Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 13

Elewa Mwelekeo wa Mungu na Utupilie Mbali Dhana zote Potovu Kumhusu Mungu

Mungu huyu ambaye kwa sasa mnasadiki, mmewahi kufikiria kuhusu Yeye ni Mungu wa aina gani? Anapomwona mtu mwovu akifanya mambo maovu, je Anayachukia? (Anayachukia.) Anapoona makosa ya mtu asiyejua, mwelekeo Wake ni upi? (Huzuni.) Anapowaona watu wakiiba sadaka Yake, mwelekeo Wake ni upi? (Anawachukia.) Haya yote yako wazi, sivyo? Anapoona mtu akiwa mzembe katika kusadiki kwake Mungu, na mtu huyo akikosa kufuatilia ukweli kwa namna yoyote, mwelekeo wa Mungu ni upi? Bado hamjaelewa jambo hili, sivyo? Uzembe ni mwelekeo ambao si dhambi, na humkosei Mungu. Watu husadiki kwamba haupaswi kuchukuliwa kama kosa. Basi mnafikiria mwelekeo wa Mungu ni nini? (Hayuko radhi kujibu swali hili.) Hayuko radhi kulijibu—mwelekeo huu ni upi? Ni kwamba Mungu huwa anawadharau watu hawa, anawabeza watu hawa! Mungu hushughulikia watu hawa kwa kutowathamini. Mtazamo wake ni kuwaweka pembeni, kutojihusisha na kazi yoyote inayowahusu, ikiwemo kuwapa nuru, mwangaza, kuwarudi au kuwafundisha nidhamu. Mtu wa aina hii kwa kweli si wa thamani kwa kazi ya Mungu. Mwelekeo wa Mungu kwa watu wanaozikera tabia Yake, na kuzikosea amri Zake za kiutawala ni upi? Chuki mno kwa kupindukia! Kwa kweli Mungu hupandwa na hasira kali na watu ambao hawaghairi kuhusu kukera tabia Yake! “Hasira Kali” ni hisia tu, hali ya moyo; haiwezi kuwakilisha mwelekeo kamili. Lakini hisia hii, hali hii ya moyo, itasababisha matokeo kwa mtu huyu: Itamjaza Mungu na chukizo la kupindukia! Ni nini matokeo ya kuchukia huku kwa kupindukia? Ni kwamba Mungu atamweka pembeni mtu huyu, na kutomwitikia kwa sasa. Atasubiri watu hawa waweze kushughulikiwa kwenye kipindi cha adhabu. Hali hii inaashiria nini? Mtu huyu angali anayo matokeo? Mungu hakuwahi kunuia kumpa mtu wa aina hii matokeo! Hivyo basi si jambo la kawaida endapo Mungu kwa sasa hamwitikii mtu wa aina hii? (Ndiyo.) Mtu wa aina hii anafaa kujitayarisha vipi sasa? Wanafaa kujitayarisha kukabiliana na zile athari mbaya zilizosababishwa na tabia zao na maovu waliofanya. Huu ndio mwitikio wa Mungu kwa mtu wa aina hii. Hivyo basi Nasema waziwazi kwa mtu wa aina hii: Usishikilie imani za uwongo tena, na usijihusishe katika kufikiria makuu tena. Mungu hatavumilia watu siku zote bila kikomo; Hatastahimili dhambi zao au kutotii kwao bila kukoma. Baadhi ya watu watasema: “Nimeweza pia kuona watu wachache kama hawa. Wanapoomba wanaguswa hasa na Mungu, na wanalia kwa machungu. Kwa kawaida wao pia wanakuwa na furaha sana; wanaonekana kuwa na uwepo wa Mungu, na mwongozo wa Mungu.” Usiseme huo upuzi! Kulia kwa machungu si lazima iwe kwamba umeguswa na Mungu au unao uwepo wa Mungu, acha hata mwongozo wa Mungu. Kama watu watamghadhabisha Mungu, je, bado Mungu atawaongoza? Nikiongea kwa ujumla, wakati Mungu ameamua kumwondoa mtu, kuwaacha watu hao, tayari mtu huyo hana matokeo. Haijalishi ni vipi wanavyohisi kutosheka kujihusu wao wenyewe wakati wanapoomba, na imani kiwango kipi walichonacho katika Mungu mioyoni mwao; tayari hii si muhimu. Kitu cha muhimu ni kwamba Mungu hahitaji aina hii ya imani kwamba Mungu tayari amemsukumia mbali mtu huyu. Namna ya kuwashughulikia baadaye pia si muhimu. Kilicho muhimu ni kwamba katika muda ule ambao mtu huyu atamghadhabisha Mungu, matokeo yao tayari yameanzishwa. Kama Mungu ameamua kutomwokoa mtu wa aina hii, basi ataachwa na kuadhibiwa. Huu ndio mwelekeo wa Mungu.

Ingawa sehemu ya kiini halisi cha Mungu ni upendo, na Anaitoa rehema yake kwa kila mtu, watu hupuuza na kusahau hoja kwamba kiini Chake halisi ni heshima vilevile. Kwamba Anao upendo haimaanishi kwamba watu wanaweza kumkosea Yeye wapendavyo na kwamba Yeye hana hisia zozote, au majibizo yoyote. Kwamba Anayo rehema haimaanishi kwamba Hana kanuni zozote kuhusiana na namna Anavyoshughulikia watu. Mungu yu hai; kwa kweli Yupo. Yeye si kikaragosi kilichofikiriwa au kitu kingine tu. Kwa sababu Yeye yupo, tunafaa kusikiliza kwa makini sauti ya moyo Wake siku zote, kutilia makini mwelekeo Wake, na kuzielewa hisia Zake. Hatufai kutumia kufikiria kwa watu ili kumfafanua Mungu, na hatufai kulazimisha fikira na matamanio ya watu kwa Mungu, kumfanya Mungu kutumia mtindo na fikira za binadamu katika namna Anavyomshughulikia binadamu. Ukifanya hivyo, basi unamghadhabisha Mungu, unaijaribu hasira ya Mungu, na unapinga heshima ya Mungu! Hivyo basi, baada ya kuelewa ukali na uzito wa suala hili, Ninasihi kila mmoja wenu mlio hapa kuwa makini na wenye busara katika vitendo vyenu. Kuwa makini na wenye busara katika kuongea kwenu. Na kuhusiana na namna mnavyoshughulikia Mungu, mnapokuwa makini zaidi na wenye busara zaidi, ndivyo ilivyo bora zaidi! Wakati huelewi mwelekeo wa Mungu ni nini, usizungumze kwa uzembe, usiwe mzembe katika vitendo vyako, na usipachike majina ovyo ovyo. Na hata zaidi, usikimbilie hitimisho kiholela. Badala yake, unafaa kusubiri na kutafuta; hili pia ndilo dhihirisho la kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Kama unaweza kutimiza hoja hii kati ya zote, na kumiliki mwelekeo huu kati ya yote, basi Mungu hatakulaumu wewe kwa upumbavu wako, kutojua kwako, na kutotumia kwako akili. Badala yake, kutokana na hofu yako ya kumkosea Mungu, heshima yako kwa nia za Mungu, na mwelekeo wako wa kuwa radhi kumtii Yeye, Mungu atakukumbuka, atakuongoza na kukuangaza wewe, au kustahimili kutokuwa mkomavu kwako na kutojua kwako. Kinyume chake, endapo mwelekeo wako kwake Yeye utakuwa usioheshimu—kuhukumu Mungu kiholela, kukisia kiholela, na kufafanua maana ya Mungu—Mungu atakupa hukumu, nidhamu, au hata adhabu; au Atakupa taarifa. Pengine kauli hii inahusisha matokeo yako. Hivyo basi, Ningali bado nataka kutilia mkazo jambo hili kwa mara nyingine, na kufahamisha kila mmoja aliye humu ndani kuwa makini na mwenye busara katika kila kitu kinachotoka kwa Mungu. Usiongee kwa uzembe, na usiwe mzembe katika matendo yako. Kabla ya kusema chochote, unafaa kufikiria: Je, kufanya hivi kutamghadhabisha Mungu? Kufanya hivi ni kumcha Mungu? Hata katika masuala mepesi, bado unafaa kujaribu kuelewa hakika maswali haya, yafikirie kwa kweli. Kama unaweza kwa kweli kutenda haya kulingana na kanuni hizi kila pahali, katika mambo yote, na kila wakati, hasa kuhusiana na masuala usiyoyaelewa, basi Mungu siku zote atakuongoza wewe, na siku zote atakupa njia ya kufuata. Bila kujali ni nini ambacho watu wanaonyesha, Mungu anaona yote waziwazi, dhahiri, na Atakupa utathmini sahihi na unaofaa kwa maonyesho haya. Baada ya kupitia jaribio la mwisho, Mungu atachukua tabia yako yote na kuijumlisha ili kuasisi matokeo yako. Matokeo haya yatashawishi kila mmoja bila shaka lolote. Kile ambacho Ningependa kuwaambia ni kwamba kila kitendo chenu, kila hatua yenu, na kila fikira yenu vyote vitaamua majaliwa yenu.

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp