Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)
Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Vikundi

Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Maneno ya Mungu ya Kila Siku
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu (Njia ya Kumjua Mungu)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)
Neno Laonekana katika Mwili (Chaguzi)

Mmeambiwa kuwa mjiandae kwa maneno ya Mungu, ya kuwa pasipo kujali mlichoandaliwa ninyi, yote yamepangwa kwa mkono wa Mungu, na kwamba hakuna haja ya kuomba kwa bidii au kusali kwenu—hayana maana. Ilhali kulingana na hali ya sasa, shida za kiutendaji mnazokumbana nazo hazifikiriki kwenu. Kama mnasubiri mipango ya Mungu tu, basi kuendelea kwenu kutakuwa polepole sana, na kwa wale wasiojua jinsi ya kupitia kutakuwa na kulaza damu kwingi. Kwa hivyo, ikiwa umeshindwa kabisa kuyalewa mambo haya, basi umechanganyikiwa na kuwa mpumbavu katika uzoefu wako. Kama huna ukweli lakini maneno tu, je, si hii ni ishara ya makosa? Makosa mengi yanaonekana ndani yenu, kundi hili. Hivi leo, hamna uwezo wa kutimiza majaribu kama vile "watendaji huduma," ama vinginevyo hamwezi kutafakari au kutimiza usafishaji mwingine unaohusiana na maneno ya Mungu. Lazima mzingatie mambo mengi ambayo mnahitajika kuyaweka katika matendo. Ambayo ni kusema kuwa watu lazima wafuate majukumu mengi wanayostahili kuyatekeleza. Hili ndilo watu wanalopaswa kufuata, na wanalostahili kufanya. Mruhusu Roho Mtakatifu afanye linalostahili kufanywa na Roho Mtakatifu; mwanadamu hawezi kulichangia lolote. Mwanadamu sharti ashike yale ambayo lazima yatendwe na mwanadamu, ambayo hayana uhusiano na Roho Mtakatifu. Si lolote bali lile ambalo lazima litendwe na mwanadamu, na lazima lifuatwe kama amri, kama ufuasi wa sheria za Agano la Kale. Ingawa sasa si Enzi ya Sheria, bado kuna maneno mengi yanayolingana na Enzi ya Sheria ambayo yanahitaji kufuatwa, na hayatendwi tu kwa kutegemea kuguswa na Roho Mtakatifu, lakini ni yale yanayostahili kufuatwa na wanadamu. Kwa mfano: Hupaswi kuihukumu kazi ya Mungu wa vitendo. Hupaswi kumpinga mtu anayeshuhudiwa na Mungu. Mbele za Mungu, utahifadhi nafasi yako, na hutakuwa mwovu. Matamshi yako yanapaswa yawe wastani, na maneno yako na matendo yako yanapaswa kufuata mpangilio wa mwanadamu aliyeshuhudiwa na Mungu. Unapaswa kuheshimu ushuhuda wa Mungu. Usipuuze kazi ya Mungu wala maneno kutoka kinywa chake. Usiige sauti na malengo ya matamshi ya Mungu. Kwa nje, usifanye lolote linalodhihirisha kumpinga mtu anayeshuhudiwa na Mungu. Haya na mengine ndiyo yanayopaswa kufuatwa na kila mmoja. Katika kila enzi, Mungu hutaja amri nyingi zinazoambatana na amri na zinazopaswa kufuatwa na mwanadamu. Kupitia hili, anazuia tabia ya mwanadamu, na kugundua ukweli wake. Tazama maneno "Onyesha heshima kwa baba na mama yako" kutoka kwa nyakati za Agano la Kale, kwa mfano. Maneno haya hayatumiki hivi leo; wakati huo, yalizuia tabia zingine za mwanadamu tu, yalitumika kuonyesha uaminifu wa imani ya mwanadamu kwa Mungu, na yalikuwa alama ya wale waliomwamini Mungu. Ingawa sasa ni Enzi ya Ufalme, bado kuna amri nyingi ambazo mwanadamu lazima azifuate. Amri za kale hazitumiki; leo, kuna mazoea mengi, mwafaka kwa mwanaadamu kutekeleza, na ambayo ni muhimu. Hayahusiani na kazi ya Roho Mtakatifu na lazima yatendwe na mwanadamu.

Katika Enzi ya Neema, mazoea mengi ya Enzi ya Sheria yaliondolewa kwa sababu sheria hizi hazikufaa hasa kazi ya wakati huo. Baada ya kuondolewa, mazoea mengi yaliwekwa ambayo yalifaa enzi hiyo, na ambayo yamekuwa amri nyingi za sasa. Mungu wa leo alipokuja, kanuni hizi zilitupiliwa mbali, na hazikuhitajika kufuatwa tena, na mazoea mengi ambayo yalifaa kazi ya wakati huu yakawekwa. Leo, mazoea haya si kanuni, lakini ili kuwa na athari; ni mazuri kwa ajili ya leo—na kesho, pengine, yatakuwa kanuni. Kwa ujumla, unafaa kufuata yale ambayo yatafanikisha kazi ya leo. Usizingatie kesho: Yanayofanywa leo ni kwa ajili ya leo. Pengine kesho kutakuwa na mazoea mazuri ambayo utahitajika kutekeleza—lakini usizingatie hayo sana, yafuate yanayofaa kufuatwa leo ili uepuke kumpinga Mungu. Leo, hakuna lolote muhimu analopaswa kufuata mwanadamu zaidi ya yafuatayo: Usimdanganye au kumficha Mungu lolote lililoko mbele ya macho yako. Usizungumze uchafu ama matamshi ya kiburi mbele ya Mungu aliye mbele yako. Usimdanganye Mungu mbele ya macho yako kwa maneno mazuri wala kwa maneno ya kuridhisha ili uweze kujipatia uaminifu Wake. Usitende bila heshima mbele za Mungu. Tii yote yatokayo kinywani mwa Mungu, wala usikatae, usipinge, ama kusaili maneno Yake. Usitafsiri unavyoona kuwa sawa, maneno yanayonenwa kutoka kinywani mwa Mungu. Chunga ulimi wako ili usikutie katika mtego wa hila danganyifu za yule mwovu. Unapaswa kulinda nyayo zako ili kuepuka kupita mipaka uliyowekewa na Mungu. Kufanya hivyo kutakufanya uzungumze maneno ya majivuno na yenye fahari kuu kulingana na mtazamo wa Mungu, na hivyo kufanya uchukiwe na Mungu. Usirudierudie maneno kutoka kinywa cha Mungu ovyoovyo, usije ukadhihakiwa na wengine na kufanywa kuwa mjinga na mapepo. Tii kazi yote ya Mungu wa leo. Hata ikiwa hauifahamu, usiihukumu; unachoweza kufanya ni kutafuta na kushiriki. Hakuna mtu atapatendea dhambi mahali pa Mungu pa asili. Huwezi kufanya lolote ila kumhudumia Mungu wa leo kwa mtazamo wa mwanadamu. Huwezi kumfunza Mungu wa leo kwa mtazamo wa mwanadamu—kufanya hivyo ni kupotoka. Hakuna anayeweza kusimama kwa niaba ya mtu aliyeshuhudiwa na Mungu; katika maneno yako, matendo, na mawazo yako ya ndani, unasimama katika nafasi ya mwanadamu. Hili ni la kufuatwa, ni wajibu wa mwanadamu, hakuna anayeweza kulibadilisha, na kufanya hivyo ni ukiukaji wa amri za utawala. Inapaswa kukumbukwa na kila mtu.

Muda mrefu ambao Mungu ametumia kuzungumza na kutamka kumemfanya mwanadamu kufikiria kusoma na kukariri maneno ya Mungu kuwa ndio wajibu wake wa kimsingi. Hakuna anayezingatia kutenda, na hata yale mnayopaswa kufuata hamyafuati, kwa hivyo hili limeleta ugumu na matatizo mengi kwa huduma yenu. Ikiwa, kabla ya kutenda maneno ya Mungu, hujayafuata yale unayopaswa kuyafuata, basi wewe ni mmoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Mungu. Kwa kufuata matendo haya, unapaswa kuwa na bidii na uaminifu. Hufai kuyachukua kuwa kama minyororo, ila uyafuate kama amri. Leo, hupaswi kuzingatia athari ambazo zinatarajiwa kufikiwa; kwa ufupi, hivi ndivyo Roho Mtakatifu anavyofanya kazi, na yeyote atakayefanya kosa lazima afe. Roho Mtakatifu hana hisia, na hazingatii ufahamu wako wa sasa. Ukimkosea leo, basi Atakuadhibu. Ukimkosea ndani ya wigo wa mamlaka Yake, basi Hatakuachilia bure. Hajali jinsi gani ulivyo makini katika kufuata maneno ya Yesu. Leo, ukifanya maovu utahukumiwa kifo. Je, itakubalika vipi kwako wewe kutofuata? Lazima ufuate—hata kama itamaanisha kupitia uchungu mdogo! Bila kujali ni dini, kundi, taifa, ama dhehebu gani, katika siku zijazo lazima yote yafuate mazoea haya. Hakuna yaliyosamehewa, na hakuna yatakayoachwa! Kwa sababu ndiyo yatakayotekelezwa na Roho Mtakatifu leo, na hayawezi kukosewa kwa wote. Ingawa si mambo makuu, lazima yatendwe na kila mtu, na ni amri zilizowekwa kwa mwanadamu na Yesu, aliyefufuka na kupaa mbinguni. Je, "Njia … (7)" haisemi kuwa ufafanuzi wa Yesu, wa kama wewe ni mwenye haki au mwenye dhambi, ni kwa mujibu wa mtazamo wako kwa Mungu leo? Hakuna anayefaa kupuuza suala hili. Katika Agano la Kale, kizazi baada ya kizazi cha Mafarisayo kilimwamini Mungu, lakini kwa ujio wa Enzi ya Neema, hawakumfahamu Yesu, na walimpinga. Hivyo basi, yote waliyoyafanya yakawa hayana maana na yalikuwa bure na Mungu hakuyakubali. Ukiweza kuelewa hili basi hutakuwa mwepesi wa kutenda dhambi. Watu wengi, pengine, wamejipima dhidi ya Mungu. Je, kumpinga Mungu kuna ladha ipi, chungu au tamu? Unapaswa kuelewa hili—usijifanye kuwa hujui. Mioyoni mwao, pengine, wengine wamesalia kutoshawishika. Bali Nakushauri, ulijaribu na kuona—hisi jinsi ladha yake ilivyo. Hili litawazuia wengi kuwa na shaka kulihusu. Watu wengi husoma maneno ya Mungu lakini wanampinga mioyoni mwao kwa siri. Baada ya kumpinga hivi, je, huhisi kama kisu kimepindwa moyoni mwako? Kama si utengano wa familia, basi ni usumbufu wa mwilini, ama mateso ya wana wa kiume na mabinti. Ingawa mwili wako umeepushwa na kifo, mkono wa Mungu kamwe hautakuacha. Je, unafikiri linaweza kuwa rahisi hivyo? Hasa, ni muhimu hata zaidi kwa wengi waliomkaribia Mungu kuzingatia hili. Muda unapoendelea, utalisahau, na, pasipo kujua, utaingia majaribuni, utaacha kujali kila kitu, na huu utakuwa mwanzo wako wa kutenda dhambi. Je, hili linaonekana duni kwako? Ikiwa utaweza kufanya hili vyema, basi una nafasi ya kufanywa mkamilifu—kupokea mwongozo kutoka kwa kinywa cha Mungu mwenyewe mbele za Mungu. Ikiwa huoni kama hili ni la muhimu, basi utakuwa taabani—utamwasi Mungu, maneno yako na matendo yatakuwa maovu, na punde au baadaye, utabebwa na dhoruba kubwa na mawimbi makuu. Mambo haya yanapaswa kuzingatiwa na kila mmoja wenu. Mtu aliyeshuhudiwa na Mungu anaweza akakosa kuwalaani, lakini Roho wa Mungu hajamalizana na wewe. Hatakuhurumia. Je, unadhania kwamba una uwezo wa kufanya makosa? Kwa hivyo, lolote Asemalo Mungu, lazima utie katika vitendo maneno Yake, na kuyafuata kwa njia zozote unazoweza. Hili si jambo rahisi!

Matamshi ya Kristo wa Siku za Mwisho (Chaguzi)

Yule tu Anayepitia Kazi ya Mungu Ndiye Anayemwamini Mungu Kweli Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko La Kumi Na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tatu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nne Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi Na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Kumi na Tisa Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Moja Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Mbili Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tatu Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tano Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Sita Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Saba Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nane Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Tisa Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya Mungu Anaongoza Majaliwa ya Wanadamu Wote Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake Maoni Wanayopaswa Kushikilia Waumini Mwanadamu Mpotovu Hawezi Kumwakilisha Mungu Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku Katika Imani Yako kwa Mungu Unapaswa Kumtii Mungu Ahadi kwa Wale Ambao Wamekamilishwa Waovu Lazima Waadhibiwe Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu Jinsi ya Kuujua Uhalisi Amri za Enzi Mpya Ufalme wa Milenia Umewasili Unapaswa Kujua kuwa Mungu wa Vitendo Ni Mungu Mwenyewe Kuijua Kazi ya Mungu Leo Je, Kazi ya Mungu ni Rahisi Jinsi Mwanadamu Anavyodhania? Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu Ngurumo Saba Zatoa Sauti—Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni Tofauti Muhimu Kati ya Mungu Aliyepata Mwili na Wanadamu Wanaotumiwa na Mungu Kumwamini Mungu Lazima Kulenge Uhalisi, Si Tamaduni za Kidini Ni Wale tu Wanaoijua Kazi ya Mungu Leo Wanaoweza Kumhudumia Mungu Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watakubaliwa na Mungu Enzi ya Ufalme Ndiyo Enzi ya Neno Yote Yanafanikishwa Kupitia kwa Neno la Mungu Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli Mazungumzo Mafupi Kuhusu "Ufalme wa Milenia Umefika" Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu Matamshi ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima - Tamko la Ishirini na Nne Je, Umekuwa Hai Tena? Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia” (Sehemu ya Nne) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Pili) Uchaguzi Kutoka kwa Vifungu Vitatu vya Neno la Mungu juu ya "Maono ya Kazi ya Mungu" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya "Kuhusu Biblia" (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Kwanza) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu “Fumbo la Kupata Mwili” (Sehemu ya Pili) Dondoo kutoka kwa Vifungu Vinne vya Neno la Mungu Kuhusu "Fumbo la Kupata Mwili" (Sehemu ya Tatu) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi” (Sehemu ya Kwanza) Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Manne ya Neno la Mungu Juu ya "Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi" (Sehemu ya Pili) Kupata Mwili Mara Mbili Kunakamilisha Umuhimu wa Kupata Mwili Je, Utatu Mtakatifu Upo? Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Kwanza) Matukio Aliyopitia Petro: Ufahamu Wake wa Adabu na Hukumu (Sehemu ya Pili) Unapaswa Kushughulikiaje Wito Wako wa Mustakabali? Inapofikia Mungu, Ufahamu Wako ni Upi? Maana ya Kuwa Mwanaadamu Halisi Unajua Nini Kuhusu Imani? Hakuna Aliye wa Mwili Anayeweza Kuepuka Siku ya Ghadhabu Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya “Wingu Jeupe” Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia Kazi katika Enzi ya Sheria Maelezo ya Kweli ya Kazi Katika Enzi ya Ukombozi Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Kwanza) Wafaa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo (Sehemu ya Pili) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Kwanza) Kuhusu Majina na Utambulisho (Sehemu ya Pili) Wale Waliofanywa Kuwa Watimilifu Ndio tu Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana Ni Jinsi Gani Mwanadamu Aliyemfafanua Mungu katika Dhana Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu? Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu Tofauti Kati ya Huduma ya Mungu katika Mwili na Wajibu wa Mwanadamu Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Kwanza) Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea (Sehemu ya Pili) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Kwanza) Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu (Sehemu ya Pili) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Kwanza) Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili (Sehemu ya Pili) Kiini cha Mwili Ulio na Mungu Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Kwanza) Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu (Sehemu ya Pili) Kiini Cha Kristo Ni Utiifu kwa Mapenzi ya Baba wa Mbinguni Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Kwanza) Kurejesha Maisha ya Kawaida ya Mwanadamu na Kumpeleka Kwenye Hatima ya Ajabu (Sehemu ya Pili) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Kwanza) Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja (Sehemu ya Pili) Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Ambao Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia Wale Ambao Hawalingani na Kristo Hakika Ni Wapinzani wa Mungu Wengi Wameitwa, Lakini Wachache Wamechaguliwa Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu? Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli Je, Wajua? Mungu Amefanya Jambo Kubwa Miongoni Mwa Wanadamu Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako Wewe U Mwaminifu kwa Nani? Maonyo Matatu Ni Muhimu Sana Kuelewa Tabia ya Mungu Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani Amri Kumi Za Utawala Ambazo Lazima Zitiiwe Na Watu Waliochaguliwa Na Mungu Katika Enzi Ya Ufalme Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu Kutanafusi kwa Mwenye Uweza Mwanadamu Anaweza Kuokolewa tu Katikati ya Usimamizi wa Mungu

0(Ma)tokeo ya Kutafuta

Usomaji