyo? Lakini licha ya kile Shetani alijaribu kufanya, Bwana Yesu alikiamini? (La.) Bwana Yesu alisema nini? (“Muabudu Bwana Mungu wako.”) Je, kirai hiki kina maana ya utendaji? (Ndiyo.) Maana gani ya utendaji? Tunaona uovu na kutokuwa na aibu kwa Shetani katika matamshi yake. Kwa hivyo iwapo mwanadamu angemwabudu Shetani, hitimisho lingekuwa nini? Angepokea utajiri na utukufu wa falme zote? (La.) Angepokea nini? Je, wanadamu wangekuwa wasio na haya na wa kuchekwa kama tu Shetani? (Ndiyo.) Hawangekuwa tofauti na Shetani basi. Kwa hivyo, Bwana Yesu alisema kirai hiki ambacho ni muhimu kwa kila mtu: “Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia,” kinachosema kwamba isipokuwa Bwana, isipokuwa Mungu Mwenyewe, ukimhudumia mwingine, ukimwabudu Shetani ibilisi, basi utagaagaa katika uchafu sawa na Shetani. Kisha utashiriki kutokuwa na haya na uovu wa Shetani, na kama tu Shetani ungemjaribu Mungu na kumshambulia Mungu. Na basi mwisho wako ungekuwa upi? Ungechukiwa na Mungu, kuangushwa na Mungu na kuangamizwa na Mungu, sivyo? Baada ya Shetani kumjaribu Bwana Mungu mara kadhaa bila mafanikio, alijaribu tena? Shetani hakujaribu tena na kisha akaondoka. Hii inathibitisha nini? Inathibitisha kwamba asili ovu ya Shetani, kuonea kijicho kwake, na ujinga na upuuzi wake yote hayastahili kutajwa mbele ya Mungu. Bwana Yesu alimshinda Shetani kwa sentensi tatu tu, na baadaye akatoroka na mkia wake katikati ya miguu yake, kuaibika sana asiweze kuonyesha uso wake tena, na hakumjaribu Bwana Yesu tena. Kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amelishinda jaribio hili la Shetani, Angeweza kuendelea kwa urahisi kazi ambayo Alipaswa kufanya na kuanza kazi zilizokuwa mbele Yake. Je, yote aliyoyasema Bwana Yesu na kufanya katika hali hii yanabeba maana kiasi ya vitendo kwa kila mtu yakitumika sasa? (Ndiyo.) Maana ya utendaji ya aina gani? Je, kumshinda Shetani ni kitu rahisi kufanya? (La.) Ingekuwa nini basi? Ni lazima watu wawe na uelewa wazi wa asili ovu ya Shetani? Ni lazima watu wawe na uelewa sahihi wa majaribu ya Shetani? (Ndiyo.) Ukiwahi kupitia majaribu ya Shetani katika maisha yako, na iwapo unaweza kuona hadi kwa asili ovu ya Shetani, utaweza kumshinda? Iwapo unajua kuhusu ujinga na upuuzi wa Shetani, bado unaweza kusimama kando ya Shetani na kumshambulia Mungu? (La, hatungeweza.) Ikiwa unaelewa jinsi kuwa na kijicho na kutokuwa na aibu kwa Shetani vinafichuliwa kupitia kwako—iwapo unatambua wazi na kujua mambo haya—bado ungemshambulia na kumjaribu Mungu kwa njia hii? (La, hatungeweza.) Utafanya nini? (Tutaasi dhidi ya Shetani na kumwacha.) Hili ni jambo rahisi kufanya? (La.) Hili si rahisi, kufanya hivi, watu wanalazimika kuomba mara nyingi, ni lazima wajiweke mbele ya Mungu, na lazima wajichunguze. Lazima watii nidhamu ya Mungu na hukumu Yake na kuadibu Kwake na kwa njia hii tu ndipo watu wataweza kujitoa polepole kutoka kwa udanganyifu na udhibiti wa Shetani.

Tunaweza kuweka pamoja mambo yanayojumuisha kiini cha Shetani kutoka kwa mambo haya ambayo amesema. Kwanza, kiini cha Shetani kwa jumla kinaweza kusemwa kuwa ovu, ambacho ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Kwa nini Nasema kiini cha Shetani ni ovu? Mtu anapaswa kuangalia matokeo ya kile Shetani anafanyia watu ili kuona haya. Shetani anapotosha na kudhibiti mwanadamu, na mwanadamu anatenda chini ya tabia potovu ya Shetani, na anaishi katika dunia iliyopotoshwa na Shetani na kuishi miongoni mwa watu potovu. Wengi wanamilikiwa na kusimilishwa na Shetani bila kusudi; mwanadamu hivyo ana tabia potovu ya Shetani, ambayo ni asili ya Shetani. Kutoka kwa yote Shetani amesema na kufanya, umeona kiburi chake? Umeona udanganyifu na kijicho chake? Kiburi cha Shetani kimsingi kinaonekana vipi? Je, Shetani daima anataka kuchukua nafasi ya Mungu? Shetani daima anataka kuharibu kazi ya Mungu na nafasi ya Mungu na kuyachukua kuwa yake ili watu waunge mkono na kuabudu Shetani; hii ni asili ya kiburi ya Shetani. Wakati Shetani anapotosha watu, huwaambia moja kwa moja kile wanachopaswa kufanya? Wakati Shetani anamjaribu Mungu, je, hatoki na kusema, “Nakujaribu, nitakushambulia”? Hakika hafanyi hivyo. Ni mbinu gani hivyo Shetani anatumia? Anashawishi, anajaribu, anashambulia, na anaweka mitego yake, na hata kwa kutaja maandiko, Shetani anazungumza na kutenda kwa njia mbalimbali ili kutimiza nia zake mbaya. Baada ya Shetani kufanya hivi, ni nini kinachoweza kuonekana kutoka kile kilichojitokeza kwa mwanadamu? Je, si watu wana kiburi? Mwanadamu ameteseka kutoka kwa upotovu wa Shetani kwa maelfu ya miaka na hivyo mwanadamu amekuwa mwenye kiburi mdanganyifu, mwenye kijicho, na asiyefikiri. Haya mambo yote yametokana kwa sababu ya asili ya Shetani. Kwa sababu asili ya Shetani ni ovu, amempa mwanadamu asili hii ovu na kumletea mwanadamu tabia hii potovu. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi chini ya tabia potovu ya kishetani na, kama Shetani, mwanadamu anaenda kinyume na Mungu, anamshambulia Mungu, na kumjaribu Yeye hadi kwa kiwango ambacho mwanadamu hamwabudu Mungu na hamheshimu katika moyo wake.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?