Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)

Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (IV) Sehemu ya Kwanza

Leo, tunafanya ushirika juu ya mada maalum. Kwa kila mmoja wenu, kuna vitu viwili vikuu tu ambavyo mnapaswa kujua, kuvipitia na kuvielewa—na vitu hivi viwili ni vipi? Cha kwanza ni kuingia binafsi kwa watu katika maisha, na cha pili kinahusu kumjua Mungu. Leo Nawapa uchaguzi: Chagua kimoja. Mngependa kusikia kuhusu mada inayouhusu uzoefu wa maisha ya kibinafsi ya watu, au mngependa kusikia inayohusu kumjua Mungu Mwenyewe? Na kwa nini Ninawapa uchaguzi huu? Kwa sababu leo Ninafikiria kufanya ushirika nanyi juu ya mambo mapya kuhusu kumjua Mungu. Lakini, hata hivyo, kwanza nitawaacha mchague kimoja kati ya vitu viwili ambavyo Nimezungumzia hivi punde. (Ninachagua kuhusu kumjua Mungu.) (Tunafikiri kwamba kufanyia ushirika maarifa ya Mungu ni bora pia.) Mnadhani mambo ambayo tumekuwa tukiyafanyia ushirika hivi karibuni kuhusu kumjua Mungu yanawezekana? Ni haki kusema kuwa ni nje ya uwezo wa watu wengi. Mwaweza kukosa kusadiki maneno haya. Kwa nini Ninasema hili? Kwa sababu mlipokuwa mkisikiliza Niliyokuwa nikisema awali, haijalishi Niliyasema vipi, au ni kwa maneno gani, moja kwa moja na kinadharia mlikuwa mnatambua Nilichokuwa nikisema, lakini tatizo lenu kubwa ni kwamba, hamkuelewa ni kwa nini Niliyasema mambo haya, ni kwa nini nilizizungumzia hizi mada. Hiki ndicho kiini cha hili suala. Na kwa hiyo, japo kusikia kwenu haya mambo kuliongeza na kuimarisha uelewa wenu kuhusu Mungu na matendo Yake, bado mnapata ugumu kumjua Mungu. Baada ya kusikia Nilichokisema, wengi wenu hawaelewi ni kwa nini Nilisema hili, na lina uhusiano gani na kumjua Mungu. Ugumu wenu wa kuelewa uhusiano wake na kumjua Mungu unahusu nini? Mmewahi kuliwazia hili? Huenda hamjawahi. Sababu ya kutoelewa mambo haya ni kwa sababu uzoefu wenu wa kimaisha ni wa juujuu sana. Ikiwa ufahamu na uzoefu wa watu kuhusu maneno ya Mungu utabaki kuwa wa juujuu, basi ufahamu wao mkubwa kuhusu Mungu utakuwa si yakini na kidhahania—utakuwa wa hali ya chini, wa kimafundisho, na wa kinadharia. Kinadharia, yanaonekana au kusikika kuwa na mantiki na razini, ila ufahamu kuhusu Mungu utokao vinywani mwa watu ni mtupu. Na mbona Ninasema kuwa ni mtupu? Kwa sababu, kwa hakika, moyoni mwako hauko wazi kama maneno kuhusu kumjua Mungu yatokayo kinywani mwako ni sawa au la, ikiwa ni sahihi au la. Hivyo basi, japo watu wengi wamesikia taarifa na mada nyingi kuhusu kumjua Mungu, ufahamu wao kuhusu Mungu haujatoka nje ya nadharia na mafundisho ya yasiyo yakini na dhahania. Kwa hiyo hili tatizo linaweza kusuluhishwa vipi? Je, mmewahi kuliwazia hilo? Ikiwa watu hawautafuti ukweli, wanaweza kuwa na uhalisi? Ikiwa watu hawautafuti ukweli, basi bila shaka hawana uhalisi, na hivyo, kwa hakika hawana ufahamu au uzoefu wa maneno ya Mungu. Je, yawezekana wasioyafahamu maneno ya Mungu wamfahamu Mungu? Hawawezi Kabisa. Haya mawili yameshikamana. Hivyo, watu wengi husema, "Kumjua Mungu kwawezaje kuwa kugumu hivi? Ninapozungumzia kujijua mimi mwenyewe, naweza kuzungumza kwa saa nyingi, ila inapofika kumjua Mungu nakoswa maneno. Hata ninapoweza kusema machache, ni kwa kushurutishwa, yanakosa uchangamfu—hata yanasikika ya kufedhehesha ninapojisikia nikiyasema." Hiki ndicho chanzo. Ukihisi kwamba kumjua Mungu ni kugumu sana, kwamba kunakuchosha, kwamba huna la kuzungumzia—huna chochote cha kufanya ushirika na kuwapa wengine, na kujipa wewe mwenyewe—basi hili linathibitisha kwamba hujayapitia maneno ya Mungu. Maneno ya Mungu ni nini? Je, maneno ya Mungu sio maonyesho ya kile Mungu anacho na alicho? Ikiwa hujapitia uzoefu wa maneno ya Mungu, unaweza kuwa na ufahamu wowote kuhusu anacho na alicho. Kwa hakika siyo. Vitu hivi vyote vimeshikamana. Ikiwa huna uzoefu wa maneno ya Mungu, basi huwezi kuelewa mapenzi ya Mungu, na hutajua tabia Yake ni nini, Anachokipenda, Anachokichukia, mahitaji Yake kwa mwanadamu ni yapi, mtazamo Wake kwa walio wazuri, na kwa wale walio waovu ni upi—kwa hakika haya yote yatakuwa tata na yenye mashaka kwako. Ikiwa mnamwamini Mungu katikati ya haya mashaka, wakati mnaposema kuwa nyinyi ni miongoni mwa wale wanaoutafuta ukweli na kumfuata Mungu, je, haya maneno yana uhalisi? Hayana! Hivyo, sasa, fanyeni uamuzi wenu: Mnachagua mada gani leo? (Tunachagua kuingia katika maisha.) Ni vipengele vipi vya mada ambavyo hamvifahamu kuhusu kuingia katika maisha? Je, mioyo yenu inawaambia kitu chochote? Bado hamjui, je mwajua? Je, dada na ndugu wengine wamechagua mada gani? (Tungependa kusikia kuhusu kumjua Mungu.) Wengi wenu mmechagua kumjua Mungu. Hivyo tuendelee kufanya ushirika kuhusu kumjua Mungu.

Nyinyi nyote mna shauku ya kuisikia mada tutakayoifanyia ushirika, sivyo? Mada tutakayowasiliana kwa karibu leo pia inahusiana na mada ya "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote" ambayo tumekuwa tukizungumzia hivi karibuni. Tumeongea mengi kuhusu jinsi "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote," ambayo makusudi yake yalikuwa kutumia njia na mitazamo mbalimbali kuwaarifu watu jinsi Mungu anatawala juu ya vitu vyote, ni kwa njia gani Anavitawala vitu vyote, na ni kwa kanuni gani anavisimamia vitu vyote, ili kwamba viweze kuishi katika hii sayari Aliyoumba Mungu. Tulizungumza pia mengi kuhusu jinsi ambavyo Mungu anamkimu mwanadamu: ni kwa njia gani Mungu anamkimu mwanadamu, ni mazingira ya kuishi ya aina gani Mungu anampa mwanadamu, na ni kwa njia na nguvu gani Anampa mwanadamu mazingira thabiti ya kuishi. Japo Sikuzungumzia moja kwa moja uhusiano baina ya utawala wa Mungu juu ya vitu vyote, uendeshaji Wake wa vitu vyote na usimamizi Wake, kwa njia isiyokuwa ya moja kwa moja Nilisema ni kwa nini Anaviendesha vitu vyote namna hii, na ni kwa nini Anamkimu na kumlisha mwanadamu namna hii—yote ambayo yanahusu usimamizi wa Mungu. Maudhui tuliyoyazungumzia yalikuwa mengi na mapana—kuanzia mazingira makubwa hadi vitu vidogo zaidi kama mahitaji na lishe ya msingi ya wanadamu; kuanzia jinsi Mungu anaviongoza vitu vyote na kuvifanya vitende kazi kwa utaratibu, hadi kwenye mazingira ya kuishi sahihi na ya kufaa Aliyoyaumba kwa ajili ya watu wa kila jamii, na kadhalika. Haya maudhui mapana yanahusu jinsi mwanadamu anaishi katika mwili. Hivi ni kusema, yote yanahusiana na vitu katika ulimwengu halisi vinavyoonekana kwa macho ya kawaida, na ambavyo mwanadamu anaweza kuvihisi, kwa mfano, milima, mito, bahari, tambarare… Hivi vyote ni vitu vinavyoweza kuonekana na kuguswa. Nizungumzapo kuhusu hewa na halijoto, mnaweza kutumia pumzi zenu kuhisi moja kwa moja uwepo wa hewa, na miili yenu kuhisi kama halijoto iko juu au chini. Miti, nyasi, na ndege na wanyama porini, vitu vinavyopaa angani, na kutembea ardhini, na wanyama wadogo mbalimbali watokezao kutoka matunduni, vyote vinaweza kuonekana kwa wanadamu kwa macho yao wenyewe na kusikika kwa masikio yao wenyewe. Japo mawanda ya vitu kama hivyo ni mapana, miongoni mwa vitu vyote vinawakilisha tu ulimwengu halisi. Vitu yakinifu ni vitu ambavyo watu wanaweza kuviona na kuvihisi, yaani, ukivigusa, utavihisi, na macho yako yakiviona, ubongo wako utakupatia umbo, picha. Ni vitu ambavyo ni halisi na kweli; kwako si dhahania, bali vina umbo; vinaweza kuwa mraba, au duara, au virefu au vifupi; na kila kimoja kinakupa taswira tofauti. Vitu hivi vyote vinawakilisha sehemu ile yakinifu ya vitu vyote. Na hivi, "vitu vyote" katika "utawala wa Mungu juu ya vitu vyote" vinajumuisha nini kwa Mungu? Havijumuishi tu vitu ambavyo watu wanaweza kuona na kugusa, bali, vilevile, visivyoonekana na visivyoshikika. Hii ni mojawapo ya maana za kweli za utawala wa Mungu juu ya vitu vyote. Hata kama vitu hivi havionekani na havishikiki kwa watu, kwa Mungu, alimradi vinaweza kuonekana kwa jicho Lake na vipo ndani ya ukuu Wake, kwa hakika vipo. Hata kama, kwa mwanadamu, ni dhahania na visivyofikirika—na hata kama, aidha, havionekani na havishikiki—kwa Mungu kwa kweli na kwa uhalisi vipo. Huo ndio ulimwengu mwingine wa vitu vyote ambavyo Mungu anatawala, na ni sehemu nyingine ya mawanda mengine ambayo Anatawala. Hii ndiyo mada ambayo tutaifanyia ushirika leo—jinsi Mungu anatawala na kuuongoza ulimwengu wa kiroho. Kwa kuwa mada hii inagusia jinsi Mungu anatawala na kusimamia vitu vyote, inahusiana na ulimwengu ulio nje ya ulimwengu yakinifu—ulimwengu wa kiroho—na kwa hivyo ni muhimu sana kwetu kuuelewa. Ni baada tu ya kushiriki na kuelewa maudhui haya ndipo watu wanaweza kuelewa kwa hakika maana ya kweli ya maneno "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote." Hii ndiyo maana tutazungumzia mada hii. Na shabaha ya mada hii ni kukamilisha dhamira ya "Mungu anavitawala vitu vyote, na Mungu anavisimamia vitu vyote." Pengine, mtakapoisikia mada hii, inaweza kuonekana ni ya ajabu na isiyoaminika kwenu—lakini bila kujali mnavyohisi, kwa kuwa ulimwengu wa kiroho ni sehemu moja ya vitu vinavyotawaliwa na Mungu, ni sharti mjifunze kitu kuhusu mada hii. Baada ya kujifunza, mtakuwa na ufahamu wa kina, uelewa na maarifa kuhusu maneno "Mungu ni chanzo cha uhai kwa vitu vyote."

Jinsi Mungu Anavyotawala na Kuongoza Ulimwengu wa Kiroho

Kwa ulimwengu yakinifu, watu wakikosa kuelewa vitu au jambo fulani, wanaweza kutafuta taarifa mwafaka, vinginevyo wanaweza kutumia njia mbalimbali kubaini asili ya habari kuvihusu. Lakini inapokuja kwa ulimwengu huu mwingine ambao tunauzungumzia leo—ulimwengu wa kiroho ulio nje ya ulimwengu yakinifu—watu hawana hasa mbinu au njia za kujifunzia chochote kuuhusu. Mbona Ninasema hivi? Kwa sababu, katika ulimwengu wa mwanadamu, kila kitu cha ulimwengu yakinifu hakijitengi na uwepo wa kimwili wa mwanadamu, na kwa sababu watu wanahisi kwamba kila kitu katika ulimwengu yakinifu hakitenganishwi na maisha yao ya kimwili na uhai wao wa kimwili, watu wengi wanafahamu tu kuhusu, au kuona, vitu yakinifu mbele ya macho yao, vitu vinavyoonekana kwao. Bali inapokuja katika ulimwengu wa kiroho—yaani, kila kilicho cha ule ulimwengu mwingine—ni haki kusema kuwa watu wengi hawaamini. Hiyo ni kwa sababu hauonekani kwao, na wanaamini kuwa hakuna haja ya kuuelewa, au kujua kitu chochote kuuhusu, kutosema chochote jinsi huu ulimwengu wa kiroho ni ulimwengu tofauti kabisa na ulimwengu yakinifu. Kwa Mungu, uko dhahiri, lakini kwa mwanadamu umejificha na si dhahiri, na kwa hiyo watu wanakuwa na ugumu kupata njia ambayo kupitia kwayo wanaweza kuelewa vipengele mbalimbali vya ulimwengu huu. Vipengele tofauti ambavyo nitazungumzia kuhusu ulimwengu wa kiroho vinahusu utawala na ukuu wa Mungu tu. Sifichui miujiza, wala Siwaambii siri zozote mnazotaka kugundua, kwani hili linahusu ukuu wa Mungu, utawala wa Mungu, na riziki ya Mungu, na kwa hivyo Sitazungumzia tu sehemu ambayo ni muhimu nyinyi kuijua.

Kwanza, hebu Niwaulize swali: katika mawazo yenu, ulimwengu wa kiroho ni nini? Kuzungumza kwa ujumla, ni ulimwengu ulio nje ya ulimwengu yakinifu, ambao hauonekani na haushikiki na watu. Lakini kwa fikra zenu, ulimwengu wa kiroho unafaa uwe ulimwengu wa aina gani? Pengine, kwa sababu ya kutoweza kuuona, mnaweza kushindwa kuufikiria. Lakini mtakaposikia hadithi kuuhusu, bado mtafikiri, hamtaweza kujizuia nyinyi wenyewe. Na kwa nini Ninasema hili? Kuna kitu kinachowatokea watu wengi wanapokuwa wachanga: mtu akiwasimulia hadithi ya kuogofya—juu ya mazimwi, na roho—wanaogopeshwa kabisa. Na kwa nini wanaogopeshwa? Ni kwa kuwa wanavifikiria vitu hivyo; hata japo hawawezi kuviona, wanahisi kuwa vipo kila pembe ya chumba chao, vimejificha sehemu fulani, au sehemu fulani yenye giza, na wanaogopa sana kiasi kwamba hawawezi kuthubutu kulala. Hasa wakati wa usiku, hawathubutu kuwa chumbani peke yao, au uani peke yao. Huo ndio ulimwengu wa kiroho wa fikra zenu, na ni ulimwengu ambao watu hudhani unaogofya. Kwa kweli, kila mtu ana fikra fulani, na kila mtu anaweza kuhisi kitu.

Hebu tuanze na ulimwengu wa kiroho. Ulimwengu wa kiroho ni nini? Hebu Niwape maelezo mafupi na rahisi. Ulimwengu wa kiroho ni sehemu muhimu, ambayo ni tofauti na ulimwengu yakinifu. Na mbona Ninasema kwamba ni muhimu? Tutalizungumzia hili kwa kina. Uwepo wa huu ulimwengu wa kiroho umeungana na ulimwengu yakinifu wa mwanadamu kwa njia isiyoweza kufumbulika. Una jukumu katika mzunguko wa uhai na mauti wa mwanadamu katika utawala wa Mungu juu ya vitu vyote; hili ndilo jukumu lake, na sababu mojawapo inayofanya uwepo wake kuwa muhimu. Kwa sababu ni mahali ambapo hapawezi kutambuliwa kwa milango mitano ya fahamu ya mwanadamu, hakuna anayeweza kubaini kwa hakika kuwepo au kutokuwepo kwake. Shughuli za ulimwengu wa kiroho zimeunganika kikamilifu na uwepo wa mwanadamu, na kwa sababu hiyo jinsi mwanadamu anaishi inaongozwa kwa kiwango kikubwa na ulimwengu wa kiroho. Je, hili linahusiana na ukuu wa Mungu? Linahusiana. Nisemapo hili, unaelewa ni kwa nini Ninajadili mada hii; Kwa sababu inahusu ukuu wa Mungu, na utawala Wake. Katika ulimwengu kama huu—ulimwengu ambao hauonekani kwa watu—kila sheria yake ya peponi, amri na mfumo wake wa utawala ni wa juu zaidi kuliko sheria na mifumo ya nchi yoyote katika ulimwengu yakinifu, na hakuna kiumbe aishiye katika ulimwengu huu anaweza kuzivunja au kujitwalia bila haki. Je, hili linahusiana na ukuu na utawala wa Mungu? Katika ulimwengu huu kuna amri wazi za utawala, sheria wazi za mbinguni, na masharti wazi. Katika viwango tofauti na katika mawanda tofauti, wasimamizi huzingatia kikamilifu katika wajibu wao na kufuata sheria na masharti, kwa kuwa wanajua matokeo ya kukiuka sheria ya mbinguni ni yapi, wanafahamu wazi jinsi ambavyo Mungu anaadhibu maovu na kutuza mazuri, na kuhusu jinsi Anavyoviendesha vitu vyote, jinsi Anavyotawala vitu vyote, na zaidi, wanaona wazi ni jinsi gani Mungu anaendesha sheria za mbinguni na masharti Yake. Je, hizi ni tofauti na ulimwengu yakinifu unaokaliwa na wanadamu? Ni tofauti kwa kiasi kikubwa. Ni ulimwengu ambao ni tofauti kabisa na ulimwengu yakinifu. Kwa kuwa kuna sheria na masharti ya mbinguni, inahusu ukuu wa Mungu, utawala, aidha, tabia ya Mungu ya kile Anacho na alicho. Baada ya kusikia hili, hamhisi kwamba ni muhimu sana Mimi kuzungumzia hii mada? Hamtaki kujifunza siri zilizomo? (Ndiyo, tunataka.) Hiyo ndiyo dhana ya ulimwengu wa kiroho. Japo unapatikana sambamba na ulimwengu yakinifu, na wakati ule ule ukiwa chini ya utawala na ukuu wa Mungu, utawala na ukuu wa Mungu ya huu ulimwengu ni makali zaidi kuliko ulivyo ulimwengu yakinifu. Ikija katika maelezo, tunafaa tuanze na jinsi ulimwengu wa kiroho unawajibikia kazi ya mzunguko wa uhai na mauti ya mwanadamu, kwa kuwa kazi hii ni sehemu kuu ya viumbe wa ulimwengu wa kiroho.

Miongoni mwa wanadamu, Ninawaainisha watu katika aina tatu. Aina ya kwanza ni wasioamini, wale wasio na imani za kidini. Wanaitwa wasioamini. Wengi wa wasioamini wanaamini tu katika pesa, wanatafuta tu maslahi yao wenyewe, wana tamaa ya vitu, na wanaamini katika ulimwengu yakinifu, si katika mzunguko wa uhai na mauti au katika semi za miungu na mapepo. Ninawaainisha kama wasioamini na ni wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni watu mbalimbali wenye imani tofauti na wasioamini. Miongoni mwa wanadamu, Ninawagawa hawa wenye imani katika aina kuu kadhaa: Ya kwanza ni Wayahudi, wa pili ni Wakatoliki, ya tatu ni Wakristo, ya nne ni Waislamu, na ya tano ni wafuasi wa Budha—kuna aina tano. Hizi ndizo aina mbalimbali za watu wenye imani. Aina ya tatu ni wale wanaomwamini Mungu, inayohusiana nanyi. Waumini kama hawa ni wale wanaomfuata Mungu leo. Hawa watu wamegawanyika katika aina mbili. Wateule wa Mungu na watendaji huduma. Hizi aina kuu zimebainishwa wazi. Basi sasa, akilini mwenu mnaweza kutofautisha wazi aina na madaraja ya binadamu. Ya kwanza ni wasioamini—nimesema wasioamini ni watu gani. Je, wale wanaomwamini Mtu Mzee aliye Angani wanahesabika kama wasioamini? Wengi wa wasioamini wanamwamini yule Mzee aliye Angani; wanaamini kuwa upepo, mvua na radi vyote vinadhibitiwa na huyu Mzee aliye Angani, ambaye wanategemea kwa upanzi wa mimea na uvunaji wa mazao—bali kwa kutaja imani kwa Mungu wanapoteza hamu. Je, hii yaweza kuitwa imani kwa Mungu? Watu kama hao wanahesabiwa katika wasioamini. Mnaelewa hili, siyo? Msifahamu visivyo vikundi hivi. Aina ya pili ni watu wa imani. Aina ya tatu ni wale wanaomfuata Mungu leo. Na kwa nini Nimewagawa wanadamu wote katika aina hizi? (Kwa sababu wana vituo na hatima tofautitofauti.) Hicho ni kipengele kimoja. Kwa sababu, wakati haya matabaka na aina mbalimbali za watu wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, kila mmoja atakuwa na sehemu tofauti ya kuenda, watapitia sheria ya mzunguko tofauti wa uhai na mauti na hii ndiyo sababu Nimewaainisha wanadamu katika hizi aina kuu.

1. Mzunguko wa Uhai na Mauti wa Wasioamini

Hebu tuanze na mzunguko wa uhai na mauti wa wasioamini. Baada ya watu kufa, wanachukuliwa na msimamizi kutoka ulimwengu wa kiroho. Na ni kitu gani chao kinachukuliwa? Sio miili yao, bali ni roho zao. Roho zao zikichukuliwa, wanawasili katika sehemu ambayo ni ofisi ya ulimwengu wa kiroho, sehemu ambayo hasa hupokea roho za watu ambao wamekufa. (Kumbuka: sehemu ya kwanza wanapokwenda baada ya mtu yeyote kufa ni pageni kwa roho.) Wanapofikishwa mahali hapa, afisa anafanya ukaguzi wa kwanza, anathibitisha majina yao, anwani, na umri. Walichokifanya maishani mwao, Kila kitu walichokifanya maishani mwao kinanakiliwa kwenye kitabu na usahihi wake unahakikishwa. Baada ya kukaguliwa, matendo na mienendo ya mtu maishani mwake vinatumika kuamua ikiwa ataadhibiwa au ataendelea kupata mwili kama mwanadamu, ambayo ni hatua ya kwanza. Je, hii hatua ya kwanza inaogofya? Haiogopeshi sana, kwani kitu cha pekee kilichofanyika ni kwamba mtu amewasili katika mahali pa giza na pageni. Hilo halitishi sana.

Katika hatua ya pili, ikiwa mtu huyu amefanya mambo mengi mabaya maishani mwake, kama ametenda vitendo vingi viovu, basi atapelekwa mahali pa adhabu ili kuadhibiwa. Hiyo ndiyo itakuwa mahali ambapo kwa hakika ni kwa ajili ya adhabu ya watu. Maelezo kuhusu jinsi watakavyoadhibiwa yanategemea dhambi walizotenda, na ni vitendo vingapi viovu walitenda kabla hawajafa—ambalo ni tukio la kwanza kutokea katika hatua ya pili. Kwa sababu ya mambo waliyoyafanya, na maovu waliyoyafanya kabla hawajafa, wapatapo mwili baada ya adhabu yao—wazaliwapo upya tena katika ulimwengu yakinifu—watu wengine wataendelea kuwa wanadamu, na wengine watakuwa wanyama. Yaani, baada ya mtu kurudi katika ulimwengu wa kiroho, wanaadhibiwa kwa sababu ya maovu waliyotenda; zaidi, kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya, katika kupata mwili kwao kunakofuata hawawi wanadamu, ila watakuwa mnyama. Baadhi ya wanyama watakaokuwa ni ng’ombe, farasi, nguruwe, na mbwa. Watu wengine wanaweza kuwa ndege kule angani, au bata au bata bukini.… Baada ya kupata mwili kama mnyama, wanapokufa wanarudi katika ulimwengu wa kiroho, na sawa na mara ya kwanza, kutegemea mienendo yao kabla hawajafa, ulimwengu wa kiroho utaamua kama wapate mwili kama mwanadamu au la. Watu wengi hutenda maovu mengi sana, dhambi zao ni nzito sana, na kwa hivyo wapatapo mwili wanakuwa wanyama mara saba hadi mara kumi na mbili. Mara saba hadi mara kumi na mbili—hilo linaogopesha? (Linaogopesha.) Ni nini kinawaogopesha? Mtu kuwa mnyama, hilo linaogopesha. Na kwa mwanadamu, ni kipi cha uchungu zaidi kuhusu kuwa mnyama? Kutokuwa na lugha, kuwa tu na mawazo sahili, kuweza tu kufanya vitu ambavyo wanyama hufanya na kula vitu ambavyo wanyama hula, na kuwa na fikira sahili na kuwa na viziada lugha vya mnyama, kutoweza kutembea wima, kutoweza kuwasiliana na wanadamu, na mienendo yoyote na vitendo vya wanadamu kutokuwa na uhusiano na wanyama. Yaani, miongoni mwa vitu vyote, kuwa mnyama kunakufanya kuwa chini zaidi ya viumbe hai wote, na ni kuchungu zaidi kuliko kuwa mwanadamu. Hiki ni kipengele kimoja cha adhabu ya ulimwengu wa kiroho kwa wale waliofanya maovu mengi na kutenda dhambi kubwa. Ukali wa adhabu utakavyokuwa, hili hubainishwa na aina ya mnyama ambaye mtu anakuwa. Kwa mfano, kuwa nguruwe ni bora kuliko kuwa mbwa? Je, nguruwe huishi vizuri au vibaya kuliko mbwa? Vibaya zaidi, siyo?. Watu wakiwa ng’ombe au farasi, je, wataishi vizuri zaidi au vibaya kuliko nguruwe? (Vizuri zaidi.) Inaonekana mkipewa fursa, mnapenda ustaarabu. Je, ingekuwa faraja zaidi kama mtu angekuwa paka? Itakuwa faraja zaidi kuliko kuwa farasi au ng’ombe. Mngeweza kuchagua kati ya wanyama, mngechagua kuwa paka, na hiyo ni faraja zaidi kwa sababu mngeweza kuupitisha muda wenu mwingi usingizini. Kuwa ng’ombe au farasi ni kazi nzito, na kwa hivyo watu wakipata mwili na kuwa ng’ombe au farasi, wanapaswa kutia bidii—ambayo inaonekana kama adhabu nzito. Kuwa mbwa ni afadhali kidogo kuliko kuwa ng’ombe au farasi, kwa kuwa mbwa ana uhusiano wa karibu na bwana wake. Aidha, siku hizi watu wengi hufuga mbwa na baada ya miaka mitatu au mitano mbwa huyu huwa amejifunza kuelewa mengi ya yale wanasema! Kwa kuwa mbwa anaweza kuelewa maneno mengi ya bwana wake, ana uelewa mzuri wa bwana wake, na nyakati zingine anaweza kutohoa tabia na mahitaji kutoka bwana wake, kwa hiyo bwana anamtunza mbwa vyema, na mbwa anakula na kunywa vyema, na akiwa na maumivu anatunzwa zaidi—je, hivi mbwa hapati maisha ya furaha? Hivyo, kuwa mbwa ni bora kuliko kuwa ng’ombe au farasi. Katika hili, ukali wa adhabu ya mtu unaamua ni mara ngapi mtu anapata mwili kuwa mnyama, na anapata mwili kuwa aina gani ya mnyama. Mnaelewa, ndio?

Kwa sababu walitenda dhambi nyingi sana walipokuwa hai, watu wengine wataadhibiwa kwa kupatiwa miili kama wanyama mara saba hadi kumi na mbili. Baada ya kuadhibiwa vya kutosha, wanaporudi katika ulimwengu wa kiroho wanapelekwa mahali pengine. Roho mbalimbali mahali hapa zimeadhibiwa tayari, na ni aina ya roho ambazo ziko tayari kupata mwili kama wanadamu. Mahali hapa panaziainisha roho katika makundi kulingana na aina ya familia watakamozaliwa, ni aina gani ya nafasi watashikilia baada ya kupata mwili, na kadhalika. Kwa mfano, watu wengine watakuwa waimbaji wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa waimbaji; wengine watakuwa wafanyabiashara wakija katika ulimwengu huu, na kwa hivyo wanawekwa miongoni mwa wafanyabiashara; na ikiwa mtu atakuwa mtafiti wa kisayansi akiwa mwanadamu, basi anawekwa miongoni mwa watafiti wa kisayansi. Baada ya kuwekwa katika makundi, kila mmoja anatumwa kulingana na wakati tofauti na tarehe iliyowekwa, sawa tu na jinsi watu hutuma barua pepe siku hizi. Katika hili kutakuwa kumekamilika mzunguko mmoja wa uhai na mauti. Tangu siku mtu anawasili katika ulimwengu wa kiroho hadi wakati adhabu yao inakamilika, wanaweza kupata mwili kama wanyama mara nyingi, halafu wajitayarishe kupata mwili kama wanadamu; huu ni mchakato mzima.

Na wale waliokamilisha adhabu yao, na hawajapata mwili kuwa wanyama, je, watapelekwa kwa haraka katika ulimwengu yakinifu kuwa wanadamu? Au watachukua muda gani ndipo waje miongoni mwa wanadamu? Ni kwa haraka gani hawa watu watakuwa wanadamu[a]? Kwa hili kuna mipaka ya kiwakati. Kila kitu kinachofanyika katika ulimwengu huu wa kiroho kinapitia mipaka ifaayo kiwakati na sheria—ambayo, Nikiieleza kutumia tarakimu, mtaelewa. Kwa wapatao mwili baada ya muda mfupi, wakati wanapokufa kuzaliwa kwao upya kama wanadamu kutatayarishwa. Wakati mfupi zaidi ni siku tatu. Kwa watu wengine, ni miezi mitatu, kwa wengine ni miaka mitatu, kwa wengine ni miaka thelathini, kwa wengine ni miaka mia tatu, kwa wengine hata ni miaka elfu tatu, na kadhalika. Hivyo basi ni nini kinaweza kusemwa kuhusu hizi sheria za kiwakati, na vipimo vyake ni vipi? Kuwasili kwa roho katika ulimwengu yakinifu, ulimwengu wa mwanadamu, kunategemea uhitaji: inalingana na nafasi itakayochukuliwa na hii roho duniani. Watu wakipata mwili kama wanadamu wa kawaida, wengi wao wanapewa mwili haraka sana, kwa sababu dunia ya wanadamu ina uhitaji mkubwa wa watu wa kawaida kama hao, na kwa hiyo siku tatu baadaye wanatumwa tena katika familia ambayo ni tofauti kabisa na ile waliyokuwa kabla hawajafa. Lakini wapo ambao wana nafasi maalum katika ulimwengu huu. "Maalum" inamaanisha kuwa hakuna uhitaji mkubwa wa hawa watu katika ulimwengu wa wanadamu; si watu wengi wanaohitajika kuishikilia nafasi hiyo, kwa hiyo basi inaweza kuwa miaka mia tatu kabla hawajapata mwili[b]. Ambako ni kusema, hii roho itakuja mara moja tu katika kila miaka mia tatu, au hata mara moja kila baada ya miaka elfu tatu. Na ni kwa nini hivi? Ni kwa sababu kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu, nafasi hiyo haihitajiki katika dunia ya mwanadamu, na kwa hiyo wanatunzwa mahali fulani katika ulimwengu wa kiroho. Tazama Confucius, kwa mfano. Alikuwa na athari kubwa katika utamaduni wa jadi wa Uchina. Kuwasili kwake kulikuwa na athari kubwa kwenye utamaduni, elimu, desturi, na kufikiri kwa watu wa wakati ule. Lakini mtu kama huyu hahitajiki katika kila enzi, na kwa hiyo alilazimika kubaki katika ulimwengu wa kiroho, akisubiri huko kwa miaka mia tatu au miaka elfu tatu kabla ya kupata mwili. Kwa kuwa ulimwengu wa mwanadamu haukuhitaji mtu kama huyu, alilazimika kusubiri bila kufanya chochote, kwa kuwa kulikuwa na nafasi chache sana kama yake, kulikuwa na machache ya yeye kufanya, na hivyo basi alitunzwa sehemu fulani katika ulimwengu wa kiroho kwa muda mrefu, bila kufanya chochote, na kutumwa wakati ambapo ulimwengu wa mwanadamu ulimhitaji. Hizo ndizo sheria za kiwakati za milki ya kiroho kuhusu haraka ambayo watu wengi wanapata miili. Iwe ni mtu wa kawaida au maalum, ulimwengu wa kiroho una sheria mwafaka na desturi sahihi kwa utayarishaji wa watu kupata mwili, na hizi sheria na desturi hutoka kwa Mungu, zinatumwa kutoka kwa Mungu, na haziamuliwi au kudhibitiwa na msimamizi yeyote au kiumbe chochote katika ulimwengu wa kiroho. Sasa mnaelewa, naam?

Tanbihi:

a. Makala asilia yameacha "ambacho kwacho hawa watu huwa wanadamu."

b. Makala asilia yameacha "kabla hawajapata mwili."

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji