Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 18

Sehemu ya Mwanzo ya Kumcha Mungu ni Kumtendea Kama Mungu

Mtu fulani amelizua swali hivi punde: Inakuwaje kwamba tunajua zaidi kuhusu Mungu kuliko alivyojua Ayubu, ilhali bado hatuwezi kumcha Mungu? Tuliligusia suala hili hapo awali kidogo, sivyo? Kwa hakika, kiini halisi cha swali hili kimeweza pia kuzungumziwa awali kwamba ingawa Ayubu hakumjua Mungu wakati huo, alimshughulikia Yeye kama Mungu, na kumchukulia Yeye kama Bwana wa mambo yote mbinguni na nchini. Ayubu hakumchukulia Mungu kuwa adui. Badala yake, alimwabudu Yeye kama Muumba wa viumbe vyote. Watu siku hizi wanampinga Mungu sana kwa nini? Kwa nini hawawezi kumcha Mungu? Sababu moja ni kwamba wamepotoshwa pakubwa na Shetani. Wakiwa na asili yao ya kishetani ikiwa imekita mizizi ndani, watu wanageuka na kuwa adui wa Mungu. Hivyo basi, hata ingawa wanasadiki katika Mungu na kumtambua Mungu, bado wanaweza kumpinga Mungu na kujiweka katika nafasi ya upinzani na Yeye. Hili linaamuliwa na asili ya binadamu. Sababu nyingine ni kwamba ingawa watu wanasadiki Mungu, hawamchukulii Yeye tu kama Mungu. Badala yake, wanamchukulia Mungu kuwa ndiye anayempinga binadamu, wakimwona Yeye kuwa adui wa binadamu, na hawawezi kupatanishwa na Mungu. Ni rahisi hivyo. Je, jambo hili halikuzungumziwa kwenye kikao cha awali? Hebu fikiria: Hiyo ndiyo sababu? Ingawa unayo maarifa kidogo ya Mungu, maarifa haya hasa ni nini? Haya siyo yale kila mtu anazungumzia? Haya si yale ambayo Mungu alikuambia? Unajua tu zile dhana za kinadharia na kifalsafa; umewahi kupitia dhana halisi ya Mungu? Je, unayo maarifa ya kibinafsi? Je, unayo maarifa na uzoefu wa kimatendo? Kama Mungu asingekuambia, ungelijua hili? Maarifa yako katika nadharia hayawakilishi maarifa halisi. Kwa ufupi, bila kujali ni kiwango kipi unachojua na ni vipi ulivyokijua hatimaye, kabla ya wewe kufikia uelewa halisi wa Mungu, Mungu ndiye adui wako, na kabla ya wewe kumshughulikia Mungu hivyo, Amewekwa kuwa mpinzani wako, kwani wewe ni mfano halisi wa Shetani.

Unapokuwa pamoja na Kristo, pengine unaweza kumhudumia kwa milo mitatu kwa siku, pengine kumhudumia Yeye kwa chai, kuyashughulikia mahitaji Yake ya maisha, ni kana kwamba unamshughulikia Kristo kama Mungu. Kila wakati jambo linapofanyika, mitazamo ya watu siku zote inakuwa kinyume cha mtazamo wa Mungu. Siku zote wanashindwa kuelewa mtazamo wa Mungu, na wanashindwa kuukubali. Ingawa watu wanaweza kupatana na Mungu juujuu, hii haimaanishi kwamba wanalingana na Yeye. Punde tu jambo linapofanyika, ukweli wa kutotii kwa binadamu unaibuka, na kuthibitisha ukatili uliopo kati ya binadamu na Mungu. Ukatili huu si wa Mungu kumpinga binadamu; si Mungu kutaka kuwa katili kwa binadamu, na si Mungu kumweka binadamu katika upinzani na kumshughulikia binadamu hivyo. Badala yake, ni hali ya upinzani huu wa kiini halisi kwa Mungu ambao unajificha katika mapenzi ya kibinafsi ya binadamu, na katika akili ya kutofahamu ya binadamu. Kwa sababu binadamu anachukulia kila kitu kinachotoka kwa Mungu kama kifaa cha utafiti wake, mwitikio wake kwa hiki ambacho kinatoka kwa Mungu na kile ambacho kinamhusisha Mungu ni, zaidi ya yote, kukisia, na kushuku, na kisha haraka sana kuingia katika mwelekeo ambao unakinzana na Mungu, na unapingana na Mungu. Baada ya hapo, binadamu atachukua hali hizi za moyo za kimyakimya na kuzua mjadala na Mungu au kushindana na Mungu hadi kufikia kiwango ambacho atatia shaka kama Mungu wa aina hii anastahili kufuatwa. Licha ya hoja kwamba urazini wa binadamu unamwambia asiendelee hivi, bado atachagua kufanya hivyo licha ya kutotaka kufanya hivyo, kiasi kwamba ataendelea bila kusita hadi mwisho. Kwa mfano, ni nini mwitikio wa kwanza kwa baadhi ya watu wanaposikia uvumi fulani au matusi fulani kumhusu Mungu? Mwitikio wa kwanza ni: Sijui kama uvumi huu ni kweli au la, kama upo ama haupo, hivyo basi nitasubiri na kuona. Kisha wanaanza kutafakari: Hakuna njia ya kuthibitisha haya; ipo kweli? Uvumi huu ni kweli au la? Ingawa mtu huyu haonyeshi juujuu, moyo wake tayari umeanza kutia shaka, tayari umeanza kumkataa Mungu. Ni nini kiini halisi cha aina hii ya mwelekeo, aina hii ya mtazamo? Je huu si usaliti? Kabla ya wao kukumbwa na suala, huwezi kuona mtazamo wa mtu huyu ni nini—yaonekana ni kana kwamba wao hawakinzani na Mungu, ni kama hawamchukulii Mungu kuwa adui. Hata hivyo, punde wanapokumbwa na suala hilo, wanasimama mara moja na Shetani na kumpinga Mungu. Hali hii inapendekeza nini? Inapendekeza kwamba binadamu na Mungu wanapingana! Si kwamba Mungu anamchukulia binadamu kama adui, lakini kwamba kile kiini halisi chenyewe cha binadamu ni kikatili kwa Mungu. Haijalishi ni kwa muda mrefu vipi ambapo mtu humfuata Mungu, ni kiwango kipi anacholipia; haijalishi vipi ambavyo mtu anamsifu Mungu, anavyojihifadhi dhidi ya kumpinga Mungu, hata akijisihi kumpenda Mungu, hatawahi kufaulu kumshughulikia Mungu kama Mungu. Si hali hii inaamuliwa na kiini halisi cha mwanadamu? Kama Utamshughulikia kama Mungu, unaweza kwa kweli kusadiki kwamba Yeye ni Mungu, unaweza bado kuwa na shaka lolote kwake Yeye? Bado kunaweza kuwa na maswali yoyote yanayomhusu Yeye katika moyo wako? Hakuwezi. Mitindo ya ulimwengu huu ni miovu kweli, kizazi hiki cha wanadamu kina uovu kweli—inakuwaje kwamba huna hata dhana zozote kuyahusu? Wewe mwenyewe umejaa uovu—inakuwaje kwamba huna dhana zozote kuhusu hayo? Ilhali uvumi mchache tu, matusi fulani yanaweza kusababisha dhana kubwa mno kumhusu Mungu, zinaweza kuleta mawazo mengi mno, hali inayoonyesha vile ambavyo kimo chako kilivyo bado kichanga! “Mnong’ono” tu wa mbu wachache, nzi wachache wabaya, hilo tu ndilo linalokupotosha? Huyu ni mtu wa aina gani? Je, unajua anachofikiria Mungu kuhusu mtu wa aina hii? Mwelekeo wa Mungu kwa hakika uko wazi sana kuhusiana na ni vipi Anavyowashughulikia watu hawa. Ni kwa sababu tu kwamba ushughulikiaji wa Mungu kwa watu hawa ni kuwapuuza—mwelekeo Wake ni kutowatilia maanani, na kutomakinikia watu hawa wasiojua. Kwa nini hivyo? Kwa sababu katika moyo Wake Hakuwahi kupangilia kuhusu kupata watu hao ambao wameahidi kuwa wakatili kwake Yeye hadi mwisho, na ambao hawajawahi kupangilia kutafuta njia ya uwiano na Yeye. Pengine maneno haya Niliyoyaongea yamewaumiza watu wachache. Kwa kweli, mko radhi kuniruhusu Mimi kuwadhuru siku zote namna hii? Bila kujali kama mko radhi au la, kila kitu Ninachosema ni ukweli! Kama siku zote Ninawadhuru namna hii, siku zote Nafichua makovu yenu, je, itaathiri taswira za majivuno kuhusu Mungu katika mioyo yenu? (Haitaathiri.) Ninakubali kwamba haitaathiri kwani kwa ufupi hakuna Mungu katika mioyo yenu. Yule Mungu wa majivuno anayepatikana ndani ya mioyo yenu, yule mnayemtetea kwa dhati na kulinda, kwa ufupi si Mungu. Badala yake ni ndoto ya kufikiria kwa binadamu; kwa ufupi haipo. Hivyo basi ni bora zaidi kama Nitafichua jibu la kitendawili hiki. Je, huu si ukweli wote? Mungu halisi hatokani na kufikiria kwa binadamu. Natumai kwamba nyote mnaweza kukabiliana na uhalisia huu, na utawasaidia katika maarifa yenu ya Mungu.

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo Ambayo Kazi Yake Itafanikisha

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp