Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II

(Sehemu ya Sita)

Ushuhuda wa Ayubu Wamliwaza Mungu

Nikiwaambia sasa kwamba Ayubu ni mtu mzuri, huenda msiweze kutambua maana iliyo katika maneno haya, na huenda msiweze kung’amua mawazo yaliyofanya Nizungumze maneno haya yote; lakini subirini mpaka siku ile mtakapokuwa mmepitia majaribu sawa na au yale yanayofanana na yale ambayo Ayubu alipitia, wakati mtakapokuwa mmepitia magumu, wakati mtakapokuwa mmepitia majaribu yaliyopangiliwa kwa ajili yenu na Mungu mwenyewe, wakati utakapojitolea kila kitu ulicho nacho, na kuvumilia udhalilishaji na ugumu ili uweze kumshinda Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu katikati ya vishawishi hivi vyote—basi utaweza kutambua maana ya maneno haya Ninayoyaongea. Wakati huo, utahisi kwamba wewe ni duni kuliko Ayubu, utahisi namna Ayubu alivyo mzuri na kwamba anastahili kuigwa; wakati huo utakapowadia, utatambua namna ambavyo maneno yale yaliyo bora yaliyozungumzwa na Ayubu yalivyo muhimu kwa yule aliyepotoka na anayeishi katika nyakati hizi, na utatambua namna ilivyo vigumu kwa watu wa leo kuweza kutimiza kile ambacho Ayubu alitimiza. Unapohisi kuwa ni vigumu, utatambua na kuona namna ambavyo moyo wa Mungu una dukuduku na wasiwasi, utatambua namna gharama aliyolipa Mungu kuwapata watu kama hao ilivyo ya juu, na jinsi kile ambacho Mungu hufanya na kutumia kwa ajili ya mwanadamu kilivyo cha thamani. Kwa sababu sasa mmeyasikia maneno haya, je, mnao ufahamu sahihi na ukadiriaji wa kweli kuhusu Ayubu? Machoni penu, je, Ayubu alikuwa kweli mtu mtimilifu na mnyofu aliyemcha Mungu na kujiepusha na maovu? Nasadiki kwamba watu wengi bila shaka watasema ndiyo. Kwani ukweli kuhusu kile ambacho Ayubu alitenda na kufichua hakiwezi kupingwa na binadamu yeyote au Shetani. Hivyo ndivyo thibitisho la nguvu zaidi kuhusu ushindi wa Ayubu dhidi ya Shetani. Thibitisho hili lilitolewa katika Ayubu, na ndio ushuhuda wa kwanza uliopokelewa na Mungu. Hivyo, Ayubu aliposhinda vishawishi vya Shetani na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, Mungu aliona tumaini kwake Ayubu, na moyo wake uliliwazwa na Ayubu. Tangu wakati wa uumbaji mpaka wakati wa Ayubu, huu ndio ulikuwa wakati wa kwanza ambao Mungu kwa kweli alipitia na kujua kuliwazwa kulikuwa nini, na kuliwazwa na mwanadamu kulimaanisha nini. Huo ndio ulikuwa wakati wa kwanza ambao Alikuwa ameona, na kupata ushuhuda wa kweli uliotokana na Yeye.

Ninaamini kwamba, baada ya kuusikia ushuhuda wa Ayubu na simulizi za vipengele mbalimbali vya Ayubu, watu wengi watakuwa na mipango ya njia iliyo mbele yao. Hivyo, pia, Ninaamini kwamba watu wengi zaidi walio na wasiwasi na woga wataanza kwa utaratibu kuwa watulivu katika mwili na akili zao, na wataanza kuhisi tulizo, hatua kwa hatua …

Vifungu vilivyo hapa chini ni simulizi pia kumhusu Ayubu. Acha tuendelee kusoma.

4. Ayubu Asikia Kuhusu Mungu Kupitia Kusikiliza kwa Sikio

Ayubu 9:11 Ona, Anapita karibu na mimi, na Simwoni: Anapita kwenda mbele pia, lakini siwezi kumwona.

Ayubu 23:8-9 Tazama, nasonga mbele, lakini hayuko huko; na nyuma, lakini siwezi kumwona: Kwa mkono wa kushoto, ambapo Yeye hufanya kazi, lakini siwezi kumwona: Yeye hujificha Mwenyewe katika mkono wa kulia, kiasi kwamba siwezi kumwona.

Ayubu 42:2-6 Najua ya kwamba Wewe unaweza kufanya kila kitu, na ya kwamba hakuna wazo linaloweza kuzuilika kutoka Kwako. Ni nani yeye anayeficha ushauri bila maarifa? hivyo, nimesema neno nisilolifahamu; vitu vilivyo vya ajabu sana kwangu, ambavyo nisivyovijua. Sikiza, nakusihi, nami nitazungumza: Nitauliza kutoka Kwako, Nawe useme kwangu. Nimesikia kukuhusu kwa kusikia na masikio: lakini sasa jicho langu lakuona. Ndiyo sababu najichukia, na kutubu kwenye mavumbi na majivu.

Ingawa Mungu Hajajifichua kwa Ayubu, Ayubu Anauamini Ukuu wa Mungu

Nguvu za maneno haya ni nini? Je, Yupo yeyote aliyetambua kwamba kunao ukweli hapa? Kwanza, ni vipi ambavyo Ayubu alijua kwamba Mungu yupo? Kisha, ni vipi alivyojua kwamba mbingu na ardhi na mambo yote yanatawaliwa na Mungu? Kunacho kifungu kinachojibu maswali haya mawili: “Nimesikia kukuhusu kwa kusikia na masikio: lakini sasa jicho langu lakuona. Ndiyo sababu najichukia, na kutubu kwenye mavumbi na majivu” (Ayubu 42:5-6). Kutokana na maneno haya tunajifunza kwamba, badala ya kumwona Mungu kwa macho yake mwenyewe, Ayubu alikuwa amejifunza kuhusu Mungu kutoka kwa hekaya. Ni katika hali hizi ndipo alipoanza kuitembea njia ya kumfuata Mungu, na baadaye akathibitisha uwepo wa Mungu katika Maisha yake, na kati ya mambo yote. Kunao ukweli usiopingika hapa—ukweli huo ni upi? Licha ya kuweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu. Katika haya, hakuwa sawa na watu wa leo? Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, matokeo yake ni kwamba ingawa alikuwa amewahi kumsikia Mungu, hakujua ni wapi Mungu alikuwa, au ni vipi Mungu alifanana, au ni nini ambacho Mungu alikuwa akifanya. Haya yote ni mambo ambayo ni ya kibinafsi; tukiongea bila mapendeleo, ingawa alimfuata Mungu, Mungu alikuwa hajawahi kumwonekania yeye au kumzungumzia yeye. Je, huu si ukweli? Ingawa Mungu alikuwa hajaongea na Ayubu au kumpa amri zozote, Ayubu alikuwa ameuona uwepo wa Mungu na kutazama ukuu Wake miongoni mwa mambo yote, na katika hekaya ambazo kwazo Ayubu alikuwa amesikia kumhusu Mungu kwa kusikia kwa sikio, na baadaye alianza maisha ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Hizi ndizo zilizokuwa asili na mchakato ambao Ayubu alimfuata Mungu. Lakini haikujalisha ni vipi alivyomcha Mungu na kujiepusha na maovu, ni vipi ambavyo alishikilia uadilifu wake, bado Mungu alikuwa hajawahi kujitokeza kwake. Hebu tukisome kifungu hiki. Alisema, “Ona, Anapita karibu na mimi, na simwoni: Anapita kwenda mbele pia, lakini siwezi kumwona” (Ayubu 9:11). Yale ambayo maneno haya yanasema ni kwamba Ayubu huenda alihisi Mungu karibu naye au pengine hakuhisi—lakini alikuwa hajawahi kuweza kumwona Mungu. Kunazo nyakati ambapo alifikiria Mungu akipita mbele yake au akitenda, au akimwongoza binadamu, lakini alikuwa hajawahi kujua. Mungu humjia binadamu wakati ambapo hatarajii; binadamu hajui ni lini Mungu atamjia, au ni wapi anapomjia yeye, kwa sababu binadamu hawezi kumwona Mungu, kwa hivyo, kwa binadamu Mungu amejificha kutoka kwake.

Imani ya Ayubu Katika Mungu Haitikisiki Kwa Sababu ya Ukweli Kwamba Mungu Amejificha Kutoka Kwake

Katika kifungu kifuatacho cha maandiko, Ayubu anasema, “Tazama, nasonga mbele, lakini Hayuko huko; na nyuma, lakini siwezi kumwona: Kwa mkono wa kushoto, ambapo Yeye hufanya kazi, lakini siwezi kumwona: Yeye hujificha katika mkono wa kulia, kiasi kwamba siwezi kumwona” (Ayubu 23:8-9). Katika simulizi hii, tunajifunza kwamba katika hali alizopitia Ayubu, Mungu alikuwa Amejificha kutoka kwake wakati wote huo; Mungu alikuwa hajajitokeza waziwazi kwake, na alikuwa hajamzungumzia waziwazi maneno yoyote, lakini katika moyo wake Ayubu alikuwa na ujasiri wa uwepo wa Mungu. Alikuwa siku zote ameamini kwamba Mungu huenda anatembea na yeye au huenda Anatenda akiwa kando yake, na kwamba ingawa hakuweza kumwona Mungu, Mungu alikuwa kando yake Akitawala mambo yote kumhusu yeye. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu, lakini aliweza kuwa mkweli katika imani yake, jambo ambalo hakuna mtu yeyote aliwahi kuweza kufanya. Kwa nini watu wengine wasiweze kufanya hivyo? Ni kwa sababu Mungu hakuongea na Ayubu au kumwonekania, na asingekuwa ameamini kwa kweli, asingeweza kuendelea, wala asingeweza kushikilia njia hiyo ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, huu si ukweli? Unahisi vipi unaposoma kumhusu Ayubu akisema maneno haya? Unahisi kwamba utimilifu na unyofu wa Ayubu, na haki yake mbele ya Mungu, ni kweli, na wala si kupiga chuku kwa upande wa Mungu? Ingawa Mungu alimshughulikia Ayubu kwa njia sawa na watu wengine, na hakujitokeza wala kuongea na yeye, Ayubu bado alishikilia uadilifu wake, bado aliamini ukuu wa Mungu, na, isitoshe, mara kwa mara alitoa sadaka za kuteketezwa na kuomba mbele ya Mungu kutokana na hofu yake ya kumkosea Mungu. Katika uwezo wa Ayubu wa kumcha Mungu bila ya kuwahi kumwona Mungu, tunaona ni kiasi kipi alichopenda mambo mazuri na ni vipi imani yake ilivyokuwa thabiti na ya kweli. Hakukana uwepo wa Mungu kwa sababu Mungu alikuwa amejificha kutoka kwake, wala hakupoteza imani yake na kumkataa Mungu kwa sababu hakuwahi kumwona Yeye. Badala yake, katikati ya kazi fiche ya Mungu ya kutawala mambo yote, alikuwa ametambua uwepo wa Mungu na akahisi ukuu wa Mungu na Nguvu za Mungu. Hakukata tamaa katika kuwa mnyofu kwa sababu Mungu alikuwa amejificha, wala hakuiacha njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu kwa sababu Mungu alikuwa hajawahi kumwonekania. Ayubu alikuwa hajawahi kuuliza kwamba Mungu aonekane waziwazi kwake ili kuthibitisha uwepo Wake, kwani alikuwa tayari ametangaza ukuu wa Mungu miongoni mwa mambo yote na aliamini kwamba alikuwa amepata baraka na neema ambazo wengine hawakuwa wamepata. Ingawa Mungu alibakia amejificha kutoka kwake, imani ya Ayubu kwa Mungu haikuwahi kutikisika. Hivyo, alivuna kile ambacho hakuna yeyote aliwahi kuvuna. Kibali cha Mungu na baraka za Mungu.

Ayubu Alibariki Jina la Mungu na Hafikirii Baraka au Janga

Kunao ukweli ambao haurejelewi katu kwenye hadithi za maandiko kuhusu Ayubu, na ukweli huu ndio utakaokuwa lengo letu leo. Ingawa Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu kwa masikio yake mwenyewe, Mungu alikuwa na nafasi katika moyo wa Ayubu. Mtazamo wa Ayubu kwa Mungu ulikuwa upi? Ulikuwa, kama ulivyorejelewa awali, “jina la Yehova libarikiwe.” Baraka yake kwa jina la Mungu haikuwa ya masharti, pasipo kujali muktadha, na bila kushurutishwa na sababu yoyote. Tunaona kwamba Ayubu alikuwa ameukabidhi moyo wake kwa Mungu, na kuuruhusu udhibitiwe na Mungu; kila kitu alichofikiria, kila kitu alichoamua, na kila kitu alichopanga katika moyo wake kilikuwa wazi kwa Mungu na wala moyo wake haukuwa umefungwa kuzuia Mungu. Moyo wake haukumpinga Mungu, na hakuwahi kuuliza Mungu kumfanyia chochote au kumpa chochote yeye, na wala hakuwa na matamanio yasiyo ya kawaida kwamba angepata chochote kutokana na yeye kumwabudu Mungu. Ayubu hakuzungumzia mabadilishano na Mungu, na wala hakutoa ombi lolote au madai yoyote kwa Mungu. Kulisifu kwake jina la Mungu kulikuwa kwa sababu ya nguvu kuu na mamlaka ya Mungu katika kutawala mambo yote, na haikutegemea kama alipata baraka au alipigwa na janga. Aliamini kwamba haijalishi kama Mungu anawabariki watu au analeta janga kwao, mamlaka na nguvu vyote havitabadilika, na hivyo, haikujalisha hali za mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Kwamba binadamu amebarikiwa na Mungu ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu, na janga linapompata mwanadamu, hivyo, pia ni kwa sababu ya ukuu wa Mungu. Nguvu na mamlaka ya Mungu vyote vinatawala na kupangilia kila kitu kumhusu mwanadamu; matukio yasiyo ya kawaida kuhusu utajiri wa binadamu ni maonyesho ya nguvu na mamlaka ya Mungu, na licha ya maoni yake mtu, jina la Mungu linafaa kusifiwa. Haya ndiyo ambayo Ayubu alipitia na kuishia kujua katika miaka ya maisha yake. Fikira na matendo yote ya Ayubu vyote vilifikia masikio ya Mungu na vikawasili mbele ya Mungu, na vikaonekana kuwa muhimu na Mungu. Mungu aliyapenda sana maarifa haya ya Ayubu na akamthamini sana Ayubu kwa kuwa na moyo kama huo. Moyo huu ulisubiria amri ya Mungu siku zote, na pahali pote, na haijalishi ni muda au mahali gani palipokaribisha chochote kile kilichomsibu. Ayubu hakutoa mahitaji yoyote kwa Mungu. Kile alichohitaji kutoka kwake kilikuwa kusubiria, kukubali, kukabiliana na kutii mipangilio yote iliyotoka kwa Mungu; Ayubu aliamini hili kuwa wajibu wake, na ndicho hasa kile ambacho Mungu Alitaka. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu wala kumsikiliza Akiongea mambo yoyote, akitoa amri zozote, akiyatoa mafundisho yoyote, au kumwelekeza kuhusu chochote. Kwa maneno ya leo, yeye kuweza kumiliki mtazamo kama huo kwa Mungu, wakati Mungu alikuwa hajampa nuru, mwongozo, au toleo kuhusiana na ukweli—hili lilikuwa lenye thamani sana, na kwake yeye kuonyesha mambo kama hayo kulitosha kwa Mungu, na ushuhuda wake ulipongezwa na Mungu, na kutunzwa na Mungu. Ayubu alikuwa hajawahi kumwona Mungu au kumsikia Mungu binafsi akitamka mafundisho yoyote kwake yeye, lakini kwa Mungu moyo wake na yeye mwenyewe vyote vilikuwa vyenye thamani zaidi kuliko wale watu ambao, mbele ya Mungu waliweza tu kuongea kuhusiana na nadharia kuu, ambao waliweza tu kujigamba na kuongea kuhusu kutoa sadaka lakini walikuwa hawajawahi kuwa na maarifa ya kweli ya Mungu na walikuwa hawajawahi kumcha Mungu kwa kweli. Kwa kuwa moyo wa Ayubu ulikuwa safi, na haukufichwa kuonekana na Mungu, na ubinadamu wake ulikuwa wenye uaminifu na ukarimu, na alipenda haki na kile kilichokuwa kizuri. Binadamu kama huyu pekee aliyemiliki moyo kama huo na ubinadamu ndiye aliyeweza kufuata njia ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Binadamu kama huyo angeona ukuu wa Mungu, angeona mamlaka na nguvu Yake, na angeweza kutimiza utiifu kwa ukuu Wake na mipangilio. Binadamu tu kama huyo ndiye angeweza kulisifu jina la Mungu kwa kweli. Hii ni kwa sababu hakuangalia kama Mungu angembariki au Angemletea janga, kwa sababu alijua kwamba kila kitu kinadhibitiwa na mkono wa Mungu, na kwamba binadamu kuwa na wasiwasi ni ishara ya ujinga, kutojua, na kutoweza kufikiria vyema, kuwa na shaka kuhusu ukweli wa ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, na ya kutomcha Mungu. Maarifa ya Ayubu hasa ndiyo ambayo Mungu alitaka. Hivyo basi, Ayubu alikuwa na maarifa makubwa ya kinadharia kumhusu Mungu kuliko ninyi? Kwa sababu kazi na matamko ya Mungu wakati huo yalikuwa machache, halikuwa jambo rahisi kutimiza maarifa ya Mungu. Mafanikio kama hayo ya Ayubu hayakuwa jambo dogo. Alikuwa hajapitia kazi ya Mungu wala kuwahi kumsikia Mungu akiongea, au kuuona uso wa Mungu. Kwamba aliweza kuwa na mtazamo kama huo kwa Mungu yalikuwa hasa matokeo ya ubinadamu wake na ufuatiliaji wake binafsi, ubinadamu na ufuatiliaji ambao watu hawana leo. Hivyo, katika enzi hiyo, Mungu alisema, “Hakuna mtu ambaye yuko kama yeye ulimwenguni, mtu aliye mkamilifu na mwaminifu.” Katika enzi hiyo, Mungu alikuwa tayari amefanya ukadiriaji wa aina hiyo kumhusu Ayubu, na Alikuwa amefikia hitimisho kama hilo. Ungekuwa ukweli zaidi kwa kiasi kipi hii leo?

Ingawa Mungu Amejificha Kutoka kwa Mwanadamu, Matendo Yake Miongoni mwa Mambo Yote Yanatosha Binadamu Kumjua Yeye

Ayubu alikuwa hajauona uso wa Mungu, wala kusikia matamshi yaliyoongelewa na Mungu, na sembuse yeye kuipitia kazi ya Mungu, lakini kumcha kwake Mungu na ushuhuda aliokuwa nao wakati wa majaribu unashuhudiwa na kila mmoja, na unapendwa, unafurahiwa, na kupongezwa na Mungu na watu wanayaonea wivu na kuvutiwa nayo, na hata zaidi ya hayo, wanaimba sifa zao. Hakukuwepo chochote kikubwa au kisicho cha kawaida kuhusu maisha yake: Kama vile tu mtu yeyote wa kawaida, aliishi maisha yasiyo ya kina, akienda kufanya kazi wakati wa macheo na akirudi nyumbani kupumzika wakati wa magharibi. Tofauti ni kwamba wakati wa miongo mbalimbali ya maisha yake isiyo ya ajabu, alipata maono kuhusu njia ya Mungu, na akatambua na kuelewa nguvu kubwa na ukuu wa Mungu kuliko mtu yeyote mwingine. Hakuwa mwerevu zaidi kuliko mtu yeyote wa kawaida, maisha yake hayakuwa sanasana yenye ushupavu, wala, aidha, yeye hakuwa na mbinu maalum zisizoonekana. Kile alichomiliki, hata hivyo, kilikuwa ni hulka iliyokuwa na uaminifu, upole na unyofu, na hulka iliyopenda kutopendelea, haki, na iliyopenda mambo chanya—hakuna kati ya mambo haya yanayomilikiwa na watu wengi wa kawaida. Alitofautisha kati ya upendo na chuki, alikuwa na hisia ya haki, hakukubali kushindwa na alikuwa hakati tamaa, na alikuwa mwangalifu sana katika kufikiria kwake. Hivyo, wakati wake usio wa ajabu duniani aliyaona mambo yote yasiyo ya kawaida ambayo Mungu alikuwa amefanya, na aliuona ukubwa, utakatifu, na kuwa na haki kwa Mungu, aliona kujali kwa Mungu, neema yake, na ulinzi wake wa binadamu, na aliuona utukufu na mamlaka ya Mungu mkuu zaidi. Sababu ya kwanza iliyomfanya Ayubu aweze kupata mambo haya yaliyokuwa zaidi ya mtu yeyote wa kawaida ilikuwa kwamba alikuwa na moyo safi, na moyo wake ulimilikiwa na Mungu na kuongozwa na Muumba. Sababu ya pili ilikuwa ni ufuatiliaji wake: ufuatiliaji wake wa kuwa maasumu na mtimilifu, na wa kuwa mtu aliyekubaliana na mapenzi ya Mbinguni, aliyependwa na Mungu, na aliyejiepusha na uovu. Ayubu alimiliki na kufuatilia mambo haya huku akiwa hawezi kumwona Mungu au kusikia maneno ya Mungu; ingawa alikuwa hajawahi kumwona Mungu, alikuwa amejua mbinu ambazo kwazo Mungu alitawala mambo yote, na kuelewa hekima ambayo Mungu anatumia ili kufanya hivyo. Ingawa alikuwa hajawahi kusikia maneno ambayo yalikuwa yametamkwa na Mungu, Ayubu alijua kwamba matendo ya kutuza binadamu na kuchukua kutoka kwa binadamu yote yalitoka kwa Mungu. Ingawa miaka ya maisha yake haikuwa tofauti na ile ya mtu wa kawaida, hakuruhusu kutokuwa wa ajabu kwa maisha yake kuathiri maarifa yake ya ukuu wa Mungu juu ya mambo yote, au kuathiri kufuata kwake kwa njia za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Machoni pake, sheria za mambo yote zilijaa matendo ya Mungu na ukuu wa Mungu ungeweza kuonekana katika sehemu yoyote ya maisha ya mtu. Hakuwa amemwona Mungu lakini aliweza kutambua kwamba Matendo ya Mungu yako kila pahali, na katika wakati wake usiokuwa wa ajabu duniani, katika kila kona ya maisha yake aliweza kuona na kutambua matendo ya kipekee na ya maajabu ya Mungu, na aliweza kuona mipangilio ya ajabu ya Mungu. Ufiche na kimya cha Mungu havikuzuia utambuzi wa Ayubu wa matendo ya Mungu, wala havikuathiri maarifa yake kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote. Maisha yake yalikuwa utambuzi, katika maisha yake ya kila siku, wa ukuu na mipangilio ya Mungu, ambaye Amejificha miongoni mwa mambo yote. Katika maisha yake ya kila siku alisikia pia na kuelewa sauti ya moyo wa Mungu na maneno ya Mungu, akiwa kimya miongoni mwa mambo yote lakini anaonyesha sauti ya moyo Wake na maneno kwa kutawala sheria ya mambo yote. Unaona, basi, kwamba kama watu wanao ubinadamu sawa na ufuatiliaji kama Ayubu, basi wanaweza kupata utambuzi na maarifa sawa kama Ayubu, na kupata ule ufahamu na maarifa sawa kuhusu ukuu wa Mungu juu ya mambo yote kama Ayubu. Mungu hakuwa amemwonekania Ayubu au kuongea na yeye, lakini Ayubu aliweza kuwa mtimilifu na mnyofu, na pia aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa maneno mengine, bila ya Mungu kumwonekania au kuongea na binadamu, matendo ya Mungu miongoni mwa mambo yote na ukuu Wake juu ya mambo yote yanatosha kwa mwanadamu ili kuweza kuwa na ufahamu wa uwepo, nguvu na mamlaka ya Mungu, nguvu na mamlaka ya Mungu yanatosha kumfanya mwanadamu afuate njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kwa sababu mwanadamu wa kawaida kama vile Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi kila mtu wa kawaida anayemfuata Mungu anafaa pia kuweza kufanya hivyo. Ingawa maneno haya yanaweza kusikika kana kwamba ni hitimisho la kimantiki, hili halikiuki sheria ya mambo. Bado ukweli haujalingana na matarajio: Kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, kunaweza kuonekana, ni hifadhi ya Ayubu na Ayubu pekee. Kwa kutaja “kumcha Mungu na kujiepusha na maovu,” watu hufikiri kwamba hii inafaa tu kufanywa na Ayubu, ni kana kwamba njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu ilikuwa imebandikwa jina la Ayubu na haikuhusiana na watu wengine. Sababu ya hili ni wazi: Kwa sababu Ayubu tu ndiye aliyemiliki hulka iliyokuwa na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na iliyopenda kutopendelea na haki na mambo yaliyokuwa mazuri, hivyo ni Ayubu tu ambaye angeweza kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Lazima nyinyi nyote muwe mmeelewa matokeo hapa—kwa sababu hakuna yule anayemiliki ubinadamu ulio na uaminifu, ukarimu, na unyofu, na ule ambao unapenda kutopendelea na haki na ule ambao ni mzuri, hakuna mtu anayeweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, na hivyo watu hawawezi kamwe kupata furaha ya Mungu au kusimama imara katikati ya majaribu. Hii pia inamaanisha kwamba, bila kujumuisha Ayubu, watu wote wangali wamefungwa na kutegwa na Shetani; wote wanashtakiwa, wanashambuliwa, na kudhulumiwa na yeye. Wao ndio wale ambao Shetani anajaribu kumeza, na wote hawana uhuru, ni wafungwa ambao wametekwa nyara na Shetani.

Kama Moyo wa Mwanadamu Una Uadui na Mungu, Mwanadamu Anawezaje Kumcha Mungu na Kujiepusha na Maovu?

Kwa sababu watu wa leo hawamiliki ubinadamu sawa na Ayubu, sembuse kiini cha asili yao, na mtazamo wao kwa Mungu? Wanamcha Mungu? Wanajiepusha na maovu? Wale wasiomcha Mungu na kujiepusha na maovu wanaweza kujumuishwa tu kwa maneno matatu: “adui wa Mungu.” Mara nyingi ninyi husema maneno haya matatu, lakini hamjawahi kujua maana yake halisi. Maneno “ni adui wa Mungu” yanayo kiini ndani yake: Hayasemi kwamba Mungu anamuona mwanadamu kama adui, lakini kwamba binadamu anamuona Mungu kama adui. Kwanza, watu wanapoanza kumwamini Mungu, ni yupi kati yao asiyekuwa na nia, motisha na tabia yake binafsi ya makuu? Ingawa sehemu moja yao inaamini uwepo wa Mungu, na imeona uwepo wa Mungu, imani yao katika Mungu bado ina hiyo motisha, na nia yao kuu ya kumwamini Mungu ni kupokea baraka Zake na vitu wanavyotaka. Katika uzoefu wa watu katika maisha yao, mara nyingi wao hufikiria, nimetoa familia yangu na ajira yangu kwa Mungu, na Amenipa nini? Lazima niongezee na kuthibitisha haya—je, nimepokea baraka zozote hivi majuzi? Nimetoa mengi sana wakati huu, nimekimbia na kukimbia na kuteseka sana—je, Mungu amenipa ahadi zozote baada ya haya? Je, Amekumbuka matendo yangu mazuri? Mwisho wangu utakuwa vipi? Ninaweza kuzipokea baraka za Mungu? … Kila mtu kila wakati hufanya hesabu kama hizi ndani ya moyo wake, na yeye hutoa madai yake kwa Mungu yanayoonyesha motisha yake, malengo na mawazo ya mabadilishano. Hii ni kusema, ndani ya moyo wake mwanadamu siku zote humweka Mungu majaribuni, siku zote anaunda njama kumhusu Mungu, akijitetea kwa Mungu kila wakati kwa sababu ya mwisho wake binafsi na kujaribu kumfanya Mungu atoe kauli, aweze kuona kama Mungu anaweza kumpa kile anachotaka au la. Wakati huohuo akimfuata Mungu, binadamu hamchukulii Mungu kama Mungu. Siku zote mwanadamu amejaribu kufanya mipango na Mungu, akitoa madai bila kusita kwake Yeye na hata akimsukuma Yeye katika kila hatua, akijaribu kupiga hatua ya maili licha ya kupewa inchi moja. Wakati huohuo akijaribu kufanya mabadilishano na Mungu, binadamu pia anabishana na Yeye, na wapo hata watu ambao, wakati majaribu yanawapata au wanapojipata katika hali ya kuteketea, mara nyingi wanakuwa wanyonge, wananyamaza na kuzembea katika kazi yao, na wanajaa malalamiko kumhusu Mungu. Tangu wakati ambapo mwanadamu alianza kumwamini Mungu, amemchukulia Mungu kama alama ya pembe inayoonyesha wingi wa neema, kisu cha Kijeshi cha Uswisi, na amejichukulia yeye mwenyewe kuwa mdaiwa mkubwa zaidi wa Mungu, ni kana kwamba kujaribu kupata baraka na ahadi kutoka kwa Mungu ni haki na jukumu lake la asili, huku jukumu la Mungu likiwa ni kumlinda na kumtunza mwananadamu na kumruzuku. Huu ndio ufahamu wa kimsingi wa “imani katika Mungu” wa wale wote wanaomwamini Mungu, na ufahamu wao wa kina zaidi wa dhana ya imani katika Mungu. Kutoka katika kiini cha asili ya mwanadamu hadi katika ufuatiliaji wake wa kibinafsi, hakuna kitu chochote kinachohusiana na kumcha Mungu. Nia ya mwanadamu katika kumwamini Mungu huenda isiwe na uhusiano na kumwabudu Mungu. Hivi ni kusema kwamba, mwanadamu hajawahi kufikiria wala kuelewa kwamba imani katika Mungu inahitaji kumcha Mungu, na kumwabudu Mungu. Kwa mujibu wa haya yote, kiini cha mwanadamu kiko wazi. Kiini hiki ni kipi? Ni kwamba moyo wa mwanadamu ni mwovu, unaficha udanganyifu na ujanja, haupendi mambo ya kutopendelea na haki na kile kilicho chanya, nao ni wenye kustahili dharau na ulafi. Moyo wa mwanadamu umemfungia Mungu nje sana, hajampa Mungu moyo wake kabisa. Mungu hajawahi kuona moyo wa kweli wa mwanadamu, wala hajawahi kuabudiwa na mwanadamu. Haijalishi jinsi gharama ambayo Mungu amelipia ilivyo kubwa, au ni kiasi kipi cha kazi Anachofanya, au ni kiwango kipi Anachompa mwanadamu, mwanadamu anabakia yule asiyeona hayo yote, na hajali kuyahusu. Mwanadamu hajawahi kumpa Mungu moyo wake, anataka tu kuujali moyo wake yeye mwenyewe, kufanya uamuzi wake mwenyewe—sababu ikiwa kwamba mwanadamu hataki kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, au kutii ukuu na mipangilio ya Mungu, wala hataki kumwabudu Mungu kama Mungu. Hivyo ndivyo hali ya mwanadamu ilivyo leo. Sasa hebu tumwangalie tena Ayubu. Kwanza kabisa, je, alifanya mabadilishano na Mungu? Je, alikuwa na nia zozote fiche katika kushikilia njia ile ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu? Wakati huo, je, Mungu alikuwa ameongea na yeyote kuhusu mwisho unaokuja? Wakati huo, Mungu alikuwa hajatoa ahadi zozote kwa yeyote kuhusu mwisho, na ilikuwa katika hali hii ndipo Ayubu aliweza kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Je, watu wa leo wanaweza kulinganishwa na Ayubu? Kunazo tofauti nyingi sana; wamo katika viwango tofauti. Ingawa Ayubu hakuwa na maarifa mengi ya Mungu, alikuwa amempa Mungu moyo wake na ulimilikiwa na Mungu. Hakuwahi kufanya mabadilishano na Mungu, na hakuwa na matamanio yoyote ya kupita kiasi au madai kwa Mungu; badala yake, aliamini kwamba “Yehova alinipa, na Yehova amechukua.” Hiki ndicho alikuwa ameona na kupata kutokana na kushikilia njia ya kumcha Mungu kwa uaminifu na kujiepusha na maovu katika miaka yake mingi ya maisha. Vivyo hivyo, alikuwa pia amepata matokeo yanayowakilishwa katika maneno: “Nasi tupokee mema kutoka mkononi mwa Mungu, nasi tusipokee mabaya?” Sentensi hizi mbili ndizo ambazo alikuwa ameona na akaja kujua kutokana na mtazamo wake wa utiifu kwa Mungu katika uzoefu wa maisha yake, na ndizo pia zilikuwa silaha zake zenye nguvu zaidi ambazo alitumia kushinda wakati wa vishawishi vya Shetani, na ndizo zilikuwa msingi wa kusimama kwake imara katika ushuhuda kwa Mungu. Wakati huu, je, bado mnamwona Ayubu kama mtu mzuri? Je, mnatumaini kuwa mtu kama huyo? Je, mnaogopa kupitia vishawishi vya Shetani? Je, mnaamua kumwomba Mungu ili aweze kuwapitisha katika majaribu kama haya ya Ayubu? Bila shaka watu wengi wasingethubutu kuombea mambo kama hayo. Ni wazi, basi, kwamba imani yenu ni ndogo kiasi cha kusikitisha; ikilinganishwa na ile ya Ayubu, imani yenu haistahili kutajwa. Nyinyi ndio adui wa Mungu, hamumchi Mungu, hamwezi kusimama imara katika ushuhuda kwa Mungu, na hamwezi kuyashinda mashambulio, mashtaka, na vishawishi vya Shetani. Ni nini kinachowafanya mstahili kupokea ahadi za Mungu? Baada ya kusikia hadithi ya Ayubu na kuelewa nia ya Mungu katika kumwokoa mwanadamu na maana ya wokovu wa mwanadamu, je, sasa mna imani ya kukubali majaribu sawa na ya Ayubu? Je, hampaswi kuwa na kusudio kidogo mjiruhusu kufuata njia ya kumcha Mungu na kujiepusha na maovu?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp