Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III

(Sehemu ya Kwanza)

Vikao hivi kadhaa vya ushirika vimekuwa na athari kubwa kwa kila mmoja wa watu. Kwa sasa, watu wanaweza hatimaye kuhisi uwepo wa kweli wa Mungu na kwamba Mungu kwa hakika yuko karibu sana na wao. Ingawa watu wamemwani Mungu kwa miaka mingi, hawajawahi kuelewa kwa kweli mawazo na fikira Zake kama wanavyozielewa sasa, wala hawajawahi kupata kwa kweli uzoefu wa matendo Yake halisi kama walio nao kwa sasa. Kama ni maarifa au matendo halisi, watu wengi wamejifunza kitu kipya na kutimiza ufahamu wa juu zaidi, na wametambua kosa lililopo katika ufuatiliaji wao wa kale, wametambua hali yao waliyopitia ya juujuu na kwamba mambo mengi sana hayaambatani na mapenzi ya Mungu, na wametambua kwamba kile ambacho binadamu amepungukiwa nacho zaidi ni maarifa ya tabia ya Mungu. Maarifa haya kwa upande wa watu ni aina ya maarifa ya utambuzi; kufikia kiwango cha maarifa ya kirazini kunahitaji ushughulikiaji wa kina na utiliaji mkazo wa utaratibu kwenye hali yao yote wanayopitia. Kabla ya binadamu kumwelewa Mungu kwa njia ya kweli, kwa dhahania inaweza kusemekana kwamba wanaamini kwa uwepo wa Mungu mioyoni mwao, lakini hawana ufahamu halisi wa maswali mahususi kama vile Yeye ni Mungu wa aina gani kwa hakika, mapenzi Yake ni nini, tabia Yake ni ipi, na mtazamo Wake halisi kwa binadamu ni upi. Hali hii huhusisha pakubwa imani ya watu katika Mungu—imani yao haiwezi kwa ufupi kufikia utakatifu au ukamilifu. Hata kama utakuwa ana kwa ana na neno la Mungu, au kuhisi kwamba umekumbana na Mungu kupitia katika hali zako ulizopitia, bado haiwezi kusemwa kwamba unamwelewa Yeye kabisa. Kwa sababu hujui fikira za Mungu, au kile Anachopenda na kile Anachochukia, kile kinachomfanya kuwa na ghadhabu na kile kinachomletea furaha, huna ufahamu wa kweli kumhusu. Imani yako imejengwa katika msingi wa hali isiyokuwa dhahiri na ile ya fikira, kwa msingi wa matamanio yako ya dhahania. Bado ingali mbali na imani halisi, na wewe bado ungali mbali na kuwa mfuasi wa kweli. Fafanuzi za mifano kutoka kwenye hadithi hizi za Biblia zimemruhusu binadamu kuujua moyo wa Mungu, kujua ni nini Yeye Alichokuwa akifikiria katika kila hatua ya kazi Yake na kwa nini Aliifanya kazi hii, nia Yake ya asili ilikuwa nini na mpango Wake ulikuwa upi Alipofanya kazi ile, namna ambavyo Alifikia fikira Zake na namna Alivyojitayarisha na kuendeleza mpango Wake. Kupitia katika hadithi hizi, tunaweza kupata ufahamu mahususi wenye maelezo ya kina, ya kila nia mahususi ya Mungu na kila wazo halisi wakati wa kazi Yake ya usimamizi ya miaka elfu sita, na mtazamo Wake kwa binadamu katika nyakati tofauti na enzi tofauti. Kuelewa kile ambacho Mungu alikuwa Anafikiria, mtazamo Wake ulikuwa upi na tabia Aliyoifichua alipokuwa Akikumbana na kila hali, kunaweza kumsaidia kila mtu kwa kina zaidi kuweza kutambua kuwepo Kwake kwa hakika, na kuhisi kwa kina zaidi ukweli na uhalisi Wake. Lengo Langu katika kusimulia hadithi hizi si kwamba watu waweze kuelewa historia ya kibiblia, wala si kuwasaidia kupata uzoefu wa vitabu vya Biblia au watu walio ndani yake, na hasa si kuwasaidia watu kuelewa maelezo zaidi kuhusu kile ambacho Mungu alifanya katika Enzi ya Sheria. Ni kuwasaidia watu kuelewa mapenzi ya Mungu, tabia Yake, na kila sehemu ndogo Yake, na kuongeza ufahamu na maarifa ya Mungu yenye uhalisi zaidi na usahihi zaidi. Kwa njia hii, mioyo ya watu inaweza, hatua kwa hatua, kufunguka kwa ajili ya Mungu na kuwa karibu zaidi na Mungu, na wanaweza kumwelewa Yeye zaidi, tabia Yake, kiini Chake, na kumjua vema zaidi Mungu wa kweli Mwenyewe.

Ufahamu wa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho vinaweza kuwa na athari nzuri kwa binadamu. Vinaweza kuwasaidia kuwa na imani zaidi kwa Mungu, na kuwasaidia kufanikisha utiifu wa kweli na uchaji Kwake. Basi, wao tena si wafuasi wasioona, au wanaomwabudu tu bila mpango. Mungu hataki wajinga au wale wanaofuata umati bila mpango, lakini Anataka kundi la watu ambao wana ufahamu na maarifa wazi katika mioyo yao kuhusu tabia ya Mungu na wanaweza kuchukua nafasi ya mashahidi wa Mungu, watu ambao hawawezi kamwe kumwacha Mungu kwa sababu ya uzuri Wake, kwa sababu ya kile Alicho nacho na kile Alicho, na kwa sababu ya tabia Yake ya haki. Kama mfuasi wa Mungu, endapo katika moyo wako bado kuna ukosefu wa ubayana, au kuna hali tata au mkanganyo kuhusu kuwepo kwa kweli kwa Mungu, tabia Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, na mpango Wake wa kumwokoa binadamu, basi imani yako haiwezi kupata sifa za Mungu. Mungu hataki mtu wa aina hii kumfuata Yeye, na pia Hapendi mtu wa aina hii akija mbele Yake. Kwa sababu mtu wa aina hii hamwelewi Mungu, hawezi kutoa moyo wake kwa Mungu—moyo wake umemfungwa Kwake, hivyo basi imani yake katika Mungu imejaa kasoro mbalimbali. Kumfuata kwake Mungu kunaweza tu kusemwa kuwa ni kwa kipumbavu. Watu wanaweza tu kupata imani ya kweli na kuwa wafuasi wa kweli kama watakuwa na ufahamu na maarifa ya kweli wa Mungu, jambo ambalo linaleta utiifu na uchaji wa kweli Kwake. Ni kwa njia hii tu ndiyo anaweza kuutoa moyo wake kwa Mungu, kuufungua Kwake. Hili ndilo Mungu anataka, kwa sababu kila kitu wanachofanya na kufikiria, kinaweza kustahimili majaribu ya Mungu, na kinaweza kumshuhudia Mungu. Kila kitu Ninachowasiliana nanyi kuhusiana na tabia ya Mungu, au kuhusu kile Alicho nacho na kile Alicho, au mapenzi Yake na fikira Zake katika kila kitu Anachofanya, na kutoka kwenye mtazamo wowote ule, kutoka kwa upande wowote ule Nakizungumzia, yote haya ni kukusaidia kuwa na uhakika zaidi kuhusu uwepo wa kweli wa Mungu, na kuelewa na kushukuru zaidi kwa kweli upendo Wake kwa mwanadamu, na kuelewa na kufahamu vyema zaidi kwa kweli kile anachojali Mungu kuhusu binadamu, na tamanio Lake la dhati la kumsimamia na kumwokoa mwanadamu.

Leo kwanza kabisa tutafanya muhtasari wa fikira, mawazo, na kila hatua ya Mungu tangu Alipomuumba binadamu, na kuangalia ni kazi gani Alitekeleza kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi mwanzo rasmi wa Enzi ya Neema. Tunaweza kisha kugundua ni fikira na mawazo yapi ya Mungu ambayo hayajulikani kwa binadamu, na kuanzia hapo tunaweza kuweka wazi mpangilio wa mpango wa usimamizi wa Mungu na kuelewa kwa kina muktadha ambao kwao Mungu alianzisha kazi Yake ya usimamizi, chanzo chake na mchakato wake wa maendeleo, na pia kuelewa kwa undani ni matokeo yapi Anayotaka kutoka katika kazi Yake ya usimamizi—yaani, kiini na kusudio la kazi Yake ya usimamizi. Kuelewa mambo haya tunahitaji kurudi hadi ule wakati wa kitambo, mtulivu na kimya ambapo hakukuwa na binadamu …

Wakati Mungu aliinuka kutoka kitandani Mwake, fikira ya kwanza Aliyokuwa nayo ilikuwa hii: kumuumba binadamu hai, halisi, binadamu anayeishi—mtu wa kuishi naye na kuwa mwenzake wa kila mara. Mtu huyu angemsikiliza, na Mungu angempa siri Zake na kuongea na yeye. Kisha, kwa mara ya kwanza, Mungu aliuchukua udongo kwenye mkono na kuutumia kumuumba mtu wa kwanza kabisa aliye hai ambaye Alikuwa amemfikiria, na kisha Akakipa kiumbe hiki hai jina—Adamu. Punde Mungu alipompata mtu huyu aliye hai na anayepumua, Alihisi vipi? Kwa mara ya kwanza, Alihisi furaha ya kuwa na mpendwa, na mwandani. Aliweza kuhisi pia kwa mara ya kwanza uwajibikaji wa kuwa baba pamoja na kujali kunakoandamana na hisia hizo. Mtu huyu aliye hai na anayepumua alimletea Mungu furaha na shangwe; Alihisi aliyefarijika kwa mara ya kwanza. Hili lilikuwa jambo la kwanza ambalo Mungu aliwahi kufanya ambalo halikukamilishwa kwa fikira Zake au hata matamshi Yake, lakini lilifanywa kwa mikono Yake miwili. Wakati kiumbe aina hii—mtu aliye hai na anayepumua—aliposimama mbele ya Mungu, aliyeumbwa kwa nyama na damu, aliye na mwili na umbo, na aliyeweza kuongea na Mungu, Alihisi aina ya shangwe ambayo Hakuwa amewahi kuhisi kabla. Kwa kweli alihisi kwamba uwajibikaji Wake na kiumbe huyu hai haukuwa na uhusiano tu katika moyo Wake, lakini kila jambo dogo alilofanya pia lilimgusa na likaupa moyo Wake furaha. Kwa hivyo wakati kiumbe huyu hai aliposimama mbele ya Mungu, ilikuwa ndiyo mara ya kwanza kuwahi kufikiria kuwapata watu wengi zaidi kama hawa. Huu ndio uliokuwa msururu wa matukio ulioanza kwa fikira hii ya kwanza ambayo Mungu alikuwa nayo. Kwa Mungu, matukio haya yote yalikuwa yakifanyika kwa mara ya kwanza, lakini katika matukio haya ya kwanza, haijalishi vile Alivyohisi wakati huo—furaha, uwajibikaji, kujali—hakukuwa na yeyote yule wa kushiriki furaha hii na Yeye. Kuanzia wakati huo, Mungu alihisi kwa kweli upweke na huzuni ambayo Hakuwahi kuwa nao mbeleni. Alihisi kwamba binadamu wasingekubali au kuelewa mapenzi Yake na kujali Kwake, au nia Zake kwa mwanadamu, hivyo basi Alihisi huzuni na maumivu katika moyo Wake. Ingawa Alikuwa amefanya mambo haya kwa binadamu, binadamu hakuwa na habari na hakuelewa. Mbali na furaha, shangwe na hali njema ambayo binadamu alimletea pia viliandamana kwa haraka na hisia Zake za kwanza za huzuni na upweke. Hizi ndizo zilizokuwa fikira na hisia za Mungu wakati huo. Mungu alipokuwa akifanya mambo haya yote, moyoni Mwake Alitoka katika furaha Akaingia katika huzuni na kutoka katika huzuni Akaingia katika maumivu, vyote vikiwa vimechanganyika na wasiwasi. Kile Alichotaka kufanya tu kilikuwa kuharakisha kumruhusu mtu huyu, kizazi hiki cha binadamu kujua ni nini kilichokuwa moyoni Mwake na kuelewa nia Zake haraka iwezekanavyo. Kisha, wangekuwa wafuasi Wake na kupatana na Yeye. Wasingemsikiliza tena Mungu akiongea na kubakia kimya; wasingeendelea kutojua namna ya kujiunga na Mungu katika kazi Yake, na zaidi ya yote, wasingekuwa tena watu wasiojali na kuelewa mahitaji ya Mungu. Mambo haya ya kwanza ambayo Mungu alikamilisha ni yenye maana sana na yanashikilia thamani nyingi kwa minajili ya mpango Wake wa usimamizi na ule wa binadamu leo.

