Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 23

Amri ya Mungu kwa Adamu

Mwa 2:15-17 Naye Yehova Mungu akamchukua mtu huyo, na kumweka ndani ya bustani ya Edeni ili ailime na kuihifadhi. Yehova Mungu akamwamrisha mtu huyo, akisema, Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa. Je, mlielewa chochote kutoka kwenye mistari hii?

Je, ni vipi ambavyo sehemu hii ya maandiko inavyo wafanya kuhisi? Kwa nini “Amri ya Mungu kwa Adamu” ilidondolewa kutoka kwa maandiko? Je, kila mmoja wenu sasa anayo picha ya Mungu na Adamu katika akili yenu? Mnaweza kujaribu kufikiria: Kama ni nyinyi mliokuwa katika tukio hilo, je, Mungu katika moyo wenu angekuwa vipi? Ni hisia gani ambazo picha hii zinafanya mhisi? Hii ni picha ya kusisimua na ya kutuliza moyo. Ingawaje kunaye Mungu tu na binadamu ndani yake, ule ukaribu kati yao unastahili kuonewa wivu: Upendo mwingi wa Mungu amepewa binadamu kwa ukarimu, unamzunguka binadamu; binadamu ni mnyofu na asiye na hatia, aliye huru kabisa na asiyejali chochote, anayeishi kwa furaha kwa uangalizi wa jicho la Mungu; Mungu anaonyesha hali ya kujali binadamu huku naye binadamu anaishi katika ulinzi na baraka za Mungu; kila kitu binadamu anachofanya na kusema kinaunganishwa kwa karibu na Mungu na hakiwezi kutofautishwa.

Mnaweza kusema kwamba hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu aliyoitoa kwa binadamu tangu kumuumba yeye. Je, amri hii ina nini? Amri hii inayo mapenzi ya Mungu, lakini pia inayo wasiwasi Wake kwa wanadamu. Hii ndiyo amri ya kwanza ya Mungu na pia ndio mara ya kwanza Mungu anakuwa na wasiwasi kuhusu binadamu. Hivi ni kusema, Mungu analo jukumu kwa binadamu tangu ule wakati alipomuumba yeye. Jukumu Lake ni lipi? Lazima amlinde binadamu, kumwangalia binadamu. Anatumai kwamba binadamu anaweza kuamini na kutii maneno Yake. Hili pia ndilo tarajio la kwanza la Mungu kwa binadamu. Na ni kwa tarajio hili kwamba Mungu anasema yafuatayo: “Unaweza kula kwa uhuru matunda kutoka miti yote ya bustani: Lakini kutoka mti wa maarifa ya mema na maovu, usiyale: kwa kuwa katika siku ambapo utakula matunda kutoka mti huo bila shaka utakufa.” Maneno haya rahisi yanawakilisha mapenzi ya Mungu. Yanafichua pia kwamba moyo wa Mungu tayari umeanza kuonyesha hali ya kujali binadamu. Miongoni mwa mambo yote, ni Adamu pekee aliyeumbwa kwa taswira ya Mungu; Adamu alikuwa kiumbe wa pekee aliye hai aliye na pumzi ya uhai ya Mungu; angeweza kutembea na Mungu, kuzungumza na Mungu. Na ndiyo maana Mungu alimpa amri kama hiyo. Mungu aliweka wazi katika amri hii kile binadamu anaweza kufanya, na vilevile akaweka wazi kile asichoweza kufanya.

Katika maneno haya machache rahisi, tunauona moyo wa Mungu. Lakini ni aina gani ya moyo tunaouona? Je, kunao upendo katika moyo wa Mungu? Je, upendo huo unao hali yoyote ya kujali ndani yake? Upendo wa Mungu na kujali kwake katika mistari hii hakuwezi kutambulika na kuthaminiwa tu na watu, lakini unaweza pia kuhisiwa vizuri na kwa kweli. Hayo ni kweli? Kwa vile nimesema tayari mambo haya, bado mnafikiria kwamba haya ni maneno machache tu rahisi? Si rahisi hivyo, kweli? Mngeweza kuona hivi awali? Kama Mungu mwenyewe angekuambia maneno hayo machache mngehisi vipi ndani yenu? Kama wewe si mtu mwenye utu, kama moyo wako ni baridi kama barafu, basi usingehisi chochote, usingethamini upendo wa Mungu, na usingejaribu kuuelewa moyo wa Mungu. Lakini kama wewe ni mtu mwenye dhamiri, mwenye ubinadamu, basi utahisi tofauti. Utahisi joto, utahisi kuwa umetunzwa na umependwa, na utahisi furaha. Je, hayo ni kweli? Unapohisi mambo haya, utatenda vipi kwa Mungu? Utahisi ukiwa umeunganishwa kwa Mungu? Utampenda na kumheshimu Mungu kutoka kwenye sakafu ya moyo wako? Moyo wako utakuwa karibu zaidi na Mungu? Unaweza kuona kutoka kwa haya namna ambavyo upendo wa Mungu ulivyo muhimu kwa binadamu. Lakini kile kilicho muhimu zaidi ni kuthamini na kufahamu kwa binadamu upendo huu wa Mungu. Kwa hakika, Mungu hasemi mambo mengi yanayofanana kwenye awamu hii ya kazi Yake? Lakini je, watu wa leo wanauthamini moyo wa Mungu? Je, mnaweza kung’amua mapenzi ya Mungu Niliyoyazungumzia muda mfupi uliopita? Hamwezi hata kutambua mapenzi ya Mungu wakati yanaonekana waziwazi, yanaweza kushikika na ni halisi. Na ndiyo maana Nasema hamna maarifa na uelewa halisi wa Mungu. Je, haya si kweli?

Neno, Vol. 2. Kuhusu Kumjua Mungu. Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp