Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Utakatifu wa Mungu (III) (Sehemu ya Nne)

Hebu turudi kuzungumza kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu. Tumeongea karibuni kuhusu mbinu mbalimbali ambazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu na ambazo kila mmoja wenu mnaweza kupitia nyinyi wenyewe, kwa hivyo sitatoa maelezo zaidi. Lakini katika mioyo yenu pengine mmechanganyikiwa kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu, ama kwa kiwango cha chini zaidi ana upungufu wa maelezo. Ni ya manufaa kwenu kwa Mimi kuzungumzia hili tena? (Ndiyo.) Je, mnataka kumwelewa? (Ndiyo.) Pengine wengine wenu watauliza: "Mbona tuzungumze kuhusu Shetani tena? Punde tunapoongea kuhusu Shetani, tunakuwa na hasira, na tunaposikia jina lake tunahisi kutotulia kila mahali." Bila kujali jinsi anavyokufanya kutotulia, lazima ukubali ukweli, na mambo haya yanapaswa kuzungumziwa kwa uwazi na kufanywa dhahiri kwa manufaa ya ufahamu wenu: kama sivyo hamwezi kweli kuepukana na ushawishi wa Shetani.

Tumezungumza hapo awali njia tano ambazo Shetani anatumia kumpotosha mwanadamu. Ndani ya hizi njia tano kuna mbinu anazotumia. Njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu ni aina ya kifuniko tu; ya kudhuru kwa siri zaidi ni mbinu zinazojificha nyuma ya sura hii ya kinafiki na anataka kutumia mbinu hizi kufikia malengo yake. Mbinu hizi ni zipi? Nipeni muhtasari. (Anadanganya, anashawishi na anatishia.) Kadri mnavyoendelea kutaja ndivyo mnavyokaribia. Inaonekana kana kwamba mmedhuriwa kwa kina na yeye na mna hisia kali kuhusu mada hii. (Anatumia pia maneno matamu na uongo, anashawishi, anadanganya, na anamiliki kwa nguvu.) Anamiliki kwa nguvu—hii inatoa fikra ya kina. Watu wanaogopa umiliki wa nguvu wa Shetani. Kuna mengine? (Huwadhuru watu kikatili, hutumia vitisho na vivutio, na hudanganya.) Uongo ni kiini cha matendo yake na hudanganya ili kukulaghai. Ni nini asili ya kudanganya? Je, kudanganya si sawa na kulaghai? Lengo la kusema uongo kwa kweli ni kukudanganya. Mengine zaidi? Zungumzeni. Niambieni yote mnayoyajua. (Hushawishi, hudhuru, hupofusha na hudanganya.) Wengi wenu mnahisi sawa kuhusu uongo huu, sivyo? (Hujipendekeza, humdhibiti mwanadamu, humkamata mwanadamu, humtishia sana mwanadamu na humzuia mwanadamu kumwamini Mungu.) Ninajua vizuri kiasi mnachomaanisha na yote ni mazuri pia. Nyote mnajua kitu kuhusu hili, kwa hivyo wacha sasa tufanye muhtasari.

Kuna njia sita za msingi ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu.

Ya kwanza ni kudhibiti na kulazimisha. Yaani, Shetani atafanya vyovyote vile kudhibiti moyo wako. "Kulazimisha" kunamaanisha nini? (Kunamaanisha shurutisho.) Hukutishia na kukulazimisha kumtii, kukufanya kufikiria matokeo usipomtii. Unaogopa na huthubutu kumpinga, kwa hivyo basi unamtii.

Ya pili ni kudanganya na kulaghai. "Kudanganya na kulaghai" yanahusisha nini? Shetani hutunga baadhi ya hadithi na uongo, kukulaghai wewe kuziamini. Hakwambii kamwe kwamba mwanadamu aliumbwa na Mungu, wala hasemi pia moja kwa moja kwamba hukuumbwa na Mungu. Hatumii jina "Mungu" kabisa, lakini badala yake hutumia kitu kingine mbadala, akitumia kitu hiki kukudanganya ili kimsingi usiwe na wazo la kuwepo kwa Mungu. Huu ulaghai bila shaka unahusisha vipengele vingi, sio tu hiki kimoja.

Ya tatu ni kufunza kwa nguvu. Je, kuna kufunza kwa nguvu? (Ndiyo.) Kufunza nini kwa nguvu? Je, kufunzwa kwa nguvu kunafanywa kwa hiari ya mwanadamu mwenyewe? Je, kunafanywa na idhini ya mwanadamu? (La.) Haijalishi kama hukuidhinisha. Katika kutojua kwako, humwaga ndani yako, kuweka ndani yako kufikiria kwa Shetani, kanuni zake za maisha na kiini chake.

Ya nne ni vitisho na vivutio. Yaani, Shetani hutumia mbinu mbalimbali ili umkubali, umfuate, ufanye kazi katika Huduma yake; hujaribu kufikia malengo yake kwa vyovyote vile. Saa zingine hukupa fadhili ndogo lakini bado hukushawishi kufanya dhambi. Usipomfuata, atakufanya uteseke na kukuadhibu na atatumia njia mbalimbali kukushambulia na kukutega.

Ya tano ni uongo na kiharusi. "Uongo na kiharusi" ni kwamba Shetani hutunga kauli na mawazo yanayosikika kuwa matamu ambayo yako pamoja na dhana za watu kufanya ionekane kwamba anatilia maanani miili ya watu ama anafikiria kuhusu maisha yao na siku zao za baadaye, wakati hakika anakudanganya tu. Kisha anakupooza ili usijue kile kilicho sahihi na kile kilicho makosa, ili udanganywe bila kujua na hivyo kuja chini ya udhibiti wake.

Ya sita ni uangamizi wa mwili na akili. Shetani huharibu kipi cha mwanadamu? (Akili yao, nafsi yao yote.) Shetani huharibu akili yako, kukufanya kutokuwa na nguvu za kupinga, kumaanisha kuwa polepole sana moyo wako unageuka kwa Shetani licha ya wewe mwenyewe. Huingiza mambo haya ndani yako kila siku, kila siku akitumia mawazo na utamaduni huu kukushawishi na kukuelimisha, polepole akiharibu utashi wako, kukufanya kutotaka kuwa mtu mzuri tena, kukufanya kutotaka tena kutotetea kile unachoita cha haki. Bila kujua, huna tena utashi wa kuogelea kinyume na mkondo dhidi ya bamvua, lakini badala yake kububujika chini pamoja nayo. "Uangamizi" unamaanisha kwamba Shetani hutesa watu sana hadi wanakuwa sio kama wanadamu wala pepo, kisha anachukua fursa ya kuwameza.

Kila ya hizi njia zote Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu inaweza kumfanya mwanadamu kutokuwa na nguvu ya kupinga; yoyote inaweza kuwa ya kufisha kwa watu. Kwa maneno mengine, chochote anachofanya Shetani na njia yoyote anayotumia inaweza kukufanya kupotoka, inaweza kukuleta chini ya udhibiti wa Shetani na inaweza kukuzamisha katika bwawa la uovu. Hizi ndizo njia Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu.

Tunaweza kusema Shetani ni mwovu, lakini ili kuthibitisha hili ni lazima bado tuangalie matokeo ya upotovu wa Shetani wa mwanadamu ni yapi na ni tabia gani na viini vipi anamletea mwanadamu. Nyote mnajua baadhi ya haya, kwa hivyo ongeeni kuyahusu. Baada ya Shetani kumpotosha mwanadamu, ni tabia gani anaonyesha ama kufichua? (Zenye kiburi na zenye maringo, zenye ubinafsi na zenye kustahili dharau, zisizo aminifu, zenye udanganyifu, zenye kudhuru kwa siri na zenye kijicho, na zisizo na ubinadamu.) Kwa ujumla, tunaweza kusema hazina ubinadamu, siyo? Wacha kaka na dada wengine wazungumze. (Zenye kiburi, zenye udanganyifu, zenye kijicho, zenye ubinafsi, zenye tamaa, za juujuu, za uwongo.) Usiseme kinachofichuliwa na baadhi ya tabia ya kipengele; Lazima useme ni nini kiini cha kipengele hicho. (Punde mwanadamu anapopotoshwa na Shetani, wakati mwingi hasa huwa mwenye kiburi na wa kujidai, wa kujigamba na mwenye majivuno, mwenye tamaa na mwenye ubinafsi. Haya ndiyo mazito sana.) (Baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, anatenda yasiyo na mawazo kimwili na kiroho. Kisha anakua mkatili kwa Mungu, anampinga Mungu, hamtii Mungu, na anapoteza dhamiri yake na akili ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo.) Yale ambayo mmesema yote kimsingi ni sawa na yana tofauti kidogo tu, na wengine wenu wanajali zaidi maelezo madogo. Kwa muhtasari, "mwenye kiburi" limekuwa jina ambalo limetajwa sana—mwenye kiburi, mwenye udanganyifu, mwenye kijicho na mwenye ubinafsi. Lakini nyote mmepuuza kitu sawa. Watu wasio na dhamiri, ambao wamepoteza akili zao na ambao hawana ubinadamu—bado kuna kitu muhimu pia ambacho hakuna yeyote kati yenu amesema. Kwa hivyo ni kipi? (Kusaliti.) Sahihi. Hakuna yeyote ambaye amesema "kusaliti." Matokeo ya mwisho ya tabia hizi ambazo zipo kwa mwanadamu yeyote baada ya kupotoshwa na Shetani ni kusaliti kwao Mungu. Licha ya kile Mungu anamwambia mwanadamu ama licha ya kazi anayomfanyia, hakubali kile ambacho anajua kuwa ukweli, yaani, hamtambui Mungu tena na anamsaliti: Haya ndiyo matokeo ya upotovu wa Shetani wa mwanadamu. Ni sawa kwa tabia zote potovu za mwanadamu. Miongoni mwa njia ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu—maarifa ambayo mwanadamu hujifunza, sayansi anayojua, ushirikina, utamaduni wa jadi, na mienendo ya kijamii anayoelewa—kuna yoyote ambayo mwanadamu anaweza kutumia kusema kile kilicho haki na kile kisicho haki? Kuna viwango vyovyote vya kufanya kazi kutoka hapa? (La.) Kuna chochote kinachoweza kumsaidia mwanadamu kujua kilicho takatifu na kilicho ovu? (La.) Hakuna viwango na hakuna msingi ambao unaweza kumsaidia mwanadamu. Hata kama watu wanajua neno "takatifu," hakuna yeyote anayejua kweli kile kilicho takatifu. Kwa hivyo mambo haya ambayo Shetani anamletea mwanadamu yanaweza kumruhusu kujua ukweli? Je, yanaweza kumruhusu mwanadamu kuishi na ubinadamu unaoongezeka? Je, yanaweza kumruhusu mwanadamu kuishi maisha ambamo anaweza zaidi na zaidi kumwabudu Mungu? (La.) Ni dhahiri kwamba hayawezi kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu, au kuelewa ukweli, wala hayawezi kumruhusu mwanadamu kujua utakatifu na uovu ni nini. Kinyume chake, mwanadamu anakuwa zaidi na zaidi mwenye uasherati, mbali na mbali zaidi na Mungu. Hii ndiyo sababu ya mbona tunasema Shetani ni mwovu. Baada ya kuchangua asili ovu nyingi za Shetani, je, mmeona Shetani kuwa na dalili yoyote ya utakatifu katika sifa zake ama katika uelewa wenu wa kiini chake? (La.) Hiyo ni ya hakika. Kwa hivyo mmeona kiini chochote cha Shetani ambacho kinashiriki usawa wowote na Mungu? (La.) Je, kuna maonyesho ya Shetani ambayo yanashiriki usawa na Mungu? (La.) Kwa hivyo sasa Nataka kuwauliza, kwa kutumia maneno yenu, utakatifu wa Mungu ni nini hasa? Kwanza kabisa, utakatifu wa Mungu unasemwa kwa uhusiano na nini? Je, unasemwa kwa uhusiano na kiini cha Mungu? Ama unasemwa kwa uhusiano na vipengele fulani vya tabia Yake? (Inasemwa kwa uhusiano na kiini cha Mungu.) Lazima tupate kidato wazi katika mada yetu tunayopenda. Inasemwa kwa uhusiano wa kiini cha Mungu. Kwanza kabisa, tumetumia uovu wa Shetani kama foili ya[c] kiini cha Mungu, kwa hivyo umeona kiini chochote cha Shetani katika Mungu? Je, kiini chochote cha mwanadamu? Mtu aniambie. (Utakatifu wa Mungu ni wa kipekee, ni mwaminifu, wa dhati na hakuna tabia potovu ndani ya Mungu. Mungu ni mwema kabisa, kama vile vitu vyote Yeye huletea binadamu.) (Kiini chote cha Mungu ni chema, yote anayofichua ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu na kwa mwanadamu kuishi kwa kudhihirisha usawa wa kawaida wa binadamu. Ni ili Aweze kweli kulinda mtu na ili mwanadamu aweze kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida.) Je, ni tu kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida? (Ni ili mwanadamu aweze kweli kujua ukweli; Utakatifu Wake ni upendo Wake wa kweli na wokovu wa wanadamu.) (Yote ambayo yamefichuliwa na kiini cha Mungu ni mema. Ukweli wa Mungu, uaminifu Wake, kutokuwa na ubinafsi Kwake, unyenyekevu Wake na upendo Wake kwa wanadamu yote yanaonyesha kiini cha utakatifu wa Mungu.) (Mungu si mwenye kiburi, hana ubinafsi na hasaliti, na katika kipengele hiki kiini takatifu cha Mungu pia kinaonekana kufichuliwa.) Mm. Kunayo mengine ya kuongeza? (Mungu hana dalili za tabia potovu ya Shetani. Chochote Shetani anacho ni hasi kabisa, wakati kile ambacho Mungu anacho ni kizuri. Tunaweza kuona kwamba Mungu yuko upande wetu daima. Kutoka tulipokuwa wachanga hadi sasa, hasa nyakati zile tulipotea njia, Alikuwa nasi, Akitutazama na kutuweka salama. Hamna udanganyifu ndani ya Mungu, hamna kusema uongo. Yeye hunena kwa udhahiri na uwazi, na hii pia ni asili ya kweli ya Mungu.) Vizuri sana! (Hatuwezi kuona tabia yoyote potovu ya Shetani katika kazi ya Mungu, hamna udanganyifu, hamna kujisifu, hamna ahadi tupu na hamna udanganyifu. Mungu ni wa pekee ambaye mwanadamu anaweza kuamini na kazi ya Mungu ni ya uaminifu na kweli. Kutoka kwa kazi ya Mungu tunaweza kuona Mungu akiwaambia watu wawe waaminifu, wawe na hekima, wawe na uwezo wa kung’amua kati ya mema na mabaya na kuwa na utambuzi wa watu, matukio, na mambo mbalimbali. Kwa haya tunaweza kuona utakatifu wa Mungu.) Je, mmemaliza? (Ndiyo.) Je, mmeridhika na mliyoyasema? Ni kiasi gani cha uelewa cha Mungu kweli upo mioyoni mwenu? Na mnaelewa kiasi kipi utakatifu wa Mungu? Najua kwamba kila mmoja kati yenu katika moyo wake ana baadhi ya kiwango cha ufahamu wa utambuzi, kwa sababu kila mtu anaweza kuhisi kazi ya Mungu kwao na, katika viwango tofauti, wao hupata vitu vingi kutoka kwa Mungu; wao hupata neema na baraka, wao hutiwa nuru na kuangaziwa, na wao hupokea hukumu na kuadibu kwa Mungu ili kwamba mwanadamu aweze kuwa na uelewa rahisi wa kiini cha Mungu.

Ingawa utakatifu wa Mungu tunaojadili leo unaweza kuonekana geni kwa watu wengi, bila kujali jinsi unaweza kuonekana tumeanza mada hii, na mtakuwa na ufahamu zaidi mnapotembea katika njia yenu kwenda mbele. Itawalazimu kuja kuhisi na kuelewa kutoka kwa uzoefu wenu wenyewe kwa utaratibu. Sasa uelewa wenu wa utambuzi kuhusu kiini cha Mungu bado unahitaji kipindi cha muda mrefu kujifunza, kuthibitisha, kuhisi na kuipitia, hadi siku moja mtajua utakatifu wa Mungu kutoka katikati ya moyo wenu kuwa kiini cha Mungu ambacho hakina dosari, upendo wa Mungu usio na ubinafsi, kwamba haya yote Mungu humpa mwanadamu hayana ubinafsi, na mtakuja kujua ya kwamba utakatifu wa Mungu hauna dosari wala haushutumiki. Hivi viini vya Mungu si maneno tu ambayo Yeye hutumia kuonyesha utambulisho Wake, bali Mungu hutumia kiini Chake kwa kimya na kwa dhati kushughulika na kila mtu. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu si tupu, wala si cha nadharia au mafundisho ya dini na hakika si aina ya maarifa. Si aina ya elimu kwa mwanadamu, lakini badala yake ni ufunuo wa kweli wa matendo ya Mungu mwenyewe na ni kiini ambacho kimefichuliwa cha kile Mungu anacho na alicho. Binadamu anapaswa kujua kiini hiki na kukifahamu, kwa kuwa kila kitu Mungu hufanya na kila neno Yeye husema ni la thamani kubwa na umuhimu mkubwa kwa kila mtu. Unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kumwamini Mungu; unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kutambua maana halisi ya maneno haya "Mungu Mwenyewe, wa Kipekee." Hutafikiria tena kwamba unaweza kuchagua kutembea njia zingine, na hutakuwa tena radhi kusaliti kila kitu ambacho Mungu amekupangia. Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani. Kando na Mungu, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuokoa kutoka kwa bahari ya mateso, ili usiteseke tena: Hili linaamuliwa na kiini cha Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu hukuokoa bila ubinafsi wowote, ni Mungu pekee anayehusika na maisha yako ya baadaye, na hatima yako na maisha yako, na Yeye anapanga mambo yote kwa ajili yako. Hili ni jambo ambalo hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kinaweza kutimiza. Kwa sababu hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kina kiini cha Mungu kama hiki, hakuna mtu au kitu kina uwezo wa kukuokoa au kukuongoza wewe. Huu ndio umuhimu wa kiini cha Mungu kwa mwanadamu. Labda mnahisi kuwa maneno haya Niliyoyasema yanaweza kweli kusaidia kimsingi katika kanuni. Lakini kama wewe unafuatilia ukweli, kama wewe unapenda ukweli, katika uzoefu wako wa baada ya hapa maneno haya hayataleta tu mabadiliko katika hatima yako, lakini zaidi ya hayo yatakuleta kwa njia sahihi ya maisha. Je, unafahamu hili, siyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo sasa mna moyo wa kupenda katika kutambua kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Ni vizuri kuwa na moyo wa kupenda. Tutamalizia hapa kujadili mada yetu ya leo juu ya kutambua utakatifu wa Mungu.

Ningependa kuwazungumzia kuhusu kitu mlichofanya kilichonishangaza mwanzoni mwa mkusanyiko wetu leo. Wengine wenu pengine mlikuwa na hisia za shukrani hivi karibuni, ama kuhisi shukrani, na hivyo mlitaka kuonyesha kimwili kile mlichokuwa nacho akilini mwenu. Hili si la kushutumiwa, na si sahihi wala makosa. Lakini ningependa muelewe kitu. Ni nini hiki? Kwanza Ningetaka kuwauliza kuhusu mlichokifanya hivi sasa. Je, kulikuwa ni kusujudu ama kupiga magoti kuabudu? Kuna yeyote anayeweza kuniambia? (Tunaamini ilikuwa kusujudu.) Mnaamini kulikuwa kusujudu, kwa hivyo ni nini maana ya kusujudu? (Kuabudu.) Kwa hivyo ni nini kupiga magoti kuabudu basi? Sijashiriki hili na ninyi awali, lakini leo nahisi ni muhimu kushiriki mada hii na ninyi. Je, mnasujudu katika mikusanyiko yenu ya kawaida? (La.) Je, mnasujudu mnaposema sala zenu? (Ndiyo.) Je, mnasujudu kila wakati mnaposema sala zenu, hali zinaporuhusu? (Ndiyo.) Hivyo ni vizuri sana. Lakini ni nini Ningependa nyinyi muelewe leo? Ni aina mbili za watu ambao kupiga magoti kwao kunakubaliwa na Mungu. Hatuhitaji kutafuta maoni katika Biblia ama tabia za watu wa kiroho, na Nitawaambia kitu kweli hapa na sasa. Kwanza, kusujudu na kupiga magoti kuabudu si kitu sawa. Mbona Mungu anakubali kupiga magoti kwa wale wanaosujudu wenyewe? Ni kwa sababu Mungu humwita mtu Kwake na humwita mtu huyu kukubali agizo la Mungu, kwa hivyo anasujudu mwenyewe mbele ya Mungu. Huyu ni mtu wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni kupiga magoti kuabudu kwa mtu anayemcha Mungu na kuepukana na maovu. Kuna watu hawa wa aina mbili tu. Kwa hivyo mko katika aina gani? Mnaweza kusema? Huu ni ukweli kabisa, ingawa unaweza kuumiza hisia zenu kidogo. Hakuna kitu cha kusema kuhusu kupiga magoti kwa watu wakati wa sala—hii ni sahihi na ndivyo inavyopaswa kuwa, kwa sababu wakati watu wanasali wakati mwingi ni kuombea kitu, kufungua mioyo yao kwa Mungu na kukutana Naye uso kwa uso. Ni mawasiliano na mazungumzo, moyo kwa moyo na Mungu. Mkiifanya kama urasmi tu, basi haipaswi kufanya hivyo. Simaanishi kuwashutumu kwa yale ambayo mmefanya leo. Mnajua kwamba nataka tu kuweka wazi kwenu ili muelewe kanuni hii, mnajua? (Tunajua.) Ili msiendelee kufanya hili. Je, watu basi wana fursa yoyote ya kusujudu na kupiga magoti mbele ya uso wa Mungu? Daima kutakuwa na fursa. Hatimaye siku itakuja lakini wakati sio sasa. Mnaona? (Ndiyo.) Je, hili linawafanya kuhisi vibaya? (La.) Hivyo ni vizuri. Labda maneno haya yatawatia moyo ama kuwashawishi ili muweze kujua katika mioyo yenu taabu ya sasa kati ya Mungu na mwanadamu na aina ya uhusiano uliopo sasa kati yao. Ingawa tumeongea na kuzungumza sana hivi karibuni, uelewa wa mwanadamu kuhusu Mungu bado uko mbali na kutosha. Mwanadamu bado ana umbali mrefu wa kwenda katika njia hii ya kutafuta kumwelewa Mungu. Si nia yangu kuwafanya mfanye hivi kwa dharura, ama kuwaharakisha kuonyesha matamanio na hisia za aina hizi. Yale mliyofanya leo yanaweza kufichua na kuonyesha hisia zenu za kweli, na Niliyafahamu. Kwa hivyo wakati mlipokuwa mkiyafanya, nilitaka tu kusimama na kuwatakia mema, kwa sababu Nataka nyote muwe wazima. Kwa hivyo katika maneno na vitendo vyangu vyote ninafanya yote ninayoweza kuwasaidia, kuwaongoza, ili muwe na uelewa sahihi na mtazamo sahihi wa mambo yote. Mnaweza kuelewa haya, sivyo? (Ndiyo.) Hivyo ni vizuri sana. Ingawa watu wana baadhi ya uelewa wa tabia mbalimbali za Mungu, kipengele cha kile anacho Mungu na alicho na kazi Mungu anafanya, wingi wa uelewa huu hauendi mbali na kusoma maneno kwenye ukurasa, ama kuyaelewa katika kanuni, ama tu kuyafikiria. Yale wanayoyakosa sana watu ni uelewa na mtazamo wa kweli unaotoka kwa uzoefu halisi. Ingawa Mungu hutumia njia mbalimbali kuamsha mioyo ya wanadamu, bado kuna njia ndefu ya kutembea kabla mioyo ya wanadamu iamshwe kikamilifu. Sitaki kumwona yeyote akihisi kana kwamba Mungu amemwacha nje kwa baridi, kwamba Mungu amemwacha ama amempuuza. Ningetaka tu kuona kila mtu katika njia ya kufuatilia ukweli na kutafuta kumwelewa Mungu, akiendelea mbele kwa ujasiri na utashi usiosita, bila wasiwasi, bila kubeba mizigo. Haijalishi umefanya makosa gani, haijalishi umepotoka aje ama vile ulivyotenda dhambi, usiwache haya yawe mizigo ama vikorokoro ziada kubeba katika ufuataji wako wa kumwelewa Mungu: Endelea kutembea mbele. Haijalishi itafanyika lini, moyo wa Mungu ambao ni wokovu wa mwanadamu haubadiliki: Hii ni sehemu ya thamani sana ya kiini cha Mungu. Mnahisi vizuri kiasi sasa? (Ndiyo.) Ninatumai kwamba mnaweza kuchukua mtazamo sahihi katika mambo yote na maneno ambayo Nimezungumza. Wacha tukomeshe ushirika wetu hapa, basi. Kwaheri kila mtu! (Kwaheri!)

Januari 11, 2014

Tanbihi:

c. Mtu/kitu kinachodhihirisha uzuri/ubora wa kingine kwa kuvilinganisha.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?