Baada ya kuviumba viumbe vyote na binadamu, Mungu hakupumzika. Asingesubiri kuutekeleza usimamizi Wake wala Asingeweza kusubiri kuwapata watu Aliowapenda mno miongoni mwa wanadamu.

Kisha, si kipindi kirefu baada ya Mungu kuwaumba binadamu, tunaona kutoka katika Biblia ya kwamba kulikuwa na gharika kubwa kote ulimwenguni. Nuhu anatajwa kwenye rekodi ya gharika, na inaweza kusemekana kwamba Nuhu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kupokea mwito wa Mungu ili afanye kazi na Yeye ili kukamilisha kazi ya Mungu. Bila shaka, wakati huo ndio uliokuwa pia wa kwanza kwa Mungu kumwita mtu ulimwenguni kufanya kitu kulingana na amri Yake. Mara tu Nuhu alipokamilisha kuijenga safina, Mungu alileta gharika katika nchi kwa mara ya kwanza. Mungu alipoiharibu nchi kwa gharika, ndiyo ilikuwa mara ya kwanza tangu kuviumba viumbe ambapo Alihisi kuzidiwa na maudhi kwa binadamu; hili ndilo lililomlazimu Mungu kufanya uamuzi wa uchungu wa kuharibu kizazi hiki cha binadamu kupitia kwa gharika. Baada ya gharika kuiharibu dunia, Mungu alifanya agano Lake la kwanza na binadamu kwamba Hatawahi kufanya hivi tena. Ishara ya agano hili ilikuwa upinde wa mvua. Hili ndilo lililokuwa agano la kwanza la Mungu na binadamu, hivyo basi upinde wa mvua ndio uliokuwa ishara ya kwanza ya agano lililotolewa na Mungu; upinde huu wa mvua ni jambo halisi lililopo. Ni kule kuwepo kabisa kwa upinde huu wa mvua ambako humfanya Mungu mara nyingi ahisi huzuni kutokana na kizazi cha binadamu cha awali ambacho Amepoteza, na huwa ni kumbusho la kila mara Kwake kuhusiana na kile kilichowafanyikia…. Mungu asingepunguza mwendo Wake—Asingesubiri kuchukua hatua ya kufuata katika usimamizi Wake. Hivyo basi, Mungu alimchagua Ibrahimu kama chaguo Lake la kwanza kwa kazi Yake kotekote Israeli. Hii ndiyo iliyokuwa pia mara ya kwanza kwa Mungu kumchagua mteuliwa kama huyo. Mungu aliamua kuanza kutekeleza kazi Yake ya kumwokoa binadamu kupitia kwa mtu huyu, na kuendeleza kazi Yake miongoni mwa vizazi vya mtu huyu. Tunaweza kuona katika Biblia kwamba hivi ndivyo Mungu alivyomfanyia Ibrahimu. Basi Mungu akaifanya Israeli kuwa nchi ya kwanza iliyochaguliwa, na Akaianza kazi Yake ya Enzi ya Sheria kupitia kwa watu Wake waliochaguliwa, Waisraeli. Tena kwa mara ya kwanza, Mungu aliwapa Waisraeli sheria na kanuni za moja kwa moja ambazo mwanadamu anafaa kufuata, na Akazieleza kwa kina. Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpatia binadamu sheria kama hizo mahususi na wastani kuhusu namna wanavyofaa kutoa kafara, namna wanavyofaa kuishi, kile wanachofaa kufanya na kutofanya, ni sherehe na siku gani wanazofaa kutilia maanani, na kanuni za kufuata katika kila kitu walichofanya. Hii ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kumpa binadamu taratibu na kanuni hizo zenye maelezo na uwastani kwa ajili ya maisha yao.

Ninaposema “mara ya kwanza,” inamaanisha Mungu hakuwa Amewahi kukamilisha kazi kama hiyo tena. Ni kitu ambacho hakikuwepo awali, na hata ingawa Mungu alikuwa Amemuumba binadamu na Alikuwa ameumba aina zote za viumbe na vitu vyenye uhai, Hakuwa amewahi kukamilisha kazi ya aina hiyo. Usimamizi wa Mungu kwa binadamu; yote ilihusu binadamu na wokovu Wake na usimamizi wa binadamu. Baada ya Ibrahimu, Mungu alifanya chaguo tena kwa mara ya kwanza—Alimchagua Ayubu kuwa ndiye chini ya sheria ndiye ambaye angestahimili majaribio ya Shetani huku akiendelea kumcha Mungu na kujiepusha na uovu na kuweza kumtolea Yeye ushuhuda. Hii pia ndiyo iliyokuwa mara ya kwanza kwa Mungu kuruhusu Shetani kumjaribu mtu na mara ya kwanza Alipoweka dau na Shetani. Mwishowe, kwa mara ya kwanza, Mungu alimpata mtu aliyekuwa na uwezo wa kusimama kama shahidi Wake huku akiwa amemkabili Shetani—mtu ambaye angeweza kumshuhudia Yeye na kumwaibisha kabisa Shetani. Tangu Mungu alipomuumba mwanadamu, huyu ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza, aliyempata ambaye aliweza kumshuhudia Yeye. Punde alipokuwa amempata mtu huyu, Mungu alikuwa na hata hamu zaidi ya kuendeleza usimamizi Wake na kuchukua hatua inayofuata katika kazi Yake, Akitayarisha chaguo Lake lifuatalo na mahali Pake pa kazi.

Baada ya kushiriki kuhusu haya yote, je, mnao ufahamu wa kweli wa mapenzi ya Mungu? Mungu anaona tukio hili la usimamizi wa binadamu, wa kuwaokoa wanadamu, kama muhimu sana kuliko chochote kingine. Huyafanya mambo haya yote si kwa kutumia akili Zake tu, wala si kwa kutumia maneno Yake tu, na vilevile Yeye hafanyi hivi hususan kwa juujuu tu—Yeye huyafanya mambo haya yote kwa mpango, kwa viwango, na kwa mapenzi Yake. Ni wazi kwamba kazi hii ya kumwokoa binadamu imeshikilia umuhimu mkubwa kwa Mungu na hata binadamu. Haijalishi kazi ilivyo ngumu, haijalishi changamoto ni kubwa jinsi gani, haijalishi binadamu ni wanyonge jinsi gani, au binadamu amekuwa mwasi wa kweli, hakuna chochote kati ya haya ambacho ni kigumu kwa Mungu. Mungu hujibidiisha Mwenyewe, Akitumia jitihada Zake za bidii za kazi na kusimamia kazi ambayo Yeye Mwenyewe Anataka kutekeleza. Yeye pia Anapanga kila kitu na kuwatawala watu wote na kazi ambayo Anataka kukamilisha—hakuna chochote kati ya haya ambacho kimefanywa awali. Ndiyo mara ya kwanza Mungu ametumia mbinu hizi na kulipa gharama kubwa kwa minajili ya mradi huu mkubwa wa kusimamia na kumwokoa mwanadamu. Huku Mungu akiwa Anatekeleza kazi hii, hatua kwa hatua Anawaonyesha binadamu bila kuficha bidii Yake, kile Alicho nacho na kile Alicho, hekima na uweza, na kila dhana ya tabia Yake. Anafichua bila kuacha chochote haya yote kwa mwanadamu kidogo kidogo, Akifichua na kuonyesha mambo haya kwa namna ambayo Hajawahi kufanya awali. Kwa hivyo, katika ulimwengu mzima, mbali na watu ambao Mungu analenga kuwasimamia na kuwaokoa, hakujawahi kuwepo na viumbe vyovyote vilivyo karibu na Mungu, ambavyo vinao uhusiano wa karibu sana na Yeye. Katika moyo Wake, yule mwanadamu Anayetaka kumsimamia na kumwokoa ndiye muhimu zaidi, na Anamthamini mwanadamu huyu zaidi ya kitu kingine chochote; hata ingawa Amelipia gharama ya juu na ingawa Anaumizwa na kutosikilizwa bila kukoma na wao, Hakati tamaa na Anaendelea bila kuchoka katika kazi Yake bila ya malalamiko au majuto. Hii ni kwa sababu Anajua kwamba hivi karibuni au baadaye, binadamu siku moja wataitikia mwito Wake na kuguswa na maneno Yake, kutambua kwamba Yeye ndiye Bwana wa uumbaji, na kurudi upande Wake …

Baada ya kusikia haya yote leo, mnaweza kuhisi kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya ni kawaida sana. Yaonekana kwamba binadamu siku zote wamehisi mapenzi fulani ya Mungu kwao kutokana na matamshi Yake na pia kazi Yake, lakini siku zote kuna umbali fulani katikati ya hisia zao au maarifa yao na kile ambacho Mungu anafikiria. Kwa hivyo, Nafikiri ni muhimu kuwasiliana na watu wote kuhusu ni kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu, na maelezo zaidi yanayoonyesha tamanio Lake la kuwapata watu aliokuwa Akitumainia. Ni muhimu kushiriki habari hii na kila mmoja, ili kila mmoja aweze kuwa wazi moyoni mwake. Kwa sababu kila fikira na wazo la Mungu, na kila awamu na kila kipindi cha kazi Yake vinafungamana ndani ya, na vyote hivi vimeunganishwa kwa karibu na, usimamizi Wake mzima wa kazi, unapoelewa fikira na mawazo ya Mungu, na mapenzi Yake katika kila hatua ya kazi Yake, ni sawa na ufahamu wa chanzo cha kazi ya mpango Wake wa usimamizi. Ni katika msingi huu ndipo ufahamu wako wa Mungu unapoanza kuwa wa kina. Ingawa kila kitu ambacho Mungu alifanya Alipoumba kwanza ulimwengu ambacho Nilitaja awali ni taarifa fulani tu kwa watu sasa na yaonekana kwamba hayana umuhimu sana katika utafutaji wa ukweli, katika mkondo wa kile ambacho utapitia kutakuwa na siku ambapo hutafikiria kuwa ni jambo rahisi sana kama mkusanyiko tu wa taarifa, wala kwamba ni kitu rahisi sana kama mafumbo fulani. Kwa kadri maisha yako yanavyoendelea na pale ambapo pana msimamo kidogo wa Mungu katika moyo wako, au unapokuja kuelewa waziwazi na kwa kina mapenzi Yake, utaweza kuelewa kwa kweli umuhimu na haja ya kile Ninachozungumzia leo. Haijalishi ni kwa kiwango kipi umeyakubali haya; ni muhimu kwamba uelewe na ujue mambo haya. Wakati Mungu anapofanya jambo, wakati Anapotekeleza kazi Yake, haijalishi kama amefanya na mawazo Yake au kwa mikono Yake, haijalishi kama ni mara ya kwanza ambapo Amelifanya au kama ni mara ya mwisho—mwishowe, Mungu anao mpango, na makusudio Yake na fikira Zake vyote vimo katika kila kitu Anachokifanya. Makusudio na fikira hizi vinawakilisha tabia ya Mungu, na vinaonyesha kile Alicho nacho na kile Alicho. Vitu hivi viwili—tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho—lazima vieleweke na kila mmoja. Punde mtu anapoelewa tabia Yake na kile Alicho nacho na kile Alicho, ataanza kuelewa kwa utaratibu ni kwa nini Mungu anafanya kile Anachofanya na kwa nini Anasema kile Anachosema. Kutokana na hayo, anaweza kuwa na imani zaidi ya kumfuata Mungu, kuufuatilia ukweli, na kufuatilia mabadiliko katika tabia. Hivi ni kusema, ufahamu wa binadamu kuhusu Mungu na imani yake katika Mungu ni vitu viwili visivyoteganishwa.

Hata ingawa kile watu wanachosikia kuhusu au kupata ufahamu huo ni tabia ya Mungu, kile Alicho nacho na kile Alicho, kile wanachofaidi ni maisha yanayotoka kwa Mungu. Baada ya maisha haya kuhemshwa ndani yako, uchaji wako wa Mungu utakuwa mkubwa zaidi na zaidi, na kuvuna mavuno haya kunafanyika kwa kawaida sana. Kama hutaki kuelewa au kujua kuhusu tabia ya Mungu au kiini Chake, kama hutaki hata kutafakari juu ya mambo haya au kuyazingatia, Naweza kukuambia kwa hakika kwamba hiyo njia unayoifuatilia katika imani yako kwa Mungu haitawahi kukuruhusu kuyaridhisha mapenzi Yake au kupata sifa Zake. Zaidi ya hayo, huwezi kamwe kufikia wokovu—hizi ndizo athari za mwisho. Wakati watu hawamwelewi Mungu na hawajui tabia Yake, mioyo yao haiwezi kamwe kuwa wazi Kwake. Punde wanapomwelewa Mungu, wataanza kuelewa na kufurahia kile kilicho moyoni Mwake kwa kivutio na imani. Unapoelewa na kufurahia kile kilichomo ndani ya moyo wa Mungu, moyo wako utaanza kwa utaratibu, kidogokidogo, kuwa wazi Kwake. Wakati moyo wako unakuwa wazi Kwake, utahisi namna ambavyo mabadilishano yako na Mungu yatakavyokuwa ya aibu na duni, madai yako kutoka kwa Mungu na matamanio yako mengi binafsi. Moyo wako unapofunguka kwa kweli kwa Mungu, utaona kwamba moyo Wake ni ulimwengu usio na mwisho, na utaingia katika ulimwengu ambao hujawahi kuupitia awali. Katika ulimwengu huu hakuna kudanganya, hakuna udanganyifu, hakuna giza, hakuna maovu. Kunao ukweli wa dhati na uaminifu; kunayo nuru na uadilifu tu; kunayo haki na huruma. Umejaa upendo na utunzaji, umejaa rehema na uvumilivu, na kupitia katika ulimwengu huu utahisi shangwe na furaha ya kuwa hai. Mambo haya ndiyo ambayo Atakufichulia utakapoufungua moyo wako kwa Mungu. Hii dunia isiyo na kikomo imejaa hekima ya Mungu, na imejaa kudura Yake; umejaa pia upendo Wake na mamlaka Yake. Hapa unaweza kuona kila kipengele cha kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, ni nini kinachomletea Yeye shangwe, kwa nini Anakuwa na wasiwasi na kwa nini Anakuwa na huzuni, kwa nini Anakuwa na hasira…. Haya ndiyo ambayo kila mmoja anayeufungua moyo wake na kumruhusu Mungu kuingia ndani anaweza kuona. Mungu anaweza tu kuingia katika moyo wako kama utaufungua kwa ajili Yake. Unaweza kuona tu kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho, na unaweza kuona tu mapenzi Yake kwako, kama Ameingia katika moyo wako. Wakati huo, utagundua kwamba kila kitu kuhusu Mungu ni chenye thamani, kwamba kile Alicho nacho na kile Alicho kina thamani sana ya kuthaminiwa. Ukilinganisha na hayo, watu wanaokuzunguka, vifaa na matukio katika maisha yako, hata wapendwa wako, mwandani wako, na mambo unayopenda, si muhimu sana. Ni madogo mno, na ni ya kiwango cha chini; utahisi kwamba hakuna chombo chochote cha anasa ambacho kitaweza kukuvutia tena, na vitu hivi haviwezi kukufanya kuvilipia gharama yoyote tena. Kwa unyenyekevu wa Mungu utaona ukubwa Wake na mamlaka Yake ya juu; aidha, katika jambo Alilofanya uliloliamini kuwa dogo mno, utaweza kuiona hekima Yake na uvumilivu Wake usio na mwisho, na utaiona subira Yake, uvumilivu Wake na ufahamu Wake kwako. Hili litazaa ndani yako upendo Kwake. Siku hiyo, utahisi kwamba mwanadamu anaishi katika ulimwengu mchafu, kwamba watu walio upande wako na mambo yanayokufanyikia katika maisha yako, na hata kwa wale unaopenda, upendo wao kwako, na ulinzi wao kama ulivyojulikana au kujali kwao kwako havistahili hata kutajwa—Mungu tu ndiye mpendwa wako na ni Mungu tu unayethamini zaidi. Wakati siku hiyo itawadia, Naamini kwamba kutakuwa na baadhi ya watu watakaosema: Upendo wa Mungu ni mkubwa na kiini Chake ni kitakatifu mno—ndani ya Mungu hakuna udanganyifu, hakuna uovu, hakuna wivu, na hakuna mabishano, lakini ni haki tu na uhalisi, na kila kitu Alicho nacho Mungu na kile Alicho vyote vinafaa kutamaniwa na binadamu. Binadamu wanafaa kujitahidi na kuwa na hamu ya kuvipata. Ni kwa msingi gani ndipo uwezo wa mwanadamu wa kutimiza haya umejengwa? Unajengwa kwa msingi wa ufahamu wa binadamu wa tabia ya Mungu, na ufahamu wao kuhusu kiini cha Mungu. Hivyo basi kuelewa tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho, ni funzo la maisha yote kwa kila mtu na ni lengo la maisha yote linalofuatiliwa na kila mtu anayelenga kubadilisha tabia yake, na kutamani kumjua Mungu.

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp