Maneno ya Mungu ya Kila Siku: Kumjua Mungu | Dondoo 35

Ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu

Mwa 22:16-18 Mimi nimeapa kujipitia, akasema Yehova, kwa maana umefanya jambo hili, na hujamzuilia mwana wako, mwana wako wa pekee: Kuwa katika kubariki nitakupa baraka, na katika kuzidisha uzao wako nitazidisha mithili ya nyota za mbinguni, na mithili ya mchanga uliopo kwenye ukanda wa pwani; na uzao wako utakuwa na mlango wa maadui zao; Na kupitia uzao wako kila taifa la dunia litabarikiwa; kwa kuwa umeitumikia sauti yangu.

Kuwapata Wale Wanaomjua Mungu na Wanaoweza Kumshuhudia Ndilo Tamanio la Mungu Lisilobadilika

Wakati huohuo Alipokuwa akijizungumzia Mwenyewe, Mungu alizungumza pia na Ibrahimu, lakini mbali na kusikiliza baraka ambazo Mungu alimpa, Ibrahimu aliweza kuyaelewa matamanio ya kweli ya Mungu katika maneno Yake yote wakati huo? Hakuweza! Na hivyo, kwa wakati huo, wakati Mungu alipoapa kwa nafsi Yake Mwenyewe, moyo Wake ulikuwa bado pweke na wenye huzuni. Hakukuwepo hata na mtu mmoja wa kuweza kuelewa au kufahamu kile Alichonuia na Alichopangilia. Wakati huo, hakuna—akiwemo Ibrahimu—aliyeweza kuongea na Yeye kwa ujasiri, isitoshe hakuna yule aliyeweza kushirikiana na Yeye katika kufanya kazi ambayo lazima Angefanya. Juujuu, Mungu alikuwa Amempata Ibrahimu na Alipata mtu ambaye angetii maneno Yake. Lakini kwa hakika, maarifa ya mtu huyu kuhusu Mungu yalikuwa kidogo mno. Hata ingawaje Mungu alikuwa amembariki Ibrahimu, moyo wa Mungu ulikuwa bado hujatosheka. Inamaanisha nini kwamba Mungu hakuwa ametosheka? Inamaanisha kwamba usimamizi Wake ulikuwa tu umeanza, inamaanisha kwamba watu Aliotaka kupata, watu Aliotamani kuona, watu Aliopenda, walikuwa bado mbali na Yeye; Alihitaji muda, Alihitaji kusubiri, Alihitaji kuwa na subira. Kwani kwa wakati huo, mbali na Mungu Mwenyewe, hakuna yeyote yule aliyejua kile Alichohitaji au kile Alichotaka kupata, au kile Alichotamani. Na hivyo basi, Kwa wakati huohuo aliokuwa akihisi sana furaha Mungu pia alihisi kuwa mwenye uzito wa moyo. Bado Hakusitisha hatua Zake, na Aliendelea kupanga hatua inayofuata ya kile ambacho lazima Afanye.

Mnaona nini katika ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu? Mungu alimpa baraka kuu Ibrahimu kwa sababu tu ya yeye kusikiliza maneno ya Mungu. Ingawaje, juujuu, hali hii yaonekana ya kawaida na suala ambalo bila shaka, ndani yake tunauona moyo wa Mungu: Mungu hasa anathamini utiifu wa binadamu kwake Yeye, na hutunzwa mno na uelewa wa binadamu kuhusu Yeye na uaminifu wake Kwake. Mungu anathamini kiasi kipi uaminifu huu? Huenda msielewe ni kiasi kipi ambacho Yeye Anauthamini, na huenda hata kusiwe na yeyote anayeutambua. Mungu alimpa Ibrahimu mwana, na wakati mwana huyo alipokua, Mungu alimwomba Ibrahimu kumkabidhi mtoto wake Kwake. Ibrahimu alifuata amri ya Mungu kwa umakinifu, alitii neno la Mungu na uaminifu wake ulimpendeza Mungu na ukathaminiwa sana na Mungu. Mungu aliuthamini kiasi kipi? Na kwa nini Akauthamini sana? Kwa wakati ambao hakuna aliyefahamu maneno ya Mungu au kuuelewa moyo Wake, Ibrahimu alifanya kitu kilichotikisa mbingu na kutetemesha ardhi, na kikafanya Mungu kuhisi hali fulani ya kutosheka kwa mara ya kwanza, kikamletea Mungu furaha ya kumpata mtu ambaye aliweza kutii maneno Yake. Uradhi na furaha hii ilitoka kwa kiumbe aliyeumbwa kwa mikono ya Mungu, na ndiyo iliyokuwa “sadaka” ya kwanza ambayo binadamu aliwahi kumpa Mungu na ambayo ilithaminiwa sana na Mungu, tangu binadamu kuumbwa. Mungu alikuwa na wakati mgumu kusubiria sadaka hii, na Aliichukulia kama zawadi ya kwanza muhimu zaidi kutoka kwa binadamu, ambaye Alikuwa amemuumba. Hii ilionyesha Mungu tunda la kwanza la jitihada Zake, na gharama ambayo Alikuwa amelipia na ikamruhusu Yeye kuliona tumaini kwa wanadamu. Baadaye, Mungu alikuwa na hata tamanio kubwa zaidi la kundi la watu kama hao wa kushinda na Yeye kumchukulia Yeye kwa uaminifu, kumtunza Yeye kwa uaminifu. Mungu alitamani hata kwamba Ibrahimu angeendelea kuishi, kwani Alipenda kuwa na moyo kama huo ukiandamana na Yeye na kuwa na Yeye Alipoendelea na usimamizi Wake. Haijalishi ni nini alichotaka Mungu, yalikuwa tu ni matakwa, wazo tu—kwani Ibrahimu alikuwa tu binadamu aliyeweza kumtii Yeye, na wala hakuwa na uelewa au maarifa hata madogo zaidi kuhusu Mungu. Yeye alikuwa mtu aliyepungukiwa pakubwa na viwango vya mahitaji ya Mungu kwa binadamu: kumjua Mungu, kuweza kushuhudia Mungu, na kuwa na akili sawa na Mungu. Na hivyo, hangeweza kutembea na Mungu. Katika sadaka ya Ibrahimu ya Isaka, Mungu aliuona uaminifu na utiifu huu wa Ibrahimu, na Akaona kwamba alikuwa amestahimili jaribio la Mungu kwake yeye. Hata ingawaje Mungu aliukubali uaminifu na utiifu wake, bado hakustahili kuwa mwandani wa Mungu, wa kuwa mtu aliyemjua Mungu, na kumwelewa Mungu, na alifahamishwa kuhusu tabia ya Mungu; alikuwa mbali sana na kuwa na akili sawa na Mungu na vilevile kuweza kufanya mapenzi ya Mungu. Hivyo basi, katika moyo Wake, Mungu alikuwa bado mpweke na mwenye wasiwasi. Kwa kadri Mungu alipokuwa mpweke na mwenye wasiwasi zaidi, ndipo Yeye alipohitaji zaidi kuendelea na usimamizi Wake haraka iwezekanavyo, na kuweza kuchagua na kulipata kundi la watu wa kukamilisha mpango Wake wa usimamizi na kutimiza mapenzi Yake haraka iwezekanavyo. Hili ndilo lilikuwa tamanio lenye hamu kubwa la Mungu, na limebakia vilevile kuanzia mwanzo kabisa hadi leo. Tangu Alipomuumba binadamu hapo mwanzo, Mungu ametamani kuwa na kundi la washindi, kundi ambalo litatembea na Yeye na linaweza kuelewa, kufahamu na kujua tabia Yake. Mapenzi haya ya Mungu hayajawahi kubadilika. Haijalishi ni muda gani bado Atasubiria, haijalishi barabara iliyo mbele ni ngumu kiasi gani, hata malengo Anayoyatamani yawe mbali kiasi kipi, Mungu hajawahi kubadilisha au kukata tamaa katika matarajio Yake kuhusu binadamu. Kwa vile nimeyasema haya, mnatambua chochote kuhusu mapenzi ya Mungu? Pengine kile ulichotambua hakina uzito sana—lakini kitajitokeza kwa utaratibu!

Kimetoholewa kutoka katika Neno Laonekana katika Mwili

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